Pages

Showing posts with label Afya - Health. Show all posts
Showing posts with label Afya - Health. Show all posts

Friday, September 7, 2012

Uzinduzi wa Mpango Wa Mpya Wa Kuboresha Maarifa Ya Utoaji Damu Kwa Wahudumu Wa Afya

Dr mohammed mohammed) Mkurugenzi wa Usimamizi Ubora Huduma kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akizungumza katika ufunguzi wa mradi unaogharamiwa na serikali ya Marekani.
Dr Margreth Mhando, Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akiwa na Dr Mohammed Mohammed wakiwa na mfano wa mkoba wenye vifaa vipya vya kutolea damu kwa njia salamabaada ya uzinduzi wa shughuli hiyo mjini Dar Es Salaam.
Sehemu ya washiriki na wakufunzi wa mafunzo ya utoaji damu salama wakisiliza ufunguzi wa kazi inayotarajiwa kupunguza uwezekano wa watoa huduma ya tiba kupata maambukizi kwa njia salama.
--
Na: Hassan Mhelela

Jumla ya watumishi 500 wa sekta ya afya watanufaika na mafunzo ya mbinu mpya za utoaji damu ya wagonjwa kwa njia salam. Mpango huo mpya ni sehemu ya mradi unaosimamiwa na Wizara ya Afya,

kwa kushirikiana na washirika na wafanyakazi wa sekta ya afya nchini Tanzania.


Kazi hiyo inatekelezwa kwa ushirikiano na Mpango Dharura wa Rais wa Marekani kwa Ajili ya Kupunguza Makali ya UKIMWI (PEPFAR) kupitia taasisi ya udhibiti na kuzuia maradhi (Centers for Disease Control and Prevention - CDC) chini ya Wizara ya Afya ya Marekani na kampuni ya BD (Becton, Dickinson and Company).
Vile vile JHPIEGO, mshirika wa kiufundi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ya Tanzania, watashirikiana katika jitihada za kusimamia na kusambaza huduma hizi zilizoongezwa ubora.


Mpango wa Tanzania Initiative for Blood-Drawing Applications (TIBA) , una malengo ya kuboresha huduma za afya na maabira katika vituo vya afya, hasa katika mikoa yenye maambukizi zaidi ya VVU/UKIMWI. Shughuli ya kutoa damu katika mwili wa mgonjwa kupitia mishipa ya damu kwa kutumia sindano ni mojawapo ya njia zinazotumika kwa wingi katika hospitali na zahanati, ingawa njia hii inakabiliwa na hatari nyingi za kiafya.

Utafiti uliofanyika mwaka 2008 katika taasisi za afya 14 ulibaini kulikuwa na asilimia 52.9 ya matukio ya kujichoma kwa sindano na kujimwagia damu ya wagonjwa asilimia 21.7 miongoni mwa wafanyakazi wa sekta ya afya. Jumla ya wafanyakazi wa huduma ya afya 500 watanufaika na mafunzo hayo kote nchini.

Monday, August 6, 2012

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUWEPO KWA MGONJWA WA EBOLA, WILAYA YA KARAGWE MKOA WA KAGERA, TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUWEPO KWA MGONJWA WA EBOLA, WILAYA YA KARAGWE MKOA WA KAGERA, TANZANIA


Utangulizi

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa umma, kuhusu tetesi zilizokuwa zimeenea hapa nchini kutoka kwenye vyombo mbali mbali vya habari kuhusu kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola,wilayani Karagwe mkoa wa Kagera.

Mnamo tarehe 3 Agosti 2012, Wizara ya Afya na Ustawi Wa Jamii ilipokea taarifa kutoka kwa mganga mkuu wa wilaya ya Karagwe ya kuwepo kwa mgonjwa aliyekuwa anahisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola, katika hospitali ya Wilaya ya Nyakahanga. Aidha,taarifa hiyo ilibainisha kuwa mgonjwa huyo alikuwa ni mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka (6|) kutoka katika kijiji cha Nyakatundu wilayani Karagwe. Mgonjwa huyu alikuwa na dalili za homa kali, kulegea, kutokwa damu puani, kutapika damu, na kukojoa damu.Maelezo kutoka kwa mama mzazi zilieleza kuwa mtoto huyu alianza kuugua kuanzia tarehe 30 Agosti 2012, ambapo alipatiwa dawa ya Septrin baada ya hospitali binafsi kuonyesha kuwa ana ugonjwa wa“Typhoid”.

Uchunguzi wa awali katika hospitali ya Nyakahanga ulionyesha kuwa mtoto huyu alikuwa anasumbuliwa na uambukizo kwenye haja ndogo (Urinary Tract Infection).Vile vile alifanyiwa uchunguzi wa kimaabara na Vipimo vya malaria, Hepatitis na Typhoid havikuonyesha kuwepo kwa magonjwa haya. Hospitali inaendelea kumpatia matibabu mtoto huyu na imewaweka mgonjwa na mama yake anayemtunza kwenye chumba maalum (Isolatiom room) kwa ajili ya uangalizi zaidi.

Aidha mnamo tarehe 4 Agosti 2012, timu za wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na timu ya mkoa wa Kagera imeweza kufika na kumfanyia uchunguzi wa kina pamoja na kuchukua sampuli za damu kwa ajili ya uchunguzi zaidi katika maabara ya Taifa ya uchunguzi wa magonjwa na Maabara za nje ya nchi, ili kubaini kama ameathirika na ugonjwa wa Ebola. Timu hiyo ya wataalamu imetoa taarifa kuwa hali ya mgonjwa huyu kwa sasa imeimarika ikiwa pamoja na kutokuwa na homa, kutapika na kukojoa damu kumekoma pia, uchunguzi uliofanywa kwa mama wa mtoto umeonyesha kuwa hana dalili zozote za ugonjwa wa Ebola.Vile vile hakuna taarifa ya mtu mwingine yeyote kwenye familia hiyo au kwenye maeneo ya kijiji hicho au cha jirani kuwa na dalili za ugonjwa huo.


Kufuatia taarifa hii, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Mkoa wa Kagera imechukua hatua zifuatazo;
• Imepeleka timu ya wataalamu mbali mbali kutoka Wizarani na mkoa kwa lengo la kwenda kufuatilia na kutoa taarifa kuhusu kuwepo kwa ugonjwa huo.
• Imetoa elimu ya Afya kuhusu njia za kuzuia kuenea ugonjwa wa Ebola pamoja na dalili za ugonjwa huu, kwa wananchi na watumishi wa afya katika hospitali ya Nyakahanga
• Kupeleka vifaa kinga katika hospitali ya Nyakahanga pamoja na maeneo ya mipakani
• Kutoa matangazo kwa jamii kwa kutumia vipaaza sauti na kupitia radioni (Radio Karagwe) kuhusu ugonjwa huu. Aidha, vipeperushi pia vimetolewa.



Hitimisho

Wizara inapenda kuufahamisha umma kuwa mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola hapa nchini.Aidha, Wizara ya Afya imejiaanda kikamilifu kukabiliana na ugonjwa huu iwapo utatokea hapa nchini.

Kwa sasa timu za wataalum zipo katika mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro na Arusha, kutoa elimu juu ya ugonjwa huu kwa wataalamu na kwa wananchi na vilevile kufuatilia ugonjwa huu sehemu za mipakani.

Wizara inaendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa haraka kwenye kituo chochote cha kutolea huduma za afya, mara wanapoona dalili za ugonjwa huu.


Imetolewa na:
kitengo cha Mawasiliano
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Tarehe 6 Agosti, 2012

Thursday, July 26, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANAO LA KWANZA KUHUSU UGONJWA WA KISUKARI KWA NCHI ZA AFRIKA, ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Kongamano la kwanza kuhusu Ugonjwa wa Kisukari kwa Nchi za Afrika, lililoanza leo jijini Arusha.
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais wa ‘International Diabetes Federation’, Jean-Claude Mbanya, baada ya kumaliza hotuba yake wakati akifungua rasmi Kongamano la kwanza kuhusu Ugonjwa wa Kisukari kwa Nchi za Afrika, lililoanza leo, jijini Arusha.
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya watoto wanaishi na ugonjwa wa Kisukari kutoka Mataifa mbalimbali ya Afrika, wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa Kongamano la kwanza kuhusu Ugonjwa wa Kisukari kwa Nchi za Afrika, lililoanza leo, jijini Arusha. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na watoto waishio na ugonjwa wa kisukari, baada ya kufungua rasmi Kongamano la kwanza kuhusu Ugonjwa wa Kisukari kwa Nchi za Afrika, lililoanza leo, jijini Arusha.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamanao hilo.
Watoto hao wakiimba wimbo maalum wa mshikamano.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais wa ‘International Diabetes Federation’, Jean-Claude Mbanya, baada ya kufungua rasmi Kongamano la kwanza kuhusu Ugonjwa wa Kisukari kwa Nchi za Afrika, lililoanza leo, jijini Arusha.

Wednesday, July 25, 2012

HOSPITALI YA AICC KUENDESHA KAMPENI YA KUPIMA KISUKARI BILA GHARAMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Arusha, Tanzania.
Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha kupitia hospitali yake ya AICC kitaendesha kampeni ya kupima kisukari bure kwa wakazi wa Arusha ili kusaidia wananchi kutambua kama wana ugonjwa wa kisukari au wapo katika hatari ya kuugua ugonjwa huo.

Kampeni hiyo itafanyika kesho (terehe 26-07-2012) katika hopitali ya AICC iliyopo jijini Arusha ambapo madaktari wa hospitali ya AICC kwa kushirikiana na madaktari wa wanaohudhuria mkutano wa Shirikisho la Madaktari wa Kimataifa pamoja na madaktari kutoka Chama cha Ugonjwa wa Kisukari Tanzania wataendesha zoezi la upimaji huo.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC, Bwana Elishilia Kaaya, amesema kuwa mbali na kupima kisukari, madaktari hao pia watatoa ushauri wa namna bora ya kuishi na jinsi ya kuzuia madhara ya kisukari kwa wale watakao kuwa wamekutwa na ugonjwa huo.

“Hospitali ya AICC inatambua umuhimu wa afya za wakazi wa Arusha na Watanzania kwa ujumla na ndio maana tumeona ni vema kufanya kampeni hii ya kupima kisukari.

Napenda kutumia fursa hii kuwaalika wakazi wote wa Arusha na vitongoji nyake kufika kwa wingi kwani mbali na kupima pia itatolewa elimu na ushauri kutoka kwa wataalamu hao.” alieleza Kaaya.

Kwa mujibu Mkurugenzi Mwendeshaji, upimaji huo utaenda sambamba na mkutano wa kwanza wa Shirikisho la Madaktari wa Kisukari wa Kimataifa ambao kwa mara ya kwanza unafanyika hapa nchini.

Mkutano huo utafanyika katika kituo cha AICC ambapo madaktari wanaohudhuria mkutano huo na wale kutoka Chama cha Ugonjwa wa Kisukari Tanzania watatoa huduma ya upimaji katika zoezi hilo.

“Tunaamini baada ya kampeni hii wananchi watakuwa wamepata ufahamu juu ya hali ya afya zao na kutumia vema ushauri wa madaktari kwa ajili ya kujikinga na kuzua athari za ugonjwa huo”, alielezea Kaaya.

Mbali na kuendesha kampeni hii, hospitali ya AICC imeanzisha kitengo maalumu cha kisukari ambapo kila wiki madaktari hutoa huduma za matibabu na ushauri kwa wagonjwa wa kisukri.

Ugonjwa wa kisukari umekuwa ukiongezeka kwa kasi duniani ambapo taarifa za Shirika la Afrya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa hadi kufikia mwaka 2011 watu milioni 366 walikuwa wanaugua ugonjwa wa kisukari na mwaka 2030 idadi inakadiriwa kufika milioni 552.

Barani Afrika watu milioni 14 na nusu wanaugua ugonjwa huo huku idadi ikitarajiwa kufika milioni 28 mwaka 2030 ikiwa ni ongezeko la asilimia 90.

Monday, July 16, 2012

Africa: Human Rights Is Essential in Fight Against HIV/Aids

OPINION

The world's collective response to HIV three decades ago can be summed up in one word: shameful. At worst, people living with HIV were, inexplicably, chained to their beds, detained, turned away from medical facilities, criminalized and deported. At best, they lost their jobs, were kicked out of schools and denied access to basic services.

We responded to a virus by humiliating, stigmatizing and punishing those infected. Our response to the virus was as painful, and sometimes as deadly as the virus itself.

Fortunately, impressive strides have since been made in the fight against HIV. In the last few years, major scientific advances have occurred and the number of new HIV infections, particularly among children, has been slowly declining, fewer people are dying from AIDS-related causes, nearly half of those people eligible for antiretroviral treatment, including in low- and middle-income countries, are now receiving it, and treatment has become the new engine for prevention. HIV is no longer the certain death sentence it once was.

And yet, the stigma and discrimination faced by HIV-positive people remains high, in every region of the world. Even today, we continue to focus on punitive approaches to HIV such as the criminalization of HIV transmission, non-disclosure and exposure. Entry restrictions against and deportation of HIV-positive non-nationals at borders are still far too common, particularly in the more affluent countries. The most vulnerable communities, the ones that least enjoy their fundamental human rights, also remain disproportionately more vulnerable to HIV infection - and this is no coincidence.

The face of HIV has always been the face of our failure to protect human rights. One of the key drivers of AIDS has always been, and remains, this failure to ensure human rights protection for marginalized communities, including prisoners, sex workers, drug users, people with disabilities and migrants, refugees and asylum seekers. Homophobia, gender discrimination, racial profiling and violence against women have further impeded efforts to effectively manage and contain the spread of HIV.

The theme of this year's International AIDS Conference, which is being held in Washington, DC, this July, is "Turning the Tide Together." It is indeed now time to turn the tide. The human rights violations that have characterized the spread of HIV - and in many cases also the fight against HIV - must be curbed.

It is time to build on the gains of the past few years to create a sustainable global response to an epidemic that still challenges us. Taking a human rights perspective on the issue is essential.

The starting point is the recognition of all people as equal in the enjoyment of their human rights. Vulnerable populations that are most at risk must not only be included in national responses to HIV, they must also be given the opportunity to participate in making the policies that will affect them.

Human rights norms must accompany public health considerations to ensure that our laws, policies and programmes do not increase vulnerability to HIV or result in further human rights violations. Broad laws and policies in many countries that criminalize non-intentional HIV transmission, exposure and non-disclosure, target specific groups for mandatory HIV testing, and restrict travel of individuals based on HIV status alone are examples of such alarmist and misguided policies.

Advances in the right direction have been made, one of which - the lifting of travel restrictions - has enabled the United States to host this important AIDS conference this year, after 22 years. But much remains to be done. Even in states where laws are on the books to protect and promote the human rights of HIV-positive people, the extent to which they are respected and enforced is not clear.

More resources certainly need to be channelled into ensuring access to good quality lifesaving antiretroviral treatment, but also to human rights programmes, including awareness raising, training of healthcare providers and law enforcement officials, access to justice for HIV-positive individuals, fighting stigma and educating young people about safe sex.

Funding the fight against AIDS in this holistic fashion is not only necessary; it is also a human rights legal obligation. The current economic crisis cannot be an excuse for diminishing our investment in the response to AIDS. This would result in a reversal in the gains made so far.

This is not a time for complacency. UNAIDS has as its goal: zero new infections, zero AIDS-related deaths and zero discrimination. At this AIDS conference, a gathering of high-level government officials, civil society, the international community and, importantly, people living with HIV, it is essential to drive home the point that in order to succeed, human rights must inform and motivate our response.

Navi Pillay is the United Nations High Commissioner for Human Rights. She wrote this article in advance of the International AIDS Conference in Washington, DC, 22-27 July.

Sunday, July 15, 2012

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii Yatembelea NHIF

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Mh. Dk. Hussein Mwinyi akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyofanya ziara yale leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo yenye lengo la kujifunza mambo mbali mbali yanayofanya na Mfuko huo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Dk. Faustine Ndungulile akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo na viongozi wakuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakati kamati yake ilipofanya ziara katika makao makuu ya Shirika hilo yaliyopo Kurasini,jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini,Mh. Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu akisalimia wadau.
Mjumbe wa Kamati hiyo na Mbunge wa Jimbo la Nzega, Dk. Hamisi Kigwangalla nae akisalimia wadau.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Ndg. Emmanuel Humba akitoa maelezo mafupi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Mh. Deogratius Mtukamazina (kulia) akitoa salamu ya Bodi yake kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyofanya ziara yale jana kwenye makao makuu ya Mfuko huo yenye lengo la kujifunza mambo mbali mbali yanayofanya na Mfuko huo.Wengine pichani ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Dk. Faustine Ndungulile,Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Mh. Dk. Hussein Mwinyi,Naibu Waziri wa Afya, Dk. Sirra Umbwa,Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI),Mh. Majaliwa K. Majaliwa.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii wakifuatia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa ukumbini hapo.
Meneja wa Idara ya Uanachama wa NHIF,Bi. Ellentruder Mbogoro akielekeza jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii walipotembelea makao makuu ya Mfuko huo,Kurasini jijini Dar es Salaam jana.
Afisa Nyaraka wa NHIF,Erastus Msigwa akiwaonyesha Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii moja ya mafaili ya Wanachama wa Mfuko huo yaliyohifadhiwa kwenye Masanduku ya Kisasa yanayotumia mfumo wa Umeme.

Tuesday, July 10, 2012

JUU YA UZUSHI UNAOENEZWA NA MH. MWIGULU NCHEMBA JUU YANGU NA CHAMA CHANGU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA UZUSHI UNAOENEZWA NA MH. MWIGULU NCHEMBA JUU YANGU NA CHAMA CHANGU


Ndugu zangu kwanza nachukua nafasi hii kuendelea kumshukuru Mungu kwa afya njema anayoendelea kunijalia mimi na Mke wangu hapa Hospitali ya KCMC. Pia niwashukuru wote walionifariji/wanaoendelea kunifariji katika kipindi chote cha matatizo yaliyotokea.

UTANGULIZI

Itakumbukwa kuwa tarehe 28/05/2012 nilipata mbaya ya gari. Ajali hiyo ilitokea maeneo ya Boma karibu na chuo cha VETA. Watu wa kwanza kufika kwenye Eneo la ajali na kutupa msaada walikuwa ni Askari Polisi waliokuwa Doria karibu na eneo lile na Raia waliofika wa pia walikuwemo MWENYEKITI WA CHADEMA (W) YA HAI pamoja na MWENYEKITI WA BAVICHA (W) YA HAI. Walisaidiana na Polisi kuchukua majeruhi (Mimi nikiwemo) pamoja na marehemu waliofariki pale hadi Hospitalini.

Baada ya kufika hospitalini pia walifika MHE.MEYA WA MANISPAA YA MOSHI (AMBAYE PIA NI DIWANI WA CHADEMA) akiongozana na baadhi ya VIONGOZI WA CHADEMA WA KATA YAKE NA BAADHI YA MAENEO YA MOSHI MJINI.. Baadaye alifika KATIBU WA CHADEMA MKOA WA KILIMANJARO AKIONGOZANA NA BAADHI YA MADIWANI WA CHADEMA WA MOSHI NA ARUSHA na Viongozi wengine ambapo nakumbuka walitokea Wilaya ya Mwanga kwenye Mikutano ya Hadhara. Tulikuwa wote hadi tunapatiwa huduma na majeruhi tukapelekwa Wodini. Siku iliyofuata nilipokea Simu kutoka kwa MHE. FREEMAN MBOWE (MWENYEKITI WA CHADEMA NA KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI) akiwa Mtwara kwa shughuli za Chama akinipa Pole kwa yaliyotokea na kunifariji.

Baadaye hali yangu ilipoimarika kidogo tukapanga taratibu za mazishi ya Marehemu Mama yangu Mzazi (R.I.P) na miongoni mwa watu waliohudhuria kwanza ni WANACHAMA WA CHADEMA, MADIWANI WOTE WA CHADEMA ARUSHA, MADIWANI WA MOSHI MJINI NA MOSHI VIJIJINI. Kutoka makao makuu ya CHADEMA waliwakilishwa na Mhe.Rwakatare na Ndg.Anthony Komu (Mkurugenzi wa Fedha na Utawala) Pia walihudhuria Baadhi ya WWABUNGE WA CHADEMA wakieleza sababu za viongozi na wabunge wengine kutokuhudhuria (Na zilikuwa Sababu za Msingi kabisa) kwa sababu hata baadhi ya viongozi wa serikali waliohudhuria walileta salam za wakubwa wao ambao nao walitamani kuhudhuria lakini kutokana na sababu mbali mbali walishindwa!..

Pamoja na hayo, MHAMA JOSEPHINE MUSHUMBUSI (MKE WA MHE.KATIBU MKUU WA CHADEMA) alinitembelea hospitalini akiwa na wajumbe kadhaa... Aliniletea salam za pole kutoka kwa KATIBU WANGU MKUU WA CHAMA. Nilifarijika sana kuona kuwa kiongozi wangu pamoja na kuwepo kwake safarini kikazi lakini bado aliweza kutuma ujumbe kwangu.

Baadaye nilihamishiwa MOI (Muhimbili) kwa ajili ya matibabu Zaidi. Nakumbuka walifika wabunge wengi sana wa CHADEMA lakini kubwa zaidi alifika MHE.FREEMAN MBOWE (MWENYEKITI WA CHADEMA KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI).

KANUSHO

Nimekuwa nikisikia kwenye vyombo vya habari kuwa Mwigulu Nchemba (Mb-CCM) Anatangaza kuwa Chama changu kimenitupa na hakina msaada wala Ushirikiano na mimi kwenye Matatizo yaliyojitokeza..

Kwanza: Sijawahi kumwajiri Mwigulu Nchemba kuwa msemaji wangu!.

Pili: Mwigulu Nchemba si mkweli na hajui chochote kuhusu mimi wala CHADEMA.

Tatu: Mwigulu Nchemba anataka nionekane sina shukrani kwa viongozi na Chama changu kwa Umoja na Ushirikiano wanaoendelea kunipatia hata sasa.

Nne: Viongozi wangu wanafuatilia kwa karibu sana matibabu yangu na Mke wangu.

MWISHO:

Naomba Mwigulu aelewe kuwa sitaki malumbano yasiyo na Tija kwangu wala kwa Wananchi wangu Walionichagua. Pia nisingependa kumtaja Marehemu Mama Yangu (R.I.P) kabla hata ya Arobaini. Zaidi ya yote akumbuke kuwa Viongozi na Wabunge wa CHADEMA wana mambo mengi ya kufanya na hawatakuwa tayari tena kujibu uongo na uzushi DHAIFU kama aliouzusha!!.

Ahsanteni Sana,
Mungu aendelee kuwabariki.
Joseph Selasini
(Mb) Rombo-CHADEMA.

via facebook.com/joseph.selasini

Thursday, July 5, 2012

TAMKO LA SIKIKA KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI

UTANGULIZI

SIKIKA ni shirika lisilo la kiserikali linalotekeleza shughuli mbali mbali zenye lengo la kuchochea upatikanaji wa huduma za afya zenye uwiano, viwango na ubora unaokubalika, gharama nafuu na zilizo endelevu. SIKIKA imekuwa mstari wa mbele kufanya tafiti katika sekta ya afya na kuhimiza utekelezaji wa sera, uwajibikaji na upatikanaji wa huduma bora nchini Tanzania.

Kama neno ‘afya’ lilivyo tafsiriwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) Mwaka 1948, sera ya afya ya Taifa (Tanzania Health Policy) ya mwaka 2007, nayo pia inatambua ‘afya’ kama hali ya ukamilifu wa binadamu kiakili, kimwili, kijamii na siyo tu kutokuwepo kwa maradhi. Afya bora ni mhimili wa maendeleo ya mtu binafsi, familia na taifa zima kwa ujumla hasa katika harakati za kuondoa umasikini uliokithiri katika taifa letu.

Katika nchi yetu, mfumo wa utoaji huduma katika sekta ya afya umegawanyika katika ngazi tatu yaani ngazi ya afya ya msingi kama vile zahanati na vituo vya afya, ngazi ya pili kama vile hospitali za wilaya au mikoa na ngazi ya hospitali za rufaa kama vile hospitali ya Muhimbili, Mbeya, Bugando, KCMC na hospitali maalumu kama taasisi ya magonjwa ya kansa ya Ocean Road au hospitali ya magonjwa ya akili ya Milembe. Hospitali hizi za rufaa hushughulika na magonjwa ambayo ama yameshindikana katika hospitali za ngazi za chini au wataalamu waliopo katika ngazi hizo na vifaa vilivyopo haviwezi kutoa huduma stahili kwa magonjwa hayo. Hivyo basi, iwapo kutakuwa na matatizo yanayoathiri utendaji wao wa kazi wa kila siku na kwa kuwa wagonjwa walioletwa katika hospitali hizi za rufaa hawawezi kurudishwa kule walikotoka (ngazi za chini), wagonjwa hawa wasio na hatia ndiyo waumiao kutokana na matatizo hayo.

Migomo ya watumishi katika sekta ya afya ni mojawapo ya matatizo yanayoweza kuathiri utendaji kazi wa wataalamu wa afya, siyo tu katika hospitali za rufaa hata pia katika hospitali za ngazi za chini. Kwa historia ya migomo hii, Mwananchi anayehitaji huduma za afya hana mchango wa moja kwa moja katika
kusababisha migomo ya watumishi wa afya. Mwananchi ameiweka serikali madarakani na analipa kodi ili serikali hiyo itoe huduma bora za kiafya kwake ili awe na nguvu za kujiletea maendeleo yake na taifa kwa ujumla.

MGOMO WA MADAKTARI

Kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na migomo ya mara kwa mara kuanzia kwa wanafunzi wa vyuo vikuu mpaka kwa wafanyankazi wa serikali. Mwaka 2001, tulishuhudia mgomo mkubwa wa wanafunzi wa chuo cha Sayansi za tiba Muhimbili wakishinikiza uboreshwaji wa mazingira ya kusomea hasa masomo kwa vitendo. Mwaka 2005, tukashuhudia mgomo mkubwa wa madaktari wa hospitali ya Muhimbili na sehemu nyinginezo waliokuwa wakidai uboreshwaji wa maslahi yao, mgomo ambao uliathiri utoaji huduma katika hospitali nyingi hasa za rufaa. Kuelekea Mwaka jana, vuguvugu la mgomo wa madaktari lilipelekea kuwepo kwa mgomo mwanzoni wa mwaka huu ambao umekuwa ukiendelea kwa vipindi tofauti hadi sasa.

Japo serikali imekuwa ikitafuta njia za mkato kuendeleza huduma katika hospitali ya Muhimbili kama vile kuleta madaktari waliostaafu ama madaktari kutoka jeshini ambao hawakidhi mahitaji ya huduma katika hospitali hiyo ya Taifa, huduma katika hospitali nyingine zisizonufaika na njia hizi za mkato hudorora siku hadi siku kwa kipindi chote cha migomo huku wananchi wakiendelea kupata taabu.

Vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kama vile kutekwa na kupigwa kwa Mwenyekiti wa kamati maalumu ya Jumuiya ya madaktari iyosimamia madai yao, Dr. Stephen Ulimboka, ubabe, vitisho na matumizi ya nguvu dhidi ya madaktari wanaodai haki zao badala ya kutatua matatizo hayo kwa njia ya amani, siyo tu vinakiuka Katiba ya nchi inayojichanganua kimataifa kama nchi ya amani bali pia vimepunguza morali ya watumishi hawa kutoa huduma kwa wananchi ambao kama tulivyosema awali hawana mchango wa moja kwa moja katika kusababisha mgogoro huu.

M a d a i y a M a d a k t a r i .

Katika mgomo huu unaoendelea, madai ya madaktari, mbali na dai la awali la kusisitiza kuondolewa kwa viongozi wakuu katika wizara ya afya wanaokwamisha maendeleo ya sekta hii, madai yao yamejikita katika sehemu kuu mbili ambazo ni uboreshwaji wa mazingira ya kazi na vifaa vya tiba na Uboreshwaji wa kipato, kinga na afya za madaktari (Mishahara, posho na Bima ya afya).

U b o r e s h w a j i w a m a z i n g i r a y a k u f a n y i a k a z i n a v i f a a v y a t i b a

Kulingana na maelezo ya madaktari, hii ndiyo hoja kubwa katika madai yao ambayo inalenga kuhimiza serikali kukarabati miundombinu ya afya, kuongeza vitanda na kuongeza upatikanaji wa vifaa vya kutendea kazi. Katika tamko la jumuiya ya madaktari Tanzania lililotolewa kwa waandishi wa habari tarehe 28 Juni 2012, sehemu ya tamko hilo inasema:

“…Madaktari wamechoka kuona huduma za afya nchini zikizidi kudorora mwaka hadi mwaka…

… Tumechoka kuona wagonjwa wakilala chini na watoto wakilala wanne katika kitanda kimoja…

…Tumechoka kuona msongamano mkubwa wa wagonjwa katika hospitali zetu huku kukiwa hakuna mpango wowote wa uboreshaji…

…Tumechoka kuona wagonjwa wakikosa dawa, vipimo sahihi na watumishi wa afya wakifanya kazi katika mazingira magumu yanayoviza ubora wa huduma na misingi ya taaluma…

… Kwahiyo, kwa moyo wetu leo, tumejitolea kutetea uboreshaji wa sekta ya afya ….’’

Sera ya Taifa ya afya ya mwaka 2007 katika kipengele kinachohusu rasilimali watu inasema;

‘… Uboreshaji wa mazingira ya kazi ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa vitendea kazi vya kutosha kwa watumishi wa afya…

… Kuweka vivutio katika sehemu zenye mazingira magumu na hatarishi ili kuwavutia wataalamu kwenda kufanya kazi katika sehemu hizo…’

Katika madai ya awali ya madaktari, walisikitishwa na wimbi kubwa la viongozi wa kisiasa na serikali wanaotibiwa nje ya nchi. Zaidi ya hayo, madaktari walibaki kuwa waidhinishaji wa rufaa za kwenda kutibiwa nje ya nchi. Hali hii, siyo tu inaweza kuongeza mwingilio wa maamuzi ya kitaalamu kwa shinikizo za watawala wa kisiasa kwa kuwashinikiza madaktari kutoa rufaa kinyume na maadili yao, bali pia inapunguza nia ya kisiasa ama ‘political will’ ya viongozi wa kisiasa na serikali katika kushughulikia kero za afya za wananchi kwa kuwa ‘wao’ wana uhakika wa matibabu nje ya nchi. Hali hii siyo tu inaondoa usawa wa kimatibabu kati ya viongozi na wananchi, na serikali kutumia fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kuboresha sekta ya afya hapa nchini bali pia nchi hushindwa kuwa na miundo mbinu ya uhakika ya kushughulikia magonjwa ya dharura ambayo muda hautaruhusu kutibiwa nje ya nchi. Nchini Malawi kwa mfano, kifo cha Rais Bingu wa Mutharika, kutokana na shinikizo la damu tarehe 5 Aprili mwaka huu kilihusishwa na serikali yake kushindwa kuboresha miundombinu na huduma za afya nchini mwake.

Katika utafiti wa Sikika kuhusu upatikanaji wa madawa na vifaa tiba uliofanyika katika wilaya 71 mwaka 2011, waganga wakuu wa wilaya waliohojiwa, walithibitisha kutokuwepo kwa gozi (gauze) katika asilimia 48 ya wilaya zote huku asilimia 44% ya wilaya zikiwa na gozi zisizotosheleza mahitaji. Katika ngazi ya vituo vya afya na zahanati, asilimia 63% hazikuwa na gozi huku asilimia 27% ikiwa haina gozi za kutosha. Kukosekana au kuwa na idadi pungufu ikilinganishwa na mahitaji uliendelea kuwepo kwa kati ya miezi mitatu hadi sita. Vivyo hivyo, katika ngazi za wilaya, glovu (surgical gloves) hazikuwepo katika asilimia 28% ya wilaya, dawa za kutibu malaria aina ya ALU asilimia 32% ya wilaya na sindano za Quinine asilimia 13% ya wilaya zote zilizoshiriki katika utafiti. Katika ngazi ya vituo vya afya na zahanati, asilimia 17% hazikuwa na glovu, asilimia 30% hazikuwa na ALU, asilimia 23% hazikuwa na sindano za Quinine na asilimia 17% haikuwa na vidonge vya Amoxcycillin. Katika utafiti huo pia, Sikika iligundua kuwa katika ngazi ya wilaya asilimia 93% ya wilaya hupata dawa na vifaa tiba chini ya maombi na mahitaji halisi na katika ngazi ya vituo vya afya na zahanati asilimia 90% hupata dawa na vifaa vya tiba chini ya maombi na mahitaji halisi.

Yapo madhara makubwa yatokanayo na upungufu wa dawa na vifaa vya tiba. Madhara hayo yaweza kupelekea kuona wagonjwa waliozidiwa au walio na dharura pekee (critical patients & emergencies) hali ambayo inajitokeza katika zahanati na vituo vya afya vingi. Madhara mengine ni kuongezeka kwa usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa kutokana na kupata kiasi kidogo, kuongezeka kwa madhara ya magonjwa yatokanayo na kutopata tiba sahihi (complications) kama ulemavu kwa watoto ambao wamekosa tiba sahihi ya malaria, kuongezeka kwa malalamiko toka kwa wananchi dhidi ya watumishi wa afya na mbaya zaidi kupungua kwa morali ya kazi kwa watumishi wa afya na kufanya kazi kinyume na misingi au maadili ya kitaalamu kama walivyosema madaktari hapo juu, ‘mazingira magumu yanayoviza ubora wa huduma na misingi ya taaluma’.

Wengi wetu ni mashahidi wa huduma zisizoridhisha katika hospitali za serikali, msongamano wa wagonjwa wodini hasa akinamama na watoto, ukosefu wa mara kwa mara wa vifaa vya tiba na matatizo mengine.

Tanzania hupoteza takribani asilimia 6% ya wagonjwa wanaohitaji huduma za CT Scan kwa mwaka. Hata hivyo, kifaa cha CT Scan katika hospitali ya Muhimbili kimeharibika kwa zaidi ya miezi saba sasa bila matengenezo ikiwalazimu wagonjwa wanaohitaji majibu ya kipimo hicho ili wapate tiba stahili, kwenda katika hospitali binafsi. Gharama za kipimo hicho katika hospitali ya Muhimbili ni takribani shilingi 170,000/= lakini katika hospitali binafsi ni kati ya shilingi 200,000/= hadi 500,000/=. Mbali ya hayo, katika ufuatiliaji wa Sikika wa mwaka 2011 kwenye wilaya 6 za mkoa wa Dar Es salaam, Pwani na

Dodoma, kati ya vituo 38 vinavyotoa huduma kwa watu waishio na VVU (Care and treatment Centers) ni vituo 13 tu vilivyokuwa na mashine za CD4+ zinazotumika kuangalia maendeleo ya tiba kwa watu waishio na VVU na kati ya hizo ni mashine tano (5) ndizo zilikuwa zikifanya kazi. Ni wajibu wa serikali kuboresha mazingira ya kazi ya watumishi wa afya na kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba kwa muda wote, kwa sababu hii Sikika tunaungana na madaktari katika kudai uboreshaji wa mazingira ya kazi kwa watumishi wa afya, kuhakikisha dawa na vifaa tiba vinapatika hasa maeneo ya vijijini ili kuboresha afya za wananchi kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

U b o r e s h a j i w a k i p a t o , k i n g a n a a f y a z a m a d a k t a r i ( M s h a h a r a , p o s h o , B i m a y a a f y a ) .


Madai mengine ya madaktari ni uboreshwaji wa mapato yao ikiwa ni pamoja na mishahara, posho ya kuitwa kazini baada ya saa za kazi (on call allowance), posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu (hardship allowance) na posho ya makazi. Vile vile madaktari wanadai posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi (risk allowance) na chanjo ambayo ni muhimu ili kuzuia uwezekano wa madaktari kupata magonjwa ambayo wanaweza kuyasambaza kwa wagonjwa wengine ambao tayari wana matatizo yao ya kiafya.

Madai ya nyongeza ya mishahara

Katika madai yao ya mishahara, madaktari walipendekeza kiwango cha shilingi milioni 3.5 kwa mwezi. Hata hivyo, wakati akiongea na madaktari Tarehe 9/2/2012, waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda alitoa ufafanuzi wa madai yanayohusu maslahi ya watumishi wa afya bila kutoa majibu ya moja kwa moja ya kiwango gani kitalipwa na serikali kama mishahara na posho kwa sababu ‘wataalamu’ walikuwa wanafanyia kazi suala hilo ili waweze kumshauri, na hadi sasa serikali haijatamka kiwango halisi itakachoweza kulipa. Pia waziri mkuu hakuweza kueleza moja kwa moja kuhusu madai ya uboreshaji wa mazingira ya kazi na upatikanaji wa vifaa tiba. Kwa sasa, mshahara wa daktari ni Tshs 957,700/= na baada ya makato ya kodi hubaki na Tshs 680,000/= kwa mwezi. Katika ufuatiliaji wa Sikika wa Disemba 2011 hadi January 2012, katika hospitali ya Regency, ilibainika kuwa hakuna daktari anayepata mshahara chini ya shilingi milioni mbili (gross pay) na Agha Khan hospitali, daktari mwenye uzoefu wa chini ya miaka minne alikuwa akilipwa shilingi milioni 1.8 kuachilia mbali mafao mengine kama vile bima ya afya, posho za nyumba n.k. Sikika inatarajia kuwa serikali pia itaboresha mishahara ya madaktari na mafao mengine ili kuongeza tija katika hospitali za umma.
Madai ya Posho

Katika madai yao, madaktari wamependekeza viwango vifuatavyo kwa posho mbali mbali: posho ya muda wa ziada wa kazi (call allowance) asilimia 5% ya mshahara kama ilivyo kisheria kwa kada yoyote; posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu asilimia 40% ya mshahara; posho ya makazi asilimia 40% au nyumba kama ilivyo kisheria na posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi asilimia 30% au chanjo (Homa ya ini-hepatitis, HIV/AIDS, TB)

Hoja za Serikali

Serikali imeendelea kusisitiza ufinyu wa bajeti na kwamba, kuwaongezea mishahara madaktari peke yao kutaondoa ulinganifu na kuongeza migogoro katika sekta nyingine. Hata hivyo, sehemu ya sheria ya kazi ya mwaka 2004 (Employment and Labour Relations Act, Kifungu cha 6: (20) (4)), inasomeka hivi “Mwajiri atamlipa mwajiriwa walau 5% ya mshahara wa msingi wa mwajiriwa kwa kila saa aliyofanya kazi usiku’’.

Kwa mahesabu rahisi, daktari alipaswa kupata angalau Tshs 47,000/= kwa saa anapofanya kazi usiku. Hata hivyo waraka wa serikali wenye Kumb. No. C/AC.17/45/01/F/73 wa tarehe 21 February 2012 kutoka kwa George D. Yambesi (Katibu Mkuu Utumishi) kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wenye kichwa, ‘Malipo ya kuitwa kufanya kazi baada ya saa za kazi (On call allowance)’ unaelekeza kulipa viwango vifuatavyo kwa siku kwa watumishi wa afya kuanzia tarehe 9 February 2012 (Siku 12 Nyuma); Wataalamu bingwa Tshs 25,000/= na madaktari wa kati Tshs 20,000/=. Katika nchi ya jirani ya Kenya kwa barua yenye Kumb No. MSPS/2/1/3A Vol.III/(77), ya tarehe 12 January 2012 toka ofisi ya Waziri Mkuu kwenda kwa Katibu Mkuu wa wizara husika, madaktari, wataalamu wa kinywa na wafamasia wanalipwa takribani Tshs 38,000/= kama posho ya ‘call allowance’ hali ambayo inaweza kusababisha kupungua kwa rasilimali watu katika sekta ya afya nchini Tanzania (Brain Drain) kwa kukimbilia nchi jirani kufuata kipato kizuri hasa wakati huu wa soko huria la ajira katika shirikisho la Afrika Mashariki.

Sikika imekuwa mstari wa mbele kupinga pesa zinazotumika kama posho za vikao kwa watumishi ambao tayari wanalipwa mishahara kwa kazi husika. Hata hivyo, katika waraka wenye Kumb. No. C/AC.17/45/01/125 wa tarehe 11 Februari 2010 wenye kichwa ‘Waraka wa Utumishi wa Serikali Na.2 wa mwaka 2010: Posho ya vikao (Sitting Allowance) Serikalini,’ viwango ‘vipya’ vya posho ya vikao vilivyotajwa ni Mwenyekiti/Katibu 200,000/=, Wajumbe 150,000/= na sekretarieti 100,000/=. Posho hizi kubwa si tu kwamba zinadhihirisha matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi bali pia zinapunguza
nguvu kazi katika sekta ya afya kwani watumishi wengi wanahangaika kutafuta nafasi ya kushiriki katika vikao badala ya kufanya kazi zao.

Hoja ya ‘ulinganifu’ au ‘lawama’ kwa sekta nyingine haina nguvu kwani nchini Marekani kwa mfano, pato la daktari ni zaidi ya mara 100 ya kima cha chini cha mshahara kwa saa katika nchi hiyo, na nchini Botswana, ambako Madaktari wengi Watanzania hukimbilia kwa sababu za kimaslahi, mshahara wa daktari ni sawa na Tshs kati ya milioni 3.2 hadi 5.8 kwa mwezi. Hoja hii pia, kwamba madaktari wakipewa mshahara mkubwa italeta malalamiko katika kada nyingine inadhihirisha jinsi ambavyo serikali inawakandamiza kimaslahi watumishi wake. Hili lilidhihirika wakati wa mgomo wa walimu mwaka 2010, Kaimu Katibu Mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA) bwana Nicholas Mgaya, alisema … ‘Tumedai kwamba Kima cha chini cha mishahara kiwe ni Tshs 315,000/=. …………lakini
serikali ikang’ang’ania Tshs 135,000/= kiasi ambacho bado ni kidogo’’ (Daily News, August, 2010). Vivyo hivyo, utafiti wa “Motivation of Health Care Workers in Tanzania: A Case Study of Muhimbili National Hospital” uliotolewa katika Jarida la East African Journal of Public Health Volume 5 Number 1, April 2008 ulionesha kuwa Asilimia 88 ya watumishi waliamini kuwa mwajiri wao hawajali (madaktari asilimia 82.4, wauguzi asilimia 90.7 na watumishi wengine asilimia 87.9). Hata hivyo sababu tatu kubwa zilizoonekana kuwafanya watumishi hao kutokuwa na motisha mzuri wa kazi ni mishahara, mazingira ya kazi, na vifaa duni vya kazi na asilimia 30 ya wauguzi walikuwa hawajaridhika na kazi zao kiasi cha kutaka kuacha kazi hizo. Hali ya kuwa serikali imekuwa haikubali mapendekezo ya watumishi wake au hata mapendekezo ya tume zinazoundwa na serikali yenyewe hasa katika uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi wa sekta ya afya kwa ujumla, inatufanya Sikika tuungane na madaktari katika madai yao.

Katika bajeti ya sasa 2012/213, kipengele cha uendelezaji wa rasilimali watu katika sekta ya afya kimetengewa bilioni 23.4 na matumizi ya kawaida (recurrent expenditure) yametengewa Tshs bilioni 24.5). Hata hivyo kati ya fedha iliyotengwa kuendeleza rasilimali watu, bilioni 21.6 sawa na asilimia 92.3% inategemea msaada wa wafadhili. Hali hii ya utegemeji inapingana na sera ya afya ya Taifa inayotamka kuwa serikali iwe mfadhili mkuu wa sekta ya afya.

Wakati huo huo, mpango mkakati wa sekta ya afya (Health Sector Strategic Plan III) umeweka malengo ya bajeti ya sekta ya afya kufikia asilimia 10% ya bajeti yote ya serikali mwaka 2015. Hii inapingana na azimio la Abuja (asilimia 15) ambalo Rais wetu alitia saini na inapingana pia na sera ya afya ya mwaka 2007 inaposema, ‘Serikali itaendelea kuongeza bajeti ya sekta ya afya …hadi kufikia azimio la Abuja….ilikukidhi mahitaji muhimu ya kisekta’ . Kwa ukiukwaji wa makubaliano ya azimio la Abuja na kutoitekeleza sera ya afya ya Taifa kama inavyotakiwa, yote haya yanadhihirisha kuwa serikali haina nia ya dhati ya kusimamia maamuzi yake katika ngazi za kimataifa na kitaifa.

Tukirejea tena katika sera ya afya ya mwaka 2007 inasema, ‘kuwepo kwa watumishi wa kutosha wenye ujuzi katika ngazi zote za kutolea huduma kulingana na vigezo vilivyokubalika’. Udaktari ni mojawapo ya fani ambazo katika nchi nyingi zimepewa jina la ‘scarce skills’ yaani ujuzi adimu. Kwa miaka kadhaa sasa, idadi kubwa ya wanafunzi wa shule katika ngazi za chini wameendelea kuyakimbia masomo ya sayansi na wanafunzi wanaodahiliwa kusomea masomo ya udaktari ni wale ambao kiwango chao cha ufaulu katika masomo ya fizikia, kemia na biologia kiko juu sana, hivyo madaktari kulipwa mishahara mikubwa ili waweze kuokoa maisha ya watanzania si tatizo, kwa maoni ya Sikika.

Tena, hoja ya ufinyu wa bajeti inakosa nguvu katika madai haya kwani, katika tafiti za Sikika tumeonyesha jinsi ambayo serikali imeendelea kuwa na matumizi mabovu ya fedha za walipa kodi na ukosefu wa vipaumbele katika matumizi yake.

Katika chapisho la Sikika lenye kichwa, ‘Matumizi yasiyo ya lazima, Taarifa fupi kuhusu mpango wa serikali katika kuangalia Upya matumizi’ toleo no. 2 la July 2010 lililotolewa kwa ushirikiano wa Policy forum linaonyesha kuwa matumizi yasiyo ya lazima serikalini yalikuwa bilioni 684 mwaka 2008/09, billioni 530 mwaka 2009/10 na bilioni 537 mwaka 2010/11. Zaidi ya hayo,, matumizi katika posho mbali mbali yaliongezeka toka bilioni 171 mwaka 2008/09 hadi bilioni 269 mwaka 2010/11. Gharama za kusafiri nje na ndani ya nchi zilikuwa bilioni 155 mwaka 2008/09 na bilioni 124 mwaka 2010/11. Gharama za mafuta ya kuendeshea na kulainisha magari ya kifahari ya serikali (Mbali na ununuzi) zilikuwa zaidi ya bilioni 52 mwaka 2010/11 na manunuzi ya magari ya serikali yaligharimu Bilioni 15.3 mwaka 2010/11 pekee. Mbali ya hayo, serikali imekosa vipaumbele katika matumizi yake mfano ni matumizi ya zaidi ya bilioni moja kwenye wizara ya afya wakati wa sherehe za Nane Nane..

Katika sekta ya afya pekee, matumizi yasiyo ya lazima (unnecessary expenditure) yaliongezeka toka bilioni 16.1 mwaka 2010/11 hadi bilioni 22 mwaka 2011/12, na inakadiriwa kufikia bilioni 25 katika bajeti ya 2012/13, posho mbalimbali zikiongoza katika matumizi. Posho hizo zinalenga watu wachache sana hasa watawala na hazina tija katika utoaji wa huduma za afya. Posho zimefanya utendaji kazi uwe hafifu na kupunguza uwajibikaji ilhali watumishi wasio katika nafasi za kitawala wakiendelea kuambulia maslahi madogo

Taarifa za CAG pia zinadhihirisha matumizi mabovu na usimizi mbovu wa rasilimali za taifa kwa mfano msamaha wa kodi uliongezeka toka bilioni 680 mwaka 2009/2010 hadi Trilioni 1.016 kwa mwaka wa 2010/11. Hii inawakilisha asilimia 18% makusanyo yote ya pato la Taifa na ni kiwango kikubwa sana kuliko nchi nyingi za Afrika. Matumizi yasiyokusudiwa bilioni 8, bilioni 31 zimelipia vifaa ambavyo havikufika na Malipo yanayotia shaka bilioni 1.4.

R a s i m a l i w a t u k a t i k a S e k t a y a A f y a

Tumeshuhudia matamko ya hospitali kadhaa hospitali za mikoa ya Mbeya, Dodoma, Morogoro, Kilimanjaro na Mwanza zikiwafukuza madaktari waliogoma badala ya kushiriki katika kutatua mgogoro huu ili warejee kazini na kuepuka kupoteza nguvu kazi yenye upungufu mkubwa katika sekta ya afya. Shirika la afya duniani (World Health Organization), linapendekeza kwamba kila daktari anatakiwa ahudumie watu wasiozidi 5,000. Kwa mujibu mkutano mkuu wa chama cha madaktari Tanzania (MAT) tarehe 10 hadi 11 August, 2010 pale Mlimani city, uwiano wa daktari mmoja kwa idadi ya watu ulikuwa 1:300 wakati wa uhuru na hali ikawa mbaya kwa kasi hadi uwiano wa 1: 30,000 mwaka 2010. Kwa upande wa wafamasia kwa mfano, wakati kukiwa na vituo vya kutolea dawa 4,185 vya serikali na 1,056 vya binafsi nchini mwaka 2009, kulikuwa na wataalamu 1,506 pekee waliopata mafunzo ya ufamasia na wafamasia 703 wenye shahada ya ufamasia. Katika utafiti wa Sikika wa HRH Tracking Study 2010, ulionyesha kuwa asilimia 54% ya wilaya zote zilizoshiriki katika utafiti zilikuwa na upungufu mkubwa wa watumishi wa afya. Hata hivyo, idadi ya watumishi wanaopangiwa vituo vya kazi na kuripoti ni asilimia 70% kwa wilaya za vijijini na asilimia 93% kwa wilaya za mijini. Zaidi ya hayo, wilaya nyingi hazipati wafanyakazi kulingana na maombi yao, kwa mfano katika utafiti huu, wilaya nyingi zilipata ni asilimia 35% ya wafanyakazi katika maombi yao, huku hali ikiwa mbaya maeneo ya vijijini.

Katika mpango wa kukuza rasilimali watu unaoisha mwaka 2013, bajeti ya jumla ya mpango huo ilikiwa bilioni 470, wastani wa bilioni 91 kwa mwaka. Mwaka 2011/12, wizara ya afya na ustawi wa jamii iliomba bilioni 66.3 ili kutekeleza mkakati wa rasilimali watu kisekta, hata hivyo serikali ilitenga bilioni 13.2 pekee na hadi kufikia January 2012, asilimia 20% (bilioni 2.7) pekee ndiyo iliyokuwa imetolewa kwa wizara.

Wakati mkakati wa kuboresha sekta ya afya (HSSP III) ukionyesha upungufu wa rasilimali watu kufikia 92,000, mpango wa ukuzaji wa afya ya msingi (Primary Health Service Development Program 2007-2017) unahitaji watumishi wa afya 137,813 kuutekeleza. Hata hivyo, udahili katika vyuo vya afya kwa mwaka 2010 ulikuwa wanafunzi 6,949 pekee, na iwapo udahili hautaongezeka, tutahitaji miaka 21 ili kuziba pengo la watumishi katika mpango wa kukuza afya ya msingi (PHSDP) iwapo mambo yatabaki kama yaliyo. Hii inaonyesha kuwa tutaendelea kuwa na upungufu wa watumishi wa afya kwa miaka mingi ijayo. Hata hivyo, katika mwendelezo wa hotuba zake za kila mwisho wa mwezi, Tarehe 01/07/2012, mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, siyo tu amedhihirisha kutokutilia maanani upungufu mkubwa wa wataalamu wa afya unaoisumbua nchi yetu, bali pia kama kiongozi wa nchi, ameonyesha jinsi ambavyo serikali ilivyo tayari kupoteza rasilimali hii adimu kwa kushindwa kutatua mgogoro kati yake na madaktari, ambao iwapo wataamua kuacha kazi wote, itatuchukua miaka mingi kuziba pengo hilo.

H i t i m i s h o

Kwanza, kutokana na mapungufu mengi tuliyoeleza hapo juu, Sikika inaona kuwa madai ya madaktari ni ya msingi na tunaamini kuwa serikali inaweza kuboresha huduma za afya na maslahi ya wafanyakazi hasa ikidhibiti matumizi yasiyo ya lazima, ikidhibiti ufujaji wa kodi za wananchi kwa baadhi ya watendaji wake, ikipunguza misamaha ya kodi na ikitekeleza mikakati iliyopo katika sera zake kikamilifu.

Pili, Sikika inaungana na madaktari, wanaharakati na wananchi kulaani vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu aliofanyiwa mwenyekiti wa kamati maalumu ya jumuiya ya madaktari Dr. Stephen Ulimboka na kupendekeza uundwaji wa tume huru yenye mchanganyiko wa wananchi katika kuchunguza tukio hilo.

Tatu, Sikika inaihimiza serikali kuacha kutumia vitisho na ubabe katika kutatua mgogoro wake na madaktari. Vitendo hivi vinaweza kupunguza morali na ufanisi wa madaktari kiutendaji na pengine kupelekea wengine kuhama sekta ya afya au kukimbilia nje ya nchi. Badala yake serikali ifanye mapatano na wataalamu hawa muhimu, ili waweze kurejea kazini haraka kutoa huduma kwa wananchi wanaoendelea kuumia kwa kukosa huduma


P.o.Box 12183 Dar Es Salaam, Phone: +255222666355/57 Fax: +255222668015 E-Mail: info@sikika.or.tz web: www.sikika.or.tz

Tuesday, July 3, 2012

Madaktari warejea kazini

Tathimini iliyofanyika kuanzia asubuhi saa mbili hadi saa 11 jioni
inaonyesha kuwa katika Idara ya Tiba, Madaktari Bingwa 19 kati ya 21
wamefika kazini ambapo watatu wako likizo. Aidha Registrars wote 12
walikuja kazini. Kliniki zote za tiba zimefanyika kama kawaida.

Katika Idara ya watoto, yenye Madakatari Bingwa 16, kati yao 14 walikuja
kazini wengine wawili wako likizo na Registrar watatu kati ya sita walikuja
kazini ambapo watatu wako likizo.

Upande wa OPD yenye Registrars saba, sita kati yao walikuja kazini na mmoja
yuko likizo. Aidha Madaktari Bingwa wote walikuja kazini.

Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili yenye Madakatri Bingwa 10, tisa
walikuja kazini na mmoja wao yuko masomoni.

Upande wa Emergency Medicine, Registrars wote 10 walikuja kazini.

Kuhusu huduma za upasuaji, wagonjwa wote waliolazwa wodini wameonwa, na
baadhi ya kliniki za huduma ya upasuaji zilifanyika. Hata hivyo, upasuaji
haukufanyika kwani hakukuwa na orodha ya wagonjwa waliopangwa kufanyiwa
upasuaji..

KWA UJUMLA, MADAKTARI WAMEREJEA KAZINI.

Imetolewa na;

Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
Julai 2, 2012

Sunday, July 1, 2012

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MUHIMBILI



Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ilikutana tarehe 28 Juni 2012 kujadili na kutathmini hali ya utendaji na utoaji wa huduma hivi sasa katika Hospitali. Imebainika kwamba utoaji huduma umeathirika kutokana na mgomo wa baadhi ya madaktari unaondelea kwa takriban wiki moja sasa tangu ulipoanza Jumamosi ya tarehe 23 Juni 2012.

Baada ya tathmini hiyo, Bodi ya Wadhamini imeagiza yafuatayo

i) Madaktari waliopo kazini waendelee na kazi kama kawaida;
(ii) Madaktari waliogoma warejee kazini kutii amri ya Mahakama Kuu Kitengo cha kazi, kwa mujibu wa Kifungu Na. 76 (1) na (2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004.
(iii) Madaktari waliopo likizo warejee kazini mara moja. Utaratibu wa kufidia likizo na nauli zao umeandaliwa.
(iv) Uongozi wa Hospitali uwachukulie hatua za kinidhamu wafanyakazi wote watakaoendelea kutokuhudhuria kazini na kufanya kazi bila sababu za msingi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu za kazi;
(v) Uongozi wa Hospitali ufute mara moja ‘rotations’ za Madaktari waliopo kwenye mafunzo kwa vitendo (interns); na(vi) Uongozi wa Hospitali uwapange (re-deploy) Madaktari na Madaktari Bingwa waliopo kwenye maeneo yaliyoathirika wakati huu wa mgomo


Aidha, Bodi ya Wadhamini inawashukuru sana madaktari na wafanyakazi wote ambao wameendelea kuwahudumia wagonjwa wetu na wananchi kwa ujumla. Vilevile, Bodi ya Wadhamini inawasihi madaktari na wafanyakazi wote wawe na subira na waheshimu sheria, kanuni na taratibu zilizopo pamoja na maadili ya taaluma zao.

Dkt. Gabriel Upunda

KAIMU MWENYEKITI
BODI YA WADHAMINI

Saturday, June 30, 2012

Kugombana na Madaktari ni Uchuro

Mgomo wa madaktari umeanza tena, siku chache zilizopita. Inasikitisha kuona kuwa tumefikia hali hiyo. Ukiniuliza nani namhesabu kama mwajibikaji mkuu aliyesababisha tatio hili, nitakuambia kuwa ni serikali ya CCM. Huo umekuwa msimamo wangu tangu pale ulipotokea mgomo wa mwanzo wa madaktari wiki kadha zilizopita. Nilieleza msimamo huo hapa.

Siku chache zilizopita, nilimsikiliza mwenyekiti wa madaktari wanaogoma, Dr.Stephen Ulimboka, akiongelea jinsi uhaba wa vitendea kazi ulivyo. Alitaja mfano wa kifaa cha "CT-scan" ambacho kimeharibika Muhimbili yapata miezi mingi iliyopita.

Kama nilivyosema katika makala yangu ya mwanzo, sera za serikali ya CCM zinasabisha upotevu mkubwa wa mali ya Tanzania, kama vile madini. Serikali yenyewe imekiri kuwa mikataba ya madini ya siku zilizopita ilikuwa ni ya hasara kwa Taifa. Lakini je, serikali imeshamwajibisha yeyote aliyehusika katika kusaini mikataba hiyo?

Je, ni kweli kuwa nchi hii haiwezi kununua hicho kifaa cha "CT-scan"? Kutokana na sera mbovu za CCM, makampuni kama Barrick yanafaidika sana na dhahabu yetu wakati sisi, ukifananisha na mapato wanayopata wao, sana sana tunaambulia mapato duni sawa na njugu kiganjani, na tunaambulia uharibifu wa mazingira na afya za watu wanaoishi maeneo ya migodini,

Kitu kimoja kinachokera katika mgogoro huu baina ya serikali na madaktari ni jinsi madai ya madaktari yanavyopotoshwa. Wako ambao wanaongea kama vile wanachodai madaktari ni posho na maslahi yao tu. Ukweli ni kuwa madaktari wana madai ya msingi ya kuwatetea wananchi. Kuna uchakachuaji wa makusudi unaofanywa kuhusu jambo hilo, ili ionekane kuwa madaktari hawajali maishai ya wananchi.

Ni kweli kuwa mgomo huu unaathiri maisha ya wa-Tanzania. Hili si jambo jema. Lakini serikali haina haki ya kuwashutumu madaktari kwa hoja hii ya kutojali maisha ya wa-Tanzania, wakati serikali hiii hiii inawakumbatia hao wanaoitwa wawekezaji ambao wengi wao wanahujumu maisha na afya za wa-Tanzania, achilia mbali kuharibu mazingira maeneo ya migodini. Serikali ingekuwa haifanyi hayo, ingekuwa na haki ya kuwaandama madaktari kwa hoja hii ya kuathiri maisha ya wa-Tanzania.

Katika mgogoro baina ya serikali na madaktari, kuna pia suala la serikali kutumia mwanya wa sheria na uamuzi wa mahakama. Serikali haifanyi haki inapokwepa kuwajibika kwa yale yanayodaiwa na madaktari, madai ambayo ni ya kweli, na yako katika uwezo wa serikali na nchi yetu hii ambayo ina utajiri mkubwa. Kama suala ni sheria na maamuzi ya mahakama, sote tunakubali kuwa sheria ichukue mkondo wake.

Lakini kinachokera ni kuwa serikali inatumia mwanya huu kufunika kile ambacho sisi wengine tunakiona ni uzembe na kutowajibika kwa serikali yenyewe. Madai ya madaktari ni ya msingi, na yako katika uwezo wa serikali hii. Kwa serikali kutowajibika hapo na kukimbilia mahakamani kuwabana madaktari kwa kipengele cha sheria tu, sio jambo la haki na haliiweki serikali katika sura nzuri, kwa mtazamo wangu.

Kama nilivyosema katika makala yangu ya mwanzo, kugombana na madaktari si jambo jema. Nilikumbushia usemi wa wahenga kuwa tusidharau wakunga na uzazi ungalipo. Napenda kuongezea kwa dhati kabisa kuwa kugombana na madaktari si dalili njema bali ni uchuro.

http://hapakwetu.blogspot.com/

Friday, June 29, 2012

HALI YA DR STEVEN ULIMBOKA INAVYOZIDI KUIMARIKA

Hali ya afya ya Dkt. Steven Ulimboka inaendelea vyema baada ya kushambuliwa na watu wasiofahamika usiku wa kuamkia juzi jijini Dar es Salaam.Ulimboka anaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhumbili (MNH), Kitengo cha mMifupa (MOI) aliko lazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) huku jopo la madaktari Bingwa wakiendelea kumnusuru Kama aonekanavyo pichani juu.Picha na Mdau Dande Francis

Wednesday, June 27, 2012

Picha za Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dkt. Steven Ulimboka Steven Baada ya Kuokotwa Maeneo ya Mabwepande

Juu ni taswira mbalimbali za Dr. Steven Ulimboka baada ya kuokotwa
Mkurugenzi wa Kituo cha haki za binadamu Dk Hellen Kejo(kushot)akiwa na Dr. Steven Ulimboka muda mfupi baada ya kuokotwa akiwa amejeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwakaribisha ikulu jijini Dar es salaam viongozi wa Chama cha madaktari nchini. Wa pili kushoto ni Mratibu wa mgomo wa madaktari, Stephen Ulimboka na Kulia ni Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi
Dr. Steven Ulimboka alipokua akieleza jambo kwenye mkutano wao(madaktari na Waziri Mkuu Mizengo Pinda Hivi Karibuni
....
UPDATE ya maelezo ya mkasa uliomkuta Dkt. Ulimboka:Dkt. Helen Kijo-Bisimba wa LHRC akinukuliwa katika EA Redio amekariri maelezo ya Dkt. Ulimboka ambayo pia yamesikika yakitamkwa na mwenyewe (Dkt. Ulimboka Steven), kupitia kituo cha redio cha CloudsFM, kwamba walikuja watu watatu waliovalia kiraia na kujitambulisha kuwa wao ni askari. Watu hao walimchukua na kumuingiza katika gari lisilokuwa na namba na kuanza kuelekea barabara ya Bagamoyo. Huko walimfunga kitambaa usoni, kamba mikononi na miguuni kisha wakampiga huku wakimwambia amekuwa akiwasumbua kwa muda mrefu na kama wangekuwa na sindano ya sumu wangemmaliza kabisa.
---
UPDATE:

Dkt. Ulimboka amefikishwa katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa huduma. Hali yake ni mbaya ila "stable".
------

Baadhi ya watu wa shirika la Tanzania Legal Human Rights Center (LHRC) walifanya juhudi za kumtafuta kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dkt. Ulimboka Steven aliyekamatawa (? tekwa) jana usiku.

Taarifa iliyotoka kwa mmoja wa wanaharakati hao inasema, walifanikiwa kumpata Dkt. Ulimboka kaitka eneo la Mwabepande, Dar es Salaam ) akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi, hajitambui (unconscious) na asiyeweza kuzungumza.

Taarifa hiyo inaongez akuwa, Dkt. Ulimboka alikuwa amepigwa vibaya sana katika sehemu mbalimbali za mwili wake na anahitaji matibabu ya haraka.

Juhudi zinafanywa kumpatia msaada unaohitajika Dkt. Ulimboka Steven.

Monday, June 25, 2012

TAARIFA KUHUSU CHANJO YA HOMA YA MANJANO KWA WASAFIRI KUTOKA TANZANIA KWENDA JAMHURI YA KISOSHALISTI YA SRI LANKA

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imepokea taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu chanjo ya homa ya manjano kwa wasafiri kutoka Tanzania kwenda Jamhuri ya Kisoshalisti ya Sri Lanka. Taarifa hii imetolewa naUbalozi wa Jamhuri ya Sri Lanka uliopo Afrika ya Kusini ambayo inaeleza utaratibu mpya wa ukaguzi na ufuatiliaji wa wasafiri katika Viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Bandaranayake, Katunakaye na Colombo nchini Sri Lanka. Kila msafiri anayeingia Sri Lanka atatakiwa kuwa na kadi ya chanjo ya homa ya manjano kama sharti la kiafya la kuingia nchini humo. Madhumuni ya utaratibu huu ni kudhibiti kuingia kwa ugonjwa wa homa ya manjano nchini Sri Lanka.

Kwa kuzingatia sharti hili muhimu,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inawajulisha kuwa wasafiri wote wenye umri zaidi ya mwaka mmoja (1) wanatakiwa siku tisa (9) kabla ya kuingia nchini SriLanka wawe wamepata chanjo ya homa ya manjano. Utaratibu huu pia,utawahusisha wasafiri wanaopita nchini Sri Lanka ambao watakuwa wanasubiri usafiri wa kwenda nchi nyingine.

Aidha, kwa wale wasafiri ambao hawastahili kuchanja chanjo hiyo kutokana na sababu za msingi za kiafya kama vile wasafiri wenye umri chini ya mwaka mmoja (1), wazee wenye umri zaidi ya miaka sitini (60), wajawazito, waathirika wa virusi vya UKIMWI na wenye matatizo mengine ya kiafya watatakiwa kuonyesha uthibitisho kutoka kwa daktari.

Wizara inapenda kuwataarifu wasafiri wote wanaosafiri kwenda au kupitia Sri Lanka kuzingati sharti hilo muhimu ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza. Vile vile, ku hakikisha unapata chanjo hiyo katika vituo vinavyotambuliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Kwa maelezo zaidi kuhusu ugonjwa wa homa ya manjano na utaratibu wa chanjo yake wasiliana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

REGINA L. KIKULI
KAIMU KATIBU MKUU
25. 06. 2012

Popular Posts