Pages

Showing posts with label Shinyanga. Show all posts
Showing posts with label Shinyanga. Show all posts

Friday, October 19, 2012

CHADEMA Wamnadi Mgombea Udiwani Shinyanga

 Dkt Slaa akimtambulisha mgombea udiwani wa chama chake wa kata ya Mwawaza,Shinyanga
 Dkt.Slaa akihutubia
 Mgombea udiwani wa CHADEMA
Ndg Wilfred Lwakatare,Mkurugenzi wa taifa wa ulinzi na usalama na mratibu wa kitaifa wa kampeni za udiwani

Huu ni mkutano wa kumnadi mgombea wa CDM wa udiwani katika kata ya Mwawaza ulioongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Dr Wilbroad Slaa.Kumbuka huu ni mkutano tu katika mojawapo ya vijiji vya kata hiyo.

Wednesday, August 8, 2012

Lazaro Nyalandu:Serikali Kufidia Mifugo Maswa

Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Lazaro Nyalandu akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Meatu alipotembelea pori la akiba la Maswa.Nyuma yake ni mbunge wa jimbo la Kisesa mkoa wa Simiyu.
Mkuu wa wilaya ya Meatu, Rosemary Kirigini akitoa taarifa yake ya maendeleo ya pori la akiba Maswa kwa naibu Waziri Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu aliyetembelea pori hilo.
Mbunge wa jimbo la Kisesa wilaya ya Meatu Mh. Mpina akitoa salamu zake kwa wafanyakazi na viongozi wa pori la akiba Maswa.
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa pori la akiba Maswa.
Naibu Waziri wa Maliasli na Utalii Mh.Lazaro Nyalandu (kushoto) akibadilishana mawazo na mbunge wa jimbo la Kisesa mkoa wa Simiyu Mh. Mpina muda mfupi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa pori la akiba la Maswa.
Baadhi ya viongozi waliofuatana na naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu kwenye boti kwenda kukagua maendeleo ya hifadhi ya kisiwa cha Saanane.
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Lazaro Nyalandu (kulia) akiwa kwenye boti akielekea kukagua hifadhi ya kisiwa cha Saanane jijini Mwanza.Picha zote na Nathaniel Limu
--
Na.NATHANIEL LIMU
Serikali imeahidi kutoa kiasi cha 6M/- kulipa fidia ya ng’ombe 22 wanaodaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na askari wa wanyamapori wa pori la akiba Maswa wilayani Meatu, mkoani Simiyu. Inadaiwa ng,ombe hao walipigwa risasi na kuuawa Desemba 2009 baada ya kuingizwa kuchungia ndani ya hifadhi hiyo, kitendo ambacho ni kinyume na sheria zinazolinda hifadhi za wanyama pori . Ahadi hiyo imetolewa juzi na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na wakazi wa kata ya Sakasaka jimbo la Kisesa.

Alisema lengo la uamuzi huo ni kuimarisha mahusiano mazuri kati ya askari wa wanayamapori na wakazi wa vijiji vinavyozunguka akiba ya pori hilo. “Pia ni sehemu ya mikakati inayochukuliwa na serikali ya kuhakikisha mgogoro wa muda mrefu kati ya uongozi wa pori la akiba Maswa na wananchi wakazi wa vijiji vinavyozunguka pori hilo,unamalizika na kurejesha amani na utulivu katika eneo hilo,” alisema Nyalandu. Katika hatua nyingine, Nyalandu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Singida kaskazini, alisema kuwa serikali inatarajia kuunda kamati huru ambayo itashughulikia kutafuta ufumbuzi wa mgogoro uliopo kwa muda mrefu katika akiba ya pori la Maswa. “Katika kamati hii,kutakuwepo na mwakilishi mmoja kutoka wizara ya mali asili na utalii na wajumbe watakaobaki watakuwa ni watu huru ambao watazitendea haki pande zote mbili.

Ni matarajio yetu kwamba taarifa itakayotolewa na kamati hiyo haitaionea au kupendelea upande wo wote, itakuwa timilifu,” alifafanua naibu waziri huyo. Nyalandu alisema kamati hiyo itatoa taarifa yake wizarani mapema kabla bunge la sasa kuhairishwa. Katika hatua nyingine, alitumia fursa hiyo kuagiza wananchi waendelee kuelimishwa vya kutosha juu ya sheria zote za hifadhi za wanyama pori ili waweze kuzitii bila ya kushurutishwa.

“Napenda kukumbusha kuwa marufuku kuchungia,kulima,kuingiza au kufanya shughuli zo zote za kijamii ndani ya hifadhi la wanyama pori. Mfugaji au mtu yeyote atakayevunja sheria halali ailizowekwa atachukuliwa hatua kali za kisheria,” alisema Nyalandu. Awali Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Rosemary Kirigini, alisema hifadhi ya pori la akiba Maswa ipo kwa mujibu wa sheria.

“Kwa hiyo, wananchi kuigiza mifugo yao ndani ya hifadhi hiyo kwa madai ya kutokuwa na maeneo ya malisho ni kuvunja sheria. Tunashauri wananchi wenye mifugo wanaopakana na pori la akiba la Maswa watafute maeneo mengine ya kupeleka makundi yao ya mifugo, au washauriwe kupunguza mifugo yao kwa kuanzisha ufugaji wa kisasa,” alisema DC Kirigini. Aidha, alisema kuwa wataendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa madai kwamba hifadhi zilizopo, ni hazina kwa vizazi vilivyopo sasa na vya baadaye kwa nchi ya Tanzania na dunia kwa ujumla. Wakati huo huo, DC Kirigini ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kubadilisha jina la akiba la pori la Maswa na kulipa jina la akiba ya pori la Meatu.

Alisema kuwa kwa vile sasa wilaya ya Maswa imegawanywa na kuwa na wilaya wilaya tatu baada ya kuanzishwa kwa wilaya ya Bariadi na Meatu,akiba ya pori hilo ambalo sehemu kubwa ipo wilaya mpya ya Meatu,hivyo kuna ulazima wa kuitwa pori la akiba la Meatu. Kwa upande wake Nyalandu alisema ombi hilo la kubadilisha jina la pori hilo linazungumzika.

Wednesday, July 18, 2012

Kampuni ya African Barrick Gold yatoa Msaada wa Chakula Shinyanga na Geita

Kutoka Kushoto: Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale, Ibrahim Marwa, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya wakipokea msaada wa sehemu ya tani 200 za mahindi kutoka kwa Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Dennis Hoof (wa pili kulia)na Makamu wa Rais wa African Barrick Gold (ABG),Utekelezaji Muundo, Peter Gereta katika hafla iliyofanyika katika Kata ya bulyanhulu wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga hivi karibuni. Maeneo yatakayonufaika na msaada huo uliogharimu kiasi cha milioni 163/- ni kwa wale waliokumbwa na uhaba wa chakula katika vijiji 14 vilivyoko Bugarama, Mwingiro na Bulyanhulu wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga na Nyang'hwale Mkoa mpya wa Geita.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya akipokea msaada wa tani 200 za mahindi kutoka kwa Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Dennis Hoof (wa pili kulia). Kushoto ni Diwani wa Kata ya Bulyanhulu, Joseph Makoba.
Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale, Ibrahim Marwa akihutubia kabla ya makabidhiano.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya akihutubia kabla ya makabidhiano. Kulia ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Dennis Hoof na Kushoto ni Diwani wa Kata ya Bulyanhulu, Joseph Makoba na Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale, Ibrahim Marwa.
Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige akibadilishana mawazo na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Dennis Hoof (katikati), na Makamu wa Rais wa African Barrick Gold (ABG),Utekelezaji Muundo, Peter Gereta.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Dennis Hoof akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya.
Kutoka Kushoto: Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Dennis Hoof , Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya na Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale, Ibrahim Marwa wakikagua sehemu ya shehena ya mahindi mara baada ya makabidhiano.
Sehemu ya viongozi wa vijiji lengwa na msaada huo waliohudhuria hafla hiyo.Picha Zote na Badi John

Monday, July 2, 2012

ATEKELEZA FAMILIA BAADA YA MKE KUJIFUNGUA WATOTO WANAOFANANA NA NYANI.

Mtoto Alhaj.
Mtoto Alhaj akiwa amesimama.
Mtoto Alhaj akiwa anatembea.
Abdulatifu Sadik (5) akipata kifungua kinywa nje ya nyumbani kwao.
Mwanaharusi Juma akiwa nje ya nyumba yake pamoja na watoto wake Ahaj (10) mwenye shati Nyekundu na Abdulatifu.Picha zote na Nathaniel Limu
---
Mjumbe wa kamati ya shule ya msingi Ndulungu tarafa ya Ndago wilayani Iramba mkoa wa Singida, Sadik Suleman Mnyawi (44), amemtelekeza mke wake mdogo Mwanaharusi Juma (34), kwa zaidi ya miaka miwili na kumsababishia maisha kuwa magumu.Imedaiwa kwamba Mnyawi amemtelekeza mke wake huyo, kwa madai kwamba amezaa watoto wawili wanaofafana na nyani.
Mjumbe huyo wa kamati ya shule, amemtelekeza mke wake mdogo na kumpora nguo zote na kumwachia zile alizokuwa amevaa tu. Pia aliondoka na matandiko yote ya kitandani na kubakisha chaga pekee.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwanaharusi awali alikuwa ameolewa na mwanaume mwingine waliobahatika kupata mtoto mmoja, Fadhili Juma (15).Alisema baada ya kuachana na mwanaume wa kwanza, mwaka 2002, aliolewa na Mnyawi ambaye amemtoroka na kumwacha bila matunzo yoyote ya watoto watatu aliozaa naye.Alisema katika kipindi cha miaka 10 ya ndoa yake na Mnyawi, walifanikiwa kupata watoto watatu kati yao, wawili wakiwa wanafanana na nyani.

“Mtoto wangu yule niliyezaa na mume wa kwanza, Fadhila Juma, yeye yupo darasa la saba mwaka huu. Ramadhani (6) ambaye nimezaa na Mnyawi, yeye anasoma darasa la kwanza hapa Ndulungu”,alisema.

Mwanaharusi alisema kwa watoto wake aliozaa na Mnaywi,Alhaj (10) na Abdulatifu (5) ambao wana sura ya mnyama kutokana na hali zao zilivyo, wameshindwa kuanza shule.
Akifafanua zaidi, alisema watoto hao wanaofanana na nyani, hawasikii wala hawasemi. Mawasiliano yao yanategemea ishara tu.

“Ukiacha matatizo yao ya kutokusikia na kuzungumza, pia wanahema kwa tabu kubwa. Kama huwaoni, ukisikia wanavyohema, unaweza ukafikiria kwamba hao zio binadamu ni nguruwe anahema”,alisema kwa masikitiko.

Mwanaharusi alisema mikono yao ni midogo mno na mifupi na ni dhaifu, matumbo na macho yao ni makubwa. Alhaji pekee ndiye mwenye uwezo wa kusimama na kutembea umbali mfupi na mwenendo wake unafanana na wa nyani.

Hata hivyo, alisema watoto hao wawili aliwazaa wakiwa wana sura za binadamu na afya zao zikiwa njema kabisa. Lakini wakati wanaendelea kukua, ndipo walipoanza kuugua mara kwa mara na kisha kubadilika sura.

“Wakati bado tunaelewana na mume wangu, tuliwahi kumpeleka Alhaji katika hospitali ya mkoa wa Singida. Alichunguzwa na alibainika kuwa na upungufu wa damu. Aliongezewa damu na kisha tuliruhusiwa kurudi nyumbani”,alisema.

Alisema baada ya kurudi nyumbani, haikuchukua muda, Alhaji alianza kuugua tena na baada ya kumshawishi mume wake Mnyawi, wampeleke hospitali ya rufaa, ndipo alipomkimbia na kuhamia kwa mke wake mkubwa.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa,alisema kuanzia wakati huo, anaishi maisha magumu mno ambayo ni ya kuomba omba. Mnyawi pamoja na familia yake, amewabembeleza wamsaidie mizigo wa kuwalea watoto hao, wamegoma kabisa.Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho, Idd Nyauli, alisema wamejitahidi kumshauri Mnyawi amrudie mke wake mdogo ili waweze kuwalea watoto wao pamaja, jitahida hizo zimegonga mwamba baada ya Mnyawi kugoma kumrudia Mwanaharusi.

Naye mratibu elimu wa kata hiyo Mwekwa Mwekwa, alisema watoto hao wawili, shule inayowafaa ni ile ya watoto wenye mtindio wa ubongo na si hizi za kawaida.Jitihada ya kumtafuta Mnyawi ambaye anaishi kijiji hicho cha Ndulungu, hazikuzaa matunda baada ya kuelezwa kwamba baada ya kusikia waandishi wa habari watafika kijijini hapo, alifunga safari na kuelekea jijini Mwanza.

Popular Posts