Pages

Saturday, June 23, 2012

PICHA ZA MAANDAMANO DONGE






TAMKO LA TAASISI ZA KIISLAMU KUHUSU KUVUNJWA KWA MUHADHARA DONGE

BISMILLAH RAHMANI RAHIM

TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU ZANZIBAR

Kila sifa njema anastahiki ALLAH (S.W.T), Rehma na Amani zimuendee Mtume Muhammad (S.A.W), watu wake, Maswahaba zake na walio wema katika Uislamu.

Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar baada ya kufuatilia kwa hatua za awali na kufanya tathmini ya hali ya mambo namna ilivyotokea tarehe 17 juni, 2012 inatoa tamko RASMI kama ifuatavyo:

Siku ya tarehe 17 juni, 2012 majira ya saa nane na nusu za mchana waislam waliondoka viwanja vya malindi eneo la mjini magharibi na msafara wa gari, vespa na Pikipiki ukielekea kwenye muhadhara Kaskazini Unguja eneo la Donge sambamba na wenzao wengine waliotoka mashamba yote ya Unguja kuelekea hukohuko Donge katika Msikiti uliopo eneo linalojulikana kwa jina la Donge pwani, tulipofika Mahonda msikiti wa Ijumaa ambao upo karibu na kituo cha polisi cha mahonda, majira ya saa tisa na dakika kumi jeshi la polisi lililovalia sare za askari wa FFU liliwazuia wananchi hao kuendelea na safari yao ya Donge nakusababisha mkusanyiko usio wa lazima.

Watu waliokuwa katika msafara huo walilazimika waingie msikitini huku wakisubiri viongozi wao wa jumuiya na taasisi za kiisilamu wawaongoze, wakati viongozi wa jumuiya na taasisi za kiisilamu walipofika eneo hilo walitoka kwenye gari ili kwenda kufanya mazungumzo na askari, ndipo FFU walipoaza kurusha mabomu ya machozi ovyo na kuwatawanya waumini hao, huu ni uvunjaji wa katiba zote mbili na ukiukwaji wa haki ya raia na uhuru wake wa kuabudu kama inavyoelezwa na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 19 (2) ambayo inasema “Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada, kueneza dini itakua huru na jambo la hiari ya mtu binafsi na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakua nje ya shuguli za mamlaka ya nchi…” rejea pia katiba ya Jamhuri ibara. 19 (1), (2), (3).

Pia kufanya hivyo ni kwenda kinyume na katiba ya Zanzibar ibara ya 16 (1) kwa kuwazuwia watu kwenda watakapo ndani ya Zanzibar…, sheria kama hii pia inaelezwa ndani ya katiba ya Jamhuri…

Ibara ya 17(1) inatamka wazi kwamba “…Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano…”. Pia kifungu kidogo cha (2) (b)(i),(ii),(iii) vimetoa maelezo zaidi.

Jeshi la Polisi limekwenda kinyume na kifungu cha 18 (1) cha sheria ya Zanzibar kwa kuzuwia uhuru wa maoni Sambamba na Kwenda kinyume na Sheria ya mwaka 1977 ya Jamhuri ya Tanzania ibara ya 18 (1) “…kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari…”

Isitoshe, juu ya ukiukwaji wote huo askari hao wamefanya unyama na uhalifu wahali ya juu kwa kuunajisi Msikiti wa Ijumaa wa Mahonda kwa kuwahujumu Raia wasio na silaha ndani ya Msikiti kwa kuwarushia mabomu ya machozi yasiojulikana idadi yake ambapo hadi hii leo msikiti huo hausaliki ndani kutokana na harufu kali ya mabomu. Pia askari hao walipiga risasi pamoja na kuingia ndani ya Msikiti na viatu na kuvunja kwa makusudi vyombo (Vespa, Pikipiki, Baskeli n.k) vilivyoegeshwa eneo la msikiti huo wa Ijumaa.

Sambamba na hilo, polisi wamevunja taa ya mbele na nyuma ya vespa ya mwandishi wa habari wa jumuiya pamoja na taa za gari inayobeba vifaa vya mihadhara kichuki baada ya kuikamata mapema tu na kuifikisha polisi, hali hii ilitokea wakati gari ikiwa kituoni chini ya kizuizi cha polisi baada ya kuikamata tokea saa saba nanusu za mchana kabla ya kufika kwa misafara inayokwenda kwenye mihadhara hadi leo hii gari hiyo inashikiliwa na polisi kituoni mahonda.

Pia katika jumla ya matukio ni kuandamwa na kufukuzwa kwa gari ya kiongozi wa Jumuiya ya Maimamu Sh. Farid Hadi Ahmed yenye Namba ya usajili Z 628 DJ aina ya NISAN X-TRAIL iliyofukuzwa kwa pikipiki inasadikiwa na watu ambao walitumwa na jeshi la polisi kwa lengo la uhalifu dhidi ya Amir Farid kitendo ambacho kilisababisha ajali ya kupinduka kwa gari hiyo na kusababisha kujigonga na mti huko Dole tukio ambalo liliripotiwa kituo cha polisi cha Muembe Mchomeke. Haya yote yaliyofanywa na Jeshi la Polisi kuwajeruhi watu wasiokua na hatia pamoja na kuharibu mali yanakwenda kinyume na katiba na sheria za nchi.

Jambo la kushtusha zaidi ni kitendo cha kuwadhililisha wanawake na kufikia hadi kuwakashifu kwa kuwachania nguo zao na kuwavua mashungi yao pia hata watoto wadogo mitaani wako walopata kipigo, kitendo cha kuwatimba wanawake kwa viatu bila ya huruma na kuwapiga marungu na kuwajeruhi vibaya sehemu za usoni na mwilini kwa ujumla, huo wote ni unyama na ukiukwaji wa haki za binaadamu.

Ilipofikia wakati wa laasiri jeshi la polisi walianza pia kupiga mabomu ndani ya msikiti wa donge pwani pamoja na kuuhujumu msikiti na waumini wakiwa wanaswali katika msikiti wa Donge skuli na kuvunja vioo vya msikiti huo, huu wote ni udhalilishaji wa dini ya Kiislamu pamoja na waumini katika eneo hilo.

Vile vile, askari wa jeshi la polisi walikata kwa visu mipira ya vyombo vya wananchi kama vile vespa na baskeli zilizokua zimeegeshwa msikitini hapo na askari hao walivunja heshma ya msikiti kwa kuingia na viatu ndani ya misikiti hiyo.

Sambamba na hilo, walimkamata mzee Kassim Shekha mwenye Umri wa miaka 50 aliekua akiswali swala ya laasir walimjeruhi vibaya miguuni kwa mlipuko wa bomu la machozi akiwa ndani ya swala, pia kijana Othman Ali (22) aliamriwa aingie Msikitini na hatimae kujikuta akipigwa kwa mateke, vibao na kuchaniwa nguo huku akiamriwa lazima atembee kwa magoti pamoja na wenziwe hadi kituoni Mahonda.

Kwa taarifa tulizozipata kutoka kwa kamishna wa jeshi la polisi Zanzibar kupitia vyombo mbali mbali vya habari ikiwemo gazeti la serikali la Zanzibar leo toleo nambari 3789 la tarehe 18 Juni, 2012 lilisema likimnukuu Kamishna huyo ndugu Mussa Ali Mussa eti hakuna alie jeruhiwa wakati taarifa za kuaminika zimeripoti watu thalathini na nne ambapo wanaume ni 27 na wanawake 9. Upotoshaji huo wa jeshi la polisi ni kuonesha namnagani jeshi la Polisi lisivyo wajali wananchi, roho na mali zao na jinsi linavyopotosha ukweli wa mambo. Pia kutokujali hata kwenda kinyume na viapo vyao vya uaminifu wanapoingia kwenye ajira, Kwa kiongozi wa Jeshi la Polisi kwa nafasi kama hiyo ya kamishna alipaswa awe mfano mzuri kwa walio chini yake.

Matukiyo yote hayo ya kunajisi Misikiti na kudhalilisha waumini wakiwa ndani ya nyumba za ibada yanazidi kujenga imani kua ni kweli yale yanaosemwa kua jeshi la Polisi linahusika kwa njia moja au nyengine katika suala zima la unajisi na uchomwaji wa Makanisa kiushiriki na ufichaji wa wahalifu kisha kutoa taarifa za uongo na kuwafanya Waislamu ndio chaka lao.

Baada ya hayo machache yaliyotangulia hapo juu pamoja na kukutana na waathirika na wananchi wa Donge, Jumuiya na Taasisi za Kiislamu inatamka kwamba:

  1. Jumuiya inasikitishwa sana na taarifa za uongo zisizo kuwa na ukweli na inalitaka jeshi la polisi na Vyombo vyote vya Dola wafanye kazi zao kwa ukweli na uaminifu kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu wakitambuwa umuhimu wa jukumu lao la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu. Kila mtu anayo haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya kitaifa na kimataifa yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu. Kwa maana hiyo tunalitaka jeshi la polisi litueleze kwa katiba gani na sheria ipi iliyotumika kuzuia uhuru wa kuabudu na kutoa mihadhara na kukusanyika waumini wa kiisilamu misikitini? Tunavyofahamu sisi jumuiya, ni kuwa jeshi la polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kuheshimu, kulinda na kutetea haki za binadamu kwa watu wote bila ya ubaguzi.
  2. Wananchi wa Donge wanasema wamechoshwa na ubaguzi na udikteta wa Shamhuna na wanaitaka serikali ya umoja wa kitaifa kupitia baraza la wawakilishi itoe ufafanuzi wa wazi kabisa, ni kwa sheria gani wananchi wa Donge wananyimwa fursa ya kufaidi uhuru wa kuabudu na uhuru wa maoni pamoja na uhuru wa kuchanganyika na ndugu zao wazanzibari? vile vile haki ya kutumia TV na DVD zao mitaani uhuru ambao unaingiliwa na masheha kwa kuwazuia watu kutizama watakacho na kufikia hadi kuwatisha kuwapeleka Polisi na hata kuwanyang’anya mali hizo jambo ambalo linaweza kusababisha uvunjifu wa amani wakati inafahamika kuwa haki zote hizo zinalindwa na katiba ya Zanizbar kwenye ibara zifuatazo 17, 18, 19 na 20.
  3. Wananchi wa Donge pia wanomba ufafanuzi kutoka baraza la wawakilishi kwani kwa miaka yote wanajiona kuwa wanabaguliwa wakati wananchi wenzao wa mashamba yote mengine katika wilaya tofauti wakipata haki kikamilifu, jee wao si wazanzibari? Ni dhambi gani waliyotenda hata wakabaguliwa kiasi hicho? Au Donge ni nchi yenye mfalme kama wafalme wa ki-Misri wakijulikana kwa jina laFIRAUNI?
  4. Wananchi wa Donge wanaliomba baraza la wawakilishi tukufu ndani ya siku kumi na nne (14) litoe ufafanuzi wa haki juu ya masuala yao yote, ikishindakana hivyo wasije wakalaumika kwa maamuzi watakayochukua. Pia wanaviomba vyama vyote vya siasa viwe makini sana kuwatetea haki zao.
  5. Jumuiya na taasisi za kiislamu zinawaahidi wananchi wa Donge kuwa ziko tayari kuwaunga mkono kwa maamuzi yoyote watakayo yachukuwa na kuwataka waislamu wote wawe tayari kwa hilo.
  6. Jumuiya za kiisilamu zinawapa pole waathirika wote na kuwapa hongera wazanzibari wote kwa uimara na kutotetereka katika kudai haki zao pamoja na kutoa wito wa kudumisha amani na utulivu, pamoja na kuwa na subra na kutolipiza kisasi.

Mwisho, Jumuiya na Taasisi za Kiislamu zinapenda ifahamike kwamba, inatoa na kupaza sauti ya ukombozi wa Zanzibar kwa njia za amani bila ya kutumia nguvu za silaha bali kwa kutumia nguvu za hoja na inaendesha harakati zake hizo za ukombozi juu ya misingi ya sheria za nchi na katiba.

Hivyo basi, wananchi wa Zanzibar kudai uhuru wa kujiamulia mambo yetu ni haki yetu ya msingi, na kwa hilo HATUNA MJADALA (MPAKA TUTAKAPOIPATA NCHI YETU INSHA-ALLAH), tutaendelea kudai haki zetu kwa kila hali bila ya kuvunja sheria za nchi.

Tunasisitiza kuendelea na kuidai Zanzibar yetu huru ingawa tunaelewa gharama ya kufanya hivyo ni kubwa ikiwemo kupoteza roho zetu na mali zetu. Na tunatamka wazi yakwamba tumechoka na ukoloni wa watanganyika wachache wasioitakia mema Tanganyika na Zanzibar.

Tutaidai nchi yetu kwa gharama yoyote mpaka kuipata Zanzibar yetu huru.

“…FREE ZANZIBAR…”

“TUACHIWE TUPUMUE”

WABILLLAH TAWFIQ

Deidre Lorenz Atembelea kituo cha Yatima wa Kituo cha Yatima cha Upendo

Mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz ambaye alitua mjini Moshi jana kushiriki kwenye mbio za kimataifa za Mt. Kilimanjaro Marathon leo alikaa na watoto wa kituo cha yatima cha Upendo kinachoendeshwa na masista wa shirika la Precious Blood mjini Moshi. Lorenz aliingia kwa kishindo katika Manispaa ya Moshi na kueleza juu ya nia yake ya kuitangaza Tanzania nchini Marekni kwa kutumia usanii wake wa filamu.

Deidre Lorenz anashiriki katika mashindano ya Mt. Kilimanjaro Marathon ambayo yanaanza kutimua vumbi tarehe 24 Jumapili kuanzia Moshi klabu hadi Rau madukani na kurudi. Mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zilianzishwa na Marie Frances kutoka katika mji wa Bethesda nchini Marekni mwaka 1991 baada ya kuombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri kuja Tanzania kuanzisha mbio za marathon.

Deidre Lorenz anawakilisha kikundi cha Actors Guild ambacho kina lengo la kukusanya pesa kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa saratani. Katika ziara yake kwenye kituo cha watoto yatima cha Upendo Deidre aliwasomea watoto hao hadithi mbalimbali za watoto. Aidha, aliwapa zawadi za fangi za kuchora, vitabu, daftari, kalamu, chocolate na zawadi nyingine kemkem zinazowaelimisha watoto.

Lorenz ameshiriki pia katika mahojiano na waandishi mbalimbali wa habari mjini Moshi na kueleza kuhusu nia yake ya kuitembelea Tanzania mara kwa mara. Amesema kuwa wazazi wake hususan bibi yake alimwambia kuwa Tanzania ni nchi yenye wanawake wenye sura nzuri sana. Aidha marafiki zake wamemwambia kuwa aje yeye kwanza ili wao waje katika mbio zinazofuata.

Klabu ya Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 inakusudia kuwatumia watu maarufu kuja Tanzania ili waweze kuutangaza utalii pamoja na mazingira ya kuwekeza. Klabu hii ina lengo la kuanzisha marathon nyingine tena ambayo itajumuisha mbio na michezo mingine ya uwanjani.

“Tutakuwa na wiki nzima ya mashindanio ya uwanjani na siku ya saba tutafanya mbio za marathon” alisema Rais wa Klabu hiyo Onesmo Ngowi alipokuwa anazungumza na waandishi wa bahari hapa Moshi. Ngowi alieleza kuwa ni muhimu Moshi/Tanzania ikawa na mashindano ya michezo mingi itakayowavutia watalii na wawekezaji wengi kuja Tanzania.

Akielezea kuhusu mikakati ya klabu yake kuendeleza mchezo wa riadha Ngowi ambaye pia ni Rais wa IBF/USBA katika bara la Afrika, Mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi alisema kuwa wameweka mikakati mingi itakayoifanya mji wa Moshi kuwa kitovu cha utalii katika mkoa wa Kilimanjaro.
Hizi mbio ni sehemu tu ya mikakati ya kuendeleza michezo katika mkoa huu ambao miaka ya sabini ulikuwa unaongoza kwa michezo katika nchi hii. “Tutashirikiana na mashirikisho ya michezo ya ndani na nje kuinua viwango vya wanamichezo wetu” alisema Ngowi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo katika mkoa wa Kilimanjaro. Alisema kuwa wameandaa mikakati mingi na kumalizia kuwa Tanzania ni yetu sote kwa hiyo tuna jukumu la kuchangia katika maendeleo yake.

Deidre Lorenz atakimbia mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon jumapili ijayo na ataondoka usiku wa jumapili kurudi nyumbani kwake New York jiji linajulikana kama “The Big Apple” na Financial Capital of the World (Jiji la Fedha Duniani)

Imetumwa na:


Grace Soka
Afisa Uhusiano


Mt. Kilimanjaro Marathon
Technology House
35-38 Ghalla Road
Moshi - Tanzania

Wakufunzi wa Sensa ya Watu na Makazi ngazi ya kitaifa

Wakufunzi wa Sensa ya Watu na Makazi ngazi ya kitaifa wakishiriki katika mafunzo ya kujaza dodoso fupi la sense ya watu na makazi leo katika mafunzo ya siku 10 yanayoendelea mjini Dodoma. Mafunzo hayo yameandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa ajili ya kuwajengea uwezo wakufunzi hao ili nao waweze kuendesha katika ngazi za mikoa mbalimbali hapa nchini.Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO-Dodoma na Ofisi ya Waziri Mkuu

PICHA MBALIMBALI TOKA VIWANJA VYA BUNGE

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge Bumbuli na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Mh. January Makamba (katikati) na Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji (kulia) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 22, 2012.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akibadilisha mawazo na mbunge wa Simanjiro(CCM)Ole Sendeka
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole- Sendeka (kushoto) na Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (kulia) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 22,2012.
Mbunge wa Mbeya Mjini joseph Mbilinyi (SUGU) akibadilishana mawazo na Mbunge Mwenzie kutoka Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe leo wakati wa mapumziko ya mchana ya Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Simanjiro,Christopher Ole Sendeka (kushoto) na Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango Malecela kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, Juni 22, 2012.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda(katikati) akibadilishana mawazo jana na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (kushoto) MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela (kulia),wakati wa mapumziko ya mchana ya kikao cha Bunge la bajeti linaloendelea mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Simanjiro,Christopher Ole Sendeka (kushoto) na Mbunge wa Viti Maalum Ester Bulaya kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 22, 2012.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dkt. Makongoro Mahanga(kushoto) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige wakati wa mapumziko ya mchana ya Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma.
Baadhi ya wabunge wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakijaza fomu za vitambulisho vya Taifa leo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

MAHAKAMA YAZUIA MGOMO WA MADAKTARI

Kufuatia Tangazo la Chama cha Madaktari nchini (MAT) la kuanza mgomo siku ya Jumamosi tarehe 23 Juni, 2012, Mahakama Kuu ya Tanzania,Kitengo cha kazi,Dar es Salaam imetoa amri ya kusitisha mgomo huo mpaka hapo pande zote mbili yaani Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

· Amri hiyo ya Mahakama imetolewa kufuatia maombi namba 73 ya 2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).Sababu za msingi amabazo zimepelekea Mahakama kuu kutoa amri hiyo upande mmoja ni pamoja na;

· Iwapo mgomo huo utatokea utakuwa na kuwa amri hii isipotolewa madhara yake ni makubwa isiyoweza kufidiwa kwa namna yoyote ile kama vile kupoteza maisha n.k

· Wajibu maombi,ambao ni MAT, inaundwa na Madaktari ambao wapo katika Sekta ambayo inatoa huduma mahsusi (essential service sector), Aidha Chama cha Madaktari Tanzania kimetangaza mgomo bila kufuatia taratibu zilizoanishwa katika Kifungu cha 76(1 na 2) cha Sheria ya Kazi (Employment and Labour Relations Act No 6 ya 2004.

Masharti hayo ni

· Kuzuia wafanyakazi walio katika Sekta Muhimu kugoma na kama wakigoma

Kuwepona makubalianao ya pamoja ya kutoa huduma za msingi wakati mgomo ukiendelea.

Kwa misingi hii,Mahakama Kuu ya Tanzania, kwa Chama cha Madktari Nchini na wanachama wake kusitisha na kutoshiriki katika mgonmo huo.

UMOJA WA WATANZANIA WA BRAZIL WAKUTANA NA MAKAMU WA RAIS

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na mmoja kati ya wajumbe wa Umoja wa Watanzania, waishio nchini Brazil,wakati alipokutana nao katika hafla ya chakula cha jioni na mazungumzo, iliyofanyika katika Hoteli ya Arena,Rio de Jeneiro, jana Juni 22, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania, waishio nchini Brazil, Ally Abdaul Faraji, baada ya kumaliza hafla wakati alipokutana nao katika hafla hio fupi ya chakula cha jioni na mazungumzo, iliyofanyika katika Hoteli ya Arena, Rio de Jeneiro, jana Juni 22, 2012. Kushoto ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Zakhia Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Katibu wa Umoja wa Watanzania, waishio nchini Brazil, Heri Juma Mbwana, wakati alipokutana nao katika hafla ya chakula cha jioni na mazungumzo, iliyofanyika katika Hoteli ya Arena, Rio de Jeneiro, jana Juni 22, 2012.
Katibu wa Umoja huo, akizungumza na kusoma risala yao kwa Mhe, Makamu wa Rais, Dkt Gharib Bilal
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza Viongozi wa Umoja wa Watanzania, waishio nchini Brazil, wakati alipokutana nao katika hafla ya chakula cha jioni na mazungumzo, iliyofanyika katika Hoteli ya Arena, Rio de Jeneiro, jana Juni 22, 2012. Kulia ni Mama Zakhia Bilal (kushoto) ni Balozi wa Tanzania, nchini Brazil, Francis Malambugi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mke wa Makam wa Rais, Mama Zakhia Bilal,Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maadhi Juma Maalim, Balozi wa Tanzania nchini Brazil Francis Malambugi, na Balozi Liberata Mulamula, wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Umoja wa Watazanaia, wakati alipokutana nao viongozi hao wa moja wa Watanzania, waishio nchini katika hafla ya chakula cha jioni na mazungumzo, iliyofanyika katika Hoteli ya Arena, Rio de Jeneiro, jana Juni 22, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamau wa Rais

Rais Jakaya Kikwete Akiifariji Familia ya Aliyekuwa Mkuu wa Utawala CCM Makao Makao Makuu Dodoma Marehemu Mwangunza Kinyamagoha

Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Mkuu wa Utawala CCM Makao Makao Makuu Dodoma marehemu Mwangunza Kinyamagoha nyumbani kwake mjini Dodoma jana.Marehemu Kinyamagoha alifariki hivi karibuni.
Rais Kikwete akiifariji familia ya Marehemu Kinyamagoha nyumbani kwake mjini Dodoma jana kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam.Picha na Freddy Maro-IKULU

Wagombea Mbalimbali wa Uongozi Klabu ya Yanga

Manji akiwasili Makao Makuu ya Yanga.
Saidi Motisha akimkaribisha mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kuingia Makao Makuu ya klabu hiyo wakati wa usaili
Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji akiteta jambo na mwanachama wa klabu hiyo, Bi. Rukia Mohamed Makao Makuu ya klabu Dar es Salaam, alikokwenda kufanyiwa usaili kwa ajili ya uchaguzi mdogo.
Manji akiwasili Makao Makuu ya Yanga.
Manji akizungumza na waandishi wa habari
Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Yanga, Sarah Ramadhani naye akiingia wakati wa usaili
Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga (mwenye tai) akiwa na mgombea wa nafasi ya ujumbe, Peter Haule baada ya kufanyiwa usaili kwa ajili ya uchaguzi mdogo.
Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa yanga, Clement Sanga (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya wanachama wa Yanga baada ya usaili
Manji akiondoka baada ya kufanyia usaili na kamati ya uchaguzi.Picha na Habari na Mdau Francis Dande

shule ya msingi Mgulani na Chemi & Cotex watembelea kituo cha Yatima cha Friends of Don Bosco Kimara.

Piscus Laswai ambaye pia ni mmoja wa yatima wanaolelewa na kituo cha Friends of DonBosco kilichopo Kimara jijini akipokea zawadi ya taa zinazotumia mwanga wa jua kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Mgulani ambazo zitawasaidia yatima hao kujisomea hasa nyakati za usiku kunapokua na tatizo la umeme.
Mwanafunzi wa darasa la saba kutoka shule ya msingi Mgulani Emmanuel George (kulia) akiwapa zawadi ya mpira wanafunzi wenzake ambao ni yatima wanaolelewa katika kituo cha Friends of DonBosco kilichopo Kimara pindi walipotembelea kituo hicho hivi karibuni chini ya uwakilishi wa Chemi & Cotex ltd.
Watoto yatima wanaoishi kituo cha Friends of DonBosco kimara jijini wakiwakaribisha wanafunzi kutoka shule ya msingi Mgulani kituoni hapo pindi walipokuja kuwatembelea yatima hao na kufahamiana zaidi hasa kielimu pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi milioni moja kutoka kampuni ya Chemi & cotex.
Watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha Friends of Don Bosco kilichopo Kimara jijini wakifurahia zawadi za miswaki na dawa za meno za Whitedent walizopewa na wanafunzi wenzao kutoka shule ya msingi Mgulani waliowatembelea kituoni hapo hivi karibuni ikiwa ni sehemu ya kufamiana zaidi katika maendeleo ya elimu kwa ujumla.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani Azungumza Kuhusu Maadhimisho ya Siku ya utumishi wa Umma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani akizungumza na waandishi wa habari (jana) mjini Dodoma kuhusu maadhimisho ya siku ya utumishi wa umma ambayo yanaadhimisho Leo tarehe 23.06.2012 kote duniani. Kuali mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni kujenga uwezo wa utekelezaji wa mkataba wa misingi na kaununi za utumishi wa umma na utawala ili kuwa nchi zinazojimudu kimaendeleo katika Afrika.Picha na tiganya Vincent-Dodoma

Timu ya Cricket ya Totteridge Yatoa Msaada wa Vifaa vya Michezo kwa Tanzania

Bwana Gulfraz, akisalimiana na Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London, Bwana Yusuf Kashangwa kabla ya makabidhiano ya msaada wa Vifaa vya mchezo kwa Timu ya Cricket ya Tanzania.
Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London nchini Uingereza, Bwana Yusuf Kashangwa (tatu kushoto), akipokea msaada wa Vifaa vya mchezo wa Cricket kwa Tanzania kutoka kwa Mwenyekiti wa Timu ya Cricket ya Totteridge Millhill, Bwana Stewart Wenham (kwanza kushoto). Msaada huo wa Vifaa vilikabidhiwa kwa Mkurugenzi, Bwana Kashangwa, ni moja ya ushirikiano mzuri uliopo baina ya Timu ya Tanzania ya mchezo wa Cricket, Shirikisho la mchezo huo hapa Uingereza na Timu ya Cricket ya Watford. Wengine pichani ni maafisa wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London.
--
Timu ya Cricket ya Watford ikiongozwa na Bwana Gulfraza Riaz, imekuwa ushirikiano wa karibu na Timu yetu ya Taifa ya mchezo wa Cricket, Tanzania, vile vile timu hiyo imekuwa mstari wa mbele kuitangaza Tanzania katika mchezo huo hapa nchini Uingereza, pamoja na kuandaa michezo ya majaribio kwa Tanzania kila mara.

Thursday, June 21, 2012

MABADILIKO YAFANYIKA BARAZA KIVULI LA MAWAZIRI

BARAZA LA MAWAZIRI KIVULI NA MABADILIKO YA WIZARA KIVULI
No.WIZARA KIVULIWIZARA YA SERIKALIKAMATI HUSIKA YA BUNGEWAZIRI KIVULINAIBU WAZIRI
1.OFISI YA WAZIRI MKUUOFISI YA WAZIRI MKUU-SHERIA NA KATIBA,
-FEDHA ,UCHUMI +MIPANGO
KUB- FREEMAN A.MBOWE
2.
WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU

1.SERA,URATIBU NA BUNGE
2.UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI
3. TAMISEMI—
ELIMU
-TAWALA ZA MIKOA
-do-
DAVID ERNEST SILINDE

-
3.MIUNDOMBINUUJENZI NA UCHUKUZIMIUNDOMBINUSAID ARFIPAULINE GEKUL
4
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS
OFISI YA RAIS
1-UTAWALA BORA
2-MAHUSIANO NA URATIBU
3- MENEJIMENT YA UTUMISHI WA UMMA
-SHERIA NA KATIBA.
-FEDHA NA UCHUMI
PROF. KULIKOYELA KAHIGI

-
5.FEDHA UCHUMI NA MIPANGOWIZARA YA FEDHAFEDHA NA UCHUMIZITTO KABWECHRISTINA MUGHWAI
6.KATIBA SHERIA NA MUUNGANOKATIBA NA SHERIA+OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANOSHERIA NA KATIBATUNDU A.LISSU
-
7.MALIASILI,UTALII NA MAZINGIRAMALIASILI NA UTALII+OFISI YA MAKAMU WA RAIS MAZINGIRAMALIASILI NA MAZINGIRAMCH.PETER MSIGWA
-
8.MAMBO YA NDANI YA NCHIMAMBO YA NDANIMAMBO YA NJE ULINZI NA USALAMAVICENT NYERERE
-
9.MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA YA MASHARIKIMAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA+ USHIRIKIANO WA AFRIKA YA MASHARIKIMAMBO YA NJE ULINZI NA USALAMAEZEKIAH D.WENJERAYA IBRAHIM KHAMIS
10.ULINZI NA JKTULINZI NA JKTMAMBO YA NJE ULINZI NA USALAMA
MCH.ISRAEL NATSE
-
11.MAJI,MIFUGO NA UVUVIMAJI NA UMWAGILIAJI+ MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVIKILIMO ARDHI NA MAJISYLVESTER M.KASULUMBAYI
SABREENA HAMZA
SUNGURA
12.KAZI,HABARI,UTAMADUNI NA MICHEZOHABARI,VIJANA NA MICHEZO+ KAZI NA AJIRAMAENDELEO YA JAMIIJOSEPH O.MBILINYICECILIA PARESSO
13.NISHATI NA MADININISHATI NA MADININISHATI NA MADINIJOHN MNYIKA
-
14.VIWANDA NA BIASHARAVIWANDA NA BIASHARAVIWANDA NA BIASHARAHIGHNESS KIWIA
-
15.AFYA, JINSIA NA JAMIIAFYA NA USTAWI WA JAMII+MAENDELEO YA JAMII JINSIA NA WATOTO-HUDUMA ZA JAMII
-MAENDELEO YA JAMII
DR. GERVAS MBASSACONCHESTA RWAMLAZA
16.ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIAELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI + SAYANSI TEKNOLOJIA NA MAWASILIANO-HUDUMA ZA JAMII
-MIUNDOMBINU
SUZAN A.LYIMOJOSHUA NASSARI
17.KILIMO NA USHIRIKAKILIMO, CHAKULA NA USHIRIKAKILIMO, MIFUGO NA MAJIROSE SUKUM KAMILI
-
18.ARDHI,NYUMBA NA MAKAZIARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZIARDHI, MALIASI NA MAZINGIRAHALIMA MDEE
-

Popular Posts