Pages

Saturday, July 28, 2012

SAFINA RADIO YA ARUSHA YAOMBEA TAIFA

Kituo cha Redio cha Safina cha jijini Arusha leo kimeandaa kusanyiko kubwa la neon la Mungu ambalo limelenga kuomboleza Taifa la Tanzania na kuongozwa na kichwa kisemacho TOBA YA TAIFA “Tubuni Dhambi zenu zifutwe” Maneno kutoka Matendo 3:19.

Kivutio kikubwa katika mkutano huu ni pale wananchi waliokuwa wakifika hapo wakiwa wamevaa magunia na viroba nah ii ni kutokana hasa na neon lenyewe lilivyokuwa likiwataka kufanya hivyo. Ambalo ni “Kwa sababu hiyo jifungeni nguo za magunia; ombolezeni na kulia kwa uchungu; kwa maana hasira kali ya Bwana haikugeuka na kutuacha”.
Mtumishi wa Mungu, Jovin Abel Msuya kutoka Safina Radio, akitoa neon la Mungu kwa wakazi wa Arusha na Vitongoji vyake waliofurika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini hapa leo kuomboleza juu ya taifa la Tanzania.
Umati wa wakazi wa Arusha na vitongoji vyake wakiwa uwanjani hapo wakipokea neno la Mungu.
Bibi huyu nae alijitokeza uwanjani hapo na Biblia yake akifuatilia neno na kuomboleza juu ya taifa lake la Tanzania.
Yalikuwa ni mafundisho muhimu sana na walio na madaftari walinukuu maandiko yaliyo kuwa yakitolewa kwa tafakuri zaidi.
Watoto nao hawakuachwa nyumbani katika maombolezo haya nao walikuwepo uwanjani hapa na wazazi wao.
Watu wakivaa viroba tayari kwa kushiriki mkutano wa maombolezo. Kiroba kimoja kilikuwa kinauzwa Tsh 1,000/= na vijana wengi waliviuza sana.
Wanahabari kutoka Star TV na ITV wa mjini Arusha wakiwa uwanjani hapo kutafuta habari za hapa na pale
Akina mama ndio mara nyingi hushiriki kikamilifu katika maombolezo juu ya tukio lolote na leo akina mama walikuwa wengi sana kuliko akina baba.
wanafunzi nao walishiriki mkutano huu wa Maombolezo juu ya Taifa la Tanzania
Mtumishi wa Mungu, Jovin Abel Msuya akiendelea kushusha maandiko juukwaani
Jua lilikuwa lina waka na wanafunzi baade walila.

MABINGWA KOMBE LA KAGAME 2012 NI YANGA YA TANZANIA

Magoli mawili yaliyopachikwa wavuni na washambuliaji wa Yanga Hamisi Kiiza katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza na lile la Said Bahanuzi katika dakika ya 90 ya mchezo yameiwezesha Yanga kuibuka Mabingwa tena wa Kombe la Kagame 2012 baada ya kuchapa bila huruma mahasimu wao Azam FC kwa goli 2-0, katika mchezo wa fainali uliochezwa leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tanzania ijnakila sababu ya kujivunia ushindi huo wa Yanga na nafasi ya pili ya Azam katika michuano hiyo ya mwaka huu ambapo Tanzania kama mwenyeji wa michuani huyo iliingiza timu 4 zikiwapo za Simba na Mafunzo zilizotolewa katika hatua ya robo fainali.

Yanga pia waliutumia mchezo wa leo kulipiza kisasi cha kufungwa goli 3-1 na Azam katika mchezo wao wa Ligi Kuu msimu uliopita na kupelekea wachezaji kadhaa wa Yanga kufungiwa baada ya kushambulia mwamuzi kwa ngumi.

MACHANGUDOA WACHAPWA VIBOKO

WATUMIA BAJAJ
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, waumini hao, wakiwa wamevaa kanzu huku wakitembea na bakora mkononi walichukua jukumu la kukodi Bajaj na kuzunguka maeneo mbalimbali jijini inapofanyika biashara hiyo haramu ya ukahaba.
BARABARA YA SHEKILANGO
Vijana hao waliolenga kukomesha biashara hiyo hasa kipindi hiki cha mfungo walianzia kwenye Barabara ya Shekilango inayokatiza kwenye viunga vya Sinza, Dar ambapo kila kituo cha daladala kuanzia Afrika Sana hadi kwenye mataa ya Shekilango waliwakuta machangu na kuwatandika viboko kabla ya kutua mitaa ya Mwenge.
KINONDONI
Baada ya kufagiafagia Sinza kwa kuwaadabisha wanawake hao ndipo zoezi likahamia mitaa ya Kinondoni ambapo nao walipokea bakora za kutosha huku wengine wakitoka nduki.

KISA KUHARIBIWA SWAUMU
Kwa mujibu wa vijana hao, walifikia hatua ya kufanya zoezi hilo baada ya muumini mmoja wa kiume kukatiza maeneo ya Corner Bar, Afrika Sana na kuvutwa kisha kuchezewa nyeti na makahaba na kusabisha kuharibika kwa swaumu yake.
Ilielezwa kuwa baada ya kukutwa na kimbembe hicho, ilibidi muumini huyo kukatiza safari yake ya kwenda kuswali msikikini mishale ya saa 2:00 usiku.

Ilisemekana kuwa aliporudi nyumbani alitawadha na kufunga safari nyingine ya msikitini na alipofika kwenye nyumba hiyo ya ibada ndipo akawasimulia waumini wenzake ambao nao walikasirishwa na kitendo hicho hivyo wakapanga kuvamia maeneo yote ya biashara hiyo ili kuwashikisha adabu.
Waandishi wetu, wakiwa kwenye mishemishe zao za kutafuta habari mishale ya saa 5 usiku waliwashuhudia waumini hao wapatao saba wakishuka kwenye Bajaj nyeusi maeneo ya Sinza wakiwa na bakora mikononi kisha kuwavaa machangu hao na kuwatandika.
Wakati wakitekeleza zoezi hilo, jamaa hao walisikia wakiwaambia: “Sisi tupo kwenye swaumu nyiye mnatutega, ala!”
HAWAHESHIMU MWEZI MTUKUFU?
Waumini hao waliongeza kuwa makahaba hao wamekuwa hawaheshimu mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan ndiyo maana wanaendeleza biashara yao hiyo ya aibu.

Kikosi kilichoipeleka Yanga fainali kombe la Kagame 2012

Kikosi kilichoipeleka Yanga fainali mwaka huu; Kutoka kulia waliosimama Nadir Cannavaro, Kevin Yondan, Said Bahanuzi, Ally Barthez, Athumani Chuji na Oscar Joshua. Waliopiga magoti kutoka kulia ni Juma Abdul, David Luhende, Haruna Niyonzima, Godfrey Taita na Hamisi Kiiza.

Kikosi kilichoipeleka Azam fainali Ya Kombe la Kagame 2012

Kikosi kilichoipeleka Azam fainali, kutoka kulia waliosimama ni Said Mourad, Ibrahim Mwaipopo, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, John Bocco na Ramadhan Chombo. Walioinama kutoka kulia ni Jabir Aziz, Salum Abubakar, Ibrahim Shikanda, Kipre Tcheche na Deo Dida.

HIZI NDIO CD/DVD BANDIA TAFADHALI USINUNUE

MKURUNGEZI wa Kampuni ya Udalali ya Msama, Alex Msama akionesha leo jijini Dar es Salaam, CD zenye nyimbo za wasanii walizokamatwa nazo watu 8 baada ya kudurufu kazi hizo za wasanii zenye dhamani ya milioni 25, Watuhumuwa hao wapo katika Kituo cha Polisi Buguruni, Dar es Salaam.
Alex Msama akichambua cd hizo leo katika Kituo cha Polisi Buguruni, Dar es Salaam.
Msama akionesha cd hizo
Msama akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu mkakati wa kuendelea kuwakamata watengenezaji na wauzaji wa CD hizo feki.
Baadhi ya CD zilizokamatwa
Majina ya watu 8 waliokamatwa wakiuza CD hizo. PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA


Na Asha Kigundula

MKURUNGENZI wa Kampuni ya Udalali ya Msama, Alex Msama akishirikiana na Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata watu 8 baada ya kudurufu kazi za wasanii zenye thamani ya sh.milioni 25.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Msama alisema wiki iliyopita walianza zoezi la kukamata watu wanaozidurufu kazi za wasanii mbalimbali ambazo wanauza kwa faida yao.

Msama alisema wakiwa maeneo ya Buguruni sheli, walifanikiwa kuzikamata kazi hizo zikiwa zinauzwa kwa bei ya chini.Alisema kuna baadhi ya kazi hata mtaani hazijaanza kutoka lakini wao wanazo na wakiuza kwa shilingi 1000 kila moja.

"Tumekuta kazi mbalimbali kama vile za muziki wa Injili, Movies, nyimbo za bendi muziki wa ndansi na taarab" alisema Msama.Alisema licha ya kukamata CD hizo za kusikiliza na kuonesha ilifanikiwa kukamata mashine moja ya kudurufu.

Msama alisema katika zoezi hilo waliwakamata watu nane wakiwa wanauza kazi hizo.Waliokamatwa ni Halfan Bakari, Hassan Bakari,Hemed Mohamed, Patrick Peter, Hashraf Rajab, Mkoya Peter na Khamis Athuman.

Msama alisema watuhumiwa hao wote wapo katika kituo cha Polisi Buruguruni kwa ajili ya uchunguzi.

WANAMICHEZO WA TANZANIA KATIKA MICHEZO YA OLIMPIKI 2012

Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe, Naibu Balozi, Mheshimiwa Chabaka Kilumanga, akiwa pamoja na Wanamichezo wa Tanzania wanaoiwakirisha nchi kwenye Michezo ya Olimpiki kwenye kijiji cha Olimpiki.
Balozi, Naibu Balozi, Maofisa wa Kamati ya Olimpiki ya Tanzania na Wenyeji wao wa kujitolea (Volunteers), wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye kijiji cha Olimpiki, London.
Wawakirishi kutoka nchi mbalimbali, wakati wa ufunguzi rasmi wa kuwakaribisha Wanamichezo wote kwenye Kijiji cha Olimpiki, shughuli hiyo ya ukaribishaji wa Wanamichezo hao ulifanya jana tarehe 26 Julai 2012. Wanamichezo hao walipata nafasi ya kukutana na ndugu na jamaa zao ilikuwapa Motisha ya Ushiriki wao kwenye Michezo hiyo.

Kongamano la Tatu la Ushirikiano wa Kimaendeleo na Upunguzaji Umaskini Kati ya China na Afrika

Waziri wa Nchi, Uhusiano na Uratibu, Mhe. Stephen Wassira (Kulia) akimsikiliza kwa makini Mhe. Fan Xiaojian, Waziri, Ofisi Kiongozi ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, inayohusika na masuala ya Maendeleo na Kupunguza Umaskini (Katikati). Kushoto ni Mkalimani wa Waziri huyo.
Washiriki wa Kongamano wakiwa makini kufuatilia mawasilisho na mada mbali mbali zilizokuwa zikitolewa.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akizungumza na mmoja wa washiriki wa Kongamano hilo Li Xin kutoka China.
Naibu Katibu Mtendaji (Uzalishaji) wa Tume ya Mipango, Maduka Kessy (Katikati) akizungumza na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo.
Wadau wa habari nao hawakuwa nyuma katika kunasa matukio ya Kongamano hilo.

WABUNGE WA BUNGE LA TANZANIA WAKIFAIDI FUTARI

Wabunge wakifuturu kwenye ukumbi wa basement, Bungeni Mjini Dodoma Julai 28, 2012. Futari hiyo iliandaliwa na wabunge waislamu na waliofuturu ni wabunge wa dini zote.

MULTICHOICE TANZANIA YAFUTURISHA WANAHABARI KATIKA HAFLA YA KUKARIBISHA MASHINDANO YA OLIMPIKI 2012

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya futari wakati wa kukaribisha michuano ya Olympics iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar.

Barbara Kambogi ametumia fursa hiyo pia kuwataarifu Watanzania kuwa Kampuni yao pendwa ya Multichoice kupitia king'amuzi chao cha DStv inawaletea chaneli maalum itakayokuwa ikuzungumzia maadili ya Uislam katika kipindi hichi cha mfungo wa Ramadan ambacho pamoja na kuwakumbusha wakubwa pia tutawaelimisha watoto kujua nini wanapaswa kufanya ndani ya Uislam.

Amesema gharama za kufunga king'amuzi zimeshushwa na kufikia shilingi 169,000 ambapo atakayejiunganisha atafurahia chaneli nane za Super Sport zitakazokuwa zikonyesha michezo ya Omlympics iliyoanza jijini London kwa muda wa saa 24.
Pia amewakumbusha Watanzania wasisahau kua Kagame Cup iko live kupitia chaneli ya Super Sport 9 ya DStv.
Baadhi ya Waandishi habari kutoka vyombo mbalimbali nchini waliohudhuria hafla hiyo wakijisevia Futari.

Mkurugenzi wa Jambo Concept Benny Kisaka.
Huku wengine wakiendelea kubadilishana mawazo.
Jane john na waandishi wengine wakipata futari
Waandishi wa habari wakienjoy futari iliyoandaliwa na kampuni ya Multichoice Tanzania.
Katikati ni Ankal Issa Michuzi sambamba na Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto (kulia).

Popular Posts