Pages

Showing posts with label Benki - Fedha - Uchumi. Show all posts
Showing posts with label Benki - Fedha - Uchumi. Show all posts

Sunday, July 8, 2012

Twiga Bancorp Yakusanya Maoni Kuhusu Huduma Zake

MKurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Mawasiliano ya Kompyuta wa Benki hiyo, Richard Kombole
---

Na Mwandishi wetu
BENKI ya Twiga Bancorp, imezindua huduma mpya ya kukusanya maoni ya wateja wa ndani na nje ya Tanzania ili kutathimini utoaji huduma wa benki hiyo.

MKurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Mawasiliano ya Kompyuta wa Benki hiyo, Richard Kombole, aliyasema hayo Dar es Salaam jana, alipozungumzia kuzinduliwa kwa huduma hiyo itakayokuwa endelevu.

Alisema wakati huu ambapo benki hiyo imekuwa inajitanua kwa kufungua matawi mbalimbali nchini, kumeonekana ulazima kwa benki kupata maoni ya wananchi kuhusiana na huduma za benki hiyo ili kuongeza ufanisi.

“Hivi juzi tulipata tuzo ya dhahabu ya kimataifa ya utoaji wa huduma bora. Hii inatupa ishara kwamba katika ngazi ya kimataifa, huduma zetu zinakubalika na kuheshimika tumeona kula ulazima wa kukusanya maoni kwa wateja wetu wa ndani,” alisema Kombole.

Alisema ikiwa na ushirikiano na benki zaidi ya 24 zenye mashine za ATM 160 nchi nzima kupitia huduma ya Umoja Switch, Twiga Bancorp imeendelea kujitanua kwa kufungua matawi katika Mikoa ya Arusha na Mwanza na karibuni itafungua tawi jipya mkoani Dodoma.

Alisema katika kuwezesha hilo, benki hiyo itatawanya fomu maalumu za kukusanya maoni ya wateja juu ya utolewaji wa huduma ambayo yatafanyiwa kazi mara moja baada ya kupokelewa.

“Katika hili mteja wetu atakuwa huru kutoa maoni yake katika suala lolote lile linaloihusu benki yetu bila ya kuwa na hofu kwani bila kuwepo kwa wateja benki yetu haiwezi kuwepo,” alisema Mkurugenzi huyo.

Katika hatua nyingine, Benki hiyo ipo katika mchakato wa kuboresha huduma za kibenki kwa kufunga mitambo ya kisasa ya kompyuta ili kuiwezesha kutoa huduma kwa mawasiliano ya kompyuta za benki hiyo na benki nyingine bila kumlazimu mteja kwenda benki.

Akizungumzia mpango huo, Kombole alisema unatarajia kukamilika na kuanza kazi Aprili mwakani ambapo wateja watatakiwa kuwasilisha taarifa zao binafsi ili kuwawezesha kuingizwa katika mfumo huo mpya wa digitali.

“Hii itatuwezesha kuweza pia kuwasiliana kirahisi na wateja wetu litakapojitokeza jambo lolote kama vile kubadilika kwa namba za akaunti au matatizo katika akaunti ya mteja bila mteja kulazimika kuja benki,” alisema Kombole.

Friday, July 6, 2012

JINSI YA KUTUMIA FEDHA KIDOGO KWA MAFANIKIO

Watu wengi husindwa kubana matumizi kutokana na kukosa elimu ya jinsi ya kutumia pesa. Baadhi wamesoma na wengine wanaendelea kusoma masomo mbalimbali yanayohusu pesa na wanahitimu vizuri, lakini wanapokuja katika uhalisia wa maisha wanajikuta wanafeli vibaya kutokana na kutoutambua umuhimu wa kuwa na nidhamu ya pesa.

Msomaji wangu nikupe dondoo kadhaa ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kukusaidia katika kubana matumizi na hatimaye hata kama kipato chako ni kidogo, kikakidhi mahitaji yako muhimu na pia kukawepo na ziada.

Usipendelee kukopa
Kuna watu wengi sana wanaishi kwa kukopa kopa vitu madukani na kwa watu. Mtindo huu ni mbaya sana kwa ukadiriaji wa matumizi, kwani haumtii uchungu mkopaji hadi pale atakapokuwa analipa. Mara nyingi ukopaji huongeza gharama, hivyo inashauriwa ukiwa na 5,000 itumie hiyo, bila kutafuta ziada kwenye deni.

Kuwa na bajeti ndogo
Katika maisha pendelea kupanga bajeti yako kwa mafungu madogo madogo hasa ya wiki. Usivuke mipango hiyo kwa kutumia bajeti ya wiki inayofuata.

Usitembee na pesa nyingi
Baadhi ya watu wanapenda kutembea mitaani huku wakiwa na pesa nyingi mifukoni. Fahamu kuwa kutembea na pesa usizozipangia bajeti utajikuta unashawishiwa kuzitumia bila mpango.

Hata hivyo, unashauriwa kujenga tabia ya kukaa nyumbani na familia yako na kama utatoka siku za mwisho wa wiki basi weka bajeti ya kiasi ambacho utakitumia. Kitendo cha kutoka huku ukiwa na fedha nyingi kwenye pochi lako ni kujishawishi kufanya matanuzi yasio na msingi.

Epuka kununua vitu kwa rejareja!
Unapopata mshaara wako au unapofikiria kuhusu matumizi ya nyumbani kwako pendelea sana kununua vitu kwa jumla ambavyo utavitumia kwa mwezi mzima. Epuka kununua vipimo vidogo vidogo kwani vinaumiza na kuvuruga bajeti.

Pika chakula nyumbani kwako
Watu wengi hasa vijana wanapenda sana kula kwenye migahawa na hotelini. Ulaji huu ni ghali, hivyo inashauriwa kila mtu ajipikie chakula chake nyumbani. Hii itamsaidia kutumia pesa kidogo katika suala la chakula.

Ifundishe familia nidhamu ya pesa
Kuna watu hawawafundishi watoto na wake zao nidhamu ya matumizi ya pesa. Mume/mke asinunue vitu ambavyo familioa haikuzitengea bajeti na asiwepo mtumia hovyo vitu vilivyonunuliwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Akiba na mipango ni muhimu
Familia lazima ijiwekee akiba benki. Utunzaji wa pesa nyumbani si wa salama na mara nyingi hushawishi matumizi. Aidha unapoweka feda benki ziwekee malengo amambo utakuwa ukiyatimiza taratibu si mpaka pesa hizo ziwe nyini.

Kuwa na familia ndogo
Ingawa ni hali halisi ya maisha ya kiafrika kwa familia moja kuwa na watu wengi lakini inashauriwa kwamba, ili kupata ziada ya kipato lazima familia iwe ndogo, vinginevyo mshahara wote unaweza kutumika kwa chakula tu. La kama familia itakuwa ni kubwa basi kila mmoja afanye kazi ili uwepo usaidianaji wa kuendesha familia.

Chanzo : http://www.mbeyayetu.blogspot.com/

Thursday, July 5, 2012

Twiga Bancorp Katika Maonyesho ya Saba Saba 2012

Wafanyakazi wa Benki ya Twiga Bancorp ambao wapo kwaajili ya kutoa huduma katika banda la Benki hiyo viwanbja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu Saba Saba wakilamba picha ya pamoja mbele ya Banda lao linalotoa huduma kamili za Kibenki
Afisa Masoko wa Twiga Bancorp Limited, Adelbert Archerd Tibikunda akiwa amekamatia tuzo ya Century International Gold Quality ERA waliyo ipata Genever kwa huduma bora .
Katika Banda la Twiga Bancorp wateja wanapata fursa ya kuweka fedha zao papo hapo baada ya kufanya mauzo ndani ya Saba Saba. Yanini utembee na fedha nyingi wakati Benki ya twiga ipo nawe pale ulipo.
Fedha katika ATM ni kwa saa 24, siku 7 za wiki, mwezi mzima na siku 360. Huduma hii katika banda la Twiga hafungwi mwaka mzima.
Utoa huduma bora ndio nguzo na ngao ya Twiga Bancorp, pichani ni mteja akiwa na furaha wakati akizungumza na Afisa Mwandamizi Mwendeshaji wa Benki ya Twiga Bancorp Limited, Lydia Matembel, alipotembelea banda lao katika viwanja vya Maonesho Saba Saba.
Afisa wa Benki ya Twiga Bancorp Limited, Ernest Kikwasi, akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo jana juu ya akaunti maalum ya watoto. Twiga Bancorp ni miongoni mwa benki zinazoshiriki katika Maonesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu JK Nyerere barabara ya Kilwa huku wakitoa huduma kamili za kibenki
Mmteja wa Twiga Bancorp akitoka kupata huduma katika banda la Benki hiyo kwa furaha baada ya kufanikiwa kutimiza alichotaka kwa wakati.
Wateja wakipata huduma ya kubadili fedha katika banda la Twiga bancorp.

Tuesday, June 26, 2012

Twiga Bancorp Yashinda Tuzo ya Dhahabu ya Utoaji Huduma Bora Duniani

Hivi karibuni Benki hiyo ilitunukiwa Tuzo ya Dhahabu iliyotolewa na jijini Geneva Uswis, tuzo hiyo inajulikana kama Century International Gold Award (ERA).

Lengo la tuzo hiyo ni kutambua ubora wa huduma zitolewazo kwa wananchi na taassisi au kampuni mbalimbali lengo lokiwa ni kuhamasisha utolewaji wa huduma bora kwa wateja.

Mtendaji Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Hussein Mbululo amesema kwamba Benki yake ilikuwa miongoni mwa Benki 100 zilizoshinda katika tuzo hizo kutoka nchi 47, tuzo hizo ziligawanywa katika makundi saba.

Amesema kujituma miongoni mwa wafanyakazi katika kuwahudumia wateja pamoja na ubunifu ndio siri kubwa ya mafanikio.

Twiga Bancorp ni Benki inayo milikiwa na serikali ya Tanzania kwa asilimia mia moja (100%).
Afisa Mtendaji Mkuu wa Twiga Bancorp, Hussein Mbululo (kulia) akipokea Tuzo ya utoaji bora wa huduma ijulikanayo kama ‘Century International Gold Quality ERA Award’, kutoka kwa Rais na Afisa mtendaji mkuu wa taasisi ya Kimataifa ya Business Initiative Directions, Jose Priento mjini Geneva-Uswisi. Twiga Bancorp imepata tuzo hiyo,kwa utoaji huduma zinazoridhisha kwa wateja, Uongozi bora, Mipango mkakati inayokidhi haja ya wateja kama inavyotambulika katika QC 100 TQM.
CEO wa Twiga Bancorp, Hussein Mbululo akisalimiana na Rais na CEO wa BID, Jose Priento mjini Geneva-Uswisi.
Afisa Mtendaji wa Twiga Bancorp, Hussein Mbululo akiwa na baadhi ya maofisa wa BID mjini geneva kabla ya kuanza utoaji Tuzo.

Popular Posts