Pages

Showing posts with label Bagamoyo. Show all posts
Showing posts with label Bagamoyo. Show all posts

Wednesday, January 2, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE ALIVYOUKARIBISHA MWAKA MPYA 2013 KIJIJINI KWAKE MSOGA NA WANAKIJIJI


Wanakiji wa Msoga wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani wakiangalia fashifashi wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya kijijini hapo. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakichangayika na wanakijiji wenzao wa kijijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, kuukaribisha mwaka mpya kwa fashifashi na ngoma za utamaduni
 ms3:Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kaka yake Mzee Selemani Kikwete kwa  wanakijiji wenzake  wa kijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakati wa sherehe za  kuukaribisha mwaka mpya kwa fashifashi na ngoma za utamaduni
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakipeana mkono wa heri na wanakijiji wenzao wa kijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, wakati wa kuukaribisha mwaka mpya kwa fashifashi na ngoma za kienyeji.Picha na IKULU

Saturday, August 11, 2012

AJALI ILIYOUWA WANAKWAYA 11 WA KENYA MTO WAMI

Baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Makole Mkoa wa Pwani wakiangalia ajali ya gari iliyotokea leo katika eneo la Mto Wami na kusababisha vifo vya watu 11 wote wakiwa raia wa Kenya.
Basi lililokuwa limewabeba raia wa Kenya waliokuwa wakielekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya mikutano ya injili likiwa limetumbukia katika korongo jirani na Mto Wami na kuua watu 11 katika Kijiji cha Makole Mkoa wa Pwani.
Baadhi ya abiria walionusurika wakiwa katika eneo la tukio kabla ya kupata msaada.Picha Zote na Mdau Francis Dande
--
WATU 11 wanaoaminika kuwa raia wa Kenya wamefariki dunia papo hapo, huku wengine saba wakiwa mahututi baada ya mabasi waliyokuwa wakisafiria kutoka Nairobi kwenda Dar es Salaam kupata ajali katika Mto Wami mkoani Pwani.Mbali na vifo hivyo, ajali hiyo pia ilisababisha majeruhi 25 na saba kati yao waliripotiwa kuwa mahututi na walipelekwa katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha kwa matibabu.
Ajali hiyo ilitokea katika Kijiji cha Makole, wilayani Bagamoyo wakati abiria hao ambao ni wanakwaya walipokuwa wakisafiri kutoka Kenya kwenda Dar es Salaam kushiriki katika tamasha la uimbaji.

Ajali hiyo ilitokea jana saa 11 alfajiri ikihusisha magari manne, mawili kati yake yakiwa ni mabasi hayo yakitokea Kenya na malori mawili ya hapa nchini.Tukio hilo pia lilifunga Barabara Kuu ya Chalinze - Segera kwa zaidi ya saa nane hivyo abiria waliokuwa wakisafiri kuelekea na kutoka mikoa ya Kaskazini ikiwamo nchi ya Kenya kwenda na kutoka Dar es Salaam kukwama.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu alisema raia hao wa Kenya ni waumini wa Kikristo na walikuwa wakielekea Dar es Salaam kwenye tamasha la kwaya.

Ajali ilivyotokea
Mangu alisema awali, mabasi hayo yalikuwa yametokea Segera, huku yakiwa yameongozana na moja ilipofika eneo la Makole ghafla liliyumba na kupinduka kisha kutumbukia kwenye korongo.Alisema basi la pili lililokuwa likifuatia nyuma lilipita eneo hilo, lakini baada ya mita 500, dereva alipigiwa simu na mwenzake kuwa amepata ajali na wametumbukia korongoni hivyo ikawalazimu kugeuza kurudi nyuma ili wakawasaidie wenzao.

“Haikuwa rahisi kwa mtu ama gari kuliona haraka hivyo wenzao walipofika hapo nao walipita bila kujua kama kuna gari limeanguka, lakini muda mfupi tu dereva alipigiwa simu na mwenzake akimjulisha kuwa amepata ajali na wametumbukia mtaroni,” alisema Kamanda Mangu.

Alisema baada ya kugeuza na kurudi eneo la ajali, baadhi ya abiria walishuka ili kuwasaidia wenzao na wakati wakiwa kwenye harakati hizo, ghafla lilitokea lori ambalo lililiparamia basi la pili ambalo pia lilitumbukia kwenye korongo.

Kamanda huyo aliongeza kuwa, wakati basi hilo likigongwa, tayari lilikuwa limegeuzwa kuangalia uelekeo wa Chalinze na kwamba baadhi ya abiria walikuwamo ndani.
Alisema baada ya lori hilo kuligonga basi hilo, liliendelea mbele kwa kasi na kugongana uso kwa uso na lori jingine lililokuwa likitokea uelekeo wa Segera, hivyo kufunga barabara hiyo kwa zaidi ya nane.

“Kwa hiyo njia ilikuwa imefungwa kuanzia saa 11:00 alfajiri hadi saa 6:30 mchana baada ya askari wetu kufanikiwa kuyaondoa malori hayo kwenye barabara kuu na sasa (jana) safari zinaendelea kama kawaida,” alisema Mangu.

Tuesday, August 7, 2012

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA SHEKHE MKUU WA KIJIJI CHA MSATA, BAGAMOYO, MKOA WA PWANI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa familia ya Marehemu Mzee Rashid Kazinyingi aliyekuwa Shekhe Mkuu wa kijiji cha Msata, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani Jumatatu Agosti 6, 2012. Marehemu Mzee Kazinyingi, aliyefariki jana akiwa na umri wa miaka 88 pia alikuwa kada wa siku nyingi wa CCM.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika kumuombea dua Marehemu Mzee Rashid Kazinyingi aliyekuwa Shekhe Mkuu wa kijiji cha Msata, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani Jumatatu Agosti 6, 2012. Marehemu Mzee Kazinyingi, aliyefariki jana akiwa na umri wa miaka 88, pia alikuwa kada wa siku nyingi wa CCM.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Mzee Rashid Kazinyingi aliyekuwa Shekhe Mkuu wa kijiji cha Msata, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani Jumatatu Agosti 6, 2012. Marehemu Mzee Kazinyingi, aliyefariki jana akiwa na umri wa miaka 88, pia alikuwa kada wa siku nyingi wa CCM.

(PICHA NA IKULU)

Tuesday, July 31, 2012

Ziara ya Wataalamu wa Chakula wa Oxfam wafanya Ziara ya Mafunzo Bagamoyo na Kuzindua Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuongoza mjadala wa hali halisi ya kilimo na uzalishaji wa chakula Bagamoyo uliofanyika kijiji cha Zinga, Bagamoyo hivi karibuni. Mjadala huu uliratibiwa na Oxfam na kuwahusisha wakulima wanawake kama mpango endelevu wa Oxfam kutambua na kuthamini mchango wa wanawake wakulima kwenye uzalishaji wa chakula.
Mkulima na mshindi wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula kutoka Nigeria, Briskila Jerome akiwahamasisha akina mama wenzake wa kijiji cha Zinga wilaya ya Bagamoyo hivi karibuni, kujiunga na shindano la 'Mama Shujaa wa Chakula' kwa upande wa Tanzania. Shindano hili linaratibiwa na Oxfam kutambua na kuthamini mchango wa wanawake wakulima kwenye uzalishaji wa chakula.
Mkulima kutoka kijiji cha Zinga wilaya ya Bagamoyo, Halima Mwinshehe akitoa hoja yake wakati wa mhadhara ulioandaliwa na Oxfam kuzungumzia kilimo na maswala ya lishe uliofanyika kijini hapo mkoani Pwani hivi karibuni. Mhadhara huu ni moja ya mpango endelevu unaoratibiwa na Oxfam kutambua na kuthamini mchango wa wanawake wakulima kwenye uzalishaji wa chakula.
Wakulima wanawake na wataalamu wa chakula kutoka Oxfam wakiangalia zao la muhogo, wakati walipotembelea moja ya mashamba ya wakulima wanawake katika kijiji cha Zinga wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani hivi karibuni. Wataalamu hawa wa chakula walikuwa nchini kwenye ziara ya mafunzo katika maswala ya lishe na mchango wa wakulima wanawake kwenye uzalishaji wa chakula.
Meneja Kampeni wa Oxfam, David Moriarty (kulia), akigawa fomu za kushiriki shindano la 'Mama Shujaa wa Chakula' kwa kina mama wa kijiji cha Zinga wilaya ya Bagamoyo hivi karibuni mara baada ya kuzindua shindano hilo. Shindano la 'Mama Shujaa wa Chakula' linaratibiwa na Oxfam kutambuwa na kuthamini mchango wa wanawake wakulima kwenye uzalishaji wa chakula.
Wakulima wanawake kutoka vikundi mbalimbali katika kijiji cha Zinga wilaya ya Bagamoyo wakipata futari baada ya kumalizika kwa mjadala wa hali halisi ya kilimo na uzalishaji wa chakula wilayani humo. Mjadala huu uliratibiwa na Oxfam na kuwahusisha wakulima wanawake kama mpango endelevu wa Oxfam kutambua na kuthamini mchango wa wanawake wakulima kwenye uzalishaji wa chakula.Picha Zote na Mdau Badi John

Sunday, July 29, 2012

Rais Dkt.Jakaya Kikwete amjulia hali bibi katika kijiji cha Msoga


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Bibi Antonia Mbagalla (85) katika kijiji cha Msoga, kata ya Chalinze Wilayani Bagamoyo wakati wa mapumziko ya mwisho wa wiki leo (Jumapili). (Picha na Freddy Maro).

Friday, June 29, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGUA HOSTEL BAGAMOYO

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wenyeji wake kwenye sherehe za "Holy Ghost Congregation 20th General Chapter katika hosteli ya Misheni ya Kikatoliki ya Stella Maris aliyoizindua leo Juni 29. 2012 huko Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza kama Mgeni Rasmi kwenye sherehe za "Holy Ghost Congregation 20th General Chapter katika hosteli ya Misheni ya Kikatoliki ya Stella Maris leo Juni 29. 2012 huko Bagamoyo, Mkoa
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita wa Marian Girls Secondary school kwenye kwenye sherehe za "Holy Ghost Congregation 20th General Chapter katika hosteli ya Misheni ya Kikatoliki ya Stella Maris aliyoizindua leo Juni 29. 2012 huko Bagamoyo, Mkoa wa Pwani
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa kwa shangwe alipowasili katika ukumbi wa mikutano kwenye sherehe za "Holy Ghost Congregation 20th General Chapter katika hosteli ya Misheni ya Kikatoliki ya Stella Maris leo Juni 29. 2012 huko Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.

Sunday, June 24, 2012

Rais Jakaya Kikwete Akagua Mradi Wa kufyetua Matofali yanayotengenezwa kwa mashine za Hydrafoam Bagamoyo

Rais Jakaya Kikwete Akikagua Mradi wa kufyetua Matofali yanayotengenezwa kwa mashine za Hydrafoam kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari ya Mboga,Wilayani Bagamoyo,Mashine hiyo yenye thamani ya shilingi Millioni Sabini 70m/-imetolewa na Rais Jakaya Kikwete kama Msaada kwa vijana Waliounda Ushirika ili kuboresha maisha yao kwa kufanya miradi mbalimbali ya Ujenzi na Uzalishaji.Picha na Freddy Maro-IKULU

Popular Posts