Pages

Showing posts with label Lindi. Show all posts
Showing posts with label Lindi. Show all posts

Friday, January 4, 2013

Hoja ya Murtaza Mangungu, Mbunge wa Kilwa Kaskazini Kuhusu Gesi Asilia

Sekta ya gesi na mafuta ni moja kati ya sekta kubwa na ngeni kwa kiasi fulani hapa nchini. 

Kwa kipindi cha miaka mingi na haswa miaka ya sabini na themanini Serikali ya awamu ya kwanza ilifanya kazi kubwa ya uwekezaji katika utafiti wa mafuta na gesi nchini  lakini bila ya mafanikio ya uwekezaji.

Hii inaweza kuwa ilichangiwa sana na siasa zilizokuwapo kwa wakati ule kwa maana ya umagharibi na umashariki na pengine imani ya wawekezaji kutokana na msimamo tuliokuwa nao kama nchi  katika suala la ukombozi wa bara la afrika dhidi ya ukoloni pia uduni wa hali ya teknologia ya wakati ule na ukweli kwamba eneo letu la nchi za mashariki mwa Afrika ilijulikana kuwa ni ukanda wa gesi asilia tu  na enzi zile gesi asilia ilikuwa haina thamani kuliko mafuta. 

Kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni, nchi yetu imefanikiwa sana kuwavuta wawekezaji katika sekta na nyanja tofauti  sana ikiwamo katika gesi na utafiti wa mafuta. Hii ni nafasi nzuri tuliyoikosa kwa miaka mingi kiasi cha kutuweka nyuma kimaendeleo ukilinganisha na nchi nyingi za afrika na dunia ya tatu.

Lakini sasa kiasi kikubwa tumeanza kuona manufaa ya uwekezaji ule japo kwa uchache na changamoto nyingi ndani yake.

Tulianza mwaka 2012 na kumaliza na mfululizo wa matukio ya aina tofauti kwa waandishi kuandika makala na habari nyingi kuhusu shughuli na sekta nzima ya gesi nchini, na mara ya mwisho kabisa kufuatia maandamano ya wanachi wa Mtwara ambao walitokea katika vyama  tofauti.

Sikuona tatizo la waandamanaji wale pamoja na ujumbe ulitolewa bali baadhi ya ujumbe  unaonyesha zipo tafsiri nyingi zaidi ya madai ya mahitajio ya manufaa ya mapato katika uwekezaji wa gesi na bomba la gesi.

Nilipata wasisiwasi mkubwa sana baada ya kuona wanaojua ukweli wa jinsi mambo yalivyo na wale wasiojua kuamua kwa dhati kabisa kuuposha umma wa watanzania  na dunia kwa ujumla.

Niliwahi kujifunza kuwa ukweli utabaki kuwa ukweli na inastahili tuseme ukweli hata kama inauma kiasi gani kwa maana hakutakuwa na dhambi wala madhara zaidi ya ukweli huo. Pia uongo inatakiwa uwekwe mahali ambapo kila mmoja utauona. 

Madai ya wale wanaojiita waandamanaji ni kuwa gesi isitoke hadi pale Serikali itakaposema wananchi watanufaikaje  lakini  pamoja na mambo yote ambayo  wamesema na kuungwa mkono naomba tuambizane kwa kuulizana. Ni lini ambapo Serikali au wawekezaji wamesema kuwa bomba litafanya kazi ya kutoa gesi Mtwara kwenda Dar es salaam pekee? Nielewavyo mie leo hii kuwa bomba linaweza pia kutumika kutoa gesi Dar es salaam kwenda Mtwara pale ambapo patakuwa na mahitaji au matumizi ya ziada katika viwanda.

Msumbiji ambao wamegundua gasi nyingi zaidi yetu wanaweza kutumia bomba la gesi kupeleka katika masoko ya Kenya,Uganda sudan Rwanda Burundi na kadhalika au nchi kama Kenya ambazo nazo zimegundua gesi wanaweza kutumia kupitisha gesi kwenda Afrika ya kusini au kwingineko.Yote haya itatupa mapato makubwa sana kama vile nchi ya Ukraine inavyonufaika kupitisha bomba la gesi inayotoka Russia kwenda Ulaya magharibi.

Inaweza  kuwa kweli  Rais alitoa ahadi kuwa lazima gesi iwanufaishe watu wa mtwara kwa kuweka viwanda mtwara. Hivi ni kweli hatufahamu kuwa upo mradi wa ujenzi wa kiwanda cha saruji ,kiwanda cha uyayushaji chuma(iron smelter) na vinginevyo? 

Siamini sana kuwa itakua ni kazi rahisi kuhamisha viwanda vya chuma, saruji, chupa, rangi na mengineyo ambayo kwa sasa vipo Dar es Salaam kutokana na uwekezaji uliofanyika kwa zaidi ya miaka 40 au zaidi kuvihamisha na kuvipeleka mtwara? Ni kweli kuwa bidhaa zizalishwazo hivi sasa wananchi wa mtwara na lindi hawazitumii?

Nimekuwa nikiona magari  mengi sana kutoka Dar es salaam kwenda Lindi  na Mtwara na bidhaa za aina tofauti  ,ambazo zinazalishwa kutokana na umeme unatokana na gesi kutoka songo songo Kilwa. Hivi manufaa tuyasemayo ni ya namna ipi ?

Katika uwekezaji wa gesi na mafuta kampuni huhitaji uwekezaji mkubwa sana ambao mara zote huhitaji kuuza hisa katika masoko ya hisa au kutegemea makampuni mengineyo kujiingiza kushiriki kuwekeza(farm in). Je, kwa maandamano haya hatutaishia kulipa fidia kwa wawekezaji baada ya kuharibu mazingira mazuri ya ufanyaji kazi?

Wakati haya yakiendelea kufanyika , tayari yapo makubaliano kadhaa ambayo yamewekwa baina ya Serikali na makampuni ya uwekezaji kwa ajili ya kuendeleza gesi iliyopatikana . Mfano mzuri ni  eneo la Rushungi Kilwa kuna kampuni kubwa kutoka Norway na mshirika wake kutoka Marekani wanafanya uchunguzi wa uwezekano wa  kujenga LNG terminal ili kuisindika gesi hiyo na sehemu mbali mbali za mwambao wa Mkoa wa Lindi na Mtwara zinafanyiwa uchunguzi wa aina huo.

Uwekezaji huu umechelewa sana kufanyika haswa ukizingatia kuwa gharama zinapanda siku hadi siku. Dunia haikusubiri na uchumi unazidi kuwa wa aina tofauti na siku za nyuma. Imani ya wawekezaji ikipotea dhidi yetu tutatumia miaka mingapi kuirejesha?

Pia ikumbukwe kuwa Serikali imewekeza pesa nyingi sana kwa kusomesha na kulipa mishahara watumishi wa sekta husika lakini pia katika uwekezaji kwa sekta hii.

Inawezekana kabisa kuwa bado manufaa hayajaonekana moja kwa moja , lakini tujiulize kuwa gharama za chakula zilizopanda hivi sasa Lindi na Mtwara zimesababishwa na nini. Pia haitoshi kuwa thamani ya ardhi imepanda mara ngapi na kuwanufaisha watu wa mikoa hii?

Hivi tangu Serikali iweke chuo cha VETA  wanafunzi wangapi kutoka Lindi na Mtwara wamekubali kujianadikisha katika masomo ili kuja kupata ajira na kushiri katika sekta gesi.

Tusitarajie kuna siku zitagawiwa pesa kwa mafungu kutoka katika mapato yatokanayo na gesi na wala hakuna nchi duniani imewahi kufanya hivyo Manufaa ya pekee ambayo wananchi wa Mtwara na Lindi na Tanzania kwa ujumla  wanaweza kuyapata ni kama ifuatavyo.

  1. Kilimo:  gesi asilia itakuza  sekta nyingine kwa maana ya kilimo.  Gesi pia inaweza kukuza kilimo kwa kuinua sekta ya kilimo kwa maana ya uzalisha wa mbolea na viatilifu vingine kama sulphur ambayo inatumika sana kuthibiti ubwiri unga ambayo inasumbua sana mikorosho.Pia wananchi wataongeza kipato kutokana na kuwa na uzalisha mkubwa katika kilimo.
  2. Umeme:  gharama za umeme zinaweza kushuka kwa kiasi kikubwa sana haswa ukizingatia kuwa kwa sasa bado gharama ziko juu.Kama ni mfano mzuri,  hivi sasa Tanesco imeshusha gharama za uunganishaji umeme ili kuvutia wateja wengi kupata huduma hiyo na kuongeza uzalishaji lakini pia kushusha gharama za uzalishaji kwa ujumla ambapo itachangia kushusha gharama za maisha na kukabiliana na mfumuko wa bei.
  3. Elimu : gesi itasaidia kukuza elimu nchini haswa maeneo ya Lindi na Mtwara kwa maana ichangie  kuboresha, lakini pia kuinua elimu kwa watanzania wengi zaidi ili kuweza kunufaisha katika sekta ya gesi na nyinginezo mtambuka 
  4. Ufugaji:  itasaidia katika ufugaji haswa ikizingatiwa sekta hii inahitaji nyama, maziwa na mayai kwa kiasi kikubwa hivyo wananchi wakishikishwa vema itasaidia sana kukuza kipato chao na kuinua uchumi wao na nchi kwa ujumla. 
  5. Viwanda:  uanzishwaji wa viwanda vya mazao ya gesi kwa maana ya petrochemical industries, hii yote itachangia kukuza ajira na mapato kwa Serikali Kuu hadi kufikia ngazi Serikali za vijiji kwa ujumla 
  6. Mazingira:  gesi itasaidia kuhifadhi mazingira kwani matumizi yake yatapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya kuni na mkaa lakini pia inaweza kuwa mbadala wa petroli na dieseli katika magari na mitambo. Hakuna atakae kataa kuwa itasaidia pia kupunguza emission na kuokoa pesa nyingi za kigeni ambazo zingeweza kufanya shghuli nyingine za kiuchumi nchini.
  7. Uwekezaji:  utalenga kutoa ajira kwa watanzania haswa vijana, lakini watanzania pia wajue haya hayatapatikana kama hawatashiriki kusoma na kupata mafunzo ya kutosha ili kuweza kupata ajira hizo. Tunapozungumzia elimu haihusu sana kupata degree au diploma, hata ngazi ya cheti tu , kwa kozi za kawaida za ufundi kama magari,umeme ,uchomeaji n.k

Serikali kwa kushirikiana na taasisi za kama TPDC, TANESCO, NDC, NARCO,VETA, TPA na wengineo washirikiane kujenga uwezo kwa watanzania kushiriki kwenye sekta na si kutegemea kuagiza kila kitu kutoka nje na wageni wakashika kazi zote kwa kigezo kuwa hatujafikia viwango vya kimataifa kufanya kazi hizo. Changamoto ya makampuni ya uwekezaji (Mult national Companies) kutumia viwango kama ni kigezo cha kuyanyima kazi makampuni yetu ya ndani haswa ya wazawa iangaliwe kwa jicho pana zaidi

Katika maelezo ya Rais ni kuwa tuanzishe mfuko wa kuhifadhi pesa mapato yatokanayo na gesi (gas fund), naona tukubaliane na hili ila maoni yangu ni vema kuanzisha sovereign development fund ambayo mapato yatumike katika uwekezaji tu na si kwa ajili ya kula na kulipa mishahara au matumizi ya kawaida.

Nchi kama Trinidad & Tobago na Thailand leo zinanufaika katika viwanda vya kemikali (petrochemical industries) ambapo hata bandari na sekta nyinginezo maana kuna multiplier effect inayotokana na uwekezaji katika sekta hii. Hivyo hapana budi Bandari ya Mtwara na Kilwa nazo zikapanuliwa ili kuweza kuinua uchumi wa mikoa ya kusini.
Kwa kuzingatia haya na kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi na wawakilishi wao kwa ujumla , itasaidia sana kuondoa dhana iliyojengeka sasa na kuwa hali ya uadui ambao hauna tija kwa ustawi wa nchi yetu.

Tumekuwa na mgogoro na nchi ya Malawi kwa muda sasa, chanzo kikubwa inahisiwa ni rasilimali hizi za gesi na mafuta. Huku hili likiendelea kumekuwa na hisia za kujitunga mgogoro mwingine baina ya Tanzania na Congo. Wakati tunayatafakari haya tumeanza kuweka migogoro ndani ya nchi, ni kweli haya ndio tunayokusudia ?

Naamini kila anayeshinikiza haya yatendeke , wanajua vizuri zaidi ya hivyo. Ni kheri kuwa makini kwa matendo na matamshi yetu kwani ipo siku tutawajibika nayo. Amani ,upendo na utulivu una thamani kubwa kuliko gesi na madini. “Kama hujui unakokwenda, huwezi kupotea njia.’’

Murtaza Mangungu(MB)
Kilwa Kaskazini na mjumbe wa POAC

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2H2uh71vF

Tuesday, August 14, 2012

VODACOM TANZANIA RAMADHAN CARE & SHARE MKOANI LINDI

Baadhi ya watoto wa shule ya Msingi ya Nyangao iliyopo Lindi Vijijini wakiwa wamebeba mfuko wa sembe mara baada ya kukabidhiwa msaada huo na Mkuu wa Kitengo cha odacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule hayupo pichani ikiwa ni mwendelezo wa kutoa misaada na kufuturisha watoto yatima na wasiona katika mikoa mbalimbali hapa nchini kwa kupitia kampeni ya Ramadhan Care and Share wakati huu wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Kaimu Afisa elimu wa shule za msingi Wilaya ya Lindi Bi.Mnyangala Kaguta akipokea msaada wa mbuzi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule kwa niaba ya watoto walemavu wasiona na wanaoona wa shule ya Nyangao iliyopo Lindi Vijijini Mkoani Lindi,wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali inayoendeshwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan
Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi mbuzi wawili Bi.Rafael Mohamed kwa niaba ya wakina mama wenzake ambao ni walemavu wasioona wa kijiji cha Mnamba kata ya Nyangao Mkoani Lindi,wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali inayoendeshwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,anaeshuhudia wapili toka kushoto ni Meneja wa Vodacom Foundation Bi.Grace Lyon.
Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi ndoo ya mafuta ya kula John Swai kwa niaba ya watoto wenzake ambao ni walemavu wasiona na wanaoona wa shule ya Nyangao iliyopo Lindi Vijijini Mkoani humo,wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali inayoendeshwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,alieshikilia mbuzi kushoto ni Meneja wa Vodacom Foundation Bi.Grace Lyon.
Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi katoni ya chumvi Mtoto mwenye ulemavu wa kutokuona Husna Rajabu, kwa niaba ya watoto wenzake ambao ni walemavu wasiona na wanaoona wa shule ya Nyangao iliyopo Lindi Vijijini Mkoani Lindi,wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali inayoendeshwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,alieshikilia mbuzi kushoto ni Meneja wa Vodacom Foundation Bi.Grace Lyon.
Meneja wa Vodacom Foundation Bi.Grace Lyon akisalimiana na baadhi ya wakina mama ambao ni walemavu wasioona wa kijiji cha Mnamba kata ya Nyangao Mkoani Lindi,wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali inayoendeshwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Baadhi ya watoto ambao ni walemavu wasioona wakifuturu wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali inayoendeshwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Meneja Mahusiano ya umma wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu akiteta jambo na baadhi ya watoto ambao ni walemavu wasioona wa shule ya msingi Nyangao Mkoani Lindi,wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa shuleni hapo kwa ajili ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali inayoendeshwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Tuesday, July 31, 2012

Rais Jakaya Kikwete Ahudhuria Mazishi ya Shemeji Yake mjini Lindi

Rais Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya shemeji yake, Marehemu Amani Kinyozi, katika makaburi ya Mitandi mjini Lindi leo Julai 30, 2012
Rais Kikwete akishiriki katika swala ya kumuombea marehemu mjini Lindi leo Julai 30, 2012.Picha na IKULU
--
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo Julai 30, 2012 amehudhuria mazishi ya shemeji yake, Marehemu Amani Kinyozi (45), aliyefariki Jumamosi iliyopita jijini Dar es salaam, na kuzikwa katika makaburi ya Mitandi mjini Lindi.

Tuesday, July 3, 2012

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Abdallah Ulega awataka Wananchi wa kilwa kushiriki shughuli za maendeleo

...Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi,Abdallah
Ulega akihutubia wananchi wa Tarafa ya Kipatimu wilayani humo.
Wananchi wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi wametakiwa kushiriki ipasavyo katika vikao mbalimbali vya serikali za mitaa ili kurahisisha Upangaji wa Mipango ya Maendeleo kufuatia hatua ya serikali kurudisha madaraka kwa ushirikiswaji kutoka ngazi ya vijiji hadi Taifa

Akihutubia katika kilele cha maadhimisho ya nane ya siku ya Serikali za mitaa yaliyofanyika kiwilaya katika kijiji cha Mtongo Kimwaga Kata ya kipatimu wilayani humo,Mkuu wa wilaya ya Kilwa ,Bw Abdallah Ulega alieleza kuwa kushiriki vema kutasaidia wilaya hiyo kupanga mipango yake shirikishi na pia jamii itatumia ipasavyo haki ya msingi kufanikisha kujenga Demokrasia.

Awali kaimu mkugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw Peter Malekela akimkaribisha mkuu wa wilaya hiyo kuhutubia hadhara hiyo baada ya kuweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho alieleza changamoto kubwa wilayani humo ipo kwa wananchi kutoshiriki kwa asilimia kubwa katika vikao mbalimbali hali inayotoa ugumu katika utekelezaji wa maamuzi yaliyoazimiwa.

Serikali za mitaa ni chombo kilichoundwa na kuwa na mamlaka ya kisheria huundwa na halmashauri za vijiji wilaya,Miji na mamlaka ya miji midogo Huadhimishwa kila tarehe 01 ya mwezi wa saba ambapo pia kunawepo Burudani mbalimbali ikiwa pamoja na kutembelea na kufungua miradi mbali mbali ya jamii.

Monday, June 25, 2012

WAZIRI MKUU KATIKA SHUGULI MBALIMBALI

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia (kulia) na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lymo kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 25, 2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua zabibu wakati alipotembelea shamba la Tendaji Agro lililopo katika kijiji cha Chikopelo wilayani Bahi, Dodoma juni 24, 2012
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na Mbunge wa Lindi Mjini , Salum Baluany kwnye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 25,2012. Kulia ni Mtoto wa Waziri Mkuu, George Bush.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Monday, June 11, 2012

MWENGE WA UHURU WATINGA MKOA WA LINDI


Mkuu wa wilaya ya Lindi mjini, Mhe, Dkt Hamid, akikabidhi Risala ya Utii kwa kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Capt. Honest Erenest katika viwanja vya shule ya msingi Rahaleo iliopo Lindi Mjini.Jana tarehe 10-06-2012.

Saturday, June 9, 2012

shule za kata wilayani Kilwa zimeanza kuwekeza katika maabara

Wanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari ya Kinjumbi wilayani Kilwa wakisoma kemia kwa vitendo katika maabara ya shule.Shule hii ipo rtakribani kilometa 70 toka Kilwa Masoko
Hivi ndivyo tukichanganya inatokea kwenye 'test tube'
Hii ni result ya huu mchanganyiko.Mananisikia?Mwanafunzi akiwaelekeza wanafunzi wenzake juu ya mchanganyiko alioufanya kwenye 'test tube' na reaction iliyotokea.
Majaribio ya maabara yakiendelea.wanafunzi hawa ni wa kidato cha nne na wanategemea kufanya mtihani wao wa Chemistry,Biology na Physics kwa vitendo.
Embu leye hiyo test tube.ingawa hatuna groves na miwani kwaajili ya kujikinga kama reaction mbaya itatokea.
tunaendelea hivi


Unaona inavyokuwa?Tunachanganya hivi







Chumba cha maabara ya shule ya sekondari ya Kinjumbi

Friday, June 8, 2012

John Mnyika Awapiga Msasa Wana Newala na Nanyumbu Juu Ya Uwajibikaji wa Serikali Kwa Wananchi,Elimu ya Katiba Mpya





Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)John Mnyika Akihutubia na akisikiliza maswali na kutoa somo la kudai uwajibikaji wa serikali kwa wananchi, elimu ya katiba mpya na M4C, kwa wanakijiji katika maeneo ya wilaya tofauti za Newala na Nanyumbu
Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)John Mnyika Akimsikilzia Katibu wa Tawi wa CUF, Bi. Zaituni baada ya kutoa somo la kudai uwajibikaji wa serikali kwa wananchi, elimu ya katiba mpya na M4C, kwa wanakijiji katika maeneo ya wilaya tofauti za Newala na Nanyumbu.Picha na Habari na Kurugenzi Ya Habari-CHADEMA

Popular Posts