Pages

Showing posts with label Wizara ya Maliasili na Utalii. Show all posts
Showing posts with label Wizara ya Maliasili na Utalii. Show all posts

Tuesday, August 14, 2012

WAFANYAKAZI 9 WATIMULIWA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uamuzi wa Serikali wa kuwafukuza kazi watumishi watatu wa wizara hiyo kutoka na ukiukaji wa sheria na utekelezaji wa majukumu yao ya kazi kufuatia sakata la usafirishaji wa wanyama pori kupitia Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kwenda Quatar.Picha na Anna Nkinda wa MAELEZO
-----
Wizara ya Maliasili na Utalii imechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wake tisa (9) kufuatia kadhia ya utoroshaji wa Wanyamapori Hai katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na masuala mengine yanayohusu Wanyamapori. Watumishi hao wamechukuliwa hatua husika kufuatia kukamilika kwa uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zikiwakabili.

(1) Waliofukuzwa kazi kutokana na ukiukaji wa sheria katika utekelezaji wa majukumu yao ni:

- Bw. Obeid F. Mbangwa - Mkurugenzi wa Wanyamapori. Wakati wa kadhia hiyo alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Matumizi ya Wanyamapori,

- Bw. Simon Charles Gwera – Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha,

- Bw Frank Mremi - Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha.

(2) Aliyeondolewa Cheo cha Madaraka kutokana na kutochukua hatua kamilifu za ulinzi ambazo zingeweza kuzuia kutokea kwa tukio la utoroshwaji wa wanyama ni:

- Bw. Bonaventura M.C. Midala – Mkurugenzi Msaidizi, Undelezaji Wanyamapori. Wakati wa tukio alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Kuzuia Ujangili.

(3) Wafuatao ni Maafisa Wanyamapori Daraja la II waliotekeleza maelekezo ya Wakuu wao wa kazi yaliyo kinyume cha Sheria ambao wamepewa Onyo Kali la Maandishi:

- Bibi Martha P. Msemo - Afisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha.

- Bibi Anthonia Anthony – Afisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Dar es Salaam.

(4) Bw. Silvanus Atete Okudo ni Mkuu wa Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha aliyeshindwa kufuatilia kupata maelekezo ya Mkurungezi wa Wanyamapori kuhusu mtumishi wake aliyekiuka Sheria katika utoaji wa vibali. Aidha, alishindwa kupeleka kwa Katibu Mkuu taarifa kuhusu mtumishi huyo ili achukuliwe hatua za nidhamu.

- Silvanus Atete Okudo – amepewa Onyo Kali la Maandishi.

(5) Wafuatao ni Maafisa ambao uchunguzi dhidi yao unaendelea:

- Bw. Mohamed Madehele – Ofisi ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori

- Bibi Mariam Nyallu – Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha – Arusha.

Wahusika wengine katika kadhia hiyo wasiokuwa waajiriwa wa Wizara ya Maliasili na Utalii watachukiliwa hatua na mamlaka nyingine husika.

[MWISHO]

Mhe. Khamis Suedi Kagasheki

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII

13 Agosti 2012

Tuesday, August 7, 2012

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Atembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii Kwenye Maonyesho ya Nanenane Mkoani Dodoma 2012

Mhe. Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikaribishwa na Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu baada ya kuwasili katika banda la Wizara katika maonyesho ya Wakulima ya Nanenane kitaifa yanayoendelea mkoani, Dodoma. Wazir Mkuu Mhe. Mizengo Pinda atembelea maonyesho ya Nyuki katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii , katika viwanja vya Nzuguni, Dodoma.
Mhe. Waziri MKuu akitoa maelezo baada ya kusikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu anaendesha mafunzo maalam ya ufugaji nyuki yanaqyotolewa ndani ya banda la Wizara ya Maliasili na Utalii.
Mhe. Waziri MKuu akiangalia sampuli za asali kutoka kwa moja ya wadau wa bidhaa za Nyuki wanaoshiriki maonyesho ya nane nane ndani ya banda la wizara ya Maliasili na Utalii.
Mhe. Waziri Mkuu akiangalia mzinga wa nyuki wasiouma katika shamba darasa la ufugaji nyuki

Wednesday, July 18, 2012

Ministry of Natural Resources and Tourism Ambassador Khamis Kagasheki at The Seattle Sounders FC in USA

Ministry Kagasheki, Dk Aloyce Nzuki and Mussa Ibahim walk across the pitch at Century Link Field in Seattle, Washington with the massive Tanzania advertising in the background
The Delegation from the Ministry of Natural Resources and Tourism & The Seattle Sounders FC meet at the Sounders Training Facility Veronica Ufunguo - Tourism Manager - Ngorongoro Shaun Angell - Account Executive, Seattle Sounders FC/Seattle SeahawksDr. Aloyce K. Nzuki - Managing Director Tanzania Tourism BoardTaylor Graham - Manager of Business Operations, Seattle Sounders FCLuke Grothkopp - Director, Partnership Development, Seattle Sounders FC/Seattle SeahawksHonorable Ambassador Khamis Kagasheki - Minister for Natural Resources and TourismRon Jenkins - Vice President, Corporate Sponsorships - Seattle Sounders FC / Seattle Seahawks Egidius Mweyunge - Assistant to Minister KagashekiIbrahim Mussa - Director of Tourism - Ministry of Natural Resources and Tourism Johnson Manase - Tourism Manager - TANAPADeo Malogo - Tourism Manager
--
Na Mwandishi Wetu, Renton, Washington.

Timu ya Seattle Sounders FC imetangaza ushirikiano na Tanzania, nchi ambayo ni nchi kubwa kabisa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.Ushirikiano huo ulitiwa saini na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Balozi Hamis Kagasheki (Mbunge) na Mmiliki wa timu ya Seattle Sounders Joe Roth katika hafla fupi iliyofanyika jana mjini Renton.


Mbali ya Waziri Kagasheki, wengine walioshuhudia kutiwa saini kwa ushirikiano huo ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mheshimiwa Balozi Mwanaidi S. Maajar, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania Dr. Aloyce Nzuki na maofisa wengine kutoka Wizara ya Utalii, Ubalozini na maofisa wa Seattle Sounders FC.
Mambo muhimu katika ushirikiano huo ni uwekwaji wa alama za vivutio vya utalii vya Tanzania katika maeneo mbali mbali kama CenturyLink Field na Starfire Sports Complex, uwanja wa mazoezi wa Sounders FC uliopo eneo la Tukwila.

Vivutio mbali mbali vya Utalii wa Tanzania vitawekwa katika maeneo hayo kama picha za Mlima Kilimanjaro, Hifadhi za Serengeti, Ngorongoro Crater na Zanzibar.

"Ushirikiano wetu na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) utasaidia kutangaza vivutio vya Utalii vya Tanzania nje ya mipaka yake kwani kuna vivutio vya ajabu mno na kuleta unafuu kwa watalii ,” alisema Mmiliki wa timu ya Sounders FC, Joe Roth. Na kuongeza kuwa ushirikiano huo utatoa nafasi muhimu kwa soko la Utalii wa Tanzania nchi ya mipaka yake.


Waziri Kagasheki mbali ya kupongeza kwa kufanikisha hatua hiyo muhimu katika sekta ya Utalii nchini alisema kuwa ushirikiano huo utatoa fursa nyingi kwa Watanzania na Wamerekani kwani utahimarisha juhudi za Wizara ya Utalii katika kukuza soko la Utalii wa Kimataifa na wa Ndani.

Mheshimiwa Kagasheki pia alisema kuwa ushirikiano huo utatoa fursa za kibiashara kwa nchi zote mbili na kuongeza uwekezaji.

Sunday, July 8, 2012

Rais Jakaya Kikwete Atembelea Maonyesho ya Sabasaba 2012

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya bidhaa zitokanazo na Wannyamapori wakati alipotembelea banda la Wizara ya Mali asili na utalii katika viwanja vya maonyesho vya Sabasaba jijini Dar es Salaam jana
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya bidhaa zitokanazo na Wannyamapori wakati alipotembelea banda la Wizara ya Mali asili na utalii katika viwanja vya maonyesho vya Sabasaba jijini Dar es Salaam jana
Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa PPF Bwana William Eriyo akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mradi wa uwekezeaji wa hoteli ya kisasa iliyojengwa na shirika la PPF mjini Mwanza wakati Rais alipotembelea banda la PPF katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam jana.Picha na Freddy Maro-IKULU

Popular Posts