Pages

Monday, January 7, 2013

Vodacom Tanzania yasaidia Sober House Pemba


Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akikabidhi ndoo ya mafuta kwa Mratibu wa Vituo vya kusaidia watumiaji wa dawa za kulevya kuachana na matumizi ya dawa hizo (Sober House) za Wete Pemba Abdulwaheed Said kwa niaba ya Vodacom Foundation. Wanaoshuhudia ni Menejja wa Vodacom Foundation Grace Lyon Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim(wa kwanza kushoto). Hafla hiyo ilifanyika wkishoni mwa wiki Chakechake Pemba.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akikabidhi dumu la dawa ya kusafishia choo kwa Meneja wa kituo cha kutibu kuachana na matumizi ya dawa za kulevya (Sober House) cha Mjini Chake Chake Kisiwani Pemba Mohammed Kassim. Wanaoshuhudia ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim(wa kwanza kulia) na Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon(wa pili kushoto). Vodacom Foundation imevipatia vituo vinne vya Wete na Chakechake vyakula na vitu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya program yake ya Pamoja na Vodacom ya kusaidia watu wenye mahitaji.
Mratibu wa vituo vya kutibu watumiaji wa dawa za kulevya kuacha kutumia dawa hizo (Sober House) vya Wete Pemba Abdulwaheed Said akishukuru kwa msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kutoka Vodacom Foundation vilivtolewa kwa Sober House nne za Kisiwani Pemba. Kutoka Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa,Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon. Meneja wa Sober Hosue ya Chakechake Mohammed Kassim na Meneja wa Mahusiano ya Nje Salum Mwalim.Mkabidhiano hayo yamefanyika kwmishoni mwa wiki Mjini Chakecahke 04.
  Meneja wa Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim(wa kwanza kulia) akishiriki chakula cha mchana na mateja wanaopata tiba ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya katika Sober House ya Chakechake Pemba. Chakula hicho kiliandaliwa na Vodacom Foundation.
Sehemu ya watu wanaopata tiba ya kuachana na matumiz ya dawa za kulevya katika Sober House za Wete na Chakecahke Kisiwani Pemba wakimsikiza kwa makini Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon(hayupo pichani)akizungumza nao wakati Vodacom Foundation ilipofika kituoni hapo kusaidia vyakula na vitu mbalimbali mwishoni mwa wiki. Hafla hiyo ilihudhuriwa pia Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa 06.
--
Vodacom mwishoni mwa wiki imetembea vituo vya kusaidia watumiaji wa dawa za kulevya kuachana na dawa hizo - Sober House Kisiwani Pemba ziara iliyomjumuisha Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa.

Ziara hiyo ililenga kutoa misaada ya kibinadamu ikiwemo vyakula na vitu vingine vya matumizi ya ndani ikwemo dawa za kusafishia vyoo, sabuni katika kwa Sober House nne zilizopo Chakechake na Wete.
Akizungumza katika Sober House ya Chakechake Waziri Profesa Mbarawa aliwataka wateja wa vituo hivyo ambao wengi wao ni vijana kuhakikisha matumaini waliyoyaonyesha ya kutaka kuachana na matumzi ya dawa za kulevya hayapotei.

Waziri Prof Mbarawa amesema uamuzi waliouchukua wa kutaka kuachana na matumiz ya dawa za kulevya ni wa msingi na unawawezesha kurudi katika maisha yao ya kawaida sanjari na kutimiza ndoto za maisha walizokuwa nazo hapo kabla ya kujitumbukiza katika matumizi ya adwa za kuelvya na kuwapotezea dira ya maisha "Nimejulishwa kwamba kuingia katika nyumba hii ni lazima mtumiaji mwenyewe ukubali kuwa yupo tayari kuachana na dawa kulevya hilo ni jambo jema na linalonyesha kwamba mnayo matumaini ya kurudi katika maisha ya kawaida yasiyohusisha matumizi ya dawa za kulevya na aina nyengine ya vilevi."Alisema Prof. Mbarawa "Mnayo mifano ya mafanikio ya wale ambao wameshapitia program hizi na wamefanikiwa na hata nyie hapa mpo ambao tayari mna siku nyingi za usafi bila kutumia dawa ama kilevi cha aina yoyote hivyo ni rai yangu kwenu kuendelea kuamini katika matumaini mliyo nayo."Aliongeza Profesa Mbarawa Akizungumzia juhudi za serikali katika kupambana na biashara ya dawa za kulevya nchini Waziri huyo amesema serikali imekuwa ikifanya kila juhudi katika kukomesha biashara hiyo.

"Serikali na hata Rais Kikwete(Jakaya)binafsi amekuwa akifanya juhudi kubwa katika kukomesha biashara hii na amekuwa akitukalisha chini mawaziri na kutuelezea mikakati mbalimbali ikiwemo kutuonesha mikanda ya video inayoonyesha athari za dawa za kulevya ambazo zinasikitisha mno."Alisema Waziri Prof Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesema changamoto kubwa inayokabili vita hii ni namna ya kukamalisha udhibiti dhidi ya mhalifu au washukiwa wanaojihusisha na biashara hizi haramu ili kuwafikisha mahakamani na hatimae sheria kuchukua mkondo wake lakini hata hivyo juhudi zipo na kuwaomba wateja hao wanaopata nafuu kutoa ushirikiano huku akkiwapongeza Vodacom.

"Nawapongeza sana Vodacom kwa kufika hapa na kuwasaidia vijana hawa ambao bado wanaweza kuwa na mchango mkubwa kwa taifa.Mimi ni mara yangu ya kwanza kutembelea Sober House, nimeguswa na naahidi kuwaleta wadau zaidi kusaidia nyumba hizi ili kazi inayofanyika humu iimarike na kutoa mchango zaidi katika mapambanao dhidi ya dawa za kuelvya nchi."Alisema Prof. Mbarawa Awali Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon alisema Vodacom imefika katika nyumba hizo ikitekeleza kwa vitendo dira yake ya kusaidia makundi yenye uhitiji kupitia program ya Pamoja na Vodacom inayotekelezwa kwa michango ya wafanyakazi na kampuni.

"Hatukifika hapa kwa bahati mbaya tunajua kazi kubwa inayofanyika katika nyumba hizi na kwa makusudi tumezijumiisha katika makundi yakunufaika na program yetu ya Pamoja na Vodacom ili kuunga mkono kazi hiyo na kuonesha upendo wetu kwenu."

"Tatizo la dawa za kulevya sio la mtu mmoja linatugusa sote kama sio ndani ya familia basi kuna ndugu, jirani au hata rafiki."Alisema Lyon na kuongeza "Wito wangu mkubwa ni kuwaomba kujitahidi kuhakikisha hamrudii kutumia dawa za kulevya na aina nyengine za vilevi mara mnapokamilisha matibabu yenu na kurudi uraiani."

Kwa upande wake Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom amepongeza utayari wa wale ambao walikuwa watumiaji kabla ya kuacha na kuona umuhimu wa kusaidia wenzao ili nao waache na kurudi katika maisha mema na masafi.

"Waanzilishi wa nyumba hizi(Sober House) ni watu wenye ujasiri na upendo mkubwa katika jamii wameliona tatizo na wamekuwa tayari kutoa ujuzi, nguvu, mali na muda wao kusaidia wengine, naamini hii ni silaha moja muhimu katika mapambano dhidi ya dawa kulevya nchini."Alisema Mwalim Wakizungumza kupitia risala yao iliyosomwa kwa niaba yao na Abdala Hassan watu hao walio katika tiba maarufu wateja wanaopata nafuu wamesema haikuwa rahisi kwao awali kuamini kuwa wangeweza kubadilika na kurudi katika maisha ya kawaida ya kutotumia dawa za kulevya.

"Na sisi tulio mele yenu ni wateja tunaopata nafuu kwa hiari zetu bila ya kulazimishwa na mtu yeyote tumeamua kubadilika kutoka janga la dawa za kulevya baada ya kuchoshwa na hali za kudhalilika,kupoteza utu wetu, kutoheshimiwa, kuwa mzigo katika familia na jamii."Alisema Hassan "Ni kweli tulikuwa hatuna maadili mema kila mmoja ana historia yake ya nyuma. Tuna shukrani kubwa kwa waasisi wa umoja huu wa N.A (Narcotics Anonymous) na Sober House kwa sababu sasa tunaishi kwa amani, upendo, utulivu bila kufanya uhalifu wa aina yoyote na tunamatumaini na matarijio ya kurejea kuwa wazalishaji bora katika jamii."Aliongeza Hassan Katika kisiwa cha Pemba zipo jumla ya Sober House tano zilizo chini ya uongozi na usimamizi wa watu binafsi ambazo Vodacom Foundation ilizipatia chakula na mahitaji mengine.Hata hivyo warataibu wa Sober House wameiomba seriklai kuzitupia macho na kuziwezesha.

Vodacom Foundation iliandaa pia chakula cha mchana kwa ajili ya wateja wanaoptaa nafuu walio katika vituo hivyo mlo ambao ulimhusisha pia waziri Profesa Mbarawa na wafanyakazi wa Vodacom waliotembelea.
Mwisho.

SKYLIGHT BAND YAANGUSHA PARTY YA KUKATA NA SHOKA KUWASHUKURU MASHABIKI NA WADAU WAKE THAI VILLAGE.



 
 
 Mabloggers wakishow love John Badi (kushoto) na King Kif.
 
 Mkurugenzi wa Perfect Lady Saloon akiwa na Mdau kwenye usiku maalum wa kuwashukuru mashabiki wa SKYLIGHT BAND.
 
 Watoto wazuri katika pozi.
 
 Model katika pozi.
 
 Blogger King Kif akiwa na Mwenyekiti wa UVCCM, Beno Malisa.
 
 Mdau Eric Ndalu na mshikaji wake.
 
 Aneth Kushaba AK 47 kazini.
 
 Haya sasa lote lako ushindwe mwenyewe.....!!!
 Hapo sasa....Chezea SKYLIGHT BAND wewe.....balaaaaa...!!!
 
 Salma Yusuf akiwajibika baada ya kutambulishwa rasmi na uongozi wa Band hiyo.
Couples iliyobamba katika usiku maalum wa Ijumaa ya kwanza kwa mwaka 2013.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya mashabiki kati ya 100 waliobahatika kuonja Shots za Tequila katika usiku maalum ulioandaliwa na SKYLIGHT BAND Ijumaa ya kwanza kwa mwaka 2013 kwa ajili ya kuwashukuru wadau na mashabiki wote wanaotoa Support kwa Band hiyo yenye miezi 4 tu tangu kuzaliwa kwake.
Wadau wakishow love kwenye sehemu maalum iliyoandaliwa na SKYLIGHT BAND kwa ajili ya Fans wao kupiga picha za kumbukumbu...Kutoka kushoto ni Justin Ndege, Dr. Sebastian Ndege (wa pili kulia) na Eddie pamoja na wadau wa bendi hiyo.
Ushers waliokuwa wakihudumia wateja wa SKYLIGHT Band wakipozi kupata Ukodak.
Warembo waliobahatika kuwahi siku hiyo walipata T shirts za bure kutoka SKYLIGHT BAND ila kwa wanaume walionunua hizo alizoshika Binti mrembo.
Kipaji kipya kilichotambulishwa rasmi katika usiku huo maalum wa kuwashukuru mashabiki na wadau wa SKYLIGHT BAND si mwingine ni Salma Yusuf binti mwenye kipaji cha kuimba na kupiga gitaa akitoa burudani usiku huo.
Pichani Juu na Chini ni Kikosi kazi cha SKYLIGHT BAND kikishambulia jukwaa kwa furaha isiyo na kifani katika usiku maalum wa kuwashukuru mashabiki na wadau wa Band hiyo.
Hapo Sasa twende kazi.... Sam Mapenzi sambamba na Aneth Kushaba AK47 wakionyesha ufundi wao.
Mmoja wa Fans wa SKYLIGHT BAND akilipanda jukwaani na kuomnyesha umahiri wake wa kucheza moja ya nyimbo za Band hiyo.
Hawakutoka mikono mitupu walizawadiwa Tshirts pamoja na Mvinyo kama inavyoonekana pichani.
Papaaaa....Justin Ndege akimwaga noti kuwatunza SKYLIGHT BAND.
Hapo sasa mduara umekolea....Full kuzungusha nyonga.
Shabiki mwingine huyo hakuweza kuvumilia alipanda Juu ya jukwaa na kucheza 'Carolina' moja ya nyimbo za SKYLIGHT BAND zinazobamba mjini.
Sura mpya zilizojitokeza kusheherekea katika usiku maalum wa SKYLIGHT BAND kuwashukuru mashabiki wake.
Wadau wakishow love katika usiku maalum wa kuwashukuru mashabiki wa SKYLIGHT BAND ikiwa ni miezi minne tu tangu kuanzishwa kwa Band hiyo ambayo imeonyesha kukubalika kwa Watanzania na hata raia wa kigeni.
Mdau John Mwansasu akiwa na marafiki.
Picha Juu na Chini ni Sura mpya za mashabiki wa SKYLIGHT BAND wakishow love mbele ya camera yetu.
 
Mdau akiwa na Watoto wazuri katika pozi.

CCM , CUF NA CHADEMA Vyawasilisha Maoni Yao Tume ya Mabadiliko ya Katiba



Mmoja wa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Andrew Chenge akiwasilisha maoni ya chama chake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo Januari 7, 2013 katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akifafanua jambo kuhusu mfumo wa uchambuzi wa maoni ya wananchi kwa viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) waliofika katika ofisi za Tume kuwasilisha maoni ya chama hicho kuhusu Katiba Mpya leo Januari 7, 2013:. Viongozi hao pia walipata fursa ya kutembelea Kitengo cha Taarifa Rasmi (Hansard) na Kitengo cha Utafiti. Kulia kwa Mwenyekiti ni Katibu wa Tume Assaa Rashid na kushoto ni Mwenyekiti wa CUF Prof. Lipumba.
  Mmoja wa Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu akiwasilisha maoni ya chama chake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatatu, Jan 7, 2013) katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba (kulia) wakiongozwa na Dkt. Salim Ahmed Salim wapokea maoni kuhusu Katiba Mpya kutoka kwa uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ulioongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Freeman Mbowe katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo Januari 7, 2013
 Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba akiwasilisha maoni ya chama chake kuhusu Katiba Mpya mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatatu, Jan 7, 2013) katika Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba na kulia kwa Prof. Lipumba ni Katibu wa Tume Assaa Rashid.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) wakiongozwa na Mwenyekiti wao Prof. Ibrahim Lipumba mara baada ya chama hicho kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Tume jijini Dar es Salaam leo Januari 7, 2013.

Popular Posts