Pages

Showing posts with label Huduma za Usafiri - Transport Services. Show all posts
Showing posts with label Huduma za Usafiri - Transport Services. Show all posts

Saturday, August 4, 2012

QATAR LAZINDUA NJIA MPYA YA KUNUNUA TIKETI ZA SAFARI KWA NJIA YA MTANDAO KWA WATEJA WAKE (NEW OFFLINE PAYMENT SOLUTION FOR CUSTOMERS)

Dar es Salaam, TANZANIA– Shirika la ndege la Qatar, ambalo linamilikiwa na serikali ya nchi ya Qatar imeanzisha rasmi njia rahisi nay a haraka ya kutoa huduma zake kwa wateja wake ambapo tiketi za safari za anga zinazotolewa na shirika hilo zitatolewa pia kwa njia ya mtandao wa kulipia kupitia mtandao wake wa usajili wa safari na kupitia kwenye tovuti ya www.qatarairways.com/tz.

Muundo huu mpya utawapa nafasi wateja wote kubook tiketi zao kwa njia ya mtandao na kulipia baadaye kuzichukua katika ofisi za Qatar. Malipo lazima yawe yamekamilika kaika masaa 48 na hamna malipo yoyote ya ziada kwa wanaofanya malipo haya kupitia mtandao.Malipo yakishafanyika, wanaweza wakafanya ‘online check in’ na wanaweza pia kuchagua viti wanavyovipendelea na kichangua pia mlo ambao wangetaka. Wale wanotumia kadi za malipo ya baadaye yaani ‘credi cards’ wanaweza wakamaliza kubook, kununua na kufanya kila kitu hapo hapo kwenye mtandao.

Mkurugenzi mkuu wa shirika hili, Bw. Akbar Al Baker alisema kwamba mfumo huu mpya wa malipo inawapa wateja njia mbadala ya kununua tiketi zao

“Wateja wetu wanaweza sasa kununua tiketi zao wakiwa mahali popote na huduma hiiinatolewa masaa ishirini na nne siku saba kwa wiki na kwa hapo hapo kuweza kujiunga na ofa zinazokuwepo mara kwa mara. Ni mfumo rahisi tu kutumia na pia inakupa wewe mteja wetu uwezo wa kuchagua njia tofauti tofauti za kupanga safari zako.”

“Shirika la ndege la Qatar limejikita kuendeleza na kuboresha huduma zake ili kurahisisha na kufanya usafiri wa anga wa kwa wateja wetu kuwa mzuri na rahisi. “alisema

Kampuni hii iliyokuwa na makao makuu yake Doha nchini Airways juzi ilizindua mtandao wake ambao rahisi kutumia na pia ambao umetengenezwa ukizingatia mahitaji ya wateja wote. Mtandao huu unakuwezesha kupata kuona kurasa nyingi na kufanya booking za safari zako kwa urahisi zaidi.

Saturday, July 28, 2012

*RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE KATIKA UZINDUZI WA HANGA LA PRECISION AIR DAR ES SALAAM

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi hanga la Precisionair katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo asubuhi.Kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt.Harrison Mwakyembe na kulia ni mwanzilishi na Mwenyekiti wa Precision air Bwana Michael Shirima.

Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la ndege la Precision Air Bw. Michael Shirima akimkabidhi zawadi Mh Rais Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya kuzinduz rasmi karakana na ndege za shirika hili (Hanga) kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere leo jijini Dar es salaam, Karakana hiyo itakuwa na ikihudumia ndege za shirika hilo la mashirika mengine pia lakini pia itapokea wanafunzi walio kwenye mafunzo ya Uinjini wa ndege kutoka katika vuo vya ndani.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe pamoja na wakuu mbalimbali wa shirika la ndege la Precision Air na wafanyakazi wa shirika hilo mara baada ya uzinduzi wa (Hanga) hiyo
Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ndege la Precision Air Bw. Alfonce Kioko alipokuwa akitoa maelezo wakati wakati Rais alipokuwa akikagua Hanga hiyo, kulia ni Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe.

Thursday, July 26, 2012

Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe Azindua Huduma Za Safari za Anga Za Qatar Aiways Kutoka KIA Kuelekea Sehemu Mbali Mbali

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakiwemo na wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),mapema leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA.
Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat kwa niaba ya shirika hilo akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakiwemo na wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),mapema leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh lakizungumza machache na pia kumkaribisha mgeni rasmi na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo mapema leo iliofanyika kwenye uwanja wa KIA.
Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat kwa niaba ya shirika hilo akimpa Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison zawadi ya yenye nembo ya ndege ya shirika hilo la Qatar.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe akimkabidhi Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika hilo Bw. Marwan Koleilat kwa niaba ya shirika hilo la ndege la Qatar zawadi ya picha yenye kivuli cha Mlima Kilimanjaro .
Kutoka kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat,Waziri wa Uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki wakijadiliana jambo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat mara baada ya kuwasili na ndege ya shirika hilo aina ya Ndege namba QR546,shoto kwake ni Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki
Wakuu wa uzinduzi wakipga makofi kwa pamoja mara baada ya uzinduzi huo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison akipiga makofi wakati kikundi cha ngoma za asili kikitumbuiza,shoto kwake ni Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat

Meli ya Mv.Kalama, Mv.Seagul na Mv.Sepideh Zafutiwa hati ya Kubeba Abiria

Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar Abdullah Husein Kombo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Afisini kwake leo Malindi Mjini Zanzibar-Picha na Nafisa Madai-Maelezo Zanzibar
--
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
26/07/2012

Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar imezifutia rasmi hati ya kufanya kazi Meli ya Mv.Kalama, Mv.Seagul na Mv.Sepideh kutokana na meli hizo kutokukidhi hali ya usalama wa abiria katika meli hizo. Aidha meli hizo zimepewa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo kuhakikisha zimeondoka katika maeneo ya Zanzibar kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya wamiliki wa Meli hizo.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar Abdullah Husein Kombo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Afisini kwake kuhusu hali ya usafiri wa baharini na usalama Zanzibar. Amesema Mamlaka hiyo imefanya tathmini na uhakiki wa kutosha na kujiridhisha kuwa Meli hizo hazifai kufanya kazi katika maeneo ya Zanzibar jambo ambalo limepelekea kuchukua hatua za kufuta hati za kufanyia kazi meli hizo.

Amefahamisha kuwa sababu kuu zilizopelekea Mamlaka kufanya maamuzi hayo ni pamoja na uchakavu,umri wa meli hizo kuwa mrefu na kupata matatizo mara kwa mara katika safari zao. Kombo amefahamisha kuwa Sheria ya Mamlaka ya Usafiri na Bandari Zanzibar ya mwaka 2006 kifungu cha 17.1 inampa mamlaka Msajili wa Meli kuifuta meli yoyote ambayo itakuwa haikidhi usalama wa abiria.

Kufuatia sheria hiyo Kombo amesema watawataka wamiliki wa Meli hizo kuzirudisha hati za kufanyia kazi meli hizo ili waende kutafuta sehemu nyengine za usajili kinyume na maeneo ya Zanzibar. Akizungumzia Meli ya Mv.Serengeti Kombo amesema wamelazimika kuiagiza meli hiyo kupunguza idadi ya abiria kutoka watu 800 hadi 350 na tani za mizigo kutoka 100 hadi 50 hadi pale ambapo watajiridhisha kutokana na hali ya meli hiyo ilivyo.


Aidha amegusia kuwa Kampuni ya Bakhresa italeta Meli kubwa ya abiria itakayofanya kazi zake Zanzibar ambapo pia Serikali ya Mapinduzi nayo iko mbioni kuhakikisha wanaleta meli inayokidhi mahitaji ya wananchi wa Zanzibar.

Wednesday, July 4, 2012

Mobile Ticketing' Yaboresha Huduma Zake

Afisa Maendeleo ya Biashara Mobile Ticketing Limited Bw.Albert Muchuruza akiwaonesha waandishi wa habari njia muhimu za kukata tiketi za mabasi kwa njia ya Mobile Ticketing kwa wasafiri wanaotumia mabasi yaendayo mikoani,anaeshuhudia kushoto ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo Juma Mgori.
Afisa Maendeleo ya Biashara Mobile Ticketing Limited Bw.Albert Muchuruza akiwaonesha waandishi wa habari njia muhimu za kukata tiketi za mabasi kwa njia ya Mobile Ticketing kwa kupitia simu za kiganjani kwa wasafiri wanaotumia mabasi yaendayo mikoani.
Meneja Masoko wa kampuni ya Selcom Pay Point Bw.Juma Mgori akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na uboreshaji wa kukata tiketi za mabasi yaendayo mikoani kwa njia rahisi za mtandao(Mobile Ticketing)katikati Afisa Maendeleo ya Biashara Mobile Ticketing Limited Bw. Albert Muchuruza.
--
KAMPUNI ya Mobile Ticketing Tanzania Limited imezidi kuboresha huduma zake kufuatia kurahisisha zaidi upatikanaji wa tiketi za kusafiria kwenye Selcom Pay Point kama zinavyopatikana huduma nyingine muhimu nchini.Uboreshaji huo umekuja kutokana na kampuni hiyo kutambua umuhimu mkubwa wa huduma hiyo katika jamii ili kuzidi kuwarahisishia hata wale wasiokuwa na simu za mikononi waweze kupata huduma hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini,Afisa Maendeleo ya Biashara wa kampuni hiyo, Albert Muchuruza, alisema kuwa amefikia uamuzi wa kuwa na huduma hiyo huku ikiendelea kushirikiana na Vodacom kwaajili ya kuhakikisha huduma hiyo ya tiketi popote inamfikia kila mwananchi hapa nchini.

"Tuko kwenye hatua za mwisho za kukamilisha vitu vichache japo huduma hii ya upatikanaji wa tiketi za Usafiri wa Mabasi wa Mabasi kupitia wakala wa Selcom Pay Point kama zinavyopatikana huduma nyingine za kulipia ANKARA za maji, umeme, ving'amuzi nk, imeshaanza kutumika hapa nchini lengo likiwa ni kuhakikisha huduma hii inapatikana kwa urahisi zaidi na kumfikia kila mtu.

Aidha, Muchuruza alisisitiza kwamba huduma hiyo ya upatikanaji wa tiketi kwenye selcom pay point imekwishaanza kufanya kazi siku chache zilizopita na kuiomba jamii itambue mchango wa kampuni yake ambao ni kurahisisha na kuweka huduma kama hiyo karibu na jamii kitu ambacho ni uzalendo.

Mbali na hayo, pia Muchuruza alisifu muitikio chanya wa wananchi juu ya utumiaji wa huduma hiyo ya tiketi popote na kusema kuwa tathmini iliyofanywa na kampuni yake inaonyesha kuwa jamii imeanza kutambua na kuelewa umuhimu na matumizi sahihi, hadi sasa muitikio ni mkubwa na wenye kuridhisha kwa kipindi kifupi cha mwezi mmoja tangu huduma hiyo kuzinduliwa mapema mwezi uliopita.

Tuesday, July 3, 2012

EMIRATES LAUNCHES BARCELONA SERVICE

*Double daily Madrid flights as of 1st July 2012
* DUBAI, UAE – 3rd July 2012 – Emirates launched flights to Barcelona today as part of a tripling of services to Spain.

The airline’s daily flight to Madrid went double daily on 1st July and coupled with the brand new Barcelona route, the carrier now offers three flights a day into the country.

The VIP delegation aboard today’s first flight to Barcelona included Salem Obaidalla, Emirates’ Senior Vice President, Commercial Operations, Europe & Russian Federation; Hiran Perera, Emirates’ Senior Vice President, Cargo Planning & Freighters; Brigadier Obaid Mehayer Bin Suroor, Deputy Director of Dubai Naturalisation & Residency Department; José Eugenio Salarich, Spain’s Ambassador to the UAE and representatives from the media.

Passengers booked from 20 countries, including the UAE, Kuwait, Saudi Arabia, South Africa, South Korea and Indonesia, also joined the inaugural flight.

“In the space of 48 hours, Spain has shot up our list of most served European countries, said Salem Obaidalla, Emirates’ Senior Vice President, Commercial Operations, Europe & Russian Federation. “Connecting Spain to our network with three flights a day from what was a daily flight to Madrid is a major boost to our operations and underscores our commitment to the Spanish market.”

In Barcelona, Fernando Suárez de Góngora, Emirates Country Manager for Spain, hosted a welcoming reception attended by Sonia Corrochano, Director, Barcelona El Prat Airport and Damià Calvet i Valero, Territory and Mobility Secretary of the regional Catalan government.

With the new Emirates’ service between Barcelona and Dubai, the Catalan capital gets connected to one of the most important cities and regions for business worldwide,” said Mr Damià Calvet. “Emirates has valued Barcelona and its airport as a good opportunity within its global growth strategy. To Barcelona and the Catalonia region, this route also represents an opportunity for the globalisation of Catalan enterprises and for the region’s economy, key elements to get over the economic crisis.”

Emirates will serve Barcelona with a 777-300ER offering 360 in a three-class configuration. Staffed by highly trained, multi-lingual cabin crew, the aircraft offers luxurious First Class Private Suites, lie-flat seats in Business Class and a new generation of comfort in Economy Class.

While relaxing and enjoying gourmet chef prepared food, passengers can lose themselves in over 600 channels of movies, TV programmes, games and music featured on the ice entertainment system.

EK 185 will depart Dubai at 0655hrs and arrive in Barcelona at 1200hrs. EK 186 will take off daily from Barcelona at 1640hrs and land in Dubai at 0100hrs the following day.
From Barcelona, passengers will be able to connect through Emirates’ traveller-friendly Terminal 3 in Dubai to popular destinations such as Mumbai, Delhi, the Seychelles and Mauritius and Manila. They will also be able to pick up Emirates’ flagship aircraft, the A380 to places such as Jeddah, Tokyo, Beijing and Sydney.
Emirates SkyCargo has been operating freighter flights to Spain since 2006, supporting the movement of clothes, one of Catalonia’s main exports to the Gulf.

Emirates Holidays, the airline’s tour operating arm, offers tailor made holidays to Barcelona, including a selection of hand-picked hotels that are among the best accommodation in the city. Its annual brochure, A World of Choice, highlights many of Barcelona’s attractions such as the Sagrada Familia Cathedral by the famous Catalan architect, Antoni Gaudi; the Gothic and El Born Quarters; Las Ramblas; and the Passeig de Gracia.

Picture 1 - The Catalonia flag hangs from the cockpit of Emirates' inaugural flight to Barcelona with Spanish First Office Fernando Arevalo on the flight deck.
Picture 2 - Emirates' first passenger flight to Barcelona arrives to a water cannon salute.
Picture 3 - Emirates' flight 185 after touching down on its inaugural flight to Barcelona.

Picture 4 - Prior to departure at Emirates’ Terminal 3 in Dubai and from right to left: Salem Obaidalla, Emirates’ Senior Vice President, Commercial Operations, Europe & Russian Federation; Brigadier Obaid Mehayer Bin Suroor, Deputy Director of Dubai Naturalisation & Residency Department; José Eugenio Salarich, Spain’s Ambassador to the UAE and Hiran Perera, Emirates’ Senior Vice President, Cargo Planning & Freighters.

Contact:
Jonathan Hill, Emirates Corporate Communications
Tel: (+9714) 708 2329, Mob: (+97150) 654 9604;
jonathan.hill@emirates.com, Visit www.ekgroup.com/mediacentre

Regards,
Gloria Lyatuu
JWT Tanzania Limited
4th Floor BMTL House,
A.H. Mwinyi Road,
P.O. Box 78769
Dar-Es-Salaam – Tanzania
Land Line: +255 22 276 2127/ +255 22 276 2135/ +255 22 276 2136/ +255 754780 224/ +255 754780225
Cell Phone:+255

Tuesday, June 26, 2012

AJALI AJALI AJALI

Basi la abiria mali ya Summry likilipita basi lingine mali ya Kampuni ya SKY LINE katika kona kali jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa abiria na mali zao. Madereva wa mabasi hawana budi kutambua dhamana waliyopewa ya kusafirihs roho za watu na kuhakikisha wanazilinda na kuepukana na ajali zisizo za lazima.

Sunday, June 24, 2012

Zambia waishukuru PrecisionAir kuanza Safari za Dar es Salaam / Lusaka

Mkurugenzi Mkuu na CEO wa Precision Air, Alfonse Kioko akizungumza wakati wa tafrija ya uzinduzi wa safari za Shirika hilo la ndege jana kutoka Dar es Salaam hadi Lusaka Zambia kupitia Lubumbash.Hafla hiyo iliyofanyika katika mji wa Lusaka Hoteli ya Taji Pamodz.
Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Uchukuzi, John Thomas James Mngodo akizungumza kaatika hafla hiyo iliyofanyika katika mji wa Lusaka Hoteli ya Taji Pamodz.
Mgeni Rasmi, Naibu Wazizi wa Usafirishaji, Kazi, Usambazaji na mawasiliano wa Zambia, Samuel Mukupa akizungumza jana katika tafrija maalum ya uzinduzi wa safari za Ndege za Kampuni ya Precision Air kutoka Dar es Salaam kwenda Lusaka kupitia Lubumbashi. Mukupa alisema mbali ya kuzidisha mahusionao baina ya Tanzania na Zambia lakini pia itawasaidia sana wafanya biashara wa Zambia katika safari zao za kibiashara Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Grace Mujuma akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Kocha Msaidizi wa Mabingwa wa Afrika, Timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo' Honor Janza nae alikuwepo.
Meneja Mkazi wa Afrika ya Kati wa Kampuni ya Precision Air, Emmanuel Mathias Ng'andu akiwa na Meneja Maweasiliano wa Kampuni hiyo Anneth Nkini wakati wa tafrija hiyo.
Viongozi wakishangilia jambo.
Wageni mbalimbali wakiwepo na wafanyakazi wa Precision Air wakifuatilia matukio.




Wageni mbalimbali wakifuatilia tafrija


Mkurugenzi wa Masoko, Patriki Ndekana , (kushoto), Meneja Mauzo, Tuntufye Mwambusi, Hilda Lema, Mariam Ismail na Meneja Mkazi wa Afrika ya Kati wa Kampuni ya Precision Air, Emmanuel Mathias Ng'andu wakipamba moto katika EDUDHA.


CEO wa Precision Air, Alfonse Kioko (kulia) akiwaongoza wafanyakazi wake kucheza EDUDH.Picha Zote Zimeletwa na Mdau Mroki Mroki

Tuesday, June 19, 2012

MELI MPYA YA KUSAFIRISHIA MIZINGO YA AZAM

Meli hiyo inavyoonekana kwa Nje
Meli hiyo inavyoonekana kwa ndani.
Meli hiyo inavyoonekana kwa Ujumla
---- .
Azam yaamua kufanya kweli na hivi karibuni meli ya kisasa iko mbioni kuzinduliwa ambayo ikawezesha watu kwenda na magari yao Zanzibar. Meli hiyo inauwezo kubeba magari 200, abiria 1500 na Mizigo tani 500.
KAMPUNI ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine inatarajia kuzindua meli kubwa ya kisasa kwaajili ya abiria waendao Dar es Salaam, Pemba na Unguja. Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15 mwaka huu meli hiyo yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa.

Mohamedi alisema shida ya usafiri itapungua kwa asilimia kubwa kutokana na meli hiyo kuwa na uwezo wa kubeba abiria 1500, Mizigo tani 500 na magari 200 ambapo abiria atakae jisikia kwenda na gari lake Zanzibar, Pemba au Dar es Salaam ataweza kufanya hivyo.

Waziri Mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hamadi Masoud, alithibitisha kwamba anataaarifa za ujio wa meli hiyo ambayo alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ya kutoa huduma tu na siyakutengeneza faida. Meli hiyo inauwezo wa kwenda kasi ya notkomail 20.

Monday, June 18, 2012

ATCL YAJIPANGA KUENDELEZA USAFIRI WA ANGA

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Kapteni Lusajo Lazaro akihutubia wahitimu wa Chuo cha Mafunzo cha ATCL baada ya kumaliza kozi ya utoaji huduma kwenye ndege katika hafla yakuwakabidhi vyeti iliyofankika Jijini Dar es Salaam jana
Mkuu wa Chuo cha Mafunzo cha ATCL kilichopo Terminal 1 Lawrence Mhomwa akihutubia wahitimu wa chuo hicho katika hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimun hawa baada ya kumaliza kozi ya utoaji huduma kwenye ndege .Hafla hiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni mmoja wa waalimu wa Chuo hicho Thecla Ndussi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Kapteni Lusajo Lazaro akimpongeza mmoja wa wahitimu wa Chuo cha Mafunzo cha ATCL baada ya kumaliza kozi ya utoaji huduma kwenye ndege .Wapili kutoka kushoto ni Kaimu Mkrugenzi wa Idara la Uendeshaji wa Shirika hilo kapteni Richard Saidi. Hafla hiyo ya utoaji vyeti kwa wahitimu ilifanyika katika Makao makuu ya shirika hilo Jijini Dar es Salaam wikiendi hii.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Kapteni Lusajo Lazaro akitoa zawadi kwa mmoja wa wanafunzi bora wa Chuo cha Mafunzo cha ATCL katika hafla ya utoaji vyeti kwa wanafunzi 39 waliomaliza kozi ya utoaji huduma kwenye ndege. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi wa shirika hilo Patrick Itule na Kaimu Mkrugenzi wa Idara la Uendeshaji wa Shirika hilo kapteni Richard Saidi (Kulia).
Tumeiva sasa. Wahitimu wa Chuo cha Mafunzo cha ATCL wakionyesha vyeti walivyokabidhiwa baada ya kumaliza kozi ya utoaji huduma kwenye ndege .Hafla hiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam jana.
Wahitimu wa Chuo cha Mafunzo cha ATCL waonyesha nyuso za furaha mbele ya kamera ya blogu hii katika hafla ya kukabidhiwa vyeti baada ya kumaliza kozi ya utoaji huduma kwenye ndege .Hafla hiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam jana
Wahitimu wa Chuo cha Mafunzo cha ATCL wakipozi kwa picha ya pamoja katika hafla ya kukabidhiwa vyeti baada ya kumaliza kozi ya utoaji huduma kwenye ndege .Hafla hiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam jana.Picha na Mpiga Picha Wetu.
---
SHIRIKA la Ndege la Air Tanzania (ATCL) limetangaza mpango wakuungana na Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) ilikutoa mafunzo mbalimbali yatakayowezesha upatikanaji wa wataalam mbalimbali wa sekta ya anga.

Akizungumza katika sherehe yakuwaga wanafunzi 39 wa Chuo cha Mafunzo cha Shirika la Ndege la Air Tanzania jijini Dar es Salaam wikiendi hii, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Kapteni Lusajo Lazaro alisema mpango huo ambao utakuwa endelevu umewekwa kwa makusudi ilikuhakikisha wataalam katika sekta ya usafiri wa anga wanakuwa na ubora unaostahili hususani wakati huu ambapo sekta ya usafiri wa anga inakuwa kwa kasi zaidi na kuvutia wawekezaji zaidi. “Tumeshasaini nyaraka za makubaliano (MOU)na NIT ilikuwezesha ufanisi wa swala hili. Nimatumaini yetu kuwa mpango huu utasaidia kupunguza tatizo la upungufu wa wataalam katika sekta ya anga nchini.

”Bila pingamizi lolote kuwa sasa tutahitaji wataalam zaidi ili kuboresha utoaji wa huduma zetu hususani katika kipindi hiki ambacho tumejikita katika utekelezaji wa mpango wetu wa maendeleo wa miaka mitano ambao unalengo la kuongeza safari na ndege nyingine katika miaka michache ijayo,” alisema. Lazaro akitoa maoni yake juu ya soko la pamoja la Afrika Mashariki ambalo limefungua milango kwa biashara huria za bidhaa na huduma ndani ya nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) alisema kuwa kampuni yake imejipanga kutumia fursa hiyo ipasavyo.

“Soko hili huria la pamoja litatengeneza fursa nyingi sana na tayari sisi kama shirika tumejipanga kuchangamkia na kuzitumiua fursa hizo ipasavyo. Tupo katika mipango ya kuongeza safari zetu zaidi na pale inapowezekana kutafanyakazi pamoja na mashirika makubwa barani. Tunahitaji wafanyakazi wenye ujuzi na walio bora ambao watatusaidia kuleta ushindani kama shirika,” aliongeza.

Kwa upande wake, mhitimu wa Chuo cha Mafunzo cha Mafunzo ya Anga cha ATCL Yasmin Khanj akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake waliohitimu alisema kuwa watatumia vizuri ujuzi wote walioupata katika chuo hicho ilikuchangia maendeleo ya sekta ya usafiri wa anga nchini.

“Hii ni hatua kubwa sana katika maisha yetu. Tunaiomba kampuni ya ATCL kutupa fursa ya kupata ujuzi zaidi kwa kutupatia nafasi kwenye kampuni ili tuweze kupata uzoefu unaohitajika ili tulete ushindani na kutoa huduma ipasavyo,” alisema.

Aidha,mkuu wa chuo cha mafunzo cha ATCL, Lawrence Mhomwa alisema kuwa wahitimu hao baada ya kumaliza mafunzo yao yaliyojumuisha mada saba katika chuo hicho zikiwa pamoja na huduma kwa wateja, usalama katika viwanja vya ndege, uhudumu ndani ya ndege,usalama ndani ya ndege na mada nyingine,wahitimu hao sasa wanauwezo wa kufanyakazi katika shirika lolote la ndege

Popular Posts