Pages

Showing posts with label Rukwa. Show all posts
Showing posts with label Rukwa. Show all posts

Wednesday, January 2, 2013

MKE WA WAZIRI MKUU MAMA TUNU PINDA ASHIRIKI MKESHA WA MWAKA MPYA SAMBAMBA NA TAMASHA LA WANAWAKE MKOANI RUKWA (RUKWA WOMEN IN ACTION)



Mama Tunu Pinda mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwasili katika ukumbi wa St. Maurus Chemchem Mjini Sumbawanga jana katika sherehe aliyoalikwa na Mkuu wa Mkoa Rukwa Injinia Stella Manyanya ya kuaga mwaka 2012 na kukaribisha mwaka 2013 iliyoenda sambamba na tamasha kubwa la mwanamke wa Rukwa RUWA (Rukwa Women in Actiion). Tamasha hilo lililobuniwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa lina lengo la kuwanunganisha wanawake wa Mkoa wa Rukwa pamoja katika tamaduni zao tofauti katika kuwainua kiuchumi na kifikra ambapo walishiriki kwa kuonyesha tamaduni zao za ngoma, mavazi na chakula. Lengo la tamasha hilo pamoja na umoja huo ni kwa ajili ya kunadi na kuhamasisha utalii wa ndani, kuwawezesha kinamama wa kipato cha chini, kuhamasisha na kuwezesha vita dhidi ya umaskini, mimba za mashuleni, lishe bora na chanjo za afya kwa watoto wachanga na wanawake wa kipato cha juu kuwawezesha wa kipato cha chini.
Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitoa hotuba yake katika tamasha hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza katika tamasha hilo kumkaribisha mke wa Waziri kuzungumza na washiriki zaidi ya mia sita walihudhuria katika tamasha hilo.
Mama Pinda (kulia), Mama Dora Rajab Rutengwe mke wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi (wa pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Stella Manyanya na wanawake wengine wakijumuika kucheza muziki wa kwaito katika kupasha misuli moto kwenye tamasha hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akionyesha vazi linalotangaza utalii wa ndani na rasilimali muhimu kama misitu, wanyama pori, na samaki.
Ilifika muda washiriki wa maonyesho hayo kupita mbele ya jukwaa kuu tayari kwa kuanza kuonyesha sanaa na mitindo mbalimbali.
Mmoja ya washiriki akionyesha moja ya vazi la kiutamaduni la asili ya makabila ya Rukwa kwa wazee wakati wa msimu wa baridi.
Katibu tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akisakata ngoma ya kinyaturu katika tamasha hilo. Kulia ni mwanae Hussein Chima.
Mama Tatu Chima mke wa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa akimpa zawadi ya shanga za kabila la kinyaturu Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda kabla ya kuanza kucheza ngoma ya kabila hilo. Kulia ni mumewe Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (wa pili kushoto) Injinia Stella Manyanya akishiriki kwenye ngoma ya kabila lake la wangoni waliojumuika kwenye tamasha hilo kuonyesha baadhi ya tamaduni zao. Wa kwanza kushoto akionyesha uwezo mkubwa katika kusakata ngoma hiyo ni mwandishi wa habari wa channel ten Judy Ngonyani.  
Mduara pia umo katika ngoma za kabila la wangoni. 
Washiriki wa kabila la wahaya wakionyesha baadhi ya mavazi ya asili ya kabila lao.
Ngoma za kihaya.
Majaji waliohusika katika katika mashindano ya tamaduni za makabila tofauti ya Mkoani Rukwa, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Kagera, Singida, Kigoma, Shinyanga na Mwanza. Mkoa wa Rukwa ulishinda katika Ngoma.
 Washiriki wa kabila la wafipa wakionyesha baadhi ya mavazi yao ya asili na baadhi ya zana zao za asili. 
 Sound ya ngoma ya kabila la wafipa ikitumbuiza katika tamasha hilo.Kigoda hutumika kusugua chungu ambacho hutoa mlio wa aina yake katika kunogeza ngoma ya kabila hilo.
 Washiriki wa kabila la wafipa wakionyesha tamaduni zao za kusaga unga na ulezi kwa kutumia zana za asili.
 Pombe ya asili ya kabila la wafipa inayotengenezwa kwa ulezi na kunyewa kwa mirija, raha duniani.
 Mambo yetu ya rusha roho nayo yalikuwepo. 
 Palikuwa hapatoshi.
Mvua ya shampen ya kukarisha mwaka mpya 2013 ikifunguliwa na mratibu wa tamasha hilo ambae pia ni Afsa maendeleo ya jamii Mkoa wa Rukwa Ndugu Deonisya Njuyui.
 Cheers kwa mwaka 2013. Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu akigonganisha glass na Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali watu Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashalla na Mke wa aliyekuwa Mbunge jimbo la Sumbawanga Mjini CCM Aeshi Hillal.
 Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Idd Kimanta akinywa togwa iliyoandaliwa na kabila la wahaya.
 Mbunge wa Jimbo la Kalambo Josephat Kandege nae akilamba tongwa.
 Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya wakionja ugali wa muhogo ulioandaliwa na kabila la Waha kutoka Kigoma.
 Ndizi kuku au Kuku ndizi kutoka katika kabila la wanyakyusa la Mkoani Mbeya.
 Maharage yaliyochanganywa na mboga za majani kutoka katika kabila la wanyakyusa la Mkoani Mbeya.
 Mshiriki Leah Mgagama kutoka katika kabila la wangoni akionysha moja ya vazi la kabila hilo na kifaa cha kuhifadhia chakula kisiharibike kijulikanacho kwa jina la "Kijamanda".
 Vazi la kitanzania likiwa na bandera ya taifa.
 Ilikuwepo mitindo mbalimbali ya mavazi.
 Onyesho la mavazi
 Onyesho ya vazi la mjamzito.
 Anthonia Nkyabonaki kutoka kabila la wahaya akionyesha mtindo wa mavazi.Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa

Friday, November 23, 2012

Katibu Mkuu wa CCM Abdurahamn Kinana Atua Mkoani Rukwa na Kusema'' Kuitwa Waheshimiwa Ndani ya CCM Sasa Basi.''


Katibu Mkuu Mpya wa CCM Abdurahaman Kinana akifungua shina la wakereketwa wa CCM la Kisesa, mkoani Rukwa.
Katibu Mkuu Mpya wa CCM Abdurahamn Kinana,na Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye , na Mzee Self Khatib wakisalimia wananchi Uwanja wa Ndege wa Rukwa.
Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye akiwa na Watoto
Katibu Mkuu Mpya wa CCM Abdurahaman Kinana akizungumza na wana-CCM leo mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa
Pikipiki za mapokezi kutoka Uwanja wa Ndege wa Rukwa.Picha na Bashir Nkromo-Rukwa
---
NA BASHIR NKOROMO, RUKWA
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ameagiza kuanzia sasa wanachama wa CCM kuacha kuitana waheshimiwa badala wake watumie jina ndugu kama alivyoasisi Mwenyekiti wa kwanza wa CCM, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

Kinana ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na viongozi wa CCM, mjini hapa, akiwa katika siku yake ya pili ya ziara ya siku nne kujitambulisha na kukagua uhai wa Chama katika mkoa huo na mikoa ya Mtwara, Geita na Arusha.

"Mimi katika maisha yangu yote ya kumfahamu Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere, sikupata kumsikia akijiita au akitaka aitwe Mheshimiwa Mwenyekiti, au Mheshimiwa Rais, sasa haya mambo ya sisi kuitama mheshimiwa tunayatoa wapi?", alihoji Kinana.

Alisema, Mwalimu Nyerere hakujiita Mheshimiwa kwa sababu na maana kubwa sana, kwa hiyo ni lazima Wana-CCM kuendelea utamaduni huo wa kuitaka ndugu kwa sababu unazuia matabaka ya ubwana na utwana.

Mapema kabla ya mkutano huo wa ndani, Kinana alifungua shina la wakereketwa wa CCM Isesa na shina la UWT, Chanji nje kidogo ya mji wa Sumbawanga, ambapo alisema hatua ayake ya kufungua matawi hayo na kushiriki kikao cha shina kinachofunguliwa na mjumbe wa shina husika, ni ishara ya kuwaagiza viongozi wa ngazi zote wa CCM kuhakikisha wanatembelea mashina na matawi.

"Hili siyo langu, ni agizo la Mkutano Mkuu wa CCM uliomaizika mjini Dodoma hivi karibuni, pale tuliazimia kwamba, ili kuimarisha uhai wa Chama lazima viongozi wa ngazi mbalimbali watembelee mashina ma matawi ili kuzijua kero zilizopo huko", alisema.

Alisema, kulingana na agizo hilo, sasa kila kiongozi wa Chama atapimwa ufanisi wake wa kikazi kwa kuangalia ni namna gani anafanya kazi zake kwa karibu sana na mashina na matawi.

Alisema, CCM imesisitiza lifanyike hilo kwa juhudi zaidi kwa sababu ni wazi kwamba wenye chama ni wanachi waliopo kwenye ngazi hizo za mashina na matawi, hivyo kwenda huko ndiko kutaimarisha chama kwa uhakika zaidi.

Katika ziara hiyo, Kinana amefuatana na wajumbe wa NEC, Nape Nnauye (Itikadi na Uenezi), Mohamed Seif Khatib (Oganaizesheni)na waziri wa TAMISEMI, Aggrey Mwanri.

Mwisho.

Thursday, September 6, 2012

MKUU WA MKOA WA RUKWA AMUOMBA MKURUGENZI WA SUMATRA KUFANYA UKAGUZI WA MARA KWA MARA WA MELI KUEPUSHA AJALI

Mkoa wa Rukwa unapakana kwa karibu sana na Nchi za Kidemeokrasia ya Kongo, Burundi na Zambia ambapo mpaka wa nchi hizo upo katika ziwa Tanganyika. Kwa kuona umuhimu wa kuziunganisha nchi hizo kibiashara Serikali imeamua kujenga bandari ya Kasanga ambayo itakuwa kiunganishi kikubwa cha kibiashara na nchi hizo. Sio bandari peke yake bali pia barabara za lami kutoka Mkoa wa Mbeya (Tunduma)-Sumbawanga hadi Kasanga ilipo bandari hiyo inaendelea kujengwa na inategemewa kukamilika mwakani 2013.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Mkurugenzi wa SUMATRA Huduma za Uzidhibiti wa Bandari na Usafiri Majini Ndugu Peter Lupatu ambaye yupo Mkoani Rukwa kwa ajili ya ukaguzi wa bandari ya Kasanga na vifaa vya usafiri wa majini katika ziwa Tanganyika ikiwemo meli ya Mv Liemba na Mv Mwongozo. Mkuu huyo Mkoa alimuomba Mkurugenzi huyo kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa vyombo vya majini hususani Meli ili kuepusha ajali mbaya zinaweza kujitokeza kama ilivyotokea kwa meli za Mv Spice Islanders na Mv Skagit katika bahari ya Hindi. Alisema ajali nyingi husababishwa na ubovu wa vyombo hivyo ambavyo vinahitaji ukarabati wa mara kawa mara.
Kushoto ni Meneja wa SUMATRA Huduma za Uzidhibiti wa Bandari na Usafiri Majini Ndugu D.B Mukasa, Mkurugenzi wa SUMATRA Huduma za Uzidhibiti wa Bandari na Usafiri Majini Ndugu Peter Lupatu na kushoto ni Afsa Mkuu wa Sumatra Mkoa wa Rukwa Chambo Ghadafi wakijadili mambo muhimu kuhusu sekta ya bandari na usafiri majini katika ziwa Tanganyika na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya. Miongoni mwa mambo waliyogundua kwenye ukaguzi wao ni pamoja na Meli kusafirisha abiria bila kutumia tiketi jambo ambalo wameshauri utaratibu huo ubadilike na abiria kukatiwa tiketi na kutambuliwa ili tatizo lolote likijitokeza iwe rahisi kulishugulikia.Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa

Sunday, July 15, 2012

UZINDUZI WA KITUO CHA UWEKEZAJI NA KITEGA UCHUMI CHA CCM, SUMBAWANGA MJINI.

Katibu wa itikadi na uenezi Taifa, Ndugu Nape Moses Nnauye akihutubia wananchi waliojitokeza katika Ufunguzi wa Kitega Uchumi cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika manispaa ya Sumbawanga leo 14 july 2012. Kitega uchumi hiko kinajumuisha milango ya maduka 37 na kituo cha mafuta ''petrol station'' ambako kipo maeneo ya sabasaba katika manispaa hiyo, Nape atakuwepo Mkoani Rukwa kwa siku mbili kwa Ziara ya Kuimarisha Chama.

Katibu wa Halmshauri kuu (NEC) Ndugu Nape Nnauye akifungua kitega Uchumi Cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Manispaa ya Sumbawanga, Mkoani Rukwa.

WANANCHI MKOANI RUKWA WAONGEA ANA KWA ANA NA VIONGOZI WA CCM

Mh. Charles Tizeba , akiwahakikishia wananchi wa Wilaya ya Sumbawanga mjini kuwa kiwanja cha ndege kitajengwa kama ilivyopangwa.
Mh.Ole Nangolo ,Naibu Wizara ya Mifugo akihutubia wananchi wa Mkoa wa Rukwa mipango madhubuti ambayo serikali inaifanyia kazi juu wa masuala yanayohusu mifugo
Wananchi wa Mkoa wa Rukwa wakiuliza maswali kwa viongozi wao na walipatiwa majibu hapo kwa papo.
Mh.Aggrey Mwanri akiiwasili kwenye viwanja vya Msakala,mkoani Rukwa ,Wilaya ya Sumbawanga Mjini.
Katibu wa Halmashauri kuuu ya Taifa akihutubia kwenye mkutano wa hadhara mkoani Rukwa

Mh.Adam Malima akizungumza na Wananchi wa Sumbawanga mjini masula mbali mbali yanayohusu kilimo na nchakula pamoja na kutatuliwa kwa tatizo la umeme.
Waziri wa maji, Prof.Jumanne Maghembe akihutubiwa wananchi wa mkoa wa Rukwa ambapo aliwapasha kuwa suala la matatizo ya maji litakuwa limekwisha karibuni
Mh. Mwigulu Nchemba akihutubia wananchi wa wilaya ya Sumbawanga mjini.
Mzee Crisant Mzindakaya akiwasalimu wananchi wa Wilaya ya Sumbawanga mjini.

Popular Posts