Pages

Showing posts with label Miundombinu -Infrastructure. Show all posts
Showing posts with label Miundombinu -Infrastructure. Show all posts

Friday, January 4, 2013

Dkt. Mwakyembe akagua uwanja wa ndege wa Songwe, Mbeya


Picture
Waziri wa uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara yake katika uwanja wa Ndege wa Songwe, Mbeya amesema kuwa uwanja huo una hadhi ya Kimataifa na ni kati ya viwanja vikubwa viwili kujengwa baada ya uhuru, ukitanguliwa na uwanja wa Mkoa wa Kilimanjaro (KIA).

(picha zote na maelezo, credit: Mbeya Yetu blog)
Picture
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) Mhandisi Suleiman S. Suleiman akimwelezea Dkt. Harrison Mwakyembe jinsi uwanja wa ndege wa Songwe unavyofanya kazi toka uzinduliwe mwezi wa 12 mwaka jana na kuwa sasa uwanja huo umebaki kukamilisha maeneo ya maegesho ya ndege kubwa kama Boeing 737.
Picture
Hili ni eneo la kutua ndege na kurukia barabara hiyo ya ndege yenye urefu wa zaidi ya kilometa 3.5 km
Picture
Huu ni mnara wa kuongozea ndege katika kiwanja hicho
Picture
Mwongoza ndege mwandamizi John Chambo akimwezea waziri Mwakyembe jinsi wananvyofanya kazi ya kuongoza ndege katika mnara huo
Picture
Sura ya mbele ya uwanja wa Songwe
Picture
Maegesho ya zimamoto
Picture
Hili ndilo eneo la maegesho ya ndege kubwa aina ya Boeing 737 ambalo mwishoni mwamwezi huu linatarajiwa kuwa limekamilika


Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2H2wxliuB

Thursday, November 8, 2012

Rais Jakaya Kikwete Azindua Rasmi Ujenzi wa Bomba la Gesi Asilia toka Mtwara hadi Dar es salaam


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua rasmi ujenzi wa bomba la gesi asilia toka Mtwara hadi Dar es salaam leo Novemba 8, 2012 maeneno ya Kinyerezi njijini Dar es salaam. Nyuma yake ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na viongozi wengine wakimsikiliza  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo miundombinu ya  bomba la gesi asilia toka Mtwara hadi Dar es salaam leo Novemba 8, 2012 maeneno ya Kinyerezi njijini Dar es salaam. Nyuma yake ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na ujumbe wa kampuni inayojenga bomba la gesi asilia kutoka Mtwata hadi Dar es salaam, Benki ya Exim ya China na viongozi waandamizi wa serikali alipowakaribisha Ikulu kwa mazungumzo baada ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa bomba hilo maeneo ya Kinyerezi jijini Dar es salaam.Picha na IKULU

UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU MKOA WA DODOMA


 Barabara za katikati ya mitaa ya manispaa ya Dodoma zikiwa zinatengenezwa kwa kiwango cha Lami.
Wajasiriamali wakiwa wameweka biashara zao kwenye moja ya mageti ya makao makuu ya CCM,kipindi hiki cha mkutano mkuu kumekuwa na maongezeko ya mahitaji ya bidhaa za chama bora Tanzania,hivyo kutoa fursa kwa wafanya biashara wengi kuuza bidhaa za chama hicho.Picha na Adam Mzee-Dodoma

Sunday, August 26, 2012

BARABARA YA MLIMA SEKENKE ILIVYOHARIBIKA

Kutokana na kilichoelezwa kuwekwa kwa lami chini yakiwango katika mlima Sekenke mkoani Singida, imeharibika vibaya kama inavyoonyesha pichani magari yakipita kwa shida baada ya lami hiyo kubomoka kwa kipindi kifupi tangu iwekwe, kama ilivyokutwa jana.Picha na Joseph Senga

Tuesday, July 31, 2012

Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda Akagua Ujenzi wa Barabara Ya Kiwango Cha Lami Manispaa ya Dodoma

Mafundi wakijenga daraja katika barabara za eneo la Kisasa kwenye Manispaa ya Dodoma Julai 29,2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami katika manispaa ya Dodoma Julai 29, 2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Sunday, July 29, 2012

MAENDELEO YA UJENZI WA BARABARA KATI YA BANDARI YA MTWARA MPAKA ZAMBIA

Hii ndiyo bango la mradi huo wa ujenzi wa barabara inayotoka mnarani hadi bandarini ambayo inasimamiwa na kampuni ya SOUTHERN LINK.
Pia bila shaka kwa Manicipal ya Mtwara mjini hii ndiyo itakuwa barabara ya kwanza kwa ukubwa na kiwango cha ubora kuliko zingine ambazo zipo katika Manicipal hiyo.
Haya ni baadhi ya Magreda ya kampuni ya Southrn Link yakipiga mzigo kukamilisha barabara hiyo.
Sehemu ya wanawake ambao wamejipatia vibarua kwa muda katika barabara hiyo ili kukuzi mahitaji kidogo ya maisha yao.

Monday, July 23, 2012

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AZINDUA MRADI WA MAJI MBEYA

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Kamishna wa Maendeleo katika Jumuiya ya Ulaya Andris Piebalgs(wapili kushoto), balozi wa jumuiya ya ulaya nchini Cerian Philberto Sebregondi(kushoto),Balozi wa Ujerumani nchini Klaus Peter Brandes na Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe wakikata utepe kuzindua rasmi mradi wa maji safi na mazingira Mjini Mbeya.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Kamishna wa Maendeleo Jumuiya ya Ulaya Andris Piebalgs(Watau kushoto) na Waziri wa Maji Profesa JumANNE Maghembe wakikagua chanzo cha maji eneo la Swaya mjini Mbeya wakati wa uzinduzi wa mradi maji safi na mazingira mjni humo.

Wednesday, July 18, 2012

UJENZI WA BARA BARA YA IRINGA MAFINGA

Vifusi vikiwa vimepakiwa kwenye malori tayari kuwekwa kwenye Barabara ya Iringa - Mafinga.

Daraja la Kaingesa Sumbawanga mkoani Rukwa

Daraja la Kaingesa likiwa kwenye hatua za kukamilika hapa Sumbawanga mkoani Rukwa,Daraja hili ni moja ya madaraja kadhaa yanayojengwa kwenye barabara kuu ya kutoka Tunduma kwenda Sumbawanga.

Saturday, July 14, 2012

UJENZI WA BARABARA YA TUNDUMA MPAKA SUMBAWANGA WAENDELEA

Barabara ikiwa tayari imeshaanza kuwekewa lami
Daraja la MPUI
Daraja la LAELA
Vijana wakiwa kazini kurekebisha mifereji kwenye barabara hiyo mpya.Picha zote na Mdau Adam Mzee

Popular Posts