Pages

Showing posts with label Katavi. Show all posts
Showing posts with label Katavi. Show all posts

Wednesday, January 2, 2013

MKE WA WAZIRI MKUU MAMA TUNU PINDA ASHIRIKI MKESHA WA MWAKA MPYA SAMBAMBA NA TAMASHA LA WANAWAKE MKOANI RUKWA (RUKWA WOMEN IN ACTION)



Mama Tunu Pinda mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwasili katika ukumbi wa St. Maurus Chemchem Mjini Sumbawanga jana katika sherehe aliyoalikwa na Mkuu wa Mkoa Rukwa Injinia Stella Manyanya ya kuaga mwaka 2012 na kukaribisha mwaka 2013 iliyoenda sambamba na tamasha kubwa la mwanamke wa Rukwa RUWA (Rukwa Women in Actiion). Tamasha hilo lililobuniwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa lina lengo la kuwanunganisha wanawake wa Mkoa wa Rukwa pamoja katika tamaduni zao tofauti katika kuwainua kiuchumi na kifikra ambapo walishiriki kwa kuonyesha tamaduni zao za ngoma, mavazi na chakula. Lengo la tamasha hilo pamoja na umoja huo ni kwa ajili ya kunadi na kuhamasisha utalii wa ndani, kuwawezesha kinamama wa kipato cha chini, kuhamasisha na kuwezesha vita dhidi ya umaskini, mimba za mashuleni, lishe bora na chanjo za afya kwa watoto wachanga na wanawake wa kipato cha juu kuwawezesha wa kipato cha chini.
Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitoa hotuba yake katika tamasha hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza katika tamasha hilo kumkaribisha mke wa Waziri kuzungumza na washiriki zaidi ya mia sita walihudhuria katika tamasha hilo.
Mama Pinda (kulia), Mama Dora Rajab Rutengwe mke wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi (wa pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Stella Manyanya na wanawake wengine wakijumuika kucheza muziki wa kwaito katika kupasha misuli moto kwenye tamasha hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akionyesha vazi linalotangaza utalii wa ndani na rasilimali muhimu kama misitu, wanyama pori, na samaki.
Ilifika muda washiriki wa maonyesho hayo kupita mbele ya jukwaa kuu tayari kwa kuanza kuonyesha sanaa na mitindo mbalimbali.
Mmoja ya washiriki akionyesha moja ya vazi la kiutamaduni la asili ya makabila ya Rukwa kwa wazee wakati wa msimu wa baridi.
Katibu tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akisakata ngoma ya kinyaturu katika tamasha hilo. Kulia ni mwanae Hussein Chima.
Mama Tatu Chima mke wa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa akimpa zawadi ya shanga za kabila la kinyaturu Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda kabla ya kuanza kucheza ngoma ya kabila hilo. Kulia ni mumewe Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (wa pili kushoto) Injinia Stella Manyanya akishiriki kwenye ngoma ya kabila lake la wangoni waliojumuika kwenye tamasha hilo kuonyesha baadhi ya tamaduni zao. Wa kwanza kushoto akionyesha uwezo mkubwa katika kusakata ngoma hiyo ni mwandishi wa habari wa channel ten Judy Ngonyani.  
Mduara pia umo katika ngoma za kabila la wangoni. 
Washiriki wa kabila la wahaya wakionyesha baadhi ya mavazi ya asili ya kabila lao.
Ngoma za kihaya.
Majaji waliohusika katika katika mashindano ya tamaduni za makabila tofauti ya Mkoani Rukwa, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Kagera, Singida, Kigoma, Shinyanga na Mwanza. Mkoa wa Rukwa ulishinda katika Ngoma.
 Washiriki wa kabila la wafipa wakionyesha baadhi ya mavazi yao ya asili na baadhi ya zana zao za asili. 
 Sound ya ngoma ya kabila la wafipa ikitumbuiza katika tamasha hilo.Kigoda hutumika kusugua chungu ambacho hutoa mlio wa aina yake katika kunogeza ngoma ya kabila hilo.
 Washiriki wa kabila la wafipa wakionyesha tamaduni zao za kusaga unga na ulezi kwa kutumia zana za asili.
 Pombe ya asili ya kabila la wafipa inayotengenezwa kwa ulezi na kunyewa kwa mirija, raha duniani.
 Mambo yetu ya rusha roho nayo yalikuwepo. 
 Palikuwa hapatoshi.
Mvua ya shampen ya kukarisha mwaka mpya 2013 ikifunguliwa na mratibu wa tamasha hilo ambae pia ni Afsa maendeleo ya jamii Mkoa wa Rukwa Ndugu Deonisya Njuyui.
 Cheers kwa mwaka 2013. Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu akigonganisha glass na Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali watu Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashalla na Mke wa aliyekuwa Mbunge jimbo la Sumbawanga Mjini CCM Aeshi Hillal.
 Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Idd Kimanta akinywa togwa iliyoandaliwa na kabila la wahaya.
 Mbunge wa Jimbo la Kalambo Josephat Kandege nae akilamba tongwa.
 Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya wakionja ugali wa muhogo ulioandaliwa na kabila la Waha kutoka Kigoma.
 Ndizi kuku au Kuku ndizi kutoka katika kabila la wanyakyusa la Mkoani Mbeya.
 Maharage yaliyochanganywa na mboga za majani kutoka katika kabila la wanyakyusa la Mkoani Mbeya.
 Mshiriki Leah Mgagama kutoka katika kabila la wangoni akionysha moja ya vazi la kabila hilo na kifaa cha kuhifadhia chakula kisiharibike kijulikanacho kwa jina la "Kijamanda".
 Vazi la kitanzania likiwa na bandera ya taifa.
 Ilikuwepo mitindo mbalimbali ya mavazi.
 Onyesho la mavazi
 Onyesho ya vazi la mjamzito.
 Anthonia Nkyabonaki kutoka kabila la wahaya akionyesha mtindo wa mavazi.Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa

Monday, September 3, 2012

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Ajionea Ukame Ulioikumba Hifadhi ya Taifa ya Katavi

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama viboko waliosongamana kwenye chemichemi ili kujinusuru na ukame ulioikumba Hifadhi ya Taifa ya Katavi, Septemba 2, 2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Monday, July 23, 2012

DC AWAFUKUZA WACHINA WALIOKUWA NA MGODI KINYUME NA SHERIA KATAVI

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe(kulia) akiwa katika eneo la msitu wa Hifadhi ya Katavi, eneo maarufu kwa jina la lyamba lya mfipa.
Na Kibada Kibada-Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Rajabu Rutengwe ameagiza kampuni ya utafiti na uchimbani madini ya Red O-Mining ltd kutoka China kusimamisha mara moja shughuli zote za utafiti kwa kuwa wamekiuka sheria za nchi kwa kufanya utafiti ndani ya pori la hifadhi ya wanyama la Rukwa Lukwati lililoko Hifadhi ya Taifa ya Katavi kinyume na sheria.
Mkuu huyo wa Mkoa alitoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kuwa wawekezaji hao wanafanya shughuli za utafiti na uchimbaji wa Madini katika pori hilo la hifadhi kinyume na taratibu za kisheria za nchi pamoja na kuwa wanayo leseni ya kufanya utafiti inayowaruhusu waliyoipata kutoka wizara ya nishati na Madini lakini hawana kibali kinachowaruhusu kufanya utafiti ndani ya hifadhi.
Pamoja na kupata leseni hiyo walipatiwa barua kutoka wizara ya Maliasili na Utalii na idara ya mazingira inayowaelekeza kuwa wakifika eneo la kufanyia utafiti wawaone wamiliki wa eneo kupitia ofisi za wanyama pori wilaya husika,ya Mpanda lakini hawakufanya hivyo, badala yake waliamua kuingia katika pori hilo la hifadhi la Katavi na kuendelea na shughuli zao za kiutafiti bila kuwa na kibari cha kufanya shughuli hizo ndani ya hifadhi kwa kuwa ni kinyume na taratibu.
Miongoni mwa mambo ya msingi ambayo Ujumbe wa Mawaziri na manaibu waziri wakiongozwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa, Ndugu Nape Nnauye waliyaongelea na kutaka yachukuliwe hatua za haraka ni pamoja na utunzaji wa mazingira, matatizo ya Ardhi na suala la Kampuni hiyo ya Utafiti wa Madini na Shamba la EFATHA MINISTRY.

Monday, July 16, 2012

MKUTANO WA VIONGOZI WA CCM MKOANI KATAVI

Naibu Waziri TAMISEMI,Mh.Aggrey Mwanri akihutubia wananchi wa Mpanda mkoani Katavi,ambapo aliwasihi kutokubali kudanganywa danganywa na pia aliwaambia wananchi serikali hii isingependa kuona wananchi wa chini akionewa, hivyo alitoa tamko la kutowalipisha ushuru wakina mama wafanya biashara ndogo ndogo mfano vitumbua na chapati.
Naibu Waziri Kilimo na chakula,Mh. Adam Malima akihutubia wananchi wa mkoa wa Katavi, juu ya masuala mabali mbali ambayo yametekelezeka likiwemo suala la umeme na pia aliwaambia wakulima kwamba serikali imeandaa utaratibu mzuri wa vocha za kilimo ambazo utatangazwa hivi karibuni.
Naibu Waziri Wizara ya Uchukuzi,Mh. Charles Tizeba akizungumzia masuala ya kuimarisha reli na pia utunzaji wa treni zetu ikiwa suala zima la usafi, pia aliwaambia wananchi serikali imeagiza mabehewa ya abiria na ya mizigo.
Mh.Nape akihutubia wananchi wa Mpanda waliofurika kwenye uwanja wa Kashaulili,ambapo alikemea vikali vitendo vya vyama vingine kuendekeza vurugu badala ya siasa.
Mh.Mwigulu Mchemba akieleza wananchi masuala muhimu ya kiuchumi na kwa nini kunakuwa na mfumuko wa bei,pia alitumia fursa hiyo kukemea mauaji yalotokea kwenye jimbo lake ambapo kijana mmoja kiongozi wa chama aliuawa na wanachama wa chama cha upinzani
Viongozi wakuu wa Chama cha Mapinduzi wakishiriki maandamano kuelekea kwenye uwanja wa Kashaulili wilaya ya Mpanda.
Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa-Itikadi na Uenezi, Mh. Nape Nnauye akisalimiana na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa wilaya ya Mpanda, mkoa wa Katavi

Thursday, July 12, 2012

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Ashiriki Mazishi Ya shemeji yake, Mzee Sadik Ismail

Waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa Mzee Sadik Ismail Katila, shemiji yake Waziri Mkuu Mizengo Pinda, katika mazishi yaliyofanyikaMjiniMpanda Julai 10, 2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka udongo kwenye kaburi la shemeji yake, Mzee Sadik Ismail Katila katika mazishi yaliyofanyika mjini Mpanda Julai 10,2012. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Tuesday, July 10, 2012

BABA MZAZI WA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AFARIKI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda amefiwa na baba yake, imefahamika.Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Jenista Mhagama alitoa taarifa hiyo bungeni mchana huu wakati akiahirisha kikao cha asubuhi cha mkutano uliokuwa ukijadili hoja ya bajeti ya Wizara ya Maji.

Mhe. Jenista alisema kuwa Pinda hatakuwepo bungeni kwa vile amekwenda kushughulikia msiba wa baba yake. Akaongeza kuwa kwa sababu ya msiba huo, Waziri Mkuu amemteua Waziri wa Afrika Mashariki, Mhe. Samwel Sitta kuwa mkuu wa shughuli za serikali bungeni kuanzia leo (Julai 10) hadi Julai 15.
--
Viongozi Mbalimbali Walimtembelea Baba Mzazi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Rais Jakaya Kikwete akipokea zawadi ya kuku kutoka Mama Albertina Kasanga ambaye ni Mama mzazi wa Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda wakati Rais Kikwete alipowatembelea akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Mpanda, Rukwa. Kushoto ni Mzee Xaveri Kayanza Pinda, Baba yake Waziri Mkuu.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Baba mzazi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Exavery Kayanza Pinda, wakati alipokuwa akipita kuelekea Kijiji cha Mwamapuli akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi Februari 20. 2012. Kulia nia Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Eng. Stella Manyanya.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitaniana na Mzee Kayanza Pinda alipokuwa anamuaga kuelekea kwenye mahafali ya Shule ya Sekondari Usevya ambapo alienda kumuwakilisha Waziri Mkuu aliyekuwa amealikwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye mahafali hayo. Miongoni mwa utani alioutoa Mzee Pinda ni pamoja na kumuita Mkuu huyo wa Mkoa "Mnyatomato" kumaanisha kuwa ni Mtoto wa Manyanya ambapo nyanya kwa kiingereza ni Tomato. Hahahahaaah!

BABA MZAZI WA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AFARIKI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda amefiwa na baba yake, imefahamika.Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Jenista Mhagama alitoa taarifa hiyo bungeni mchana huu wakati akiahirisha kikao cha asubuhi cha mkutano uliokuwa ukijadili hoja ya bajeti ya Wizara ya Maji.

Mhe. Jenista alisema kuwa Pinda hatakuwepo bungeni kwa vile amekwenda kushughulikia msiba wa baba yake. Akaongeza kuwa kwa sababu ya msiba huo, Waziri Mkuu amemteua Waziri wa Afrika Mashariki, Mhe. Samwel Sitta kuwa mkuu wa shughuli za serikali bungeni kuanzia leo (Julai 10) hadi Julai 15.
--
Viongozi Mbalimbali Walimtembelea Baba Mzazi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Rais Jakaya Kikwete akipokea zawadi ya kuku kutoka Mama Albertina Kasanga ambaye ni Mama mzazi wa Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda wakati Rais Kikwete alipowatembelea akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Mpanda, Rukwa. Kushoto ni Mzee Xaveri Kayanza Pinda, Baba yake Waziri Mkuu.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Baba mzazi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Exavery Kayanza Pinda, wakati alipokuwa akipita kuelekea Kijiji cha Mwamapuli akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi Februari 20. 2012. Kulia nia Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Eng. Stella Manyanya.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitaniana na Mzee Kayanza Pinda alipokuwa anamuaga kuelekea kwenye mahafali ya Shule ya Sekondari Usevya ambapo alienda kumuwakilisha Waziri Mkuu aliyekuwa amealikwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye mahafali hayo. Miongoni mwa utani alioutoa Mzee Pinda ni pamoja na kumuita Mkuu huyo wa Mkoa "Mnyatomato" kumaanisha kuwa ni Mtoto wa Manyanya ambapo nyanya kwa kiingereza ni Tomato. Hahahahaaah!

Popular Posts