Pages

Wednesday, October 24, 2012

Rais wa Zanzibar Dk Ali Shein Awaapisha Makatibu Wakuu Wapya Zanzibar


Nd,Mussa Haji Ali, Muda mfupi baada ya kuapishwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar,leo
Dk.Juma Malik Akili,Katibu Mkuu Wizara ya Miundimbinu na Mawasiliano.
Ali Khalil Mirza, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Makaazi Maji na Nishati.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Nd,Mussa Haji Ali, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar,leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Dk.Juma Malik Akili, kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,katika hafla iliyofanyika IkuluMjini Zanzibar leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akibadilishana mawazo na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,baada ya kuwaapisha Makatibu wakuu wa Wizara mbali mbali na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa Zanzibar,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar,leo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Kikwete Afungua Mkutano Mkuu wa nane wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Mjini Dodoma


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa UVCCM Bw. Benno Malisa alipowasili ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufungua Mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya hiyo ya vijana wa chama tawala leo Oktoba 23, 2012
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi toka kwa  Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa UVCCM Bw. Benno Malisa katika  ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya hiyo ya vijana wa chama tawala leo Oktoba 23, 2012
Nderemo baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwasili ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufungua Mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya hiyo ya vijana wa chama tawala leo Oktoba 23, 2012.
Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa UVCCM Bw. Benno Malisa akihutubia katika  ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya hiyo ya vijana wa chama tawala leo Oktoba 23, 2012
Meza kuu na sehemu za wajumbe katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya hiyo ya vijana wa chama tawala leo Oktoba 23, 2012
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano huo
Bendi ya muziki ya Vijana Jazz Orchestra 'Wana Pambamoto' ikitumbuiza kwa wimbo maalumu katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma ikiwa ni shamra ya kufungua Mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya hiyo ya vijana wa chama tawala leo Oktoba 23, 2012
 Wanachama wa umoja wa vijana kutoka nchi rafiki mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na wajumbe baada ya kufungua mkutano huo
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na viongozi wa Chipukizi wa  UVCCM
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na viongozi wa UVCCM pamoja na ujumbe wa viongozi wa jumuiya za vijana toka nchi mbalimbali marafiki.Picha na IKULU

Monday, October 22, 2012

President Banda in Dubai for World Energy Forum


Malawi’s President Mrs. Joyce Banda on Sunday arrived in Dubai, the United Arab Emirates (UAE), where she is expected to address the 2012 World Energy Forum in the Persian Gulf city on Monday, October 22, 2012.
“Indeed, the President has arrived in Dubai for this extremely important Summit. She arrived around twenty minutes to seven (twenty minutes to five, Malawi time) in the morning.
“As you are aware, Energy is one of the five major priority areas that the Government of Malawi has singled out for attention in line with the Economic Recovery Plan (ERP) launched recently. It is therefore extremely important that the President shares her vision with her counterparts and the international community as regards the energy sector development in Malawi,” said Tusekele Mwanyongo, State House Press Officer, in a telephone interview from Dubai.
At the Summit, the President is also expected to participate in the signing ceremony by Heads of State to declare October 22, as the ‘World Energy Day’, according to the Press Officer.
President Banda in Dubai.-Photo by Govati Nyirenda/Mana
The President was met on arrival at Dubai International Airport by senior UAE Government officials, Malawi’s Ambassador to Kuwait, Younos Abdul Karim, Malawi’s Minister of Environment and Climate Change Management and her deputy, Catherine Gotani Hara and Ibrahim Matola, respectively, Deputy Malawi Ambassador to Kuwait, Alison Liwanda, Secretary for Environment, Dr. Yanira Ntupanyama and CEO for the Malawi Regulatory Authority (MERA), Dr. Alex Chiwaya, among others.
The World Energy Forum 2012 will be held from October 22-24, 2012 in under the patronage of His Highness Sheikh Mohammad Bin Rashid Al Maktoum, Vice President and Prime Minister of the United Arab Emirates and Ruler of Dubai. This will be the first time that this High-Level International Energy Conference will be taking place outside the headquarters of the United Nations.
The United Nations has designated 2012 as the International Year of Sustainable Energy for All. At the Forum, leaders from Member States of the United Nations, international organizations, and corporations will seek tangible progress towards cleaner, safer, and more sustainable energy as well as achieving universal access to modern energy services.
While in Dubai, President Banda is also scheduled to meet various international investors interested to invest in the Energy Sector in Malawi as well as Airports, Roads, Highways, Industrial and Institutional Projects.
According to Mwanyongo, the President is also scheduled to meet Malawians living in the United Arab Emirates.
One of the primary objectives of this conference is to chart a roadmap for a sustainable energy mix that can fuel global economic and social development. The forum provides a unique opportunity to exchange new ideas on global energy issues from the perspectives of policy, technology, and business.
The World Energy Forum 2012 is expected to be attended by over two thousand delegates, including several heads of state, scores of national energy ministers, and top leaders from the industry.
Deputy Envoy Liwanda welcomes President Banda.-Photo by Govati Nyirenda

Kilele cha mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)Mjini Dodoma


Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiiimba na kucheza nyimbo mbalimbali katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma alipowasili leo kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
Mwenyekiti wa UWT  Sophia Simba akiongea katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma baada ya kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa UWT  Sophia Simba na Katibu Mkuu Amina  Makilagi katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma baada ya kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
Sehemu ya wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT wakicheza segere
Sehemu ya wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT
Wanachama wakongwe wa UWT na CCM wakishangilia
Sehemu ya wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT wakirushwa na Sizya Mazongela wa kundi la Segere
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wakongwe wa UWT katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma  baada ya kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wake wa viongozi katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma baada  kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
  Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na wanachama wakongwe wa UWT Ikulu ndogo Dodoma katika mchaplo aliowaandalia wajumbe wa Umoja huo baada ya kutoka katika  ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).Picha na IKULU

Maalim Seif Sharif Hamad:'CUF itaendelea kuwaunganisha Watanzania.'


 Wafuasi na wapenzi wa CUF wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad wakati akiwahutubia katika viwanja vya Buguruni jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akiwahutubia wafuasi ya wapenzi wa chama hicho katika viwanja vya Buguruni jijini Dar es Salaam.
  Aliyekuwa Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa ADC Bw. Al-Badawi akizungumza katika mkutano wa hadhara wa CUF baada ya kuamua kurejea CUF akitokea ADC. Kabla ya kwenda ADC na baadae kurejea CUF Al-Badawi alikuwa mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Temeke
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akimkabidhi shati la chama hicho kijana Joseph Christian ambaye alikuwa katibu mwenezi wa CHADEMA tawi la Chuo Kikuu Dodoma. Joseph amekihama CHADEMA na kujiunga na CUF kwenye mkutano wa hadhara huko Buguruni jijini Dar es Salaam.Picha na Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar 
---
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amesema chama chake kitaendelea kutetea na kutekeleza sera yake ya kuwaunganisha watanzania popote walipo bila ya ubaguzi wa aina yoyote. 

Amesema operesheni mchakamchaka hadi mwaka 2015 iliyozinduliwa na chama hicho hivi karibuni imekuwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera hiyo,na kwamba tayari imeanza kuleta mafanikio katika mikoa iliyoanza kutekelezwa ukiwemo mkoa wa Arusha.


Maalim Seif ametoa kauli hiyo katika viwanja vya Buguruni jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwahutubia wafuasi na wapenzi wa chama hicho kwenye mkutano maalum wa hadhara uliolenga kuwakaribisha wanachama wapya na kuwapokea wanachama walioamua kurejea CUF baada ya kukihama na kuhamia vyama vyengine.Katika mkutano huo Maalim Seif aliwapokea na kuwapa kadi za chama hicho wanachama kadhaa walioamua kurejea chama hicho wakitokea chama cha ADC wakiongozwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa ADC Bw.Al-Badawi.

Kabla ya kujiunga na ADC, Bw. Al-Badawi alikuwa mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Temeke, na sasa ameamua kurejea CUF kwa kile alichokieleza kuwa ni ubabaishaji ndani ya chama hicho kipya kinachohusishwa na mbunge wa jimbo la Wawi Mhe. Hamad Rashid Mohd.
Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema Tanzania imekuwa ikipita katika kipindi kigumu cha migogoro na uvunjifu wa amani, mambo ambayo yanapaswa kupigwa vita ili kurejesha hali ya amani na kuvumiliana.
Amedai kuwa chanzo kikuu cha migogoro ya kijamii ikiwemo ya ardhi na mizozo ya kidini inatokana na kutokuwepo kwa mikakati imara ya kuendesha nchi, na kwamba viongozi wanapaswa kujifunza kutokana na migogoro hiyo, ili kuweka mikakati imara ya kuendesha nchi kwa uhakika. 
 
“Nchi haiendeshwi kwa kuigiza, bali kwa kuwa na viongozi wenye dira ya mabadiliko kwa maendeleo ya wananchi”, alisisitiza Maalim Seif.
Amesema kutokana na viongozi kutokuwa na dira na mikakati imara ya kuendesha nchi, Watanzania wameshindwa kunufaika na rasilimali za nchi yao ambazo ni nyingi na zinaweza kuwabadilisha kiuchumi.
Amefafanua kuwa iwapo wananchi watanufaika moja kwa moja na rasilimali zao, wataweza kuzitunza na kuzilinda ili ziwe endelevu, na kwamba kinyume chake ni kuzihujumu rasilimali ambazo watahisi haziwanufaishi.
“Popote pasipo na haki hakuna amani, tunataka kila Mtanzania ajihisi kuwa ana haki sawa katika nchi hii, sio kuwa na raia wa madaraja, yaani daraja la kwanza, la pili na latatu”,alifahamisha huku akishangaliwa na umati wa watu waliojitokeza kwenye mkutano huo.
Katika hatua nyengine, aliyekuwa katibu mwenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika tawi la Chuo Kikuu Dodoma bw. Joseph Christian amejiengua katika chama hicho na kujiunga na CUF.
Akizungumza katika mkutano huo bw. Joseph amesema ameamua kujiengua CHADEMA na kujiunga na CUF kwa madai kuwa chama hicho kimekuwa kikiendeshwa kwa misingi ya undugu na ukabila, na kuwatelekeza vijana wenye lengo la kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini.
Amewatahadhamisha vijana kuwa makini na sera za chama hicho na kuacha kukurupuka kuvamia sera za vyama wasivyovifahamu.Nae Mwenyekiti wa ADC Wilaya ya Kinondoni Bw. Saburi Mtoro, ambaye pia ameamua kukihama chama hicho na kujiunga na CUF amemuahidi Katibu Mkuu wa CUF kuwa wanachama wote wa ADC katika Wilaya hiyo watajiunga na CUF.

UFUNGUZI WA MKUTANO WA AKINA MAMA WAJASIRIALIAMALI KUTOKA NCHI ZA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa akina Mama Wajasiliamali kutoka Nchi za Ukanda wa Afrika, uliofanyika leo Oktoba 22, kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, ukiwa ni mkutano wa kwanza kufanyika nchini Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa akina Mama Wajasiliamali kutoka Nchi za Ukanda wa Afrika, uliofanyika leo Oktoba 22, kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, ukiwa ni mkutano wa kwanza kufanyika nchini Tanzania. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

VIONGOZI WAPYA WA IDARA YA IDARA YA WANYAMAPORI HAWA HAPA


  Prof.Jafari Ramadhani Kideghesho, Mkurugenzi Msaidizi, Matumizi Endelevu ya Wanyamapori
   Prof. Alexander Nyangero Songorwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.
--

Profesa Alexander Nyangero Songorwa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori (Wildlife Division ) kuziba nafasi iliyokuwa wazi.Kabla ya kuteuliwa Profesa Nyangoro alikuwa Profesa Mshiriki katika Usimamizi wa Wanyamapori, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro. Pia ndiye aliyekuwa Mkuu wa Idara hiyo ya Usimamizi wa Wanyamapori SUA.

Wakati huohuo, Profesa Jafari Ramadhani Kideghesho ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi, kuiongoza Sehemu ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori (Sustainable Utilisation of Wildlife Section). Kabla ya uteuzi huo Profesa Ramadhani alikuwa Profesa Mshiriki katika Usimamizi wa Wanyamapori katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro.
Uteuzi huo umetekelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bibi Maimuna Tarishi kwa mamlaka aliyo nayo kwa mujibu wa kifungu cha 6 (1) (b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002. Utekelezaji wa
uteuzi huo ni kuanzia tarehe 24 Septemba 2012.
 
Mkurugenzi mpya wa wanyamapori, Profesa. Songorwa, ni msomi katika fani ya Wanyamapori. Anayo shahada ya kwanza (B.Sc.) ya Sayansi katika Zoolojia na Ekolojia ya Wanyamapori ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (mwaka 1987), Shahada ya uzamili (MSc) katika Mipango na Maendeleo Vijijini ya ChuoKikuu cha Guelph, Ontario, Canada (1994) na shahada ya uzamivu (PhD) katika Uhifadhi Maliasili ya Chuo Kikuu cha Lincoln, New Zealand (1999).
 
Kabla ya kujiunga na SUA mwaka 2001, Prof. Songorwa alikuwa mwajiriwa wa Idara ya Wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utalii kuanzia mwaka 1982.
 
Akiwa Wizarani Profesa Songorwa alihudumu katka nafasi mbali mbali zikiwemo Askari Wanyamapori, Mkuu wa Kanda na Msaidizi wa Mkuu wa Mradi katika Pori la Akiba la Selous. Pia alihudumu kama Afisa Mwandamizi katika Mradi wa Uhifadhi Shirikishi wa Wanyamapori, Makao Makuu, Dar es salaam.

Naye Profesa Kideghesho siyo mgeni katika Idara ya Wanyamapori. Kabla ya kujiunga na na SUA mwaka 1999 Prof. Kideghesho alikuwa mwalimu katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka (CAWM-Mweka), Moshi kuanzia 1993.

Kitaaluma Prof. Kideghesho ana shahada ya kwaza (B.Sc.) katika Kilimo ya SUA (1993), Shahada ya Uzamili (MSc) katika Biolojia ya Uhifadhi ya Chuo Kikuu cha Kent, Uingereza (1996), na Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Norway kilichopo mjini Trondheim (2006).

George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Simu 0784 468047
22 Oktoba 2012 

Bandari Dar Mabingwa Inter-Ports Games


Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mh. Baraka Konisaga akikabidhi kikombe cha ushindi wa kwanza kwa mwakilishi wa washindi wa kwanza wa mpira wa kikapu, Kisanta kutoka Makao Makuu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania mara baada kukamilika kwa michezo ya inter-ports iliyofanyika jijini Mwanza hivi karibuni.
 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mh. Baraka Konisaga akikabidhi kikombe cha ushindi kwanza wa michezo ya inter-ports, kapteni wa timu ya mpira wa pete, Judith Ilunda kutoka Bandari ya Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mh. Baraka Konisaga akikabidhi kikombe cha ushindi kwanza wa michezo ya inter-ports, kapteni wa timu ya mpira wa miguu, Vitalis Salila wa Bandari ya Dar es Salaam.
---
Na Mwaandishi Wetu
Bandari ya Dar es Salaam imeibuka na ushindi wa jumla katika michezo ya inter-ports games ambayo imefanyika jijini Mwanza hivi karibuni na kufungwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mh. Baraka Konisaga.

Michezo hiyo imefanyika jijini huko kwa muda wa siku tano ambapo zaidi ya wanamichezo 400 wafanyakazi wa Bandari walishiriki michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu, pete, kikapu, riadha, bao na kuvuta kamba.

Akizungumza kabla ya kukabidhi vikombe na zawadi nyingine kwa wanamichezo hao, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana aliwaasa wanabandari kuendelea kushiriki michezo kwa ajili ya kujenga afya zao lakini kubwa zaidi kutekeleza majukumu yao ya kila siiku kwa ufanisi.
“Leo isiwe mwisho wa kushiriki michezo endeleeni kushiriki ili kuoboresha afya zenu lakini pia niwashauri kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi na mkumbuke kwamba mmepewa dhamana kubwa na taifa lenu hivyo ni wajibu wenu kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa,” amesema Konisaga.

Katika michezo hiyo Bandari ya Dar es Salaam iliibuka na vikombe vingi zaidi ambapo katika mpira wa soka waliibuka washindi wa kwanza kwa kujinyakulia alama nyingi huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Makao Makuu.

Kwa upande wa mpira wa pete mshindi ni Bandari ya Dar es Salaam na nafasi ya pili ilinyakuliwa na Bandari ya Tanga. Katika mchezo wa kikapu nafasi ya kwanza ilikwenda Makao Makuu wakati Bandari Tanga wakinyakua nafasi ya pili.

Nafasi ya kwanza ya mchezo wa kuvuta kamba wanaume ilikwenda kwa Bandari ya Dar es Salaam na nafasi ya pili ilinyakuliwa na Bandari ya Tanga.   Mchezo wa kamba wanawake nafasi ya kwanza ilikwenda kwa Bandari ya Dar es Salaam na Bandari ya Tanga ilishika nafasi ya pili.
Kwa upande wa riadha Bandari ya Dar es Salaam iliibuka tena kidedea huku Bandari ya Tanga ikishika nafasi ya pili. Kwa upande wa wakimbiaji mita mia moja kwa wanawake medali ya dhahabu ilikwenda kwa mkimbiaji kutoka Makao Makuu, medali ya fedha ilikwenda kwa mkimbiaji wa Bandari ya Tanga na mshindi wa tatu alikuwa mkibiaji kutoka Bandari ya Dar es Salaam aliyeibuka na medali ya shaba.

Kwa upande wa wakimbiaji wa mita mia moja wanaume medali ya dhahabu ilichukuliwa na mkimbiaji wa Bandari ya Dar es Salaam, fedha mkimbiaji wa Bandari ya Dar es Salaam na shaba ilikwenda kwa mkimbiaji kutoka Bandari za Maziwa (Mwanza, Kigoma na Kyela).
Kwa upande wa mita mia nne wanawake dhabau ilikwenda Bandari ya Dar es Salaam, fedha ilikwenda Bandari ya Dar es Salaam na shaba ilikwenda kwa mkimbiaji wa Makao Makuu. Kwa upande wa mita mia nne wanaume dhahabu ilikwenda Tanga, fedha ilikwenda Makao Makuu na shaba ilinyakuliwa na Bandari ya Dar es Salaam.

Kwa upande wa mchezo mkongwe na wa jadi maarufu kama bao, Bandari ya Dar es Salaam iliibuka tena na ushindi wakati nafasi ya pili ilikwenda kwa Bandari ya Tanga. Kwa upande wa wachezaji bora wa kila mchezo, mlinda mlango mahiri wa timu ya Mtwara, Douglas Bahati aliibuka mshindi.

Kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete, Matalena Mhagama ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa aliibuka kidedea na nafasi ya kwanza. Kwa upande wa timu bora ya kuvuta kamba Makao Makuu waliibuka na ushindi huku Bandari ya Mtwara ikiibuka na ushindi wa timu bora ya kuvuta kamba wanaume.

Mchezaji bora wa riadha ni Lucy Kyoma kutoka Bandari ya Dar es Salaam. Bandari zilizoshiriki katika michezo hiyo ni pamoja na Bandari Dar es Salaam, Mtwara, Tanga, Mwanza, Kyela, Kigoma na Makao Makuu yenyewe. Michezo hiyo hufanyika mara moja kila mwaka kwa kuwashirikisha wanabandari na hufanyika mara moja kwa kila kituo.

-mwisho-

Popular Posts