Pages

Showing posts with label Morogoro. Show all posts
Showing posts with label Morogoro. Show all posts

Friday, August 31, 2012

TAMKO LA CHADEMA KUHUSU MAUAJI MKOANI MOROGORO

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapinga kauli za Serikali, Jeshi la Polisi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) zenye kulipotosha taifa kuhusu mashambulizi na mauji yanayoelezwa kufanywa na askari Mkoani Morogoro na badala yake kinataka uchunguzi huru ufanyike haraka kwa mujibu wa Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (Inquest Act).

Kauli zilizotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani zina mwelekeo wa kulilinda Jeshi la Polisi ambalo askari na maofisa wake ni sehemu ya watuhumiwa wa mauaji, badala ya kuwezesha ukweli kuthibitika na hatua kuchukuliwa kwa wahusika.

Hivyokutokana na kujirudiarudia kwa mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola CHADEMA kinatoa mwito kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye kwa mujibu wa katiba ibara ya 33 ni mkuu wa nchi, kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu aingilie na kuwezesha uchunguzi wa kina.

Ikumbukwe kwamba tarehe 27 Agosti 2012 Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro lilifyatua risasi za moto na kupiga mabomu ya machozi wananchi na wanachama wa CHADEMA waliokuwa wamejikusanya kwa ajili ya kuelekea kwenye mkutano halali wa CHADEMA na wengine waliokuwa wakiendelea na shughuli zao eneo la Msamvu, hivyo kusababisha kifo cha raia mmoja asiye na hatia na kujeruhi wengine wawili.

CHADEMA kinaukumbusha umma kwamba kwa mauaji hayo na mengine katika maeneo mbalimbali nchini serikali inayoongozwa na CCM kupitia vyombo vya dola inaendelea kukiuka Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inatambua kwamba uhai ni haki ya msingi kwa raia wote.

CHADEMA hakikubaliani na hatua zilizochukuliwa na Serikali mpaka sasa kuhusu tukio husika pamoja na maelezo yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani tarehe 28 Agosti 2012 ambayo kwa sehemu kubwa yametokana na taarifa zisizo za kweli kutoka kwa maofisa wa Jeshi la Polisi ambao ni sehemu ya watuhumiwa wa mauaji husika.

CHADEMA haina imani na timu iliyoundwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi kuchunguza tuhuma za askari kufyatua risasi na mabomu ya machozi na kusababisha mauaji kwa kuwa tayari serikali na Jeshi la Polisi wametoa maelezo yenye kutofautiana kwa kiwango kikubwa na maelezo ya mashuhuda waliokuwepo na ushahidi wa picha za eneo la tukio.

Wakati Serikali na Jeshi la Polisi wakitoa maelezo kuwa marehemu alikutwa umbali wa mita 300 na kupelekwa hospitali na wasamaria wema, mashuhuda wameeleza wazi kuwa askari walifika jirani na eneo lake na ofisa mmoja akaonyesha ishara na ndipo risasi za moto na mabomu ya machozi yakafyatuliwa mojawapo kumpata marehemu na kudondoka.

Mashuhuda wote waliohojiwa wanaeleza kwamba bunduki ya polisi ndiyo ilielekezwa na kufyatuliwa kwa marehemu, maelezo pekee yanayotofautiana ni kuwa baadhi wameeleza kuwa ni bunduki ya risasi za moto na wengine wa wameeleza kuwa ni bunduki ya kufyatulia mabomu ya machozi.

Mara baada ya kudondoka gari hilo liliondoka na gari lingine la polisi lilifika likiongozwa na Kamanda wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia cha Mkoa ambaye alitoa amri ya gari lingine kumbeba Ali Hassan Singano (Zona) na kuondoka naye, hivyo si kweli kwamba matukio hayo yalitokea mbali na eneo bali pembeni ya meza ya muuza magazeti huyo karibu na barabara ya kwenda Iringa eneo ambalo polisi ilikuwa ikifanya mashambulizi.

Kauli zilizotolewa na Serikali kuwa Jeshi la Polisi lilizuia maandamano ya CHADEMA yaliyopangwa kufanyika Mkoani Morogoro kwa sababu ya sensa ya watu na makazi si za kweli kwa kuwa sababu pekee zilizotolewa ni ufinyu wa barabara na kuwa maandamano yalipangwa siku ya kazi. Ushahidi wa suala hili ni barua ya Jeshi la Polisi lenyewe ya 23 Agosti 2012 yenye Kumb. Na. MOR/A.25/1/VOL. II/202.

CHADEMA kinaujulisha umma kwamba Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro ndilo lililoacha kuheshimu utawala wa sheria na makubaliano yaliyofikiwa baada ya mazungumzo yaliyohusisha kikosi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kikiongozwa na Kamanda wa Operesheni za Jeshi hilo Simon Siro na hivyo kuwa chanzo cha mauaji yaliyotokea na madhara mengine kwa wananchi waliokuwepo maeneo yaliyorushiwa mabomu ya machozi.

Ikumbukwe kwamba awali CHADEMA kilipanga kufanya maandamano na mikutano katika Jimbo la Morogoro Mjini tarehe 4 Agosti 2012 na kuwasilisha taarifa kwa Jeshi la Polisi kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo, Polisi wakakataa kufanyika kwa maandamano na mikutano kwa kisingizio cha Sikukuu ya Nanenane, mgomo wa walimu na ratiba kugongana na ile ya mikutano ya CCM, sababu ambazo zilibainika kwamba hazikuwa na msingi wowote.

Baada ya mvutano na mazungumzo CHADEMA ilikubali kutii sheria na kuzingatia matakwa ya Jeshi la Polisi pamoja na kuwa yalitolewa kinyume cha Sheria kwamba maandamano na mkutano wa CHADEMA vifanyike mara baada ya siku ya kuanza kwa sensa tarehe 26 Agosti 2012 na CHADEMA ilipendekeza tarehe 27 Agosti 2012 ambayo Jeshi la Polisi liliikubali.

Polisi walifanya hivyo wakielewa ukubwa wa barabara za Morogoro na pia wakitambua kwamba ilikuwa ni siku ya kazi, hata hivyo tarehe 23 Agosti 2012 Jeshi la Polisi liliandika barua ya kueleza kwamba limetoa kibali cha mkutano (suala ambalo si mamlaka yake kisheria) na pia limekataza maandamano.

CHADEMA kikaamua kwa mara nyingine tena kurudi katika meza ya mazungumzo na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, tarehe 24 Agosti 2012 ambapo polisi ilikubali maandamano ikiwemo ya watembea kwa miguu na kupendekeza njia mbadala na tarehe 26 Agosti 2012 mazungumzo yakaendelea kwa lengo la kukagua barabara.

Hata hivyo, kufuatia shinikizo la Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile kinyume na Sheria ya Jeshi la Polisi ambayo imetoa mamlaka kwa Mkuu wa Polisi Wilaya kuhusu taarifa za mikutano, polisi ikarejea katika msimamo wa kukataza mapokezi ya watembea kwa miguu na badala yake tarehe 26 Agosti 2012 bila sababu za misingi ya kisheria na zisizozingatia haki za kikatiba ikapendekeza kwamba yafanyike mapokezi kwa kutumia magari.

Maelezo ya Waziri wa Mambo ya Ndani kuwa iwapo vyama vya siasa visiporidhika na mazingira kama hayo yapo mamlaka ya kukata rufaa yanapotosha kwa kuwa Sheria ya Jeshi la Polisi na Sheria ya Vyama vya Siasa hazijaweka utaratibu wa rufaa hivyo njia pekee ya kisheria ni kutumia mahakama.

Jeshi la Polisi lingeheshimu utawala wa sheria na mazungumzo lingeruhusu CHADEMA ifanye maandamano na kutoa ulinzi mpaka eneo la mkutano kwa muda mfupi badala yake jeshi hilo likaamua kutumia nguvu kubwa na kusababisha mauaji, barabara kufungwa kwa muda mrefu na kuathiri wananchi waliokuwa wakiendelea na kazi zao.

Iwapo wanachama na wananchi waliokuwa wamekusanyika kuwapokea viongozi na kuelekea kwenye mkutano wangekuwa wamekiuka sheria Jeshi la Polisi lingeweza kuwakamata kwa mujibu wa sheria, hata hivyo hakuna kiongozi yoyote wa CHADEMA aliyefunguliwa jalada mpaka sasa katika kituo chochote cha polisi kwa kudaiwa kukiuka sheria.

Kinyume chake Jeshi la Polisi ambalo likiwa kwenye mazungumzo lilikubali kuwa mapokezi yafanyike kwa msafara wa vyombo vya moto, lakini tarehe 27 Agosti 2012 likaamua kupiga mabomu ya machozi kwa wananchi na wanachama wa CHADEMA waliokuwa wamekusanyika eneo la Msamvu wakiwasubiri viongozi bila hata ya kusubiri kuona iwapo yangefanyika matembezi ya miguu kuelekea eneo la mkutano au maandamano ya magari na vyombo vingine vya usafiri.

Kitendo cha Jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa kinyume cha sheria na kusababisha mauaji na kufunga barabara kwa muda mrefu kiliwafanya wanachama wa CHADEMA na wananchi kwa ujumla kutawanyika kuelekea eneo la mkutano na wengine kuingia barabarani kutembea kuelekea eneo la mkutano na hatimaye polisi walipoona wamesababisha hali hiyo wakaamua kulinda misafara hiyo mpaka eneo la mkutano hali inayodhihirisha kuwa uamuzi kama huo ungechukuliwa kutoka mwanzo yasingetokea madhara yoyote.

Kwa kuzingatia utofauti mkubwa baina ya maelezo yanayotolewa na Serikali na Jeshi la Polisi kuhusu matukio husika na ukweli halisi ulivyotokea, CHADEMA kinasisitiza kuwauchunguzi huru ufanyike kwa mujibu wa Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (Inquest Act) Sura ya 24 ya Sheria za Tanzania.

CHADEMA kwa mara nyingine kinaitaka Serikali inayoongozwa na CCM kurejea katika kifungu cha 3 cha Sheria ya Uchunguzi wa Vifo, ambacho kinatoa mamlaka ya Waziri mwenye dhamana na masuala ya Sheria kuanzisha Mahakama ya Kuchunguza Vifo hivyo (Coroner’s Court) katika maeneo ya serikali za mitaa kwa kushirikiana na Jaji Kiongozi.

CHADEMA kinaikumbusha Serikali kuwa, kufuatia kauli ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mawaziri Vivuli husika kueleza bungeni taarifa za mauaji yaliyofanywa na vyombo vya dola kwa nyakati mbalimbali, Waziri Mkuu na Mawaziri wengine waliahidi bungeni kwamba sheria hiyo itaanza kutumika kuchunguza vifo vyenye utata.

Katika muktadha huo uchunguzi wa kifo cha Ali Zona haupaswi kufanywa na timu ya polisi bali sheria hiyo sasa ianze kutumika.

Kwa upande mwingine, CHADEMA imeheshimu taratibu za maziko zilizopangwa na familia ambapo mwili wa marehemu ulisafirishwa jana tarehe 28 Agosti 2012 kwenda Mkoani Tanga kwa ajili ya maziko na CHADEMA kuwasilisha rambirambi zake za awali, taarifa zaidi kuhusu ushiriki kwa CHADEMA kwenye maziko zitaelezwa baada ya majadiliano yanayoendelea na familia.

CHADEMA kwa kuheshimu mazungumzo na utawala wa sheria kwa mara nyingine tena tarehe 28 Agosti 2012 CHADEMA kimesitisha Operesheni za Maandamano na Mikutano yake ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) kwa rai iliyotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) ili kupisha kukamilika kwa zoezi la sensa ambayo imetokana pia na maelezo ya mamlaka zingine za kiserikali.

CHADEMA inatambua kwamba wakati maandamano ya CHADEMA yametolewa rai kuwa yasitishwe kupisha sensa, maandamano ya wagombea wa CCM kurudisha fomu za uchaguzi wa ndani ya chama chao yameachwa yakiendelea katika barabara kadhaa nchini bila kusitishwa kwa kisingizio hicho.

Aidha, wakati CHADEMA ikiheshimu mazungumzo na kusogeza ratiba yake mbele ya tarehe 26 Agosti 2012 mpaka tarehe 27 Agosti 2012 kupisha sensa hatua ambayo ilifanywa pia na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ambayo ilitangaza ratiba yake kuendelea baaada ya tarehe hiyo.

Tume hiyo inaendelea na mikutano yake ya hadhara inayokutanisha wananchi katika kata za mikoa mbalimbali wakati huo huo zoezi la sensa likiendelea lakini kwa mikutano ya CHADEMA inaonekana kufanyika kwake ni kuingilia sensa.

CHADEMA inataka Serikali na Polisi kueleza iwapo matukio haya na mengine hayana mwelekeo wa ubaguzi na uhujumu wa vuguvuvugu la mabadiliko linaloendelea nchini kwa kurejea ukweli kuwa maisha ya wachache yanaweza kuwekwa mashakani lakini si mabadiliko kwa maslahi ya wengi.

CHADEMA itaeleza hatua za ziada itakazochukua baada ya kupata ripoti ya uchunguzi wa mwili wa marehemu (post mortem) uliofanyika tarehe 28 Agosti 2012 na uamuzi wa Serikali kukubali au kukataa mwito wa kutumia Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (Inquest Act) kuwezesha uchunguzi huru.

Imetolewa
tarehe 29 Agosti 2012 na:
John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi

Monday, August 27, 2012

MKUTANO WA CHADEMA MOROGORO MJINI

Katibu mkuu wa Chama chama cha Demokrasi na Maendeleo Dkt Wilbrord Slaa akihutubia wananchi wa Manispaa ya Morogoro katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Ndege mkoani Morogoro.
Katibu mkuu wa Chama chama cha Demokrasi na Maendeleo Dkt Wilbrord Slaa akiongoza umati uliohudhuria mkutano wa hadhara wa Operesheni Sangara-Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) baada ya mtu mmoja kudaiwa kupigwa risasi na kufariki dunia wakati wengine wawili nao wakidaiwa kujeruhiwa kwa kupigwa na risasi na askari wa jeshi la polisi.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 5 asubuhi eneo la Msamvu barabara kuu Dar es Salaam-Morogoro wakati askari hao wakiwatawanya umati mkubwa wa wanachama na wafuasi wa chama hicho waliokuwa wakisubiri viongozi wa juu wa chama hicho ili waandamane kuelekea katika mkutano wa hadhara uwanja wa Ndege mkoani Morogoro leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Morogoro na vitongoji vyake, katika mkutano wa hadhara wa operesheni sanga ,kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Uwanja wa Ndege
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Morogoro waliojitokeza katika mkutano huo.
Makamu Mwenyekiti Chadema Zanzibar Said Issa Mohamed akifafanua jambo kwa wananchi hao.
Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Igunda kupitia Chadema, Joseph Kashinde akizungumza na wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
Mbunge wa viti Maalum Chadema Suzan Mungi akimwaga sera za chama hicho.
Mbunge wa jimbo la Ubungo Jijini Dar es Salaam John Mnyika akipanda jukwaani wakati akiwasili katika uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.
Sehemu ya umati ambao ni wakazi wa Manispaa ya Morogoro na vitongoji vyake katika mkutano huo.Picha Zote na Juma Mtanda

FFU WALIVYODHIBITI MAANDAMANO YA CHADEMA MOROGORO

Wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema

Askari waliokuwa katika eneo la tukio kabla ya kuanza kwa maandamano hayo

Moshi wa mabomu yaliolipuliwa kutawanya maandamano ya chadema leo mjini morogoro




Gari la chadema lililokuwa likiongoza maandamano hayo

Mmoja wa kiongozi wa chadema akiwa amekamatwa akiwa ndani ya gari la polisi

Wafuasi wa chadema wakiwa na maandamao hayo mjini morogoro
Huyu ni Ally Zona muuza magazeti wa Msamvu Morogoro akiwa hajitambui baada ya kutandikwa risasi na Polisi wakati wa vurugu za kuzuia maandamano ya chadema leo. Picha kwa hisani ya Father Kidevu

Friday, August 17, 2012

MKUTANO WA CHADEMA KILOSA

Sehemu ya Umati Mkubwa wa Wana Kilosa wakifwatilia kwa umakini hotuba mbalimbali kutoka kwenye mkutano wa CHADEMA
-
Vuguvugu la M4C linaloongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA limeonekana kutikisa chama cha wananchi CUF wilayani Kilosa ambapo mbali ya wanachama wengi sana wa CUF kujiunga CHADEMA pia Mjumbe wa mkutano Mkuu CUF Taifa Bwana Wille Lemi alijitoa rasmi katika CUF na kukabidhiwa kadi na Kiongozi wa upinzani nchini ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa.

Katika mkutano huo Dr Slaa aliwataka wananchi wa vyama vyote kuunganisha nguvu kwa pamoja chini ya vuguvugu la M4C ili kuhakikisha katika uchaguzi mkuu ujao wananchi wanapata serikali itakayojali maslahi yao chini ya CHADEMA.

Dr Slaa pia alishukuru mwitikio wa wanakilosa kutokana na mkutano huo kufurika umati mkubwa wa watu.Mbali na CUF kupoteza wanachama wengi pia mamia ya wanaCCM walikihama chama chao na kujiunga rasmi CHADEMA kuunganisha nguvu katika vuguvugu la M4C.Idadi ya wanachama wapya waliojiunga CDM katika mkutano wa Kilosa ulikuwa zaidi ya elfu moja.

Kilosa ilikuwa ni mojawapo ya maeneo yenye wanachama wengi wa CUF lakini inaonekana ziara ya Dr Slaa imesimika rasmi CHADEMA kama chama kinachopendwa zaidi Kilosa.

Sunday, August 12, 2012

Mmoja wa majeruhi wa ajali ya basi la Shabiby

basi la Shabiby lililokuwa likitokea mkoani Dodoma kwenda Dar es Salaam na kusababisha mabasi matatu kuacha njia katika eneo la Mkundi Makunganya barabaraba kuu Dodoma-Morogoro ambapo katika ajali hizo zaidi ya abiria 40 walijeruhiwa mkoani Morogoro
Basi la kampuni ya Allys Sport Bus linalosafirisha abiria kutoka Dar es Salaam na Mwanza likiwa limeacha njia na kupinduka baada ya kutokea ajali inayodaiwa kusababishwa na basi la Shabiby lililokuwa likitokea mkoani Dodoma kwenda Dar es Salaam na kusababisha mabasi matatu kuacha njia katika eneo la Mkundi Makunganya barabaraba kuu Dodoma-Morogoro ambapo katika ajali hizo zaidi ya abiria 40 walijeruhiwa mkoani Morogoro
Askari wa Kikosi cha Usalam Barabarani Wakiwa Eneo la Tukio
Mmoja wa majeruhi wa ajali ya basi la Shabiby, Deogratias Mrai akiwa katika wodi namba moja ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro akiuguza majeraha aliyopata kufuatia basi hilo walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka katika eneo la Mkundi-Makunganya Manispaa ya Morogoro lililokuwa likitoka Dodoma kwenda Dar es Salaam na kusababisha mabasi matatu kuacha njia katika eneo la Mkundi Makunganya barabaraba kuu Dodoma-Morogoro ambapo katika ajali hizo zaidi ya abiria 40 walijeruhiwa.
--
Na : Juma Mtanda

Kutoka Morogoro -- WATU 45 wamejeruhiwa kwenye ajali baada ya mabasi matatu waliyokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka eneo la Mkundi kwa Makunganya nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro, katika Barabara ya Morogoro - Dodoma.

Ajali hiyo ilitokea saa 2:30 asubuhi kwa kuhusisha mabasi matatu, Kampuni ya Shabiby lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam, Allys Sport na Sumry yaliyokuwa yakitokea Morogoro kwenda Mwanza.

Baadhi ya majeruhi waliokuwa wakisafiri na basi la Shabiby walisema basi hilo lilianza kuyumba na baadaye kuacha njia kisha kupinduka.

Mmoja wa abiria hao, Rashid Shaaban alisema baada ya basi hilo kupinduka, ghafla waliona basi jingine la Sumry likiacha njia na kupinduka wakati lilipojaribu kulipita gari jingine jirani na eneo hilo.

Alisema kuwa wakati kukiwa na msongamano wa magari katika eneo hilo la ajali, basi jingine la Allys Sport liliacha njia na kupinduka na hivyo kutokea ajali tatu katika muda usiozidi dakika 10.

Shaaban alisema baada ya ajali hizo walitokea watu waliokuwa wakijifanya kutaka kutoa msaada, lakini lengo lao lilikuwa ni kuiba mali za majeruhi. Hata hivyo, alisema lengo lao hilo halikufanikiwa kwani muda mfupi baada ya kutokea, askari walifika na kuimarisha ulinzi.

Katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, madaktari na wauguzi walionekana kuzidiwa na wagonjwa kutokana na idadi kubwa ya majeruhi waliokuwa wakihitaji huduma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alithibitisha kutokea kwa ajali hizo na kusema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa zimetokana na utelezi na mwendo kasi.

Saturday, August 11, 2012

Operation Sangara yaingia wilaya ya Ulanga mkoa wa morogoro

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilibrod Slaa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mgeta katika jimbo la Kilombero mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya mikutano ya operesheni Sangara.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa akiongozana na viongozi mbali mbali wa chama hicho, walipokuwa wakivuka katika kivuko cha mto Kilombero wakitokea jimbo la Kilombero kuelekea jimbo la Ulanga Magharibi, katika mikutano ya Operesheni Sangara inayoendelea katika mkoa wa Morogoro. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa mkoa wa Tabora, Kansa Mbaruok.Picha na Joseph Senga

Wednesday, August 8, 2012

Askari Polisi Mwenye Namba F 3276, Donald Mathew (33)Ajinyonga Juu ya Mti Katika Daraja la Shani Mkoani Morogoro

Nakala ya barua ya askari Dunga kwa Waziri wa Mambo ya Ndani
Baadhi ya wananchi na maaskari wakijadiliana jambo kwenye mwili huo wa Afande Dunga
--

Na Danstan Shekidele
Siku chache kabla ya kifo chake askari polisi mwenye namba F 3276, Donald Mathew (33), aliyejinyonga juu ya mti katika daraja la Shani, mkoani Morogoro alimwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani kueleza kinachodaiwa kuwa ni ufisadi unaofanywa na vigogo wa polisi nchini, imebainika.

Polisi huyo aliyefahamika sana kwa jina la Dunga aliwahi kutoa tuhuma nzito dhidi ya maofisa, wakaguzi na polisi wa kawaida, mkoani Morogoro mwaka jana lakini hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya maofisa hao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fustine Shilogile, jana alisema jeshi hilo, lilipokea taarifa za kujinyonga Mathew jana asubuhi.

Alisema askari huyo, aijinyonga kwa kutumia vipande vya kamba ya kanga ambavyo viliunganishwa na hakuacha ujumbe wowote unaoeleza sababu ya kuchukua uwamuzi huo.

Alisema askari huyo kabla ya kufanya tukio hilo, alionekana mitaani akinywa pombe katika Baa ya Shani.

Alisema baada ya kuonekana amelewa, Mathew aliamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu, kitendo kilichofanya baadhi ya askari polisi waliokuwa eneo hilo, kumfuata na kumsihi avae nguo.

Alisema marehemu, alihamishiwa mkoani Singida kikazi, lakini Novemba, mwaka jana aliamua kuacha jeshi.

“Pamoja na kwamba marehemu aliacha kazi mwaka jana, sisi kama jeshi bado tunamtambua kama askari mwenzetu… kwa msingi huo tutasafirisha mwili wake Agosti 8, mwaka huu kwenda nyumbani kwake mkoani Kilimanjaro,” alisema Kamanda Shilogile.

Alipoulizwa kama kifo cha Mathew kimesababishwa na baadhi ya askari waliohusishwa kwenye tuhuma za kuhusika na biashara za dawa za kulevya, Kamanda Shilogile alisema uchunguzi unaendelea, na kwamba ikibainika kama kuna askari aliyehusika atachukuliwa hatua kali.

Hata hivyo, askari huyo mwishoni mwa mwaka jana, alitoa tuhuma mbalimbali ambazo zilichapishwa katika moja ya magazeti linalotoka mara mbili kwa wiki, zikiwatuhumu askari 9 wa kikosi cha kupambana na majambazi wa kutumia silaha kupokea rushwa kutoka kwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.

Tuhuma nyingine alizotoa ni polisi kukamata majambazi wenye silaha, lakini huachiwa baada ya kupewa fedha na mali mbalimbali, hivyo kushindwa kuwafikisha kituoni.

Alisema tuhuma nyingine ni polisi kuwakamata wafanyabiashara wa pombe haramu aina ya gongo na bangi bila kuwachukulia hatua zozote baada ya kuhongwa.

Tuhuma nyingine, zinazodaiwa kufanywa na askari hao ni kushirikiana na matapeli, kutapeli raia wa kigeni na kushirikiana na majambazi kuvunja maduka na kuiba mali za wafanyabiashara nyakati za usiku.

Tuesday, July 31, 2012

Mazishi Ya Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Kilosa na Mwenyekiti wa Mkoa, Alhaji Abdallah Shaweji

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mkuu wa mkoa wa Moropgoro, Joel Bendera (kulia) wakishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa mbunge wa zamani wa jimbo la Kilosa na Mwenyekiti wa mkoa huo, Alhaji Abdallah Shaweji, wakati wa mazishi yaliyofanyika leo, Wami Dakawa, wilayani Mvomelo, Morogoro. Alhaji Shaweji alifariki jana.Picha na Bashir Nkoromo

Monday, July 16, 2012

MKUTANO WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WAFANYIKA MOROGORO

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nyumba la taifa (NHC) Nehemiah Kyondo Mchechu akifafanua jambo wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika mkutano wa shirika hilo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa likimeo la miradi mbalimbali katika ujenzi wa nyumba za biashara katika ukumbi wa Glonency Nane Nane mkoani Morogoro
Mhariri msanifu mkuu wa gazeti la mwananchi Communications Ltd (MCL) Rashid Kejo akichangia jambo katika mkutano huo.
Mkurugenzi Miliki katika shirika la nyumba la taifa (NHC) Hamad Abdalla akifafanua jambo kuhusu kitengo hicho wakati wa mkutano huo kulia ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) Theophil Makunga.
Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda kushoto akizungumza jambo katika mkutano wa shirika la nyumba la taifa (NHC) na wahariri wa vyombo vya habari wenye lengo la kuwaelezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo likimeo la miradi ujenzi ya nyumba za biashara ambao umefanyika mkoani Morogoron katika ukumbi wa Glonency Nane Nane mkoani hapa, kulia ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) Theophil Makunga.
Mhariri wa gazeti la Daily News, Marycelina Masha akichangia jambo katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Kyando Mchechu (kushoto), akizungumza na waandishi wa hariri wa vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa shirika hilo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa likimeo la miradi mbalimbali katika ujenzi wa nyumba za biashara katika ukumbi wa Glonency Nane Nane mkoani Morogoro.
WAHARIRI Watendaji wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) Frank Sanga gazeti la Mwanaspoti kushoto gazeti la The Citizen, Bakari Machumu kulia akibadilishana mawazo wakati wakielekea katika chumba cha mkutano wa shirika la nyumba la taifa (NHC) na wahariri wa vyombo vya habari uliohusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo juu ya miradi mbalimbali ya ujenzi ya nyumba za biashara ambapo mkutano huo ulifanyika Glonency Hoteli Nane Nane mkoa wa Morogoro.

Friday, July 13, 2012

Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Fereji katika Maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Duniani

Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Dunia, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Fereji (aliyesimama). Kushoto ni Mwenyeji wa Maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Dunia, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera.

Mwenyeji wa Maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Dunia, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (aliyesimama) akisoma hotuba ya utangulizi, katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku hiyo. Kulia ni Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Dunia, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Fereji
Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bi Joyce Mkinga (Kushoto)akimpa vipeperushi na nyaraka zinazoelezea majukumu na kazi za Tume ya Mipango kwa maelezo kwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Dunia, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Fereji, (Wa pili kulia.
Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bi Joyce Mkinga (Kushoto) akitoa maelezo kwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Dunia, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Fereji, (Wa pili kulia) wakati alipotembelea Banda la Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku hiyo. Wa kwanza kulia ni mwenyeji wa maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo.
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Dunia, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Fereji akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa mkoani Morogoro.

Tuesday, July 10, 2012

MAKAMU WA RAIS WA AFRIKA KUSINI MKOANI MOROGORO

MAKAMU WA RAIS WA AFRIKA KUSINI , KGALEMA MOTLANTHE, AKIPANDA MTI ENEO LA MAKABURI YA WAPIGANIA UHURU WA ANC , MAZIMBU, MJINI MOROGORO.
MAKAMU WA RAIS WA AFRIKA YA KUSINI AKITOA HESHIMA BAADA YA KUWEKA SHADA LA MAUA KWENYE MOJA YA KABURI LA MPIGANIA UHURU WA ANC , ENEO LA MAZIMBU,MJINI MOROGORO.
MAKAMU WA RAIS WA NCHINI AFRIKA KUSINI,KGALEMA MOTLANTHE ( KATIKATI) AKIANGALIA MOJA YA KABURI LA MPIGANIA UHURU WA ANC , ENEO LA MAZIMBU,MJINI MOROGORO.
MAKAMU WA RAIS WA AFRIKA KUSINI AKITOKA KUTEMBELEA HOSPITALI YA MAZIMBU AMBAYO ILIKUWA IKITUMIWA NA WAPIGANIA UHURU WA ANC, AMBAPO KWA SASA IMEKARABATIWA NA KUONGEZWA MAJENGO MAPYA.
BURUDANI KWA MGENI RASMI,MAKAMU WA RAIS WA AFRIKA KUSINI ALIPOTEMBELEA SHULE YA MSINGI CHIEF ALBERT LUTHULI, MAZIMBU MJINI MOROGORO.
BAADHI YA RAIA WA AFRIKA KUSINI WALIOAMBATANA NA MAKAMU WA RAIS WA NCHI HIYO HAPA NCHINI
--
Makamu wa Rais wa Afrika ya Kusini, Kgalema Motlanthe, Julai 9, mwaka huu alifanya ziara ya siku moja Mjini Morogoro, ililiyokuwa mahusisi kwa ajili ya kutembelea eneo la Mazimbu, ilikuwa kambi ya wapingania uhuru wa Chama cha ANC.

Ziara hiyo ilikuwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 20 tangu harakati za ukombozi wa Afrika Kusini zilipomalizika ,katika Kambi hiyo , ANC iliacha majengo na vitu mbalimbali vilivyokabishiwa Serikali ya Tanzania, pia yapo makaburi kadhaa walimozikwa mashujaa hao, ambapo Makamu huyo wa Rais aliweza kuzuru na kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu ya wapigania uhuru hao pamoja na kupanda mti.

Kabla ya kufanya shughuli hiyo,alipata fursa ya kutembezwa maneo mbalimbali yakiwemo majengo yaliyokuwa yakitumiwa na wapigania uhuru hao, ikiwemo Shule ya Msingi na Awali, Shamba la Mifuko, Kiwanda cha samani pamoja na Hospitali .

Popular Posts