Pages

Saturday, June 9, 2012

shule za kata wilayani Kilwa zimeanza kuwekeza katika maabara

Wanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari ya Kinjumbi wilayani Kilwa wakisoma kemia kwa vitendo katika maabara ya shule.Shule hii ipo rtakribani kilometa 70 toka Kilwa Masoko
Hivi ndivyo tukichanganya inatokea kwenye 'test tube'
Hii ni result ya huu mchanganyiko.Mananisikia?Mwanafunzi akiwaelekeza wanafunzi wenzake juu ya mchanganyiko alioufanya kwenye 'test tube' na reaction iliyotokea.
Majaribio ya maabara yakiendelea.wanafunzi hawa ni wa kidato cha nne na wanategemea kufanya mtihani wao wa Chemistry,Biology na Physics kwa vitendo.
Embu leye hiyo test tube.ingawa hatuna groves na miwani kwaajili ya kujikinga kama reaction mbaya itatokea.
tunaendelea hivi


Unaona inavyokuwa?Tunachanganya hivi







Chumba cha maabara ya shule ya sekondari ya Kinjumbi

MKUTANO WA CCM JANGWANI JUMAMOSI JUNI 9 2012


Maelfu wakiwa wamefurika kwenye mkutano wa hadhara wa CCM unaofanyika jioni hii kwenye Viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ni wa kuwapongeza viongozi wa mashina na matawi waliochaguliwa katika uchaguzi wa CCM ulifanyika kwa ngazi hizo mkoani Dar es Salaam
Wilaya ya Kinondoni wakishangilia baada ya kutambulishwa.
Watu wakionyesha kuwa na shamrashamra baada ya kukaa nafasi zao.
Wa Ilala wakiingia viwanja vya Jangwani.
Watu kutoka Temeke wakiingia viwanja vya Jangwani.
Wa Mbagala wakiingia viwanja vya jangwani.
Mfuasi wa Chadema akiwa na fulana kenye ujumbe
Mfuasi wa CCM akionyesha fulana lenye ujumbe hivi sasa viwanja vya jangwani jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa CCM

KUHUSU MKUTANO WA 8 WA BUNGE LA BAJETI

1.0 UTANGULIZI:
Mkutano wa Nane wa Bunge unatarajiwa kuanza tarehe 12 Juni, 2012 na kumaliza shughuli zake tarehe 22 Agosti, 2012. Mkutano huu utakuwa na shughuli mbalimbali kama vile Kiapo cha Utii kwa Waheshimiwa Wabunge wateule, kujadili Makadirio ya matumizi na mapato ya serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Maswali kwa Waziri Mkuu na Maswali ya kawaida pamoja na chaguzi mbalimbali ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi baada ya uteuzi wa Mheshimiwa Rais kwa baadhi ya wabunge kuingia katika Baraza la Mawaziri.

2.0 MUDA WA MKUTANO WA NANE WA BUNGE:
Kanuni ya 97(1) ya Kanuni za Bunge Toleo la Mwaka 2007, imeweka kiwango cha juu cha siku zitakazotumika kwa ajili ya mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Serikali kuwa ni siku tano. Pia, Kanuni ya 99(1) imeweka kiwango cha siku zisizozidi hamsini kwa ajili ya Bunge kujadili utekelezaji wa Wizara zote za Serikali.
Hivyo basi katika Mkutano huu wa Nane jumla ya siku nne (4) zimetengwa kwa ajili ya kujadili na kupitisha Bajeti ya Serikali, na jumla siku aronbaini (40) zimetengwa kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara nyingine zote.

3.0 SHUGHULI ZA SERIKALI:
Kwa mujibu wa Kanuni 17 (1) (d) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la 2007, Shughuli ambazo zitatekelezwa katika Mkutano huu utakaokuwa wa siku 49 za kazi ni kama ifuatavyo:

3.1. KIAPO CHA UTII:
Kwa mujibu wa Kanuni ya 24 ya Kanuni za Bunge, Toleo la 2007 na kufuatia uteuzi uliofanywa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 66 (1) (e) kutakuwa na kiapo cha Utii kwa Wabunge wateule wafuatao:-
1. Mhe. James Francis Mbatia;
2. Mhe. Janet Zebedayo Mbene;
3. Mhe. Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo; na
4. Mhe. Saada Mkuya Salum.

3.2 Miswada ya Sheria:
Miswada ya Sheria itakayosomwa kwa Mara ya Kwanza na hatua zake zote: [Chini ya Kanuni ya 83 ya Kanuni za Bunge] ni kama ifuatavyo:
· Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2012 (The Finance Bill, 2012).
· Muswada Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali wa Mwaka2012 (The Appropriation Bill, 2012).

3.3 Kujadili Bajeti:
Majadiliano ya Bajeti ya Serikali yanaongozwa na Kanuni zilizopo katika Sehemu ya Tisa ya Kanuni za Bunge inayohusu Utaratibu wa Kutunga Sheria kuhusu mambo ya Fedha. Kanuni ya 96(2) inaelekeza kuwa Hotuba ya Bajeti lazima iwasilishwe Bungeni na Waziri wa Fedha kabla ya tarehe 20 mwezi Juni kwa kila Mwaka.

Kutokana na kanuni hiyo, Bajeti ya Serikali itasomwa siku ya alhamisi tarehe 14 Juni 2012 ambapo Nchi zote za Afrika Mashariki zitasoma Bajeti zao kama ambavyo walisha kubaliana.

Katika siku hiyo baada ya kipindi cha Maswali, Waziri anayehusika na Mipango atawasilisha na kusoma hotuba yake ya Hali ya Uchumi wa nchi na jioni kuanzia saa 10.00 Waziri wa Fedha atasoma Hotuba ya Bajeti ya Serikali.

Kutokana na Utamaduni wetu baada ya kusoma Bajeti hiyo Bunge litaahirishwa kwa siku moja kwa lengo la kuwapatia Wabunge nafasi ya kusoma na kutafakari Hotuba ya Hali ya Uchumi na Hotuba ya Bajeti ya Serikali na kujiandaa kwa majadiliano yatakayoanza tarehe 18 Juni, 2012 hadi tarehe 21 Juni, 2012.

Kwa Mujibu wa Kanuni ya 98 (2) Siku ya Alhamisi tarehe 21 Juni, 2012, Bunge litapiga kura ya uamuzi wa Bajeti ya Serikali. Siku hii ni muhimu sana kwa Wabunge wote kuwa Ukumbini kwa sababu kura hupigwa kwa kuita majina.

Tarehe 22 Juni, 2012 Bunge litajadili na kupitisha Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2012 (The Finance Bill, 2012). Tarehe 25 hadi 29 Juni, 2012 kwa muda wa siku tano kutakuwa na mjadala wa Hotuba ya Waziri Mkuu juu ya utekelezaji wa Shughuli za Serikali katika Mwaka wa Fedha unaomalizika, na matarajio ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha unaofuata. Mjadala wa Hotuba za Mafungu ya Wizara nyingine utaanza tarehe 02 Julai, 2012 kwa mtiririko kama unavyoonekana kwenye ratiba hadi tarehe 20 Agosti, 2012.

4.0 SHUGHULI NYINGINE:
4.1 MASWALI:
(i) Maswali ya Kawaida:
(Chini ya Kanuni ya 39(1) ya Kanuni za Bunge, Toleo la 2007):
Itakumbukwa kuwa, nyakati za vikao vya Bajeti, Maswali yanayowekwa kwenye orodha ya Shughuli za Bunge ni kumi tu kwa siku za kawaida na matano siku za Alhamisi, Hivyo, katika Mkutano huu inatarajiwa kuwa, Maswali 454 yataulizwa na kujibiwa.

(ii) Maswali kwa Waziri Mkuu:
(Chini ya Kanuni ya 38(1) ya Kanuni za Bunge, Toleo la 2007):
Utaratibu wa kumuuliza Maswali Mheshimiwa Waziri Mkuu kila Alhamisi kama tulivyokubaliana utaendelea na inakadiriwa kuwa maswali yasiyopungua 64 yataulizwa.

4.2 UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA BUNGE:
Kwa mujibu wa Kanuni ya 11 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007 kutakuwa na uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Mheshimiwa George Boniface Simbachawene (Mb) aliyeteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini.

4.3. UCHAGUZI WA MJUMBE WA BUNGE LA AFRIKA:
Kwa mujibu wa Kanuni ya 12 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007 kutakuwa na uchaguzi wa mjumbe wa Bunge la Afrika ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Mheshimiwa Stephen Julius Massele (Mb) aliyeteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini.

Imetolewa na :
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma
na Uhusiano wa Kimataifa
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
Tarehe 8, Juni, 2012

WANAOWANIA TUZO ZA TASWA 2011

Mwenyekiti wa Kamati ya tuzo za Chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA Bw. Masod Saanane akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa City Sports Lounge jijini Dar es salaam jana, kulia ni katibu mkuu wa TASWA Amir Mhando
----
MAJINA YA WALIOTEULIWA KUWANIA TUZO YA WANAMICHEZO BORA MWAKA 2011/MWANAMICHEZO BORA WA TANZANIA MWAKA 2011, ITAKAYOFANYIKA JUNI 14 MWAKA HUU
KIKAPU:
WANAWAKE
DORITHA MBUNDA :-JKT QUEENS
EVODIA KAZINJA:-JKT QUEENS
FARAJA MALAKI:-JESHI STARS
WANAUME
ALPHA KISUSI-Vijana
FILBERT MWAIPUNGU:-ABC
GILBERT BATUNGI:-ABC
NETIBOLI:
LILIAN SYLIDION
DORITHA MBUNDA
GOFU
WANAWAKE:
Madina Iddi (Umri miaka 27)
Hawa Wanyeche (Umri miaka 26)
Ayne Magombe (Umri miaka 24)


WANAUME:
Frank Roman
Nuru Mollel
Issac Anania
GOFU WA KULIPWA:
FADHILI SAIDI NKYA.
YASINI SALEHE
HASSANI KADIO

OLIMPIKI MAALUM
Ahmada Bakar
Amina Daud Simba-kisahani na tufe
Othman Ally Othman-mkuki, kisahani na tufe.
Cio..
PARALIMPIKI
WANAUME
ZAHARANI MWENEMTI
JOSEPH NZIKU
YOHANA MWILA
WANAWAKE
FAUDHIA CHAFUMBWE
SIWEMA KILYENYI
JANETH MADISE
NGUMI ZA RIDHAA
SULEIMAN SALUM KIDUNDA
VICTOR NJAITI
ABDALAH KASSIM
CIO…

WAOGELEAJI
(WANAWAKE)
MAGDALENA MOSHI
GOURI KOTECHA
MARIAM FOUM

WANAUME
AMMAAR GHADIYALI
OMARI ABDALLAH

JUDO...
MBAROUK SELEMANI MBAROUK
UNDER 81KG MEN JUDO PLAYER
MOHAMED KHAMIS JUMA
OVER 90KG MEN JUDO PLAYER
AZZAN HUSSEIN KHAMIS
UNDER 60KG Judo player

CIO…
WAVU…

WANAWAKE
ZUHURA HASSAN-JESHI STARS
THERESIA Ojode -JESHI STARS DAR
EVERLYNE ALBERT- MAGEREZA
WANAUME
MBWANA ALLY- MZINGA CORPORATION - MOROGORO
KEVIN PETER -MAGEREZA – DAR
FARHAN ABUBAKAR- MAFUNZO ZNZ
CIO…
NGUMI ZA KULIPWA
Benson Mwakyembe
Nasibu Ramadhan
Francis Cheka
Nassib Ramadhan
Fadhil Majia

TENISI:
WANAUME
WAZIRI SALUMU
OMARY ABDALAH
HASSANI KASSIMU

WANAWAKE
REHEMA ATHUMANI
MKUNDE IDDY
VIOLET PETER
Cio…

BAISKELI
Wanawake
Sophia Hussein
Sophia Anderson
WANAUME:
Richard Laizer
Hamisi Hussein

WACHEZAJI WA TANZANIA WANAOCHEZA NJE
Henry Joseph-Soka
Mbwana Samatta-Soka
Sophia Mwasikili-Soka
MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI
Theresia Ojode- wavu (Jeshi Stars)
SHOMARI KAPOMBE- (soka) SIMBA
Salum Abubakari-Azam (soka)
MCHEZAJI WA NJE ANAYECHEZA TANZANIA
Haruna Niyonzima-Yanga (soka)
Kipre Tchetche-Azam (soka)
Emmanuel Okwi-Simba (soka).

SOKA (WANAWAKE)
Asha Rashid-Mburahati Queens
Mwanahamisi Omary-Mburahati Queens
Fatuma Mustapha-Sayari
Ito Mlenzi-JKT

WANAUME
John Bocco-Azam
Aggrey Morris-Azam
Juma Kaseja-Simba
RIADHA
WANAWAKE
Zakia Mrisho
Mary Naali
Jaqueline Sakila

WANAUME
Dickson Marwa
Alphonce Felix

MIKONO
WANAWAKE
Abinery Kusencha-JKT Ruvu
Kazad Mtong-Magereza Kiwira
Faraji Shaibu Khamis-Nyuki Zbar
WANAUME:
Doris Mangara-Magereza Kiwira
Zakia Seif-Ngome Dar
Mary Kimiti-Magereza Kiwira.
Cio…
KRIKETI
WANAWAKE
MoniCa Pascal
Asha Daudi
Esther Wallace

WANAUME
Kassimu Nassoro
Benson Mwita
Riziki Kiseto
TUZO YA HESHIMA-ITATANGAZWA SIKU HIYO
MWANAMICHEZO BORA WA TANZANIA 2011-ATAPATIKANA MIONGONI MWA WASHINDI WA KILA MCHEZO.

MASOUD SANAN-
MWENYEKITI KAMATI YATUZO
08/06/2012

SMZ Kutumia Billioni 648 Bajeti Ya 2012-13

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Zanzibar anayeshughulikia Fedha Uchumi Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee (pichani) akiwasilisha mwelekeo wa Bajeti ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013 ambapo makadirio ya mapato na matumizi ni Sh.bilioni 648.9.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Zanzibar anayeshughulikia Fedha, Uchumi , Mipango na Maendeleo, Omar Yussuf Mzee (kulia) akitoa taarifa ya mwelekeo wa Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka 2012/2013 kwa wandishi wa habari kwenye ukumbi wa ofisi yake Vuga mjini Zanzibar jana.Picha na Martin Kabemba.

TAMKO LA JOHN MNYIKA NA HATUA ALIZOCHUKUA DHIDI YA WIZARA YA MAJI

Kufuatia Wizara ya Maji kukaa kimya bila kujibu barua toka Ofisi ya Mbunge kwa zaidi ya mwaka mmoja, nimeamua kuchukua hatua za kibunge kwa kuwasilisha kwa Katibu wa Bunge, taarifa na maelezo ya hoja binafsi kutaka Bunge, katika mkutano unaotarajiwa kuanza tarehe 12 Juni 2012, lipitishe maazimio ya kuwezesha uwajibikaji wa Wizara husika na mamlaka zake katika kushughulikia masuala ambayo nimeyaeleza katika hoja husika.

Ikumbukwe kwamba, tarehe 20 Mei 2012 nilitoa mwito kwa Waziri Profesa Jumanne Maghembe kuueleza umma hatua saba za haraka zaidi za Wizara ya Maji kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jimbo la Ubungo na Jiji la Dar es salaam mara baada ya Waziri kurejea ofisini kutoka katika ziara hiyo ya vyanzo vya ruvu juu na ruvu chini na kufanya mikutano na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) pamoja na Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO).

Nilichukua hatua ya kutoa taarifa kwa umma baada ya Wizara kuwa na utendaji mbovu wa kutojibu barua ambapo katika kipindi cha kati ya mwaka 2011 mpaka 2012 nimeandika jumla ya barua nne kwa Wizara husika kwa niaba ya wananchi kwa nyakati mbalimbali bila kupata majibu yoyote.

Katika ya hatua hizo ambazo Waziri nilieleza anapaswa kuzisimamia katika Wizara ya Maji ni; Mosi, kuchukuliwa kwa hatua dhidi ya kashfa ya taifa ya kati ya mwaka 2003 mpaka 2010 ambapo Serikali ilitekeleza Mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam na maeneo ya Bagamoyo na Kibaha (Dar es salaam Water Supply and Sanitation Project-DWSSP) uliotumia dola milioni 164.6 hata hivyo mpaka sasa katika maeneo mengi mtandao wake maarufu kama mabomba ya wachina hautoi maji.

Pili; kuwasilisha bungeni Mpango Maalum wa kuboresha huduma za Majisafi na uondoaji wa Maji Taka katika Jiji la Dar es salaam uliopitishwa mwezi Machi 2011 kwa ajili ya kuidhinishwa, kutengewa bajeti kamili ya utekelezaji wa haraka katika mwaka wa fedha 2012/2013 na kusimamiwa ipasavyo kwa msukumo wa kibunge badala ya ahadi za ujumla za kwenye ziara.
Tatu; Waziri kueleza hatua zilizopangwa kuchukuliwa kufuatia ziara yake kuhakikisha Mpango wa dharura wa kupunguza kero ya maji ulionza kutekelezwa na Wizara ya Maji kwa kushirikiana na DAWASA kuanzia Juni 2010 unaohusisha uchimbaji wa visima 24 uliopaswa kukamilika Oktoba 2011 unawekewa muda wa ukomo wa kukamilika ndani ya miezi mitatu katika maeneo ambayo miradi haijakamilika mpaka hivi sasa.

Nne; Waziri kukubaliana na pendekezo nililotoa bungeni kwa nyakati mbalimbali la Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi wa thamani ukilinganisha na ufanisi (Value for Money) wa Mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam na maeneo ya Bagamoyo na Kibaha (Dar es salaam Water Supply and Sanitation Project-DWSSP) kwa kurejea ukaguzi wa kiufundi (technical Audit) uliofanywa na kampuni ya Howard Humphreys.

Tano; Waziri kuhakikisha Wizara ya Maji inaisimamia EWURA ifanye ukaguzi wa kiufanisi (performance audit) wa miradi ya visima vya maji takribani 200 ambavyo vilichimbwa na serikali na kukabidhiwa kwa DAWASCO, jumuiya za wananchi na taasisi mbalimbali lakini haitoi huduma inavyostahili kwa kadiri ya malengo ya awali. Aidha, Wizara ya Maji ihakikishe EWURA inaharakisha kutunga kanuni za udhibiti wa ubora na bei ya huduma ya maji kwa upande wa sekta binafsi katika Jiji la Dar es Salaam.

Sita; Waziri kuwezesha Kamati husika ya Bunge ijadili taarifa ya ukaguzi wa ufanisi kuhusu usimamizi wa usambazaji wa maji katika maeneo ya mijini (performance audit report on the management of water distribution in urban areas) ya Januari 2012 iliyotolewa na CAG kabla ya mkutano wa nane wa bunge ulipangwa kuanza tarehe 12 Juni 2012 ili maoni na mapendekezo yazingatiwe wakati wa mchakato wa bajeti.

Saba; Wizara ya Maji kuhakikisha Serikali inawasilisha kwenye mkutano wa tisa wa bunge muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali za majisafi na majitaka (Water Supply and Sanitation Miscellaneous Amendment Bill) ili kushughulikia upungufu uliojitokeza katika utekelezaji wa sheria zilizopo na kuweka mfumo thabiti wa usimamizi wa sekta ya maji nchini.

Imetolewa Dar es salaam tarehe 8 Juni 2012 na:

John Mnyika
Mbunge wa Jimbo la Ubungo

Popular Posts