Pages

Friday, November 23, 2012

MBEKI MGENI RASMI MAJADILIANO YA UONGOZI AFRIKA DAR ES SALAAM


 Rais Mstaafu wa awamu ya pili ya utawala huru wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki (kulia) akifafania jambo wakati wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya. Mbeki alikuwa Mgeni Rasmi katika mdahalo huo.
 Mwenyekiti wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo, ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mdahalo huo jijini Dar es Salaam leo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Prof. Joseph Semboja, akizungumza katika mdahalo huo.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili ya utawala huru wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki (kulia) akikiwa mwenye tabasamu wakati Mwenyekiti wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya akitoa ufafanuzi wa majadiliano.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya na Mwenyekiti wa Mdahalo wa Uongozi Afrika, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Prof. Joseph Semboja (katikati) wakimsikiliza Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Afrika Kusini Ami Mpungwe ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara na Mwenyekiti wa Tanzanite One muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Mgemi rasmi wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo. 
Mawaziri Wakuu Wastaafu wa Tanzania, Cleo David Msuya (kulia)  na Salim Ahmed Salim wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya kuanza Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA BALOZI WA KOREA, NCHINI TANZANIA KWA MAZUNGUMZO


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Korea nchini Tanzania, IL Chung, wakati alipofika ofisini kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Korea nchini Tanzania, IL Chung, mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo.

Katibu Mkuu wa CCM Abdurahamn Kinana Atua Mkoani Rukwa na Kusema'' Kuitwa Waheshimiwa Ndani ya CCM Sasa Basi.''


Katibu Mkuu Mpya wa CCM Abdurahaman Kinana akifungua shina la wakereketwa wa CCM la Kisesa, mkoani Rukwa.
Katibu Mkuu Mpya wa CCM Abdurahamn Kinana,na Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye , na Mzee Self Khatib wakisalimia wananchi Uwanja wa Ndege wa Rukwa.
Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye akiwa na Watoto
Katibu Mkuu Mpya wa CCM Abdurahaman Kinana akizungumza na wana-CCM leo mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa
Pikipiki za mapokezi kutoka Uwanja wa Ndege wa Rukwa.Picha na Bashir Nkromo-Rukwa
---
NA BASHIR NKOROMO, RUKWA
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ameagiza kuanzia sasa wanachama wa CCM kuacha kuitana waheshimiwa badala wake watumie jina ndugu kama alivyoasisi Mwenyekiti wa kwanza wa CCM, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

Kinana ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na viongozi wa CCM, mjini hapa, akiwa katika siku yake ya pili ya ziara ya siku nne kujitambulisha na kukagua uhai wa Chama katika mkoa huo na mikoa ya Mtwara, Geita na Arusha.

"Mimi katika maisha yangu yote ya kumfahamu Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere, sikupata kumsikia akijiita au akitaka aitwe Mheshimiwa Mwenyekiti, au Mheshimiwa Rais, sasa haya mambo ya sisi kuitama mheshimiwa tunayatoa wapi?", alihoji Kinana.

Alisema, Mwalimu Nyerere hakujiita Mheshimiwa kwa sababu na maana kubwa sana, kwa hiyo ni lazima Wana-CCM kuendelea utamaduni huo wa kuitaka ndugu kwa sababu unazuia matabaka ya ubwana na utwana.

Mapema kabla ya mkutano huo wa ndani, Kinana alifungua shina la wakereketwa wa CCM Isesa na shina la UWT, Chanji nje kidogo ya mji wa Sumbawanga, ambapo alisema hatua ayake ya kufungua matawi hayo na kushiriki kikao cha shina kinachofunguliwa na mjumbe wa shina husika, ni ishara ya kuwaagiza viongozi wa ngazi zote wa CCM kuhakikisha wanatembelea mashina na matawi.

"Hili siyo langu, ni agizo la Mkutano Mkuu wa CCM uliomaizika mjini Dodoma hivi karibuni, pale tuliazimia kwamba, ili kuimarisha uhai wa Chama lazima viongozi wa ngazi mbalimbali watembelee mashina ma matawi ili kuzijua kero zilizopo huko", alisema.

Alisema, kulingana na agizo hilo, sasa kila kiongozi wa Chama atapimwa ufanisi wake wa kikazi kwa kuangalia ni namna gani anafanya kazi zake kwa karibu sana na mashina na matawi.

Alisema, CCM imesisitiza lifanyike hilo kwa juhudi zaidi kwa sababu ni wazi kwamba wenye chama ni wanachi waliopo kwenye ngazi hizo za mashina na matawi, hivyo kwenda huko ndiko kutaimarisha chama kwa uhakika zaidi.

Katika ziara hiyo, Kinana amefuatana na wajumbe wa NEC, Nape Nnauye (Itikadi na Uenezi), Mohamed Seif Khatib (Oganaizesheni)na waziri wa TAMISEMI, Aggrey Mwanri.

Mwisho.

Tume ya Mabadiliko ya Katiba Yakusanya Maoni Tarime,Mara



Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphery Polepole (aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa vipengele vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa wananchi wa Kata ya Mliiba, Wilaya ya Tarime mkoani Mara wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume hiyo jana alhamisi Nov.22, 2012. Wajumbe wengine wa Tume, wa kwanza kulia Nassor Mohammed, Maria Kashonda na Riziki Ngwali.
Wananchi wa kijiji cha Mangucha Kata ya Nyanungu Wilaya ya Tarime mkoani Mara wakifuatilia mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya uliotishwa na Tume ya Mabadlliko ya Katiba jana  alhamisi Nov. 22, 2012 katika kijiji hicho.
---
Na Ismail Ngayonga-Tarime, Mara

MKAZI wa Kata ya Kata ya Mliiba Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Marco Magubo (31) amependekeza ni vyema Katiba Mpya ikataze vyama vya siasa vinavyoingia madarakani mara baada ya kushinda uchaguzi wa Rais visipeperushe bendera yake na badala yake kuweka bendera ya Taifa.

Akitoa maoni yake jana (Alhamisi Nov. 22, 2012) kuhusu Katiba Mpya kwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba alisema kitendo cha kupeperusha bendera ya chama kilichoingia madarakani kitaongeza chuki kwa wanachama wa Chama kingine cha siasa kilichoshindwa uchaguzi.

Aidha Magubo alisema Rais anayeingia madarakani anawakilisha maslahi ya wananchi wote na hivyo si busara kwa Chama kilichoshida uchaguzi kupeperusha bendera ya Chama chao kwani Kiongozi huyo haongozi wanachama wa chama chake pekee bali wananchi wote katika taifa.

“Tazama Marekani ambao hivi majuzi tu walifanya uchaguzi mkuu wa Rais, katika kampeni za vyama vyao hatukuweza kuona bendera ya Republican wala Democracy ambavyo vyote vilishiriki uchaguzi na badala yake tuliona wananchi wakipeperusha bendera ya Taifa lao na hatukuona bendera ya Republican wala Democracy” alisema

Alisema kwa kuwa Tanzania ni nchi ya umoja, amani na mshikamano ni vyema  Katiba Mpya ikewe kipengele cha kukataza bendera za vyama vyao na badala ya wamwachie Kiongozi aliyopo madarakani kutetea hoja za wananchi wote.

Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu, Abdulrahman Kinana Aung'uruma Sumbawanga na Kuhudhuria Kikao Cha Shina


Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu, Abdulrahman Kinana akipokea saluti ya Chipukuizi wa CCM, wakati wa mapokezi yake kwenye Uwanja wa Ndege wa  Sumbawanga mkoani Rukwa, alipowasili mkoani Rukwa, jana, akiwa katika ziara yake ya siku nne kujitambulisha, kukagua na kueleza kwa wananchi utekelezaji wa Ilani ya CCM katika mkoa huo na mikoa ya Mtwara, Geita na Arusha.
Kinana akimsalimia aliyekuwa mbunge wa Sumbawanga mjini Hilary Aeshi, kwenye Uwanja wa Ndege wa  Sumbawanga mkoani Rukwa, jana.
Kinana akimsalimia Mwanasiasa mkongwe, Chrisant Mzindakaya, kwenye Uwanja wa Ndege wa sumbawanga, mkoani Rukwa, jana
Mjumbe wa Shina namba moja la Kisesa mkoani Ruwa,  Simoni Kibona akimsalimia kwa furaha, Kinana alipofika kwenye tawi hilo, jana na kushiriki kikao cha hilo ikiwa ni sehemu ya kuhimiza viongozi kutembelea mashina na matawi ya CCM ili kuimarisha chama.
Wajumbe wa mkutano wa shina namba moja la Kisesa mkoani Rukwa wakimsikiliza Kinana wakati akiwahutubia, aliposhiriki mkutano wao uliofanyika jana.
Kinana akifurahia ngoma ya kina mama wa shina la Isesa, mkoani Rukwa
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Aggry Mwanri  akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jana mjini Sumbawanga
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nape akihutubia  mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jana mjini Sumbawanga
Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohamed Seif Khatib akisalimia wananchi wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
Wananchi wakiwa na ujumbe wao kwenye bango katika mkutano wa CCM uliofanyika Sumbawanga mjini mkoani Rukwa jana.
Wana-CCM wakiwa na bango la kumpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdylrahman Kinana, mpongeza Kinana katika mkutano uliofanyika jana Sumbawanga mjini mkoani Rukwa.Picha na Bashir Nkromo-idara ya itikadi na Uenezi-CCM

Popular Posts