Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe(kulia) akiwa katika eneo la msitu wa Hifadhi ya Katavi, eneo maarufu kwa jina la lyamba lya mfipa. |
Na Kibada Kibada-Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Rajabu Rutengwe ameagiza kampuni ya utafiti na uchimbani madini ya Red O-Mining ltd kutoka China kusimamisha mara moja shughuli zote za utafiti kwa kuwa wamekiuka sheria za nchi kwa kufanya utafiti ndani ya pori la hifadhi ya wanyama la Rukwa Lukwati lililoko Hifadhi ya Taifa ya Katavi kinyume na sheria.
Mkuu huyo wa Mkoa alitoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kuwa wawekezaji hao wanafanya shughuli za utafiti na uchimbaji wa Madini katika pori hilo la hifadhi kinyume na taratibu za kisheria za nchi pamoja na kuwa wanayo leseni ya kufanya utafiti inayowaruhusu waliyoipata kutoka wizara ya nishati na Madini lakini hawana kibali kinachowaruhusu kufanya utafiti ndani ya hifadhi.
Pamoja na kupata leseni hiyo walipatiwa barua kutoka wizara ya Maliasili na Utalii na idara ya mazingira inayowaelekeza kuwa wakifika eneo la kufanyia utafiti wawaone wamiliki wa eneo kupitia ofisi za wanyama pori wilaya husika,ya Mpanda lakini hawakufanya hivyo, badala yake waliamua kuingia katika pori hilo la hifadhi la Katavi na kuendelea na shughuli zao za kiutafiti bila kuwa na kibari cha kufanya shughuli hizo ndani ya hifadhi kwa kuwa ni kinyume na taratibu.
Miongoni mwa mambo ya msingi ambayo Ujumbe wa Mawaziri na manaibu waziri wakiongozwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa, Ndugu Nape Nnauye waliyaongelea na kutaka yachukuliwe hatua za haraka ni pamoja na utunzaji wa mazingira, matatizo ya Ardhi na suala la Kampuni hiyo ya Utafiti wa Madini na Shamba la EFATHA MINISTRY.