Kwa kweli uongozi wa tawi umefarijika sana kuona wanachama wengi waliweza kuhudhuria sherehe hizo za ufunguzi wa tawi lao. Vile vile, sura hii imeonyesha namna gani chama cha mapinduzi ni chama bora kinachoweza kuwaunganisha wanachama wake popote duniani ili waweze kujiusisha na siasa ndani ya nchi yao. Hii ni fursa nyingine itakayowawezesha wanachama wa CCM kuchangia maoni bora yatakayowezesha kuimarisha chama na kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi wa nchi yao. Tunawasisitizia watanzania CCM ni chama tawala ambacho kina penda amani na utulivu sio chama cha vurugu na tunawahakikishia wanachama wote wa ccm muishi na watanzania wengine kwa upendo, amani na utulivu na kuweza kushirikaana na watanzania wenzetu katika mambo ya kila siku bila kujali tofauti za kisiasa. Sisi sote ni watanzania. Wana CCM tuwe mfano bora kwa jamii.
Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba:
1. Binadamu wake ni sawa bila kujali rangi, dini, kabila au maeneo aliyotokea mwanachama wake.
2. Kila mwananchi anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake. Kumshirikisha mwanachama kuchangia maoni yake ili kuimarisha sera na utekelezaji katika chama chake.
Amani , Upendo, Uzalendo na utaifa ni msisitizo mkubwa wa chama cha Mapinduzi kwa mtanzania popote alipo duniani. Sera hizi za CCM zimeifanya Tanzania kuwa kisiwa cha Amani na Utulivu barani Afrika.
TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
ASANTENI SANA
Imetolewa na mwenyekiti wa tawi-DMV- Marekani
loveness Mamuya