Diwani wa Kata ya Kwadelo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Alhaj, Omary Kariati akiendesha trekta wakati akiwasili kwenye hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa maji katika kata hiyo, jana. Jumla ya sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3, alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki zilipatikana pamoja na gunia 37 za alizeti yenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Kushoto ni Mwenyekiti wa wakulima wa Kwadelo, Sheikh Khamis Nchallo. .
Trekta 64 za wakulima wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, ambazo wamezipata kwa jitihada za diwani wa kata hiyo, Omary Kariati kutoka Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa- SUMA JKT, zikiwa zimeegeshwa eneo la mkutano ulioitishwa na diwani huyo, kwa ajili ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa maji wa kata hiyo, jana. Wakulima hao walifika na trekta hizo na kuwa mstari wa mbele kuchangia mradi huo wa maji. Jumla ya sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3, alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki zilipatikana pamoja na gunia 37 za alizeti yenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Wakazi wa Kata ya Kwadelo, wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, wanakabiliwa na uhaba wa maji safi na salama kwa zaidi ya miaka 20 sasa, kutokana na miundombinu iliyozinduliwa mwaka 1973, na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, wakati wa uhai wake, kufa kwa kukosa uangalizi. Pichani Diwani wa Kata hiyo, Omary Kariati (wapili kulia) na Msaidizi wake Bakari Ndee wakionyesha tangi la maji lililozinduliwa na Baba wa Taifa ambalo sasa halifanyi kazi. Diwani alionyesha tangi hilo, wakati wa harambee ya kuchangisha fedha za kufufua mradi wa maji. Sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3, alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki zilipatikana. Pia gunia 37 za alizeti zenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe zilichangwa kwa ajili hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa wakulima wa Kwadelo, Sheikh Khamis Nchallo.
Mkazi wa Kijiji cha Makirinyi, Khadija Mussa, akikabidhi kiroba cha alizeti kwa diwani wa Kata ya Kwadelo, Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Omary Kariati kuchangia ujenzi wa zahanati ya Kijiji hicho, wakati wa harambee ya kutafuta fedha za ujenzi wa zahanati, uliondeshwa na diwani huyo, jana. Jumla ya magunia 17 yenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, na sh. milioni 9.2 vilipatikana, ikiwa ni pamoja na sh. milioni 7 zilizochangwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.
Diwani wa Kata ya Kwadelo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Alhaj, Omary Kariati, akionyesha mtaro ulichimbwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere wakati wa uhai wake mwaka 1973, kwa ajili ya mradi wa maji katika Kata ya Kwadelo, Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, jana. Hata hivyo mradi huo ambao ulikuwa ukihudumia watu 1,200 wakati huo, umekufa miaka 20 iliyopita na sasa diwani huyo anaunganisha nguvu za pamoja za wananchi na serikali ya CCM kuufufua. Kwadelo sasa ina watu 11,800.
Msichana katika kijiji cha Kwadelo, Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma akitumia baiskeli kutafuta maji, katika kijiji cha Makiranya, jana.
Wazee wa Kata ya Kwadelo, wakipungua mikono kumuaga Diwani wa Kata hiyo, Omary Kariati, alipokuwa anaondoka baada ya kuendesha harambee kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufuma mradi wa maji, jana.Picha na Bashir Nkromo