Na Andrew Chale
CHAMA cha Kijamii CCK, kimeitaka Serikali kuchukua busara katika kumaliza mgogoro wa mpaka wa Tanzania na Malawi unaogombewa kwa sasa na kuachana kauli za kushabikia vita.
Katika taarifa yao iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, na kusainiw ana Katibu Mkuu, Renatus Muabhi ilisema kuwa busara za viongozi wa Tanzania, zimekua za mashaka sambamba na utashi mdogo na kauli zao za kuzungumzia vita bila ya kutafuta njia mbadala za mazungumzo.
“Ni kana kwamba viongozi wa Serikali hawajui hatari za waziwazi zitokanazo na vita, pasipo kujiuliza nani ni fundi wa vita!” alisema Muabhi.
Muabhi pia aliendelea kusema kuwa, hata enzi za Mwalimu Nyerere, kabla ya kuhamua kuingia vitani mwaka 1979 alitafutya suluhu mara kwa mara toka umoja wa mataifa akitaka kemeo.
“Sisi leo tunaongea kama vile vita inapinanwa na Mawazir!, ni lazima hekima itumike katika kutatua mgogoro wa aina zozote, na hata kuiga wenzetu wa Kenya walivyotatua mgogoro na Uganda juu ya mgogoro wa Migingo ambao ilifikia mpaka Mahakama ya Kimataifa ICJ” alisema.
Aidha, kwa upande wa mgogoro wa walimu, CCK ilisema kuwa Serikali inapaswa kukumbuka kuwa mgogoro sio harusi wala sherehe. “Migomo ni lugha ya watu ambao wanahisi hawasikilizwi, historia ya migomo inapaswa iangaliwe upya” alisema.
Ambapo walisema kuwa kwa migomo hii ndio nchi yetu na nchi zingine zinapata ukombozi toka katika mikono ya wakoloni.
-