Pages

Monday, November 12, 2012

TUHUMA DHIDI YA SIFA ZA MAJAJI, TARATIBU MAMLAKA YA MAPENDEKEZO NA UTEUZI


YAH: TUHUMA DHIDI YA SIFA ZA MAJAJI, TARATIBU
MAMLAKA YA MAPENDEKEZO NA UTEUZI
 
1.0. Utangulizi

Hivi karibuni zimetolew atuhuma kupitia Vyombo vya Habari mbalimbali hapa nchini dhidi ya SIFA za Majaji, TARATIBU, MAMLAKA ya Mapendekezo na Uteuzi wa Majaji unaofanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Miongoni mwa tuhuma hizo ni kwamba baadhi ya Majaji hawana SIFA stahili za kuwa Jaji na wngine kuwa hawakuteuliwa Majaji kwa mujibu wa Katiba ya Sheria husika.

1.1 Sifa za kuwa Jaji

Sifa za kuwa Jaji wa Mahakama Kuu zimetajwa na Ibara ya 109(7) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Sifa hizo ni kuwa na Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu kinachotambulika na Tume ya Vyuo Vikuu, na pia awe:

a) Amekuwa Hakimu;  au
b) Amekuwa Mtumishi katika taasisi ya umma; au
c) Amekuwa Wakili kwa muda usiopungua miaka kumi.

Aidha, Ibara ya 118(3) ya Katiba inataja sifa za Jaji wa Mahakama ya Rufani.
wa Sheria za Tanzania, tabia na weledi (Qualities of a Judicial Officer, Legal Knowledge and Experience, Professional Qualities). Tume pia huzingatia usawa wa kijinsia na kuhakikisha kuwa Majaji kwa pamoja wanatoa sura ya Utaifa wa Tanzania kwa mujibu wa maelekezo ya Ibara ya 8(2) ya Katiba.

2.3 Kuwasilisha Majina yaliyochambiliwa (Short-listing)

Baada ya majina kuchambuliwa, Tume huwasilisha majina hayo kwa Mheshimiwa Rais.

2.4 Upekuzi (Vetting)

Zoezi hili hufanyika kwa kuchunguza kwa undani zaidi tabia, maadili na mienendo ya waliopendekezwa. mara zote hatua hii hufanyika kabla ya uamuzi wa Mamlaka ya Uteuzi.

2.5 Uteuzi (Appointment)

Hatua hii ni ya Mwisho ambapo Mheshimiwa Rais humteua Jaji kwa mujibu wa Ibara ya 109 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

3.0 Msimamo wa Tume

Kuanzia mwaka 2006 hadi 9 Novemba 2012, Mhe. Rais ameteua Majaji wa Mahakama Kuu 61 na kufikisha idadi ya jumla ya Majaji wa Mahakam Kuu kuwa 66 ukilinganisha na jumla ya Majaji 35 waliokuwepo katika kipindi kushia mwaka 2003. Katika kipindi chote hicho Mamlaka ya Uteuzi yaani Mhe. Rais amekuwa akiteua Majaji wengi zaidi kuliko nafasi zilizoachwa wazi baada ya Majaji kustaafu kwa mujibuw a sheria, ili kukidhi mahitaji ya Mahakama na ukuaji wa demokrasia nchini.

Popular Posts