Pages

Wednesday, June 27, 2012

Tunalaani kupigwa na kuumizwa kwa dr ulimboka


Watanzania wapenda amani , utulivu , uhuru na mabadiliko popote mlipo .

Kuanzia usiku wa jana muda wa saa 6 hivi , Taifa letu limeanza kuandika historia mpya baada ya kutekwa kwa Dr Ulimboka ambaye ni Kiongozi wa chama cha madaktari Tanzania na ambaye aliongoza mgomo wa kwanza wa madaktari kote nchini .

Dr Ulimboka alipigiwa simu na mtu aliyekuwa anawasiliana nae mara kwa mara baadaye alitekwa nyara na watu wasiojulikana na kuondoka nae usiku huo huo bila ya taarifa zozote .

Daktari huyu amepatikana maeneo ya Bunju akiwa amepigwa vibaya na kupatikana na majeraha sehemu kadhaa za mwili wake na sasa hivi yuko wodi ya MOI kwa ajili ya matibabu zaidi lakini hali yake bado ni mbaya na hawezi kuzungumza chochote .

Tunalaani kabisa kitendo hiki cha utekeji nyara wa mtu asiyekuwa na hatia kisha kumdhuru kwa nia ya kuondoa uhai wake .

Vitendo hivi ni vigeni kabisa miongoni mwa watanzania haswa wa kizazi cha sasa ambao wamezoea kuishi kwa kuaminiana na kwa ujirani mwema kwa kipindi kirefu .

Pamoja na kulaani hivyo tunaomba mamlaka husika yaani serikali kuchukuwa hatua kali dhidi ya watekaji nyara hao walioendesha kitendo hiki kwa kuanza na kujua wale aliowasiliana nao mara ya mwisho mpaka kumpeleka huko alikofanyiwa hivyo .

Kwa tekinologia za sasa tunaamini ushahidi mwingi umeshajiweka wenyewe hadharani ni jukumu la serikali na wadau wengine wa ulinzi na usalama kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria .

Mwisho tunaomba wananchi haswa madaktari waache mgomo na waendelee na kazi zao bila hofu yoyote na kama kuna majadiliano yoyote yafanyike kwa njia za amani na kwa muda wa kazi sio kutafutana usiku au baada ya kazi ili kuleta usalama na kuaminiana.

Yona F Maro

Popular Posts