Pages

Monday, September 3, 2012

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad Ziarani Marekani na Uingererza

Viongozi na watendaji mbali mbali wa Serikali wakimshindikiza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad wakati akijiandaa kuelekea nchini Marekani na Uingereza kwa ziara ya kikazi. Picha na Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
--
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ameondoka nchini leo kuelekea nchini Marekani na Uingereza kwa ziara ya kikazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif ataanza ziara yake mjini North Caroline Marekani, ambako atahudhuria mkutano wa kimataifa ulioandaliwa na taasisi ya National Democratic Institute, inayoshughulikia masuala ya kukuza demorasia ulimwenguni.

Makamu wa Kwanza wa Rais amekuwa na uhusiano wa muda mrefu na taasisi hiyo, akiwa katika jitihada za kupigania demokrasia nchini Tanzania na ulimwenguni kwa ujumla, katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili iliyopita.

Katika ziara hiyo Maalim Seif anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa serikali za Marekani na Uingereza, pamoja na viongozi wa taasisi zinazoshughulikia sera za mahusiano ya kimataifa.

-Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais ameagwa na viongozi na watendaji mbali mbali wa serikali wakiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Fatma Abdulhabib Fereji, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdillahi Jihadi Hassan na Waziri wa Afya Mhe. Juma Duni Haji.

Popular Posts