Wadau, hii hapa chini ni maudhui ya barua iliyotoka Wizara ya Kazi na Ajira
yenye kumb na. HC 250/328/04/87 ya tarehe 30 Agost, 2012 kwenda kwa:
Mkurugenzi Mkuu,
Geita Gold Mine.
Mkurugenzi Mkuu,
Williamson Diamond Ltd.
Meneja Mkuu,
North Mara Gold Mine Ltd.
Mkurugenzi Mkuu,
Resolute Tanzania Ltd.
MenejaMkuu,
El-Hilary Mineral Ltd.
MkurugenziMtendaji,
Tulawaka, (Pangea Mineral Ltd.)
Mkurugenzi Mtendaji,
Buzwagi Gold Mine.
MenejaMkuu,
Ausdril Co. Ltd.
YAH: ZIARA YA KAMATI YA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA HIFADHI YA JAMII
Tafadhali husika na kichwa cha habari hapo juu.
Kufuatia kutungwa kwa Sheria Na. 5 ya marekebisho ya Sheria za Hifadhi za
Jamii ya mwaka 2012. Wadau mbalimbali walionyesha kutoridhika na mabadiliko
hayo ya sheria, hali hii ilisababisha kupitishwa kwa Azimio la Bunge la
tarehe 6 Agosti, 2012 ambalo pamoja na mambo mengine liliagiza wizara
husika kupitia upya sheria hiyo na kuishauri serikali ipasavyo kuhusu fao
la kujitoa.
Katika kutekeleza agizo hilo, Wizara ya Kazi na Ajira imeunda kamati ya
wataalamu kutoka sekta ya hifadhi ya jamii kupitia sheria hiyo na kuishauri
serikali ipasavyo katika kutekeleza majukumu yako. Kamati itatembelea wadau
wa sekta mbalimbali kwa lengo la kukusanya maoni.
Ukiwa mmoja wa wadau wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, unaombwa kuteua
wawakilishi wafuatao;
a) Idara ya Utumishi na Rasilimali Watu (1)
b) Wachimba Migodi (1)
c) Chama cha Wafanyakazi (TAMICO) (1)
Kamati inaomba kukutana na wawakilishi waliotajwa hapo juu tarehe 6
Septemba, 2012 saa 4.00 asubuhi katika ukumbi wa NSSF, Mwanza.
Aidha, unaombwa kugharamia gharama za washiriki wako.
Nakutakia kazi njema.
S.H. Kinemela
Kny: KATIBU MKUU
Katibu na mwenyekiti wa Tawi la chama cha wafanyakazi (TAMICO-GGM)
wameteuliwa kuhudhuria mkutano huo wa kukusanya maoni. Tutahakikisha maoni
yote ya wafanyakazi yaliyokwishatolewa yanajumuishwa katika kamati hii bila
kuchakachuliwa kwa namna yoyote ile.
Thomas Sabai,