
Vijana wa CCM wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu Asha Kipangula

Jeneza likiingizwa nyumbani kwa marehemu mjini Iringa

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, John Chiligati akiagana na baadhi ya waombolezaji kabla ya mwili wa aliyekuwa Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Mayr Chipangula, kuondoka Hospitali ya Taiafa Muhimbili Dar es Salaam,jana asubuhi kupelekwa Iringa kwa ajili ya maziko.

Msafara wa kuupeleka mkoani Iringa mwili wa marahemu Asha Kipangula ukiwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro jana, ukitokea Dar es Salaam, ambapo kwenye ofisi hiyo ulisimamishwa kwa muda kutoa fursa kwa wana-CCM na waombolezaji wenmgine kuaga

Muombolezaji akiangua kilio nyumbani kwa marehemu mjini Iringa

Mmoja wa viongozi wa CCM akilia kwa huzuni baada ya mwili kufika Morogoro jana

Katibu wa CCM, Mary Chatanda akiangua kilio mwili wa marehemu Asha Chipangula ulipofikishwa nyumbani kwao Iringa jana jioni

Sheikh Mohammed Kairo akiongoza dua, mwili wa marehemu Asha Kipangula uliowasili mjini Morogoro jana

Nape akizungumza na baadhi ya waombolezaji mjini Morogoro. Aliyesimama ni Kada wa CCM, Asas

Kiongozi wa msafara, LKatibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itiladi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akijadiliana na baadhi ya viongozi mwili ulipowasili mjini Morogoro. Baadhi ya viongozi hao ni Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Sixtus Mapunda.Picha na Bashir Nkromo