Pages

Wednesday, May 30, 2012

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mohd Aboud na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Saidi Mwema Walipotembelea Kanisa Lilochomwa Moto Huko Zanzibar

Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud akielezea jambo kwa Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga wakwanza kulia kuhusiana na kuchomwa moto kwa Kanisa hilo liliopo Kariakoo Mjini Zanzibar katikati ni Mkuu wa Jeshi la Polisi I,G,P Saidi Mwemwa.
Mku wa Jeshi la Polisi I,G,P Saidi Mwema akitoa hotuba kwa Maaskofu na baadhi ya waumini wa Kikristo katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar lililochomwa moto,ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.kuliani kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Abdalla Mwinyi na kushoto yake ni Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Abdalla Mwinyi Khamis akitoa hotuba na kuonyesha Umoja na Mshikamano uliokuwepo kati ya Waislam na Wakristo kwa Picha ambayo imebuniwa na Mchoraji wa kingereza na kuwataka kuendelea na mshikamano wao ili kuzidi kuleta amani nchini.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akielezea kwa Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud na Viongozi wengine mbalimbali kile kilichotokea baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akibubujikwa na Machozi kwa kuguswa na hotuba iliokuwa ikitolewa na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa na baadhi yao kuhusishwa na tukio hilo.
Mkuu wa Dini ya Kiislam Afisi ya Mufti wa Zanzibar Thabit Noman Jongo akitoa hotuba ya Dini inavyoeleza kuhusiana na kudumisha Amani na Usalama katika nchi na kuondosha mifarakano na chuki na kuharibu mali.Katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar ambalo limechomwa moto.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akimuonesha Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohd Aboud maeneo yalioathirika zaidi baada ya Kanisa hilo kuchomwa moto katika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.Picha na Yussuf Simai-Zanzibar

Popular Posts