Wakati
Zanzibar Sakata la Waislamu kuendeleza kitimtim kufuatia kutoonekana
kwa Kiongozi wa Kundi la Uamsho Vurugu zimeendelea kutawala eneo la
Darajani na kusababisha Polisi kulazimika kutumia mabomu ya machozi
kutawanya watu.
Jijini
Dar es Salaam hali si tofauti na hiyo maeneo ya Kariakoo maduka kadhaa
yamefungwa kufuatia vurugu kama hizo baada ya Swala ya Ijumaa kufuatia
pia kukamatwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania
Sheikh Ponda yamekuwa ni matokeo ya vurugu watu kukimbizana huku Polisi
wakidhibiti Usalama na Amani kuelekea harijojo.(Picha na Maktaba).
Maeneo
ya Posta karibu na Wizara ya Mambo ya Ndani Askari wameweka utepe wa
kudhibiti watu kuingia katika maeneo hayo kitendo kilichosababisha
shughuli nyingi kusimama.
Pichani
ni Jeshi la Wananchi Tanzania likiwasilia maeneo ya Kariakoo kuongezea
nguvu kwa ajili ya kutuliza ghasia.
Pichani ni Vipeperushi vilivyotolewa na Waumini wa Dini ya Kiislamu kabla ya maandamano leo
Picha juuu Doria kali ya jeshi la polisi ikiendelea jijini Dar es Salaam hivi sasa
Akari wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)Wakipita maeneo ya kariakooo mchana huu baada ya vurugu kutokea.
---
---
DAR ES SALAAM
Vurugu
kubwa zimetokea mchana huu katika maeneo yanayozunguka eneo la Kariakoo
na kusababisha hofu kubwa na Polisi wamelazimika kutumia mabomu ya
machozi na kutawanya mikusanyiko ya watu waliokuwa wamejiandaa
kuandaamana kuelekea katika Ikulu ya Magogoni jijini.
Maduka
yote katika maeneo hayo yamefungwa na shughuli mbalimbali zimesimama
pamoja na Ofisi mbalimbali zimefungwa kutokana na hofu kubwa iliyotanda.