Pages

Wednesday, June 6, 2012

Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Wananchi CUF Yalaani Taarifa ya UVCCM

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF- Chama Cha Wananchi)
JUMUIYA YA VIJANA - JUVICUF
Office of the Secretary General
Party Headquarters, P.O. Box 3637, Zanzibar, Tanzania
E-mail:cufhabari.co.uk Homepage: www.cuftz.org


Our Ref: CUF/HQ/JUVICUF/003/2012/Vol 13 Date: 06/06/2012


Jumuiya ya vijana ya Chama cha Wananchi CUF imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kikao cha baraza kuu la UVCCM iliyotolewa katika vyombo vya habari na Katibu Mkuu wake Martin Shigella kuhusiana na vurugu zilizotokea Zanzibar hivi karibuni. Kwa mujibu wa taarifa hiyo aliyoitoa amesema, serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar inahusika na vurugu hizo.


Sisi vijana wa JUVICUF tunalaani kauli hiyo kwani juhudi za kuipata serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar haikuwa kazi nyepesi jambo ambalo linajulikana na wazanzibari, watanzania na ulimwengu mzima. Serikali ya umoja wa kitaifa imepataikana kwa taabu nyingi baada ya Zanzibar kupoteza muelekeo wake, ustawi wake na roho za watu wake.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe Dr Ali Moh’d Shein alitoa taarifa rasmi kuhusiana na vurugu hizo. Kauli hiyo ya UVCCM ambayo imejaa shutuma dhidi ya serikali ya Dr Shein anayoiongoza, ambayo imekuja mara baada Rais wa kutoa taarifa yake rasmi kuhusiana na vurugu hizo ni ya utovu wa nidhamu wa wazi unaopaswa kulaaniwa na kukaripiwa kwani inaweza kuwa ni sawa na cheche ya moto katika nyasi kavu. Kuvurugika kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ambayo inafanya kazi zake kikatiba na kuaminiana ni kurejesha nyuma umoja na maendeleo yaliyopatikana.

JUVICUF inatoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu, wavumilivu, na kuitumia fursa ya kutoa mawazo yao bila ya jazba, pamoja na kutowanyima wengine nafasi ya kuwasilisha mitazamo yao. Vitendo vya watu wachache kuchoma makanisa na kuharibu mali za watu ni vya uvunjifu wa sheria na kinyume na Utamaduni wa Kizanzibari; uchunguzi wa kina ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria, bila uonevu wala upendeleo.

Tahadhari iwepo ya kuepuka matumizi ya mabavu yanayoweza kuleta hamasa kwa wananchi, hatimaye ikachochea vitendo vya hujuma dhidi ya watu na mali zao, na pia kuepuka tabia isiyokuwa ya haki, ya kuwabambikizia kesi wananchi. Ni lazima kwa wakati huu, na haraka iwezekanavyo, Serikali ikazungumza na Masheikh, bila ya kuona muhali, na kwa uwazi kabisa, ili kutafuta suluhu ya kudumu, kwa faida ya Nchi na Taifa kwa Ujumla.

HAKI SAWA KWA WOTE

…………………………………….
Khalifa Abdalla Ali
KATIBU MKUU

Popular Posts