Pages

Monday, June 4, 2012

Taarifa kwa Umma:KONGAMANO LA TAIFA LA UCHUMI, 6 JUNI 2012, DAR ES SALAAM

KONGAMANO LA TAIFA LA UCHUMI, 6 JUNI 2012, DAR ES SALAAM

Mtandao wa wanataaluma Tanzania (TPN) ni wadau muhimu wa maendeleo ya Tanzania, TPN imeamua kuandaa Kongamano la Taifa la Uchumi kujadili mafanikio, changamoto na kupendekeza njia mbadala/suluhishi kwa ajili ya Uchumi wetu ili Tanzania iweze kuwa hali ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Kongamano hili litafanyika jumatano tarehe 6 Juni 2012 katika Jiji la Dar Es Salaam,
Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Mtaa wa Shaaban Robert , mkabala na IFM.
Muda ni kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni

Maudhui ya kongamano hili ni : Kujenga Tanzania ijayo endelevu
"kubadilisha namna ya kufanya mambo yetu"
Kushiriki ni BURE piga simu au tuma ujumbe mfupi wa jina lako kwa
+255 (0784/0767/0713) 618320, 0716 898685, 0784 482597 au barua pepe kwa magesa@hotmail.com , pmagesa@gmail.com , pharesmagesa@yahoo.com
(chakula na vinywaji vitagawiwa kwa washiriki waliothibitisha, tafadhali tunaomba wote wanaotaka kushiriki wathibitishe ushiriki wao haraka iwezekanavyo).

Ni matumaini yetu kuwa watanzania wengi watahudhuria ikiwa ni pamoja na watanzania wa kawaida, wafanya maamuzi muhimu na watunga sera, watunga sheria (wabunge) na wanadiplomasia, wakuu / wawakilishi wa mashirika ya muhimu katika uchumi kama Usafiri, Utalii, Mawasiliano, Madini, Nishati, Ujenzi na sekta ya Kilimo, taasisi za fedha, Viwanda, Biashara, jamii na sekta nyingine nyingi.

Kongamano hili litawashirikisha wasemaji muhimu (wataalam katika maeneo yao) na wachangia mada ambao ni magwiji kiuchumi na masuala ya jamii, pia kutakuwa na majadiliano ya wazi kwa umma.

Kwa njia hii tunatarajia kujenga jukwaa la mazungumzo ya kitaifa kuhusu hali ya uchumi wetu na kushirikisha wananchi kwa ujumla katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu ya kawaida yanayotukabili sasa.

Sisi wanataaluma tuna nia ya kufanya tukio hili kila mwaka.

Mada zifuatazo zitawasilishwa katika kongamano hili:

1. Ndiyo tunaweza kwa kutumia uwezo wetu wa ndani na Phillemon CG Kisamo, Mkurugenzi Mtendaji, Peak Performance International (T) Ltd

2. Je elimu yetu na mfumo wa mafunzo ni "injini" kwa ajili ya ukuaji wa uchumi ? na Masozi David Nyirenda, Mtaalamu katika Mipango ya Elimu, Uongozi, Fedha, Uchumi ya Elimu na Mafunzo ya Sera; Afisa Mwanamizi, Mamlaka ya Elimu Tanzania

3. Uongozi Kama Uwakala Katika Utawala Bora, na Dickson Hyasint Hyera, Mkuu wa Ukaguzi, KCB Bank Tanzania Ltd na Mkurugenzi Mshauri, Konsalt

4. Ukulima wa kibiashara na Raymond J. Menard, Mkurugenzi Mtendaji - Cheetah Development

5. Vizuizi visivyo vya kikodi (NTB) na madhara katika juhudi za Ushirikiano wa Kikanda nini LAZIMA kufanyika? Na Ndugu Lyimo wa TradeMark East Africa

6. Mikutano ya G20 G8 na Ahadi kwa Tanzania kuna manufaa au athari yoyote ?

7. Viwanda Vidogo (kuangalia nini kilitokea kwa mipango ya kuanza katika serikali ya awamu ya kwanza) na nini kifanyike sasa na kila mmoja mdau

9. Uwekezaji katika Kilimo nini kifanyike katika muda mfupi, kati na mrefu juu ya masuala ya umiliki wa ardhi na nishati vijijini

10. Maeneo makubwa ajira kwa ajili ya kuzalisha ajira kama suala mtambuka katika serikali na sekta binafsi, Je sheria za kazi ni maridhawa na kuna mazingira mazuri katika hali halisi, katika Tanzania na katika kanda?

11. Jinsi gani Madini na gesi zinaweza kutumika kukuza Uchumi Tanzania na Fred Msemwa Matola, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ukaguzi wa Ndani, Nishati na Maji (EWURA)

12. Biashara ya Kilimo , bidhaa na Huduma , mzunguko wa thamani na maendeleo, usimamizi na ufadhili - chombo kamili kwa ajili ya kupunguza umaskini uliokithiri na Herment A. Mrema wa Africa Rural Development Support Initiative.

13. Fursa na Changamoto kwa kutumia njia rasmi na Elimu ya Ujasiriamali usio rasmi juu ya kujenga kizazi cha pili cha Wajasiriamali wa Tanzania na Dr Donath Olomi, Mkurugenzi Mtendaji-Taasisi ya Maendeleo ya Usimamizi na Ujasiriamali (IMED)

14. Taifa lenye Afya ni muhimu kwa kukuza Uchumi: jukumu la Tiba Asilia na virutubisho Chakula na Benson Mwasaga Mahenya, Mkurugenzi - ACG / Tanscott CPA.

Pia kutakuwa na watoa mada na wachangiaji wengine.

Wajumbe wote watashiriki katika majadiliano kwa , baadhi ya masuala yanaweza kuibuliwa kutoka ukumbi ili mradi yalingane na maudhui.

Kongamano hili limedhaminiwa na kuwezeshwa na:

1. African Barrick Gold Plc (ABG)
2. Car Track (T) Ltd
3. SIA Ltd (SME in Action)
4. Professional Approach Group
5. Mbezi Garden Hotel Ltd
6. Geo Fields (T) Ltd
7. New Solutions Inc. Ltd
8. ID Cards Solutions Ltd
9. www.gushit.com
10. Haak Neel Productions ltd

Bado wadhamini wanakaribishwa kushiriki, wawasiliane nasi.
Nawakaribisha watanzania wote waje kushiriki katika kongamano hili muhimu.
Nashukuru kwa kunisikiliza.

PHARES MAGESA
RAIS – MTANDAO WA WANATAALUMA TANZANIA (TPN)

Popular Posts