YAH: VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013
Ndg. Waandishi wa Habari
Mwaka 2011/2012 Kambi ya Upinzani Bungeni ilitangaza Vipaumbele vyake
katika Bajeti Mbadalaambavyo vilikuwa:
1. Kupunguza misamaha ya kodi mpaka 1% ya pato la Taifa kutoka 3%
2. Kupunguza kodi kwenye bidhaa za mafuta ya petrol na dizeli ili
kupunguza mfumuko wa bei
3. Kufuta mfumo wa posho za vikao (Sitting allowances).
4. Kupeleka sehemu ya tozo ya ujuzi (Skills Development levy-SDL)
kwenye bodi ya mikopoya elimu ya juu.
Masuala haya pamoja na mengine yalikuwa sehemu ya Bajeti kivuli
iliyowasilishwa Bungeni na Kambi ya Upinzani.
Mapendekezo mawili,
(1) Kodi za mafuta ya Petrol na Diseli na
(2) Tozo ya SDL yalikubaliwa na kutekelezwa. Pendekezo la misamaha ya
kodi lilikubaliwa lakiniSerikali imeshindwa kulitekeleza na pendekezo
la kufutilia mbali posho za vikao halikukubaliwa.
Kambi Rasmi ya Upinzani inataka maelezo ya kina ya kwa nini Serikali
imeshindwa kutekeleza ahadiyake iliyoitoa Bungeni kwamba misamaha ya
kodi itapungizwa mpaka kufikia 1% ya pato la Taifa.Halikadhalika Kambi
ya Upinzani inarejea wito wake wa kufutwa kwa Mfumo wa posho za
vikao(sitting allowances)
Serikali imependekeza Bajeti ya Tshs. 15trillioni kutoka Tshs. 13
trillion. Hata hivyo ni dhahirikwamba Bajeti ya 2011/12 ilikuwa ina
changamoto kubwa za utekelezaji. Serikali ieleze itawezajekutekeleza
Bajeti ya 15trillioni?
Katika Bajeti Mbadala ya 2012/2013 Kambi ya Upinzani itajikita katika
maeneo yafuatayo nakuishinikiza Serikali kuyatekeleza.
1.Kuendelea kushinikiza kupunguzwa kwa misamaha ya kodi mpaka 1% ya
Pato la Taifa. Hivi sasamisamaha ya kodi ni sawa na misaada yote
kutoka nchi wahisani, Tshs 1.03 trillioni ni sawa na 3% yaPato la
Taifa.
2. Kuelekeza raslimali fedha kwenye maendeleo vijijini hasa kujenga
miundombinu kama barabara za vijijini na umeme vijijini.
3. Kuelekeza fedha za kutosha kukarabati Reli ya Kati na kufufua njia
za Reli za Tanga, Moshi na Arusha.
4.Kuongeza wigo wa kutoza tozo la ujuzi (Skills Development Levy)
ambapo sasa waajiri wote walipe ikiwemo Serikali na mashirika ya umma.
Pia kupunguza tozo hili mpaka 4% ambapo 1/3itaenda VETA na vyuo vya
Ufundi na 2/3 itaenda Bodi ya Mikopo ili kukabili changamoto yamikopo
kwa wanafunzi.
5.Kushusha kima cha chini cha kodi ya mapato (PAYE) mpaka 9% ili
kuwezesha wananchi wa haliya chini kubaki na fedha za kutumia na
kukuza uchumi.
6.Kuongeza mapato ya ndani na kupunguza mikopo ya kibiashara kwa
kuhakikisha mapato ya ndaniyanafikia 20% ya pato la taifa, kuongeza
nguvu za kisheria na udhibiti ili TRA ikusanye mapato zaidikwenye
kampuni za simu na kwenye shughuli za uchimbaji wa madini, mafuta na
gesi.
7.Kutayarisha Taifa kuwa na uchumi wa Gesi.
8.Kupunguza /kufuta kodi kwenye bidhaaa za vyakula kwa muda maalum ili
kushusha mfumuko wabei.
9.Kuweka mfumo mpya wa elimu kwa kushirikisha sekta binafsi katika
kutoa elimu kwa ubora zaidi,ikiwemo kuundwa kwa chombo cha Udhibiti wa
Elimu(Regulatory authority)
10.Kutoa vipaumbele na unafuu vya kikodi kwa viwanda vya ndani
vinavyotumia malighafi za nchni hasa za kilimo na zenye kuongeza ajira
kama Korosho,Pamba na Mkonge.
Kambi ya Upinzani itaendelea kufuatilia kwa karibu sana suala la kukua
kwa deni la Taifa
amabalolimefikia hadi Tshs 22 trillioni na kutaka ukaguzi maalum
kuhusu akaunti ya Deni la Taifa.
Kambi ya Upinzani itawekeza kusimamia kwa karibu suala la matumizi
yasiyo na tija ya Serikali hasakwenye magari na posho mbalimbali na
Kwamba fedha nyingi zitumike kwa miradi mikubwa yamaendeleo ili kukuza
ajira. Halikadhalika namna ya kupta fedha za kutekeleza mpango
waMaendeleo wa Miaka mitano
Zuberi Kabwe Zitto(Mb) Waziri Kivulu-Fedha na Uchumi.