Pages

Friday, August 3, 2012

Balozi Seif Ali Iddi:Vijana Tumieni Vyema Fursa za Kilimo,Ufugaji na Uvuvi

Waziri wa Mifugo na Uvuzi wa Zanzibar Mh. Abdillah Jihadi Hassan aliyevaa suti nyeupe akiuliza swali kwa mtaalamu wa utengenezaji wa boti kutoka shirika la Uvuvi la Mwanza . Kati kati ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye ni mgeni rasmi wa sherehe za Wakulima nane nane kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohd Shen akifuatilia ufafanuzi wa jibu la swali hilo. Kushoto ya Balozi ni Naibu Waziri wa Kilimo na Mifugo wa Tanzania Bara Mh. Adam Malima.
Wazalishaji wa mazao ya nafaka kutoka Wilaya ya Singida wakimpatia maelezo mgeni rasmi wa uzinduzi wa sherehe za Wakulima nane nane Kitaifa mkoani Dodoma Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba ra Rais wa Zanzibar Dr. Sheni jinsi ya uzalishaji wa mazao hayo Kitaalamu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif, Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar Mh. Jihad Hassan pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo na Mifugo wa Tanzania Bara Mh. Adam Malima wakipatwa na butwaa kwa jinsi wajasiri amali wa manispaa ya Singida walivyokuwa mahiri katika kusarifu Boga kwenye mapishi tofauti ikiwemo pia Keki.
Wataalamu wa Kituo cha sana za Kilimo Arusha { Camartec } wakimpatia Maelezo Balozi Seif Ali Iddi ya usanifu na utengenezaji wa vifaa mbali mbali kwa ajili ya matumizi ya taasisi, Vikundi vya ushirika pamoja na jumuiya za uzalishaji mali.
--
Vijana Nchini wametakiwa kuzitumia fursa zilizowekwa na Serikali zote mbili katika sekta za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi ambazo tayari zimeonekana kuwanufaisha watu wengi waliojaribu kufuatilia kwa makini.

Wito huo umetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohd Shein wakati akizindua sherehe za Siku kuu ya Wakulima Nane nane mwaka 2012 katika Viwanja vya Maonyesho ya Kilimo Nzuguni Mkoani Dodoma.

Dr. Shein katika Hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema ni muhimu kwa Vijana kutambua kuwa wana nafasi nzuri ya kuendeleza Maisha yao na kutoa mchango mkubwa wa Maendeleo ya Taifa kwa kujishughulisha katika Kilimo, Uvuvi na Ufugaji.

Alisema inasikitisha kuona baadhi ya Vijana wamekuwa na ndoto za kupata utajiri wa haraka ambao matokeo yake wanajiingiza katika harakati zisizo na muelekeo zinazoishia kujitumbukia katika vitendo viovu vinavyozorotesha jitihada za Taifa za kutafuta Maendeleo.

“ Dhana ya kuwa maisha bora yako mijini imeshapitwa na wakati. Mashambani kunaweza kuwa na maisha bora zaidi kuliko mijini kwa sababu hakungojei mshahara wa mwezi bali kuna mshahara wa kila siku”. Alisisitiza Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba Vijana wakati huu ni vyema wakazingatia zaidi kuwa wao ndio nguzo kubwa ya Maendeleo ya Taifa lolote lenye nia ya kuleta Maendeleo ya kudumu. Alisema Sekta ya Kilimo bado inaendelea kuwa mhimili wa Uchumi wa Taifa kwa vile inatoa ajira ya zaidi ya asilimia 77.5% ambapo Wananchi waliowengi wanaishi Vijijini.

Balozi Seif alifafanua kwamba Serikali zote mbili zitaendelea kutekeleza mipango tofaui katika sekta hizo kwa kushirikisha wananchi ili kuwawezesha na kuongeza kipato chao na hatimae waweze kuchangia kikamilifu katika ukuaji wa pato la Taifa.

Aliwahakikishia Wananchi kwama Serikali zote zitajitahidi kuwajengea mazingira bora Wakulima, Wavuvi na Wafugaji ya kumudu kununua bei za pembejeo, huduma za Matrekta kwa lengo la kupata msukumo wa kuimarisha shughuli zao.

Alisisitiza kwamba mpango huo unalenga kwenda sambamba na utoaji wa mafunzo na Elimu bora kwa wote watakaojishughulisha na Sekta hizo za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi.

Aliwakumbusha Wananchi kuongeza bidii katika matumizi ya rasilimali ya Bahari, Maziwa, Mito katika kuendeleza Sekta ya Uvuvi ambayo inasikitisha kuona kuwa mchango wa sekta hiyo katika pato la Taifa ni asilimia 1.5% tu.

Balozi Seif aliongeza kwamba Jamii inapaswa kuendelea kupiga vita vitendo yote vya Uvuvi haramu ili kuifanya shughuli hiyo iwe ya kudumu na inayozingatia mahitaji ya Jamii kwa sasa na hapo baadaye. “ Ni muhimu sasa kutunza mazingira yetu kuliko wakati mwengine wowote kutokana na tatizo la tabia Nchi inayoikumba Dunia. Hatuna budi sote tuzingatie kauli isemayo “ yatunze mazingira ili nawe yakutunze”. Alitilia mkazo zaidi Balozi Seif Ali Iddi.

Aliwapongeza waandaaji wa maonyesho hayo ya nane nane kwa jitihada zao zilizopelekea kufanikisha maandalizi yanayoridhisha na kuwaomba Wananchi kuhudhuria kwa wingi ili kujifunza mbinu bora na za Kisasa za uzalishaji katika sekta za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi. “ Nimefurahi kuona kuwa Wakulima, Wavuvi na Wafugaji kutoka Mikoa yote ya Tanzania wako hapa kwa ajili ya kujifunza na kusherehekea sherehe hizi. Shrehe zimefana sana.Hongereni sana”.

Balozi Seif alikuwa akimwaga sifa kem kem. Akitoa Salamu za Wakulima Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Tanzania {TASO } Bwana Angrei Moyo aliimba Serikali kuandaa sera Maalum kwa wote ya uendeshaji wa sherehe za nane nane kwa lengo la kuondoa matatizo ya mawasiliano katika ushiriki wa wadau wa Sekta hiyo.

Bwana Moyo utekelezaji wa pamoja ktika sekta hizo muhimu kwa uchumi wa Taifa zinaweza kuleta tija kwa faida ya Jamii yote ya Watanzania hasa Wakulima, Wavuvi na afugaji. Mwenyekiti huyo wa Chama cha Wakulima Tanzania pia alisisitiza umuhimu wa Teknolojia ulenge zaidi kwa wadau hao ili kuimariha mbinu za Kisasa za Uzalishaji.

Akimkaribisha Mgei rasmi katika uzinduzi wa Sherehe hizo za wakulima nane nane Naibu Waziri wa Kilimo na Ushurika Mh. Adam Malima ameyashukuru mashirika yote ndani na nje ya Nchini kwa juhudi zao za kusaidia Sekta ya Kilimo ambayo ndio mama kwa Uchumi wa Taifa. Mh. Malima alisema uungaji wao mkono umepelekea kuongeza kasi ya uzalishaji hasa kwa wakulima wa kipato cha chini vijijini ambao wanafkia asilimia 77.5% ya watu wote Nchini Tanzania.

Mapema asubuhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipata fursa ya kukagua mradi mkubwa wa shamba la Mizabibu katika Wilaya ya Chamwino unaoshirikisha Wakulima wa eneo hilo katika mpango wa ukulima wa bega kwa bega.

Balozi Seif amepongeza hatua za kuanzishwa kwa maradi huo ambao ni mfano kwa vile umeanzishwa na Wakulima wenyewe jambo ambalo linafaa kuigwa na Sekta nyengine za uzalishaji nchini.

Alisema uwezo wa Wananchi wa kujiajiri wenyewe uo endapo Wataalamu watawaandalia miundo mbinu boraitakayokidhi mahitaji yao sambamba na uwezeshwaji kifedha.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif pia alipata fursa y kutembelea mabanda mbali mbali ya ualishaji wa Washirika hao wa sekta ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji kutoka mikoa mbali mbali Nchini Tanzania. Ujumbe wa mwaka huu wa maadhimisho ya sherehe za nane nane unasema Kilmo kwanza zalisha Kisayansi na Teknolojia kukidhi mahitaji ya idadi ya Watu Nchini .

Na
Othman Khamis Ame
Ofisi Ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Popular Posts