Mwananchi wa Kijiji cha Jambiani akiwasilisha maoni yake kwa njia ya Barua kwa Tume.
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakikusanya Maoni ya Wananchi wa Kijiji cha Jambiani kulia ni Kaimu mwenyekiti wa tume hiyo Dk Salim Ahmed Salim
Vijana wa Kijiji cha Jambiani wakisoma baadhi ya Vifungu vya Katiba ya Zamani kabla ya kuingia katika ukumbi wa kutoa maoni yao katika skuli ya Jambiani.
Wazee wa Jambiani wakiwa nje ya Ukumbi wa kutolea maoni ya Marekebisho ya Katiba wakibadilishana mawazo baada ya kutumia haki yao kisheria ya kutowa maoni yao juu ya uundaji wa Katiba Mpya ya Tanzania
wananchi wa kijiji cha jambiani wakisubi zao yao nao waweze kutowa maoni yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania, ilipofika katika viwanja vya Skuli ya Wilaya ya Kusini Unguja.
Wananchi wa Kijiji cha Jambiani wakiwa katika utaratibu wa kupanga mstari ili kuweza kutowa maoni yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipofika Kijijini hapo kukusanya maoni ya Wananchi wa Jambiani katika viwanja vya Skuli ya Jambiani.
Wananchi wa Kijiji cha Jambiani wakiwa katika utaratibu wa kupanga mstari ili kuweza kutowa maoni yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipofika Kijijini hapo kukusanya maoni ya Wananchi wa Jambiani
Wananchi wa Shehia za Paje na Bwejuu wakiwa katika viwanja vya mpira bwejuu wakisikiliza maoni ya wananchi wanayoyatowa mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania.Picha Zote na Mapara Othman-Zanzibar