Pages

Monday, November 19, 2012

VIJANA NCHINI WATAKIWA KUJIFUNZA ELIMU YA UJASIRIAMALI ILI KUONGEZA THAMANI KATIKA KAZI NA BIASHARA.


Mwezeshaji katika mafunzo ya Ujasiriamali katika Wiki ya Ujasiriamali Duniani Austin Makani (kushoto) akitambulisha meza kuu wakati wa Hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu na kufunga Mafunzo hayo. Mgeni rasmi Mkuu wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Ulingeta Mbamba (katikati), Mratibu Mipango wa Kitengo cha Ujasiriamali cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDEC) Bw. Elia Yobu (kulia), Makamu Mwenyekiti wa ZAYEE Bw. Omar Said Shabaan (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Professional Approach Development Bi. Lillian Secelela Madeje (kushoto) na Katibu Mkuu wa Shirika Lisilo la Kiserikali la ZAYEE (Zanzibar Association for Youth Education and Empowerment) Fatma Mabrouk Khamis (wa pili kushoto).
Pichani Juu na Chini ni Mkuu wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Ulingeta Mbamba akitoa hotuba wakati wa kufunga mafunzo ya Ujasiriamali kwa Vijana yaliyoandaliwa na Asasi ya ZAYEE (Zanzibar Association for Youth Education and Empowerment) na kutolewa na Kitengo cha Ujasiriamali cha Chuo Kikuu cha DSM (UDEC).
Dkt. Mbamba amesema mafunzo hayo ni muhimu sana kwa vijana kwa kuwa yatawawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi, umahiri, tija zaidi na yatawasaidia sana katika kufanya shughuli zao za kila siku ziwe za kujiajiri wenyewe au kuajiriwa.

Katika mafunzo hayo jumla ya vijana 103 (68 kutoka Dar es Salaam na 35 kutoka Zanzibar) wamejifunza mambo mengi pamoja na Ujasiriamali, Fursa za Biashara zilizopo na Changamoto zake, Jinsi ya kupata Wazo la Biashara pamoja na Mpango wa Biashara.
Katibu Mkuu wa ZAYEE Bi. Fatma Mabrouk Khamis akiwapa nasaha wakufunzi wa mafunzo ya Ujasiriamali na kuwataka elimu waliyoipata hapo ikazae matunda katika kazi na biashara wanazozifanya ili kuongeza tija itakayosaidia kukuza uchumi binafsi wa Taifa.Pia ameahidi kuwafikia vijana wa Mikoani kuwapa mafunzo ya Ujasiriamali yatakayowezesha kuimarisha biashara zao.
Mwenyekiti wa Shirika Lisilo la Kiserikali la ZAYEE (Zanzibar Association for Youth Education and Empowerment) Bw. Masoud Salim Mohamed akizungumza na wahitimu hao ambapo ametoa fursa kadhaa na kuwataka kujijengea utamaduni wa kujiendeleza.
Mkurugenzi Mkuu wa Professional Approach Development Bi. Lillian Secelela Madeje akizungumzia umuhimu wa wajasiriamali kutumia michanganuo ya biashara katika kukuza biashara zao.
Katibu Mkuu wa ZAYEE Bi. Fatma Mabrouk Khamis akipokea cheti kufuzu mafunzo ya ujasiriamali wakati wa wiki ya Ujasiriamali Duniani kutoka kwa Dkt. Mbamba ambayo kwa Tanzania ndio mara ya kwanza kufanyika.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Ujasiriamali wakipokea vyeti baada ya kuhitimu.
Pichani Juu na Chini baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo yaliyomalizika jana jijini Dar es Salaam.
Meneja Maendeleo ya Biashara wa Kibo Palace Hotel Charity Githinji (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya Ujasiriamali jinsi ya kupata wazo la biashara.
Wahitimu wa Global Entreprenuership Week Tanzania katika picha kumbukumbu pamoja na mgeni rasmi pamoja na wawezeshaji.
Bi. Fatma Mabrouk Khamis (wa pili kushoto) na Mwakilishi kutoka ILO pamoja na baadhi ya wahitimu.

Popular Posts