Pages

Monday, November 19, 2012

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu wa Bunge, Wiliam Lukuvi Amjulia Hali Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Isimani mkoani Iringa baada ya Kuvamiwa na Majambazi


Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu wa Bunge, Wiliam Lukuvi (Katikati) akimjulia hali Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Isimani mkoani Iringa, Angelo Burgio wakati alipomtembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa jana. Picha na Mpiga Picha wetu.  
---
 
Geofrey Nyang’oro na Pius Kadinde Iringa

IDADI ya watu wanaotuhumiwa kuhusika na ujambazi katika matukio mawili tofauti kwenye Parokia za Kanisa Katoliki za Kihsesa na Isimani mkoani Iringa imeongezeka na kufikia nane huku mmoja wa watu waliokamatwa akiwa ni Dereva wa Paroko wa Parokia ya Isimani, Padri Angelo Burgio.
Tukio hilo ambalo lilisababisha mapadri wawili wa Parokia ya Isimani ambao ni Paroko wa Kanisa hilo Padri Burgio na msaidizi wake Padri Herman Myala na mlinzi wa Parokia ya Kihesa, Batholomeo Nzigilwa kujeruhiwa na kulazwa katika hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa lilitokea usiku wa Novemba 15 na 16 mwaka huu.

Akitaja orodha hiyo mpya huku akisisitiza kuwa msako wa kuwatafuta watuhumiwa wengine unaendelea Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda alisema miongoni mwa watuhumiwa waliokamatwa ni pamoja na Dereva wa Paroko huyo ambaye hivi karibuni ndiye aliyemsindikiza kwenda kuchukua fedha Benki.
“Idadi ya watuhumiwa hadi sasa imefikia 8 na kati ya watuhumiwa wanne waliokamtwa jana katika msako unaoendelea hivi sasa mmoja wao ni Dereva Baba Paroko na ndiye aliyempeleka hivi karibuni kwenda Iringa Mjini kuchukua fedha,” alisema Kamuhanda.Kwa habari zaidi bofya na Endelea......>>>>>

Popular Posts