Pages

Sunday, July 8, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Hussein A. Kattanga kuwa Mtendaji Mkuu wa Idara ya Mahakama

Bwana Hussein A. Kattanga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Hussein A. Kattanga kuwa Mtendaji Mkuu wa Idara ya Mahakama kuanzia tarehe 1 Julai, 2012.

Uteuzi wa Bwana Kattanga ni sehemu ya utekelezaji wa Muundo Mpya wa Mahakama, na utekelezaji wa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Namba 4 ya Mwaka 2011.

Sheria hii inaanzisha Kada Mpya ya Waendeshaji wa Mahakama, yaani Court of Administrators.

Hadi anateuliwa kushika wadhfa wake wa sasa, Bwana Kattanga alikuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
5 Julai, 2012

Popular Posts