Pichani, Naibu Balozi wa Tanzania, London, Mheshimiwa Chabaka Kilumanga (pili kushoto), akiwapokea rasmi Wanamichezo wa Tanzania, watakao wakilisha Taifa katika Michezo ya Olimpiki jana kabla ya kufanya mazungumzo mafupi na Raisi wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, katika Hotel ya Churchill, jijini London, Uingereza.
Raisi wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe (mbele Kulia), Mkuu wa Msafara, Bwana Hassan Jarufu (mbele kushoto), wakiwafanya mazungumzo na Wanamichezo wa Tanzania katika Michezo ya Olimpiki, itakayofanyia nchini Uingereza mwaka huu 2012.
Raisi wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete,wakiwa katika picha ya pamoja na Wanamichezo wa Tanzania katika Michezo ya Olimpiki, itakayofanyia nchini Uingereza mwaka huu 2012.
--
Timu ya Tanzania itakayoiwakilisha nchi katika michezo ya Olumpiki, itakayofanyika nchini Uingereza, leo wamepata nafasi ya kukutana na kufanya mazungumzo mafupi na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, katika Hotel ya Churchill Hotel, mjini London, Uingereza. Mheshimiwa Raisi Kikwete, aliwapa Baraka za Watanzania na kuwaomba wajitahidi na kuliwakilisha vyema Taifa na kurudisha jina la Tanzania katika ramani ya michezo kama ilivyokuwa siku za nyuma.Wanamichezo hao ambao watalikisha Taifa, wameweka kambi yao katika Chuo Kikuu cha Bradford (Bradford University), katika mji wa Bradford, kabla ya kuhamia rasmi kwenye kijiji cha michezo hiyo (Olympic Village) tarehe 24 July, tayari kabisa kwa kuanza ushiriki wao katika mashindao hayo ya Olimpiki.