Pages

Saturday, July 14, 2012

TAARIFA JUU YA HALI YA UTENDAJI WA VIONGOZI WA BUNGE

TAARIFA KWA UMMA JUU YA HALI YA UTENDAJI WA VIONGOZI WA BUNGE

Taarifa hii ni matokeo ya ufuatiliaji wa shughuli za Bunge na mijadala ya Wabunge juu ya mahitaji ya umma kwao kwenye maendeleo, uongozi, kuimarisha utawala bora, uwajibikaji wa serikali na haki za binadamu na kuimarisha usimamizi wao kwa serikali kupitia mijadala yao katika vikao vya Bunge. Taarifa hii inahusika na utendaji wa viongozi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka 2011.

Kwa Ujumla:

Kumekuwa na upendeleo wa vyama katika kujadili na kuchangia hoja na kuonekana Mh Spika na Wenyeviti wa vikao kutumia vibaya kanuni za bunge kuwadhibiti wabunge kulingana na vyama vyao. Mfano ni pale Mh Spika alipomzuia Mh Tundu Lissu kumwuliza swali Mh Mizengo Pinda juu ya mauaji ya raia mikononi mwa vyombo vya dola kwa madai kuwa kuna kesi mahakamani juu ya hoja hiyo. Pamoja na Mh Lissu kujitahidi kufafanua tofauti zilizopo kati ya kesi inayomkabili yeye na wenzake na hoja anayoiulizia, bado Mh Spika ameendelea kuizuia hoja hiyo. Kulingana na maoni ya wabunge 36, Watendaji 22, wachambuzi 11 na wananchi 48 waliohojiwa, ubora wa uongozi wa bunge kwa mwaka 2011 ni kama ilivyo hapa chini:

NAFASI

JINA

SIFA YA KIPIMO

ALAMA WASTANI

MAONI YA WASHIRIKI

1

NDUGAI,

JOB

YUSTINO

USIKIVU KWA WABUNGE

2.5

Amejitahidi sana kukwepa upendeleo wa kisiasa na kuilinda serikali; haoneshi utashi wake kumiliki mamlaka aliyopewa na Kanuni za Bunge anapoongoza vikao.

UZINGATIAJI KANUNI

2.625

UPENDELEO WA KISIASA

2.5625

UZINGATIAJI HOJA

2.375

USHABIKI BUNGENI

3

JUMLA

KIWANGO

13.0625

WASTANI

2.6125

2

SIMBACHAWENE,

USIKIVU KWA WABUNGE

2.125

Msikivu kwa Wabunge haswa wenye HOJA zenye maslahi kwa Taifa; Amejitahidi sana kukwepa upendeleo wa kisiasa na kuilinda serikali; Anayumbishwa na makundi au siasa.

GEORGE

BONIFACE

UZINGATIAJI KANUNI

2.3125

UPENDELEO WA KISIASA

3.28125

UZINGATIAJI HOJA

2.09375

USHABIKI BUNGENI

3.4375

JUMLA

KIWANGO

13.25

WASTANI

2.65

3

MAKINDA,

ANNE

SEMAMBA

USIKIVU KWA WABUNGE

3.03125

Imara kwenye kanuni na kuzingatia hoja; Anayumbishwa na ushabiki kisiasa; si msikivu kwa wabunge.

UZINGATIAJI KANUNI

2.65625

UPENDELEO WA KISIASA

3.46875

UZINGATIAJI HOJA

2.75

USHABIKI BUNGENI

2.9375

JUMLA

KIWANGO

14.84375

WASTANI

2.96875

Anajitahidi sana kuzingatia kanuni; Anayumbishwa na makundi kisiasa; si msikivu kwa wabunge.

4

MHAGAMA,

JENISTER

JOAKIM

USIKIVU KWA WABUNGE

3.21875

UZINGATIAJI KANUNI

3.15625

UPENDELEO WA KISIASA

3.5

UZINGATIAJI HOJA

3.53125

USHABIKI BUNGENI

3.3125

JUMLA

KIWANGO

16.71875

WASTANI

3.34375

5

MABUMBA,

SILVESTER

MASELE

USIKIVU KWA WABUNGE

4.25

Haoneshi ushabiki wa wazi wa kisiasa; hushindwa kuhimili mivuto ya makundi na upendeleo wa kisiasa; Si msikivu kwa wabunge.

UZINGATIAJI KANUNI

4.25

UPENDELEO WA KISIASA

3.78125

UZINGATIAJI HOJA

3.90625

USHABIKI BUNGENI

3.25

JUMLA

KIWANGO

19.4375

WASTANI

3.8875

ANGALIZO LA VIWANGO:

1.00 – 1.49 = Uongozi Mzuri Sana,

1.50 – 2.49 = Uongozi Mzuri

2.50 – 3.49 = Uongozi wa Wastani

3.50 – 4.49 = Uongozi Dhaifu

4.50 – 5.0 = Uongozi Dhaifu Sana

Kwa Ujumla

Taarifa hii imeonesha mapungufu kadhaa kwenye uongozi na utendaji wa kazi wa viongozi wa Bunge na hivyo kutoa changamoto kwa viongozi wa Bunge na wabunge kuimarisha utendaji wao iwapo wangependa kutekeleza wajibu wao kwa jamii. Ni matarajio yetu kuwa wabunge watatumia taarifa hii kuimarisha mjadala wa bajeti ya 2012/13 unaoendelea, ikiwa ni pamoja na kendeha na kusimamia vema vikao na mijadala ya Bunge na kutoa changamoto kwa utendaji wa serkali kwa maslahi ya jamii.

Tunakumbusha pia kuwa bado Bunge limeendelea kutumia muda vibaya kwa wabunge kuendeleza vijembe, kebehi, shukrani, pongezi na salamu. Hata baada ya miaka miwili sasa baada ya Uchaguzi na Serikali kuundwa bado wabunge wameendelea kutoa shukrani kwa Rais, wapiga kura wao na wengineo. Matumizi haya ya muda yanapunguza mijadala na mwendelezo wa ushiriki wa wabunge kwa ufasaha.

Mapendekezo

1. Ipo haja ya wabunge kujiangalia kwa karibu uwezo na utayari wao kujadili maswala ya maslahi kwa taifa bila kuingiza ushabiki na maslahi binafsi.

2. Iangaliwe upya akidi ya wabunge katika kupitisha hoja (angalau iwe robo tatu na sio nusu ya wabunge kama ilivyo sasa).Hii iendane na haja kwa Mhe, Spika kujiridhisha bila kuacha shaka juu ya idadi ya kura za wabunge kwenye hoja husika, na haswa walioshiriki mjadala baadala ya kuingia kwa ajili ya kupiga kura tu;

3. Spika atumie mamlaka na kanuni za Bunge ili kudhibiti maudhui, mantiki na maana ya mijadala ya Bunge bila kuathiri maslahi ya taifa. Katika hili Mhe Spika, Naibu na Wenyeviti wa Bunge,wana dhamana ya kuhakikisha ushabiki wa kisiasa haupati nafasi kuvuruga Bunge

4. Tunaona ipo nafasi kubwa kwa Spika kusaidia na kuelekeza bunge ili lifanye kazi zake vizuri zaidi. Spika atumie nafasi hii baadala ya yeye kuangukia kwenye ushabiki na kuilinda serikali.

Imetolewa na Taasisi ya Raia ya Haki za Kisiasa na Mwenendo wa Bunge,

CIVIL AND POLITICAL RIGHTS WATCH

Marcossy Albanie

Mkurugenzi Mtendaji

Popular Posts