Wanakijiji wa Kimbiji,Wilayani Temeke,nje kidogo ya jiji la Dar-es-salaam, wamekuwa
wakipata usumbufu wa vitisho na kuharibiwa mazao na makazi yao kutoka baadhi
wanajeshi wa JWTZ,ambao wanania ya kutaka kuyachukua maeneo ya wanakijiji
wa Kimbiji kwa kutumia nembo ya Jeshi (JWTZ),kinyume cha sheria
Kuanzia mwaka jana 2011 wanajeshi wa JWTZ wamekua na tabia za kuvamia mashamba
ya wanakijiji Kimbiji na kuvunja makazi ya wananchi ambao wameipigia kura serikali
ya hawamu ya nne,na huku vyombo vya dola vikiwa vimenyamaza kimya.
Wanakijiji wa Kimbiji wanalalamikia Serikali ya wilaya,mkoa hadi Serikali kuu,kuwa
unyama,unyanyaswaji uharibifu unaofanywa na wanajeshi hao wa JWTZ dhidi ya
wananchi wa Kimbiji hauwezi kuvumiliwa, Kwani ni haibu na udhuni mkubwa kuona
vyombo vya dola vikiwa vinanyamaza kimya na huku wapiga kura walioipigia kura
serikali wananyanyaswa na Wanajeshi JWTZ .
Wanakijiji wa Kimbiji,Wilaya Temeke,wanazifahamu haki zao na maeneo yao ya
asili ambayo wamekua wakiishi kama wenyeji .Pia wanafahamu fika kuwa hakuna
eneo lolote linalomilikiwa na Jeshi bali wanajeshi wanataka kuchukua mashamba
na makazi ya watu kwa maslahi yao binafsi!
JESHI LINAGEUKA CHOMBO CHA KUANGAMIZA WENYEJI WA DAR,
NA UTAMADUNI WAO ! KINYUME CHA KATIBA
Inajulikana wazi kikatiba kuwa kila raia anayo haki ya kulindwa na kulindiwa
mali zake na katiba ya nchi ambayo ndio muongozo wa nchi,
Lakini wakazi wa kijiji na wenyeji wa hasili ya mkoa wa Dar-es-salaam wanajikuta
wanafukuzwa katika maeneo yao ya hasili ,tena maeneo ambayo yapo nje ya jiji !
Wakazi hawa wa Kimbiji, wanalalamikia serikali kuwa Jeshi JWTZ badala ya kuwalinda
limegeuka kuwa hadui wa kutaka kuwanyaka na kuwafukuza katika makazi yao !
ya asili ,
WANAJESHI WANAJARIBU KUTUMA BARUA ZA VITISHO KIJIJINI,
Cha kushangaza ni kuwa baadhi ya maofisa wa Jeshi wanatumia barua zenye
nembo ya jeshi kuzipeleka katika serikali ya kijiji hili kutaka kunyang'anya
maeneo ya watu. Wanakijiji na uongozi wao wanashangazwa sana sana
na unyama huu,ambao ni uvunjaji wa sheria,katiba ya nchi na haki za binadamu !
Wanakijiji wa Kimbiji,wilayani Temeke,Dar-es-salaam, hawajawahi hata siku
moja kukaa kikao na serikali au wizara ya Ardhi, na kujulishwa kuwa kijiji
chenu kitakua cha kijeshi ! Utafiti wa kina unaonyesha kuwa makazi na mshamba
ya kimbiji ni mali ya wanakijiji,hakuna eneo la wanajeshi.
HAIWEZEKANI KUHAMISHA WANAKIJIJI AMBAO NI WAKAZI WA ASILI,
HETI MAOFISA WA JESHI WAPEWE VIWANJA VYA KUJENGA MAKAZI !
kufanya hivyo ni kuwafukuza wenyeji wa hasili na kuua utamaduni wao,pia ni
kuenda kinyume cha katiba ya nchi.
Haiwezekani Serikali ikae kimya na raia wake ambao wameipigia kura wananyanyaswa
na chombo kama JWTZ kwa vitisho vya mtutu wa bunduki na magwanda ya kijeshi !
Wakijiji wanaiomba Serikali na tahasisi za haki ya binadamu kuingilia kati mateso haya.
Labda kwa maelezo zaidi wasiliana na Uongozi wa Kijiji,Diwani simu Na. 0713768082
Mwenyekiti: Simu namba 0713846688