Pages

Thursday, July 12, 2012

SIMBA SC YATWAA KOMBE LA URAFIKI UWANJA WA TAIFA

Ubao wa matangazo ukionyesha Simba 5 Azam FC 3 kwenye uwanja wa Taifa.
Waziri asiyekuwa na Wizara maalum Zanzibar Mh. Machano Othman Said akimkabidhi kombe la ubingwa wa michuano ya Urafiki nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma mara baada ya timu ya Simba kuifunga timu ya Azam FC magoli 5-3 kwa penati, baada ya kutoka suluhu magoli 2-2 katika kipindi cha dakika tisini, kwenye mchezo mzuri na wa kuvutia kwa timu zote uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo hivyo kuifanya Simba kuibuka mabingwa wa kombe hilo.
Wachezaji wa timu ya Simba wakimnyanyua juu juu golikipa wao Juma K. Juma baada ya kupangua penati mbili katika mchezo huo uliokuwa wa fainali katika michuano ya Urafiki.
Mashabiki wa timu ya Azam FC wakishangilia timu yao.
Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia timu yao. Picha/Fullshange Blog.

Popular Posts