Pages

Tuesday, July 10, 2012

Fatma Fereji:Ukataji wa Miti Ovyo Husababisha Uharibifu Mkubwa wa Mazingira Jambo Ambalo Hufanywa na Wananchi wa Zanzibar Hususani Akinamama

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Mhe, Fatma Abdulhabib Fereji
---
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Mhe, Fatma Abdulhabib Fereji amesema kuwa ukataji wa miti ovyo husababisha uharibifu mkubwa wa mazingira jambo ambalo hufanywa na wananchi wa Zanzibar hususan akinamama ndio wachangiaji wakubwa kutokana na kuwekeza maisha yao katika kilimo cha mwani.


Aliyasema hayo huko katika ukumbi wa baraza la Wawakilishi nje kidogo na mji wa Zanzibar alipokuwa akijibu suala la Mhe. Salehe Nassor Juma aliyetaka kujua wizara inampango gani wa kutoa utaratibu mbadala kwa kinamama kuweza kuwapatia njia bora ya kufungia kamba zao za mwani badala ya kutumia miti .


Alisema kwamba anakiri kuwa akinamama wengi wameweza kujiajiri wenyewe katika kilimo cha mwani kazi hiyo ndio inayowawezesha kujikimu kimaisha hivyo suala la kuwakataza akinamama hao kwa ghafla bila ya kuwapatia njia nyengine ya kutumia itakuwa ni gumu kwa wizara hiyo ikizingatia ni sehemu moja ya maisha yao .


Aidha alisema kuwa serikali kupitia taasisi zake zikiwemo wizara ya Mifugo na Uvuvi ,Kilimo na Mali asili pamoja na Ofisi ya Makamo ya Kwanza wa Rais ziliweza kupanga mipango maalum ambayo itaweza kuwapatia mbinu endelevu ambayo haitoweza kuathiri miti ambayo wakulima wa mwani kuacha kutumia miti
ya asili.

Na
Khadija Khamis –Maelezo-Zanzibar

Popular Posts