Sent: Tuesday, 7 August 2012, 15:33
Subject: : Yah: Uzinduzi wa Tawi la Chadema-London Kwenye Bar(Pub).
Kwako Mheshimiwa Katibu Mkuu wa Chadema Bwana Slaa.
Napenda kuleta kwako maoni yangu na Waislam wenzangu waliopo hapa Uingereza kwa kitendo cha Chama chako kuamua kufungua Tawi lake hapa UK Ndani ya bar ikiwa ni kipindi cha Mwezi wa Ramadhani.
.
Ni Jambo jema na zuri kwa chama chako kuwa na Matawi nje ya nchi kama ulivyofanya hivi karibuni nchini marekani lakini kwa hapa Uingereza ambapo uzinduzi wake utafanyika Leo majira ya saa mbili usiku takriban masaa saba kuanzia muda huu.
Kuna Mambo kadhaa ambayo yanatuweka kwenye wakati mgumu hasa sisi Waislam ambao tuko kwenye Mwezi mtukufu wa Ramadhani kwani shughuli yenyewe inafanyika Bar na hata muda wa kufuturu kwa wale tuliofunga ndio muda huo huo ambao shughuli hiyo itakuwa ikifanyika Kwenye Bar ya Thatched House maeneo ya East london.
Mheshimiwa Katibu mkuu kama nilivyosema kuwa kitendo cha chadema kuwa na tawi hapa uingereza ni hatua kubwa katika maendeleo ya demokrasia ya nchi yetu.lakini ingekuwa vizuri zaidi kama Chama chako kingejaribu kuwatizama watanzania wote bila kujali dini zao au sehemu ya Muungano wa nchi yetu wanaotoka.
Waislam hatuna tatizo kwenda kushiriki uzinduzi wa chama cha Chadema ndani ya Mwezi wa Ramadhan ikiwa tu muda wa shughuli uwe muafaka(Convenience)usiingilia ne na masuala kama haya ya kufuturu. watendaji wako walikuwa na fursa ya kutafuta ukumbi hata wa pound hamsini au pound mia moja lakini kwenye neutral ground ambapo hakuna pombe na kumbi za namna hiyo ziko nyingi East london.
Mwezi huu wa Ramadhani kwa huku Uingereza sisi tuliofunga tunafuturu kuanzia saa mbili na dakika 40 na kuendelea za usiku.Hapo ndipo linapokuja tatizo la muda wa shughuli hii ambayo ni muhimu kwa kila Mtanzania mpenda demokrasia kama ambavyo chadema yenyewe imekuwa ikijipembejea(ikijinasibu) kuwa ni chama cha demokrasia. kutengwa kwa baadhi ya Watanzania kwenye kushiriki demokrasia ya nchi yetu ni kitendo ambacho hakikutegemewa kupewa nafasi na Chama makini kama chadema.
Mheshimiwa Slaa ni vyema nikupe taarifa kuwa Watanzania wengi tuliopo hapa Uingereza wanaotoka visiwa vya Zanzibar ni wengi kwa idadi kubwa na ni washiriki wazuri wa Siasa za nchi yetu waswahili wana msemo wao "Wengi wape" na hiyo ndio demokrasia. Eneo hilo la East london watanzania wengi wao wanaoishi hapo ni Wazanzibar kuanzia barking,East Ham, Upton Park,Ilford na Dagenham wingi wao kiasi cha kuweza kununua Msikiti wao, Hapo utakapofanyika mkutano wa chadema eneo la Barking ni hatua chache sana kuna msikitiki wa Watanzania(walking distance), wamenunua Bar na kuifanya kuwa msikiti siku kama ya ijumaa huswaliwa swala tatu kutokana na wengi wao. Kitendo cha kuwa na msikiti wao eneo ni kukuthibitishia idadi kubwa ya Watanzania waislam wanaishi eneo hilo kwa hali yeyote ile ilitakiwa chadema watazame hali za Watanzania wenzi wao.
Mheshimiwa Slaa katiba ya Nchi yetu imekataza ubaguzi wa kidini au kijiografia na wewe hili unalitambua.Nchi hii ya Uingereza masiala ya equal opportunity policy ni ya lazima kwa kila taasisi ambayo inafanya shughuli zake hapa uingereza na ukija kwenye discrimination nalo ni jambo ambalo halivumiliki kuna sheria nyingi za kulinda haki na hadhi ya binadamu wote.
Mimi siamini kuwa Watanzania wawe toka kisiwani au wawe wa dini ya kikristo,waislam au wanaomini jadi wasiwe na mchango wowote kwenye kuleta demokrasia kwenye siasa ya nchi yetu.Wewe mwenyewe kuna Mambo mengi ya siasa utakuwa umejifunza kwa Wanasiasa wenzi wako kama mheshimiwa Hamad Rashid,mheshimiwa Jussa,Mabare Marando,James Mapalala,Austine Mrema,Hamad Rashid ambaye alikuwa kiongozi wako wa Kambi ya upinzani bungeni na kabla yake alikuwepo Mama Fatma Maghimbi kama kiongozi wako, nina imani hao viongozi wamekupa ujasiri na muongozo mkubwa.
Mheshimiwa Slaa nakuandikia wewe nikijua ndiye mtendaji mkuu wa Chama hivyo una uwezo wa kulihamisha zoezi kutoka kwenye Bar ya Thatched na kutafuta neutral ground hata pale kwenye msikiti wa Watanzania kuna ukumbi ambao unakodishwa kwa bei ndogo. lakini ili kulifanya zoezi lifanikiwe vizuri kuna Community Halls ziko nyingi na unaweza kupata wakati wowote na kutumia ukumbi wa msikiti nako itakuwa ni kuwabagua wasio waislam. muda ulipo wa masaa haya saba unatosha au si vibaya hata kulifanya zoezi hili kwa weekend.
Mheshimiwa Slaaa unaweza kutizama Blog za Mjengwa.blogspot.com au jestina George ukaona tangazo la chama chako kufanya shughuli hii muhimu na ya kihistoria lakini kwa bahati mbaya ndani ya BAR. hata imagine ya chama inaharibika kwa tukio muhimu la kihistoria kufanyikia Bar. inaonekana hamkuwa serious au hamko serious, mara nyinyi chadema mmekuwa mkija kwenye mikutano ya Chama cha Conservative cha hapa na Cuf wamekuwa wakija kwenye mikutano ya liberal Dem. hapa Uingereza hakuna mikutano inayofanyika bar huwa kwenye kumbi mbali mbali.
Kwa heshima kubwa naomba nikurejeshe kwenye Tangazo la chama liliko kwenye blog mbali mbali.
"Chadema inapenda kuwatangazia watanzania wote waishio London na sehemu za jirani kuwa kutakuwa na mkutano wa ufunguzi wa Tawi la Chadema london,Tawi ambalo litafunguliwa na mheshimiwa Godless Lema,ufunguzi huo utafanyika Thatched house Pub iliyopo Barking siku ya leo 7/08/2012 saa 20.00 mbili usiku Mawasiliano chris lukosi 07404279633,07903828119"
Mheshimiwa Slaa nina amini una uwezo mkubwa wa kurekebisha kasoro hii ambayo ina misingi ya udini na ubaguzi wa kijiografia ya nchi yetu na kinyume na katiba ya nchi yetu.
nina imani nawe kama mtu makini na Muadilifu,hatuwezi kuwasiliana na Bwana Lema kwa vile tayari mahakama kuu imekutana na hatia ya ubaguzi wa kidini kiasi cha kuvuliwa ubunge wake, mtu ambaye amewabagua Watu wa Arusha kwa dini na jinsia akileta ubaguzi huo huku ughaibuni ambako sisi Watanzania tunategemeana kwenye shida na raha, yeye ataondoka baada ya siku kadhaa huku nyuma kishatugawa na kuondoa umoja wetu wa watanzania.Hapa Uingereza kuna chama kikongwe kabisa kwa siasa za nje Cuf ambacho kina matawi Marekani na Canada na sehemu nyingine lakini hakijawahi kuwabagua watanzania walio nje mikutano yao yote hufanya kwenye kumbi ambazo mtu yeyote anaingia.halikadhalika CCM nao wana Tawi lao hapa mikutano yao haijafanyika bar katika kipindi kama hichi cha Mwezi wa Ramadhani.
Mwisho naomba nikukumbushe maoni ya mzee Mtei muasisi wa chadema pale ilipoundwa tume ya Katiba alilalamika sana kuwa tume ina wajumbe wengi wenye majina ya kiislam hasa waliotoka Zanzibar akahisi kuwa Haki hakufuatwa na akakosa raha kabisa.
.kitendo cha kuzindua chama Bar ni kuwakimbiza waislam wasiombe au wasishiriki nafasi za uongozi. ingekuwa Mwezi wa kawaida ambao si kama huu Ramadhai wapo waislam wanaokwenda bar lakini wengi wao ukifika mwezi mtukufu hawaendi Bar, jee watashiriki vipi kwenye Chama chako?usisahau minong'ono mingi kuwa chadema ni Chama chenye mlengo wa kikristu,kwa matendo haya ya Lema ni kuthibitisha shutuma au hisia hizo.
Mheshimiwa Dr.Slaa samahani kwa kukuchosha ila kwa heshima na taadhima naomba kuwasilisha kilio cha Waislam watanzania waliopo Uingereza dhidi ya vitendo vya ubaguzi wa wazi unaofanywa na chama chako.
Nakutakia kazi njema na natarajia ya kuwa utalifanyia kazi ombi letu sisi Waislam wa Uingereza.
Ni mimi mpenda demokrasia na Maendeleo.
-