Pages

Tuesday, July 3, 2012

MKUU WA WILAYA YA NACHINGWEA AANZA KAZI KWA KISHINDO

MKUU wa wilaya ya Nachingwea,Regina Chonjo akiandika maswali ya wananchi


mkuu wa wilaya ya Nachingwea,Regina Chonjo akiwa katika picha ya pamoja na akina mama wa wilaya hiyo

Muasisi wa TANU NA CCM,BI KANDURU AKIMPA MKONOMKUU WA WILAYA YA NACHINGWEA BI Regina Chonjo baada ya Mkuu huyokutembelea makazi ya Bibi huyo ambaypo alipata ufadhili wa kujengewaNyumba hiyo na kusikitishwa na Alivyotapeliwa katika ujenzi wake

Mzee Mnali akiuliza swali katika mkutano huo


WAZEE WA NACHINGWEA WAKIMSIKILIZA MKUU WA WILAYA YAONA BILA KUSITA WALIDAI KUSHANGAZWA KUPATA WITO WA MKUU WA WILAYAKUKUTANA NA WAZEE KWA KUWA KATIKA HISTORIA YAO HAWAJAWAI KUNA AUKUSIKIA JAMBO HILO KWAO



MKUU wa wilaya ya Nachingwea,Regina Chonjo amekerwa na hali ya uchafuuliozagaa kwenye maeneo mbalimbali ya mji wa Nachingwea na kuitakajamii kushirikiana naHalmashauri kujenga tabia ya usafi.

Mwandishi wa mtandao huu wa http://www.francisgodwin.blogspot.com/ kutoka mkoani Lindi Abdulaziz Video anaripoti kuwa ,Chonjo alisema kuwa licha ya kuwa na virimba katika maeneo mengi yamji bado wananchi wanaendelea kutupa taka ovyo na kufanya kila eneokuwa ni dampo.

“Kwa kweli hali ya mji wetu ni mbaya kwani hata siku ambayo nilifikanilionahali hiyo na nilishamweza mwenyekiti wa halmashauri kuwa halisi ya kupendeza na kumpataka kuweka mkakati wa kuwashirikishawananchi”alisema ChonjoAlisema kuwa kama watu wakishirikishwa kikamilifu wanaweza kubadilikakitabia na kujali usafi na mji wetu ukawa wa mfano kwa usafi kamailivyo mji mingine ambayo tabia ya usafi ni ya kawaida.

Kauli ya mkuu huyo wilaya aliitoa jana wakati akizungumza na wazee wamaeneo ya mji wa Nachingwea aliokutanao kwenye ukumbi wa chuo chaualimu kwa lengo la kujitambulisha na kubadilishana mawazo.

Awali swala la hali ya uchafu uliokithiri kwenye maeneo mbali mbaliya mji wa Nachingwea lilisemwa na mmoja wa wazee hao,Albert Mnaliambaye alisema kuwa maeneo ya yaliyo wazi yamegeuka kuwa madampo kwanikila eneo linatumiwa kutupia taka.

Mnali aliisema kuwa halmashauri imezidiwa na taka kwani takazinazozalishwa ni nyingi ikilinganishwa na uwezo wa kuzisomba kwanihalmashauri halina gari la kuzolea taka.

Mnali aaliishauri hamashauri kumtafuta mzabuni atakayekuwa na jukumula kuzoa taka badala ya kufanywa na halmashauri.

Popular Posts