Pages

Monday, July 2, 2012

WANAFAMILIA WA JAY DEE WATEMBELEA WATOTO YATIMA

Pichani Juu Wanafamilia wa Lady Jay Dee wakipakua chakula kilichoandaliwa Nyumbani Lounge kwa ajili ya kula pamoja na watoto yatima wa kituo cha Maunga Centre.
Pichani Juu na Chini ni Wanafamilia wa Jay Dee wakipakia mizigo tayari kuelekea kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre kwa ajili ya kukabidhi msaada.

Baadhi ya wanafamilia katika pozi kabla ya kuanza safari ya kuelekea kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre.

Kiongozi wa msafara LadyJay Dee akielekea kupanda usafiri maalum ulioandaliwa.

Wanafamilia ndani ya basi kuelekea Maunga Cente kituo cha watoto yatima kwa shughuli nzima ya kukabidhi msaada.

Wanafamilia Ester Ulaya Cathbert na Maggie wakifanya shopping katika maduka ya Kinondoni njiani kuelekea kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre.

Judith G. Habash a.k.a Komando Binti Machozi Lady Jay Dee akiwasili na Familia yake katika Kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre kilichopo maeneo ya Kinondoni Hananasifu.

Wanafamilia wa Jay Dee wakishuka kwenye basi baada ya kuwasili.
Vijana wa Familia ya Jay Dee wakishusha msosi ulioandaliwa Nyumbani Lounge kwa ajili ya watoto yatima wa Kituo cha Maunga Centre.
Baadhi ya zawadi zilizopekwa na Jay Dee Family katika kituo cha kuelea watoto yatima cha Maunga Centre.
Mwanafamilia wa Jaydee Wise Monica Kaaya akionyesha Upendo kwa mmoja wa watoto yatima wa kituo cha Maunga Centre.
Mlezi wa kituo cha Maunga Centre Bi. Zainabu Bakari akionyesha chumba wanacholala watoto wa kiume katika kituo hicho.
Hiki ni chumba wa wasichana.
Hapa ni mahali wanapotundikia neti.
Hiki ni choo wanachotumia yatima hao ambacho hakijaezekwa na bati.
Sehemu wanatotumia kupikia chakula.
Mtoto Khadija Mussa akisoma Risala kwa mgeni rasmi Komando Lady Jay Dee na Familia yake (hawapo pichani) ambapo amezungumzia changamoto ya mahali wanapoishi haparidhishi na kuwataka wadau kujitokeza kuwasaidia kuboresha eneo lao ikiwemo Choo, Sehemu ya kulala pamoja na ada za twisheni kwa watoto hao.
Wanafamilia wakisikiliza risala ya Kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre.
Lady Jay Dee na baadhi ya wanafamilia wakipiga makofi baada ya risala kusomwa na mtoto Khadija Mussa (hayupo pichani).
Lady Jay Dee akipokea risala kutoka kwa mtoto Khadija Mussa.
Lady Jay Dee akikabidhi msaada uliotolewa na Familia yake vikiwemo Mchele, Maharage, Mafuta ya Kupikia, Sabuni za Kufulia, Nguo, Juisi pamoja na vingine vingi. Anayepokea msaada huo ni Mlezi wa Kituo hicho Bi. Zainabu Bakari (kushoto) pamoja na mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho Khadija Mussa.Jay Dee Family inawakaribisha wadau wote watakaoguswa kutoa mchango chcochote walichonacho kupitia Jay Dee Family. Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Judyjaydee@yahoo.com.
Lady Jay Dee akibadilishana mawazo na walezi wa kituo hicho baada ya kukabidhi msaaada huo.
Mwanafamilia Ester Ulaya (kushoto) akiteta jambo na Komando Binti Machozi Lady Jay Dee.
Pichani Juu Wanafamilia wa Lady Jay Dee wakipakua chakula kilichoandaliwa Nyumbani Lounge kwa ajili ya kula pamoja na watoto yatima wa kituo cha Maunga Centre.
Watoto wa kituo cha Maunga Centre wakipata chakula cha mchana kilichoandaliwa na Jay Dee Family.
Vijana wa Jay Dee Family wakiwajibika kuhudumia chakula kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre.
Mlezi wa kituo cha Maunga Centre Bi Zainabu Bakari ambapo amezungumzia changamoto zinazowakabili ni sehemu ya kuishi wahudumu wa kituo hicho, mishahara ya kuwalipa wahudumu na makazi ya wahudumu wa kituo hicho.Bi. Zuhuru Bakari alisema kituo hicho kinalea watoto 30 ambapo watoto 20 wanalelewa nje ya kituo kwa baadhi ya walezi waliowachagua wao kutokana na ufinyu wa eneo jumla yake inatengeneza idadi ya watoto 50.
Mwanafamilia Ester Ulaya akizungumza kwa niaba ya Jay Dee Family ambapo amesema watakuwa bega kwa bega na kituo hicho na kuendelea kuwatafutia wafadhili wa kusaidia kituo hicho.
Baadhi ya wanafamilia katika pozi na walezi wa kituo hicho.
Wanafamilia katika picha ya pamoja na walezi wa kituo hicho pamoja na watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo hicho.
Zainul Mzige wa MO BLOG alijumuika na Familia ya Jay Dee katika kutoa msaada kwa watoto yatima wa kituo cha Maunga Centre.
Wanafamilia wa Jay Dee katika picha ya pamoja baada ya kuhitimisha zoezi zima la kutoa msaada kwa kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre.

Popular Posts