Meneja Mkuu wa Nokia Tanzania Samson Mwajwala,akionesha aina ya simu ya Nokia Asha 200 inayouzwa kwa shilingi 149,999 pamoja na muda wa bure wa maongezi na MB 125.Simu ingine ya Nokia Asha 302 inauzwa kwa shilingi 219,000 wateja watapata MB 500 kwa miezi sita mfululizo baada ya kuweka muda wa maongezi wa Shilingi 1000, 2000, au 5000 huku huduma ya facebook, twitter na Wikipedia zikiendelea kuwa bure,katikati Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Vodacom Tanzania Bw. Mngopelinye Kiwanga na Meneja bidhaa wa Vodacom Elihuruma Ngowi.

Meneja Mkuu wa Nokia Tanzania Samson Mwajwala,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya aina ya simu ya Nokia Asha 200 inayouzwa kwa shilingi 149,999 pamoja na muda wa bure wa maongezi na MB 125.Simu ingine ya Nokia Asha 302 inauzwa kwa shilingi 219,000 wateja watapata MB 500 kwa miezi sita mfululizo baada ya kuweka muda wa maongezi wa Shilingi 1000, 2000, au 5000 huku huduma ya facebook, twitter na Wikipedia zikiendelea kuwa bure,katikati Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Vodacom Tanzania Bw. Mngopelinye Kiwanga na Meneja bidhaa wa Vodacom Elihuruma Ngowi.
Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Vodacom Tanzania Bw. Mngopelinye Kiwanga, akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa simu aina ya Nokia Asha 200 na Nokia Asha 203, Nokia Asha 200 inayouzwa kwa shilingi 149,999 pamoja na muda wa bure wa maongezi na MB 125.Simu ya Nokia Asha 302 inayouzwa kwa shilingi 219,000 wateja watapata MB 500 kwa miezi sita mfululizo baada ya kuweka muda wa maongezi wa Shilingi 1000, 2000, au 5000 huku huduma ya facebook, twitter na Wikipedia zikiendelea kuwa bure,wanaoshuhudia kushoto ni Meneja Mkuu wa Nokia Tanzania Samson Mwajwala na kulia ni Meneja bidhaa wa Vodacom Elihuruma Ngowi.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini wakati wa uzinduzi wa simu aina ya Nokia Asha 200 na Nokia Asha 203, Nokia Asha 200 inayouzwa kwa shilingi 149,999 pamoja na muda wa bure wa maongezi na MB 125.Simu ya Nokia Asha 302 inayouzwa kwa shilingi 219,000 wateja watapata MB 500 kwa miezi sita mfululizo baada ya kuweka muda wa maongezi wa Shilingi 1000, 2000, au 5000 huku huduma ya facebook, twitter na Wikipedia zikiendelea kuwa bure.
--
Dar es Salaam, Julai 18, 2012 ...
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imeingia katika ubia na kampuni ya Nokia katika kutoa ofa ya aina mpya ya simu za Nokia kwa Watanzania.
Aina ya simu ambazo zimeingizwa katika ofa hiyo mpya ni simu aina ya Nokia Asha 200 na Nokia Asha 203 ambazo ni katika mpango maalum wa Vodacom wa kupunguza gharama za huduma za simu kwa vijana.
Kupitia simu hizo, wateja wataweza kupata huduma nafuu kwa simu ya Nokia Asha 200 inayouzwa kwa shilingi 149,999 na watapata muda wa bure wa maongezi na MB 125. Kwa simu ya Nokia Asha 302 inayouzwa kwa shilingi 219,000 wateja watapata MB 500 kwa miezi sita mfululizo baada ya kuweka muda wa maongezi wa Shilingi 1000, 2000, au 5000 huku huduma ya facebook, twitter na Wikipedia zikiendelea kuwa bure.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ofa hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Vifaa wa kampuni ya Vodacom Tanzania Bw. Mngopelinye Kiwanga, amesema kuwa ofa hiyo inalenga kuongeza soko kwa kampuni hiyo na kukuza utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa, na kuongeza kuwa vijana, ambao wanachukua idadi kubwa ya watu katika taifa, ni vyema wakapata huduma nafuu za mawasiliano ili kuchangia katika ukuaji wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
"Tunaamini kwa mpango huu, tutawafikia wateja wengi zaidi iwezekanavyo," alisema Kiwanga, na kuongezea kuwa kutakuwa na maboresho mbalimbali ya mtandao na ubora wa bidhaa, suala litakalo wawezesha wateja kufikiwa na huduma na kutanabaisha kuwa zipo ofa nyingi na bidhaa ambazo kampuni hiyo inatarajia kutoa kwa wateja wake ndani ya Mwaka huu.
" Napenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa tutaendelea kuboresha na kuleta huduma nzuri na bora kwa ajili yao ili kukidhi mahitaji yao ya kila siku na kuwa na mahusiano mazuri na wateja wetu," alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Nokia Tanzania Samson Majwala, amesema kuwa simu hizo zina sifa nzuri na ni rahisi kuzitumia, suala ambalo litawavutia watu wengi kununua na kuzitumia kwa urahisi.
"Simu hizi ni nzuri na rahisi kutumia. Nina imani kuwa wateja watafurahia na kuzitumia," alisema Majwala.