Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Mh. Dk. Shukuru Kawambwa (kulia) akitoa shukrani kwa kampuni ya simu za mkononi ya TIGO kwa kuwezesha kufanikisha mchango wa fedha shilingi Milioni 26 za Kitanzania kwa ajili ya kununua madawati kuwasaidia watoto wenye uhitaji hapa nchini kutokana na matembezi ya hiari yaliyofanyika mwezi wa Machi mwaka huu. Kaimu Meneja Mkuu TIGO Bw. Andrew Hodgson (katikati) na Kushoto ni Mtalaam wa Promoshen, Mahusiano na Udhamini wa TIGO Bw. Edward Shila.
Mkurugenzi wa Tasisi ya Hassan Majaar Trust (HMT) Bi. Zena Tenga (katikati) akitoa shukrani kwa kampuni ya TIGO baada ya kukabidhiwa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 26 zilizopatikana katika mfuko wa matembezi ya hiari ya TIGO ambapo amesisitiza kuwa nia ya Taasisi yake ni kuhakikisha kila mwanafunzi anapata dawati ili kukuza kiwango cha Elimu hapa nchini. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Michango wa HMT Dr. Sinare Yusuf na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya HMT Balozi Bertha Semu Somi.
Kaimu Meneja Mkuu TIGO Bw. Andrew Hodgson (katikati) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 26 Mwenyekiti wa Kamati ya Michango wa HMT Dr. Sinare Yusuf ambapo amesema mpango huo ni kulingana na dhamira ya kushirikiana na jamii katika kuelewa mahitaji ya jamii zinazotuzunguka maeneo tunayofanyia biashara. Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Mh. Dk. Shukuru Kawambwa.
Pichani ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Mh. Dk. Shukuru Kawambwa (kushoto) Mwenyekiti wa Kamati ya Michango wa HMT Dr. Sinare Yusuf (kulia) na Kaimu Meneja Mkuu TIGO Bw. Andrew Hodgson. Chini ya mradi wa shule tano kutoka Wilaya mbili (Njombe na Makete) zilizoko mkoa wa Iringa zitapokea madawati 135 kwa shule ya Maendeleo, 196 Umoja, Kumbila 200, Makonde 152, na Mbela 37.
Katika mradi huo Shule zilichaguliwa kulingana kuwepo kwaa haja kubwa zaidi ambapo mradi huo hautanufaisha tu shule na wanafunzi, bali kwa kununua madawati ndani ya nchi kutasaidia katika kutengeneza nafasi za ajira kwa wafanyabiashara na vijana katika maeneo hayo na hivyo kuleta maendeleo ya kiuchuni katika sehemu hizo.