KIKUNDI cha Vijana wa ngoma za asili cha Kyela mkoa wa Mbeya kilikuwa burudani kubwa wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi wa uendelezaji wa bonde la mto Songwe uliohusisha nchi mbili za Tanzania na Malawi,vijana hao walionyesha uwezo mkubwa wa kucheza ngoma za asili
WAZIRI wa Uchukuzi nchini Tanzania,Dk Harrison Mwakyembe (kushoto) na Waziri wa Maendeleo ya Maji na Umwagiliaji kutoka Malawi,Ritchie Bizwick Muheya wakifungua kitambaa kilichowekwa kwenye jengo jipya la makao makuu ya Mradi wa Maendeleo ya Mto Songwe mjini Kyela mkoa wa Mbeya juzi ulipozinduliwa rasmi.
WAWAKILISHI kutoka Malawi na Tanzania wakipiga picha ya pamoja baada ya Waziri wa Uchukuzi,Dk Harrison Mwakyembe(wa tatu kutoka kulia walioketi) alipomaliza kuzindua mradi wa maendeleo ya mto Songwe anayefuatia upande huo ni Waziri wa Maendeleo ya Maji na Umwagiliaji wa Malawi,Ritchie Bizwick Muheya na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Malawi, Sandaram Maweru,Kutoka kushoto ni mwakilishi wa AfDB,DanielVerdeil,Katibu Mkuu wizara ya Maji, Christopher Sayi na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro.Picha Zote na Christopher Nyenyembe-Kyela