Pages

Saturday, January 5, 2013

TAMKO LA JUVICUF JUU YA UTAPELI WA KUTOA GESI MTWARA

M'Kiti wa Jumuiya ya Vijana Ya Chama Cha Wananchi-CUF, Leo ameongea na Vyombo vya Habari. Na haya ndio Maelezo ya Press ya Leo.
NI HAKI YA MSINGI KABISA WANANCHI WA MKOA WA MTWARA KUANDAMANA KUPINGA GESI KUPELEKWA DAR ES SALAAM.WAKATI HAWAJUI HATIMA YAO.
TAREHE: 05/01/2013

Jumuiya ya vijana CUF Taifa inaendelea kuunga mkono harakati zinazoendelea mkoani Mtwara za kupinga mpango wa serikali wa kujenga bomba la kusafirishia gesi asilia kutoka mtwara hadi dare s salaam, jumuiya ya vijana CUF taifa inaamini gesi inahamishwa kwa matakwa ya watu Fulani na sio kwa manufaa ya taifa kama inavyoelezwa na serikali, jumuiya haioni sababu ya kiuchumi ya kuhamisha gesi Mtwara kupeleka Dar es salaam au sehemu nyingine yeyote ile kwa kuzingatia yafuatayo:-

1. Uamuzi wa kuhamisha gesi sio wa kiuchumi na haukuzingatia misingi ya kiuchumi kwani kama serikali ingeamua kujenga mitambo ya kufulia gesi (Plants) mkoani Mtwara ingeokoa mabilioni ya pesa yanayotumika kusafirishia gesi asilia toka Mtwara kwenda Dar es Salaam, inasemekana bomba moja la mita tano (5) inagharimu fedha za kitanzania takribani bilioni tatu (3), hii ni hatari tujiulize umbali uliopo kati ya Mtwara na Dar nikilometa ngapi? Kwani ni zaidi ya kilometa 560 mara hiyo bilioni 3 tunazani ni pesa kiasi gani zitatumika kwa ajli ya mradi huo?kwanini wasifanye opportunity cost ya kujenga hizo plants Mtwara? ili kuokoa gharama za usafirishaji wa gesi wanasafirisha na wanaenda kujenga plants nyingine Dar hivi hatuoni Taifa linaingia gharama mara mbili?

2. Ujenzi wa vinu vya kufulia gesi asilia Mtwara utasaidia kuchochea maendeleo ya mikoa ya kusini kwa kuwahakikishia ajira vijana ambao kila siku wanapanga mikakati ya kwenda Dar kutafuta ajira na maisha bora! Lazima Taifa lifanye diversification of economy kwani hata mataifa ya Ulaya na Marekani yalifanikiwa kwa kufanya diversification of economy sio kila mradi tuupeleke Dar es Salaam, tunasababisha population na kufanya uchumi kuwa concentrated in a single area hii ni hatari kwa mipango ya muda mrefu ya taifa hili.

3. Kujengwa kwa mitambo hiyo katika mikoa ya kusini itasaidia kuchochea maendeleo ya miundo mbinu mbalimbali kama barabara, bandari, na reli kwa lazima serikali itajenga miundo mbinu imara kwa ajili ya kusafirisha gesi iliyo tayari kwa kutumiwa na watumiaji mbalimbli kutoka mikoa tofauti tofauti, Taifa linahitaji mawazo yakinifu ya kuwasaidia wananchi wenye kipato cha chini hasa wanaotoka mikoa ya kusini.

Jumuiya ya vijana inashangazwa na kauli tata inayotolewa na viongozi wa Serikali ya CCM kwani ikumbukwe kuwa tarehe 25/07/2011 kwenye maadhimisho ya siku ya mashujaa Rais Kikwete aliwahutubia wananchi wa Mtwara na kuwahakikishia kuwa katika utawala wake atainua mikoa ya kusini kiviwanda na kumtaka Meya wa Manispaa ya Mtwara – Mikindani kutenga maeneo kwa ajili ya wawekezaji, wananchi wanahoji utawala wake unaelekea ukingoni hauna hata dalili ya kiwanda kimoja badala yake kunazoezi la kutaka kuhamisha gesi hiyo na kupelekwa Dar es Salaam, je hivi kweli Rais Kikwete na CCM yake wana mapenzi ya dhati na watu wa kusini?
Jumuiya ya vijana CUF Taifa inaendelea kushangazwa na taarifa ya Waziri wa nishati na madini Mheshimwa Sospeter Muhongo kwa kudai kuwa eti asilimia kumi na nne (14%)tu ya gesi iliyogunduliwa ndiyo inatoka Mtwara, kwanini sasa wasipeleke mradi huo wa bomba la kusafirishia gesi sehemu nyingine badala ya Mtwara? Jumuiya inasisitiza kuwa wanamtwara hawapingi gawio la pato linalotokana na gesi kutumika sehemu nyingine yeyote ya nchi, kwani ikumbukwe kuwa hata kwenye ushuru wa zao la korosho ambalo limekuwa zao la pili kuingizia ushuru wa Taifa mwaka jana wananchi hawajahoji lolote juu gawio la ushuru huo?

Kwa hiyo Jumuiya ya vijana CUF Taifa inashangazwa na kauli ya viongozi wa CCM ya kusema kuwa wanamtwara wanahitaji gesi iwanufaishe wao wakati ukweli ukijulikana kuwa kilio cha wanamtwara nikutaka uwekezwaji unaotokana na gesi ufanywe Mtwara na Lindi kama ilivyofanywa kwenye viwanda vya sukari, kwani miwa inalimwa Tuliani, Mtibwa, na Kilombero – Morogoro na viwanda viko huko kwa nini gesi iwe Mtwara plant iwekwe Dar es Salaam?

Kwa hiyo Jumuiya ya vijana CUF Taifa inaunga mkono gesi kutosafirishwa kupelekwa Dar es Salaam.

Imetolewa na,
Jumuiya ya Vijana CUF Taifa,

Friday, January 4, 2013

UAMUZI WANGU WA KUJIUNGA NA NCCR – MAGEUZI






Ndugu Deogratius Kisandu aliyeshika Kadi, Kulia kwake ni Ndg. Florian Rutayuga ( Afisa Utawala wa Chama) na Katikati ni Ndugu Faustin Sungura (Kaimu Katibu Mkuu) 



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


UAMUZI WANGU WA KUJIUNGA NA NCCR – MAGEUZI
Ndugu wanahabari,
Mimi ninaitwa Deogratius Kisandu, nimehitimu katika Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa huko Lushoto (SEKUCO) nina Shahada ya Elimu Maalum, Siasa na Utawala.
Nilikuwa mwanachama na kiongozi wa CHADEMA katika nafasi za; Katibu wa Wilaya ya Lushoto na Katibu wa Vijana wa Mkoa wa Tanga (Bavicha).
Mwaka 2010 niligombea ubunge katika jimbo la Lushoto, nilishika nafasi ya pili kwa kupata kura 5000+ dhidi ya mgombea wa CCM aliyepata kura 14000+ .
Ndugu wanahabari, 
Kwa muda mrefu nikiwa ndani ya CHADEMA, tumekuwa katika maelewano mabaya na hata pengine kujengewa chuki na fitina pale nilipojaribu kuhimiza viongozi wenzangu kufuata katiba ya Chama chetu.
Mwishoni mwa mwaka jana (2012) niliamua kujivua uanachama ndani ya CHADEMA na kuahidi kujiunga na Chama kingine.Vile vile nilisema siku hiyo nitaeleza sababu za msingi zilizonifanya nijivue uanachama na kukabidhi kadi ya Chama hicho.


1. Mnamo mwaka 2012 nilitangaza nia yangu ya kugombea urais kupitia CHADEMA. Msimamo huo umenijengea chuki na uhasama kwa viongozi wakuu wa CHADEMA akiwemo muasisi wa Chama hicho Mzee Edwin Mtei, kupinga vijana kuonesha dhamira zao.
Nimejiridhisha kwamba, CHADEMA ina watu wake inaowataka wagombee urais na hususan watu wa Kaskazini mwa nchi hii.
Yaliyonikuta mimi pia yamewahi kuwatokea marehemu Chacha Zakayo Wangwe, Zitto Zuberi Kabwe na John Magane Shibuda pale walipojaribu kuwania nafasi hiyo ndani ya Chama.
Inasikitisha sana kwa watu wanaotaka kugombea urais wanasakamwa, wale ambao hawataki kugombea na wala kutangaza kugombea urais ndiwo wanaolazimishwa kugombea nafasi hiyo.
Itakumbukwa kwamba, Dkt. Wilbroad Peter Slaa hakuwahi kujitangaza kuwa anataka kugombea urais, bali amekuwa analazimishwa kugombea urais, hata juzi Mwenyekiti wa CHADEMA ameonekana kumlazimisha Dkt. Slaa kugombea urais (2015).
2. Mnamo mwaka 2012, Dkt. Slaa ametangaza na kukiri kuwa anamiliki Kadi ya Chama Cha Mapinduzi na kwamba Kadi hiyo ililipiwa ada kwa miaka 20 hadi mwaka 2017.
Ninajua kuwa Dkt. Slaa anayo haki ya kuwa na Kadi hiyo kwa sababu aliinunua kwa fedha zake na hivyo ni mali yake.
Binafsi siridhiki na vitendo vya Dkt. Slaa, amekuwa anahamasisha watu wanaotoka CCM wamkabidhi Kadi za CCM. Je, hao nao hawakununua kwa fedha zao? Je, hawataki nao kuwa na kumbukumbu kama yeye? Bila shaka kuna siri kubwa imejificha nyuma ya pazia.
3. CHADEMA haitaki kuona vijana wanaochipukia wanakuwa na umaarufu ndani ya Chama hicho. Kwenye ziara za M4C wamekuwa wanawatumia watu wasioijua CHADEMA, wanazunguka nao Mikoani, wanawaacha vijana waliokipigania Chama hadi kikafika hapa kilipo.
Watu wanaopata nafasi nyeti ndani ya Chama hicho ni wale tu wenye udugu au uhusiano na viongozi wakuu wa Chama. Mfano mzuri ni mgawanyo wa vitu maalum vya ubunge.
Zaidi ya nusu ya viongozi wa juu wa Chama wamehakikisha ndugu zao au wake zao ndio wamepata nafasi hizo, zingine zinagawiwa kwa njia za kudhalilishana. Hivi sasa kuna mmoja wa wabunge wa viti maalum ana ujauzito wa mmoja wa viongozi wakuu wa Chama.
Ndugu wanahabari, 
Yapo mambo mengi na ambayo siwezi kuyamaliza kwa leo, ila kwa ufupi nianze na hayo ili yakikanushwa ndipo nitaeleza mengine.
Baada ya kusema hayo, ninatangaza sasa rasmi kuwa, kuanzia leo tarehe 04/01/2013 nitajiunga na Chama cha NCCR-Mageuzi.


SABABU ZA KUJIUNGA NA NCCR-MAGEUZI
1. Ni Chama kikongwe, waasisi na waanzilishi wa mageuzi hapa nchini. Ni Chama kilichopitia migogoro na misukosuko mingi ambacho ninaamini kimekomaa.
2. Ni chuo kizuri cha wanasiasa,watu wengi wamepitia hapa, wakafundwa na baadaye wakatamaniwa hata vyama vingine. Mifano michache ni Dkt. Masumbuko Lamwai, Dkt. Festus Limbu, Steven Wasira (CCM) na Ndesamburo, John Mnyika, Joseph R. Selasini, Chiku Obwao, Suzana Kiwanga, Profesa Mwesigwa Baregu, Mabere Marando nk.
Ninaamini kwamba, kujiunga kwangu na Chama hiki nitajifunza mambo mengi.
3. NCCR-Mageuzi ni Chama na kipimo cha demokrasia kwa vitendo. Ni Chama ambacho hakina mtu mmoja tu kwa ajili ya nafasi ya za uongozi, yeyote ana nafasi ya kugombea nafasi anayotaka na mkutano mkuu wa Chama ndio uamue nani anafaa kuwa mgombea urais.
Mfano, Mwaka 1995 Chama kilimsimamisha ndugu A.L. Mrema kugombea urais. Mwaka 2000 Chama kilimsimamisha ndugu Edith S. Lucina kugombea urais. Mwaka 2005 Dkt. E.A. S. Mvungi aligombea urais na mwaka 2010 Chama kilimsimamisha ndugu Hashim S. Rungwe aligombea urais. Hii ni tofauti na baadhi ya vyama vingine.
4. Nilipotangaza kugombea urais kupitia CHADEMA, niliwekewa mizengwe, nikajengewa chuki. Nilitangaza kugombea urais, lakini sikutangaza kwa mwaka gani, kwani mwaka 2015 umri wangu wa kikatiba wa kugombea urais hauniruhusu, nilikusudia baada ya mwaka 2015, lakini kwa CHADEMA inaonekana wana wagombea wao wa Kaskazini kwa miaka hamsini ijayo.
Ninaamini ndani ya NCCR-Mageuzi, umri wangu ukifika, mkutano mkuu ndio utaamua na siyo kiongozi mmoja.
Baada ya kusema hayo, ninaomba sasa nikabidhiwe Kadi ya NCCR-Mageuzi.


----------------------------------04/01/2013
D. KISANDU

Dkt. Mwakyembe akagua uwanja wa ndege wa Songwe, Mbeya


Picture
Waziri wa uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara yake katika uwanja wa Ndege wa Songwe, Mbeya amesema kuwa uwanja huo una hadhi ya Kimataifa na ni kati ya viwanja vikubwa viwili kujengwa baada ya uhuru, ukitanguliwa na uwanja wa Mkoa wa Kilimanjaro (KIA).

(picha zote na maelezo, credit: Mbeya Yetu blog)
Picture
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) Mhandisi Suleiman S. Suleiman akimwelezea Dkt. Harrison Mwakyembe jinsi uwanja wa ndege wa Songwe unavyofanya kazi toka uzinduliwe mwezi wa 12 mwaka jana na kuwa sasa uwanja huo umebaki kukamilisha maeneo ya maegesho ya ndege kubwa kama Boeing 737.
Picture
Hili ni eneo la kutua ndege na kurukia barabara hiyo ya ndege yenye urefu wa zaidi ya kilometa 3.5 km
Picture
Huu ni mnara wa kuongozea ndege katika kiwanja hicho
Picture
Mwongoza ndege mwandamizi John Chambo akimwezea waziri Mwakyembe jinsi wananvyofanya kazi ya kuongoza ndege katika mnara huo
Picture
Sura ya mbele ya uwanja wa Songwe
Picture
Maegesho ya zimamoto
Picture
Hili ndilo eneo la maegesho ya ndege kubwa aina ya Boeing 737 ambalo mwishoni mwamwezi huu linatarajiwa kuwa limekamilika


Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2H2wxliuB

Hoja ya Murtaza Mangungu, Mbunge wa Kilwa Kaskazini Kuhusu Gesi Asilia

Sekta ya gesi na mafuta ni moja kati ya sekta kubwa na ngeni kwa kiasi fulani hapa nchini. 

Kwa kipindi cha miaka mingi na haswa miaka ya sabini na themanini Serikali ya awamu ya kwanza ilifanya kazi kubwa ya uwekezaji katika utafiti wa mafuta na gesi nchini  lakini bila ya mafanikio ya uwekezaji.

Hii inaweza kuwa ilichangiwa sana na siasa zilizokuwapo kwa wakati ule kwa maana ya umagharibi na umashariki na pengine imani ya wawekezaji kutokana na msimamo tuliokuwa nao kama nchi  katika suala la ukombozi wa bara la afrika dhidi ya ukoloni pia uduni wa hali ya teknologia ya wakati ule na ukweli kwamba eneo letu la nchi za mashariki mwa Afrika ilijulikana kuwa ni ukanda wa gesi asilia tu  na enzi zile gesi asilia ilikuwa haina thamani kuliko mafuta. 

Kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni, nchi yetu imefanikiwa sana kuwavuta wawekezaji katika sekta na nyanja tofauti  sana ikiwamo katika gesi na utafiti wa mafuta. Hii ni nafasi nzuri tuliyoikosa kwa miaka mingi kiasi cha kutuweka nyuma kimaendeleo ukilinganisha na nchi nyingi za afrika na dunia ya tatu.

Lakini sasa kiasi kikubwa tumeanza kuona manufaa ya uwekezaji ule japo kwa uchache na changamoto nyingi ndani yake.

Tulianza mwaka 2012 na kumaliza na mfululizo wa matukio ya aina tofauti kwa waandishi kuandika makala na habari nyingi kuhusu shughuli na sekta nzima ya gesi nchini, na mara ya mwisho kabisa kufuatia maandamano ya wanachi wa Mtwara ambao walitokea katika vyama  tofauti.

Sikuona tatizo la waandamanaji wale pamoja na ujumbe ulitolewa bali baadhi ya ujumbe  unaonyesha zipo tafsiri nyingi zaidi ya madai ya mahitajio ya manufaa ya mapato katika uwekezaji wa gesi na bomba la gesi.

Nilipata wasisiwasi mkubwa sana baada ya kuona wanaojua ukweli wa jinsi mambo yalivyo na wale wasiojua kuamua kwa dhati kabisa kuuposha umma wa watanzania  na dunia kwa ujumla.

Niliwahi kujifunza kuwa ukweli utabaki kuwa ukweli na inastahili tuseme ukweli hata kama inauma kiasi gani kwa maana hakutakuwa na dhambi wala madhara zaidi ya ukweli huo. Pia uongo inatakiwa uwekwe mahali ambapo kila mmoja utauona. 

Madai ya wale wanaojiita waandamanaji ni kuwa gesi isitoke hadi pale Serikali itakaposema wananchi watanufaikaje  lakini  pamoja na mambo yote ambayo  wamesema na kuungwa mkono naomba tuambizane kwa kuulizana. Ni lini ambapo Serikali au wawekezaji wamesema kuwa bomba litafanya kazi ya kutoa gesi Mtwara kwenda Dar es salaam pekee? Nielewavyo mie leo hii kuwa bomba linaweza pia kutumika kutoa gesi Dar es salaam kwenda Mtwara pale ambapo patakuwa na mahitaji au matumizi ya ziada katika viwanda.

Msumbiji ambao wamegundua gasi nyingi zaidi yetu wanaweza kutumia bomba la gesi kupeleka katika masoko ya Kenya,Uganda sudan Rwanda Burundi na kadhalika au nchi kama Kenya ambazo nazo zimegundua gesi wanaweza kutumia kupitisha gesi kwenda Afrika ya kusini au kwingineko.Yote haya itatupa mapato makubwa sana kama vile nchi ya Ukraine inavyonufaika kupitisha bomba la gesi inayotoka Russia kwenda Ulaya magharibi.

Inaweza  kuwa kweli  Rais alitoa ahadi kuwa lazima gesi iwanufaishe watu wa mtwara kwa kuweka viwanda mtwara. Hivi ni kweli hatufahamu kuwa upo mradi wa ujenzi wa kiwanda cha saruji ,kiwanda cha uyayushaji chuma(iron smelter) na vinginevyo? 

Siamini sana kuwa itakua ni kazi rahisi kuhamisha viwanda vya chuma, saruji, chupa, rangi na mengineyo ambayo kwa sasa vipo Dar es Salaam kutokana na uwekezaji uliofanyika kwa zaidi ya miaka 40 au zaidi kuvihamisha na kuvipeleka mtwara? Ni kweli kuwa bidhaa zizalishwazo hivi sasa wananchi wa mtwara na lindi hawazitumii?

Nimekuwa nikiona magari  mengi sana kutoka Dar es salaam kwenda Lindi  na Mtwara na bidhaa za aina tofauti  ,ambazo zinazalishwa kutokana na umeme unatokana na gesi kutoka songo songo Kilwa. Hivi manufaa tuyasemayo ni ya namna ipi ?

Katika uwekezaji wa gesi na mafuta kampuni huhitaji uwekezaji mkubwa sana ambao mara zote huhitaji kuuza hisa katika masoko ya hisa au kutegemea makampuni mengineyo kujiingiza kushiriki kuwekeza(farm in). Je, kwa maandamano haya hatutaishia kulipa fidia kwa wawekezaji baada ya kuharibu mazingira mazuri ya ufanyaji kazi?

Wakati haya yakiendelea kufanyika , tayari yapo makubaliano kadhaa ambayo yamewekwa baina ya Serikali na makampuni ya uwekezaji kwa ajili ya kuendeleza gesi iliyopatikana . Mfano mzuri ni  eneo la Rushungi Kilwa kuna kampuni kubwa kutoka Norway na mshirika wake kutoka Marekani wanafanya uchunguzi wa uwezekano wa  kujenga LNG terminal ili kuisindika gesi hiyo na sehemu mbali mbali za mwambao wa Mkoa wa Lindi na Mtwara zinafanyiwa uchunguzi wa aina huo.

Uwekezaji huu umechelewa sana kufanyika haswa ukizingatia kuwa gharama zinapanda siku hadi siku. Dunia haikusubiri na uchumi unazidi kuwa wa aina tofauti na siku za nyuma. Imani ya wawekezaji ikipotea dhidi yetu tutatumia miaka mingapi kuirejesha?

Pia ikumbukwe kuwa Serikali imewekeza pesa nyingi sana kwa kusomesha na kulipa mishahara watumishi wa sekta husika lakini pia katika uwekezaji kwa sekta hii.

Inawezekana kabisa kuwa bado manufaa hayajaonekana moja kwa moja , lakini tujiulize kuwa gharama za chakula zilizopanda hivi sasa Lindi na Mtwara zimesababishwa na nini. Pia haitoshi kuwa thamani ya ardhi imepanda mara ngapi na kuwanufaisha watu wa mikoa hii?

Hivi tangu Serikali iweke chuo cha VETA  wanafunzi wangapi kutoka Lindi na Mtwara wamekubali kujianadikisha katika masomo ili kuja kupata ajira na kushiri katika sekta gesi.

Tusitarajie kuna siku zitagawiwa pesa kwa mafungu kutoka katika mapato yatokanayo na gesi na wala hakuna nchi duniani imewahi kufanya hivyo Manufaa ya pekee ambayo wananchi wa Mtwara na Lindi na Tanzania kwa ujumla  wanaweza kuyapata ni kama ifuatavyo.

  1. Kilimo:  gesi asilia itakuza  sekta nyingine kwa maana ya kilimo.  Gesi pia inaweza kukuza kilimo kwa kuinua sekta ya kilimo kwa maana ya uzalisha wa mbolea na viatilifu vingine kama sulphur ambayo inatumika sana kuthibiti ubwiri unga ambayo inasumbua sana mikorosho.Pia wananchi wataongeza kipato kutokana na kuwa na uzalisha mkubwa katika kilimo.
  2. Umeme:  gharama za umeme zinaweza kushuka kwa kiasi kikubwa sana haswa ukizingatia kuwa kwa sasa bado gharama ziko juu.Kama ni mfano mzuri,  hivi sasa Tanesco imeshusha gharama za uunganishaji umeme ili kuvutia wateja wengi kupata huduma hiyo na kuongeza uzalishaji lakini pia kushusha gharama za uzalishaji kwa ujumla ambapo itachangia kushusha gharama za maisha na kukabiliana na mfumuko wa bei.
  3. Elimu : gesi itasaidia kukuza elimu nchini haswa maeneo ya Lindi na Mtwara kwa maana ichangie  kuboresha, lakini pia kuinua elimu kwa watanzania wengi zaidi ili kuweza kunufaisha katika sekta ya gesi na nyinginezo mtambuka 
  4. Ufugaji:  itasaidia katika ufugaji haswa ikizingatiwa sekta hii inahitaji nyama, maziwa na mayai kwa kiasi kikubwa hivyo wananchi wakishikishwa vema itasaidia sana kukuza kipato chao na kuinua uchumi wao na nchi kwa ujumla. 
  5. Viwanda:  uanzishwaji wa viwanda vya mazao ya gesi kwa maana ya petrochemical industries, hii yote itachangia kukuza ajira na mapato kwa Serikali Kuu hadi kufikia ngazi Serikali za vijiji kwa ujumla 
  6. Mazingira:  gesi itasaidia kuhifadhi mazingira kwani matumizi yake yatapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya kuni na mkaa lakini pia inaweza kuwa mbadala wa petroli na dieseli katika magari na mitambo. Hakuna atakae kataa kuwa itasaidia pia kupunguza emission na kuokoa pesa nyingi za kigeni ambazo zingeweza kufanya shghuli nyingine za kiuchumi nchini.
  7. Uwekezaji:  utalenga kutoa ajira kwa watanzania haswa vijana, lakini watanzania pia wajue haya hayatapatikana kama hawatashiriki kusoma na kupata mafunzo ya kutosha ili kuweza kupata ajira hizo. Tunapozungumzia elimu haihusu sana kupata degree au diploma, hata ngazi ya cheti tu , kwa kozi za kawaida za ufundi kama magari,umeme ,uchomeaji n.k

Serikali kwa kushirikiana na taasisi za kama TPDC, TANESCO, NDC, NARCO,VETA, TPA na wengineo washirikiane kujenga uwezo kwa watanzania kushiriki kwenye sekta na si kutegemea kuagiza kila kitu kutoka nje na wageni wakashika kazi zote kwa kigezo kuwa hatujafikia viwango vya kimataifa kufanya kazi hizo. Changamoto ya makampuni ya uwekezaji (Mult national Companies) kutumia viwango kama ni kigezo cha kuyanyima kazi makampuni yetu ya ndani haswa ya wazawa iangaliwe kwa jicho pana zaidi

Katika maelezo ya Rais ni kuwa tuanzishe mfuko wa kuhifadhi pesa mapato yatokanayo na gesi (gas fund), naona tukubaliane na hili ila maoni yangu ni vema kuanzisha sovereign development fund ambayo mapato yatumike katika uwekezaji tu na si kwa ajili ya kula na kulipa mishahara au matumizi ya kawaida.

Nchi kama Trinidad & Tobago na Thailand leo zinanufaika katika viwanda vya kemikali (petrochemical industries) ambapo hata bandari na sekta nyinginezo maana kuna multiplier effect inayotokana na uwekezaji katika sekta hii. Hivyo hapana budi Bandari ya Mtwara na Kilwa nazo zikapanuliwa ili kuweza kuinua uchumi wa mikoa ya kusini.
Kwa kuzingatia haya na kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi na wawakilishi wao kwa ujumla , itasaidia sana kuondoa dhana iliyojengeka sasa na kuwa hali ya uadui ambao hauna tija kwa ustawi wa nchi yetu.

Tumekuwa na mgogoro na nchi ya Malawi kwa muda sasa, chanzo kikubwa inahisiwa ni rasilimali hizi za gesi na mafuta. Huku hili likiendelea kumekuwa na hisia za kujitunga mgogoro mwingine baina ya Tanzania na Congo. Wakati tunayatafakari haya tumeanza kuweka migogoro ndani ya nchi, ni kweli haya ndio tunayokusudia ?

Naamini kila anayeshinikiza haya yatendeke , wanajua vizuri zaidi ya hivyo. Ni kheri kuwa makini kwa matendo na matamshi yetu kwani ipo siku tutawajibika nayo. Amani ,upendo na utulivu una thamani kubwa kuliko gesi na madini. “Kama hujui unakokwenda, huwezi kupotea njia.’’

Murtaza Mangungu(MB)
Kilwa Kaskazini na mjumbe wa POAC

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2H2uh71vF

Rais Jakaya Kikwete Akutana na Mkuu wa Kijeshi wa Umoja wa Mataifa Luteni Generali Babacar Gaye


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  na Mshauri Mkuu wa Kijeshi wa Umoja wa Mataifa Luteni Generali Babacar Gaye baada ya kuonana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.Kushoto ni  Mkuu wa Majeshi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mshauri Mkuu wa Kijeshi wa Umoja wa Mataifa Luteni Generali Babacar Gaye baada ya kuonana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.Kushoto Mbele ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mahadhi Mahadhi Juma Maalim, akifuatiwa na Mkuu wa Majeshi Tanzania  Jenerali Davis Mwamunyange, na wa pili kulia ni Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi na wengine ni maafisa waandamizi katika JWTZ na Umoja wa mataifa.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja  na Mshauri Mkuu wa Kijeshi wa Umoja wa Mataifa Luteni Generali Babacar Gaye baada ya kuonana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.Kushoto Mbele ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mahadhi Juma Maalim, akifuatiwa na Mkuu wa Majeshi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange, na wa pili kulia ni Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi na wengine ni maafisa waandamizi katika JWTZ na Umoja wa mataifa.Picha na IKULU

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Atembelea Hifadhi ya Katavi


 Simba jike akiwa katika mawindo kwenye hifadhi ya Katavi.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda atembelea hifadhi ya katavi  na kuweza kuona wanyama waliopo katika hifadhi hiyo. Kulia ni mkewe Tunu Pinda akiwa ana tumia kiona mbali kuangalia simba waliokuwa katika mawindo kwa nyuma ni Sheni Abdallah Mkurugenzi Mkuu wa Katuma Bush Lodge iliyopo katika hifadhi ya katavi.Picha na Chris Mfinanga

MAZISHI YA MSANII SAJUKI


Picture
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ' Sajuki' nyumbani kwao wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es Salaam leo
Picture
Mke wa Rais, Mama, Salma Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es Salaam leo Januari 4, 2013.
Picture
Picture
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba akimpokea Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Mhe. Zitto Kabwe alipokuwa akiwasili msibani (nyumbani).
Picture
Picture
Picture
Picture
Picture
Rais Kikwete (aliyevaa koti la kijivu, miwani na kushikamanisha vidole) akiwa na baba mzazi wa marehemu (aliyevaa kanzu) na Simon Mwakifamba (aliyevaa shati la rangi ya machungwa) na Meya wa Ilala, Jerry Slaa (aliyevaa suti nyeusi, na miwani) wakati wa shughuli ya maziko ya SaJuKi yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Picture
Rais Kikwete akiwa ameshika sepetu kwa ajili ya kuliwekea udongo kaburi la Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) katika shughuli ya maziko yaliyofanyika mchana wa leo kwenye Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam.
Picture
Rais Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya msanii Sajuki leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Picture
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete akiwa ni mmoja ya waombolezaji waliojitokeza katika maziko ya msanii huyo.
Picture
Rais Kikwete akijadiliana jambo na Rais wa Shirikisho la Wasanii wa Filamu nchini Simon Mwakifwamba mara baada ya mazishi kwenye makaburu ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo, kushoto ni baba mzazi wa marehemu Mze Juma Kilowoko.
Picture
Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh Zitto Kabwe akifafanua jambo mbele ya baadhi ya Wanahabari kabla ya mazishi
Picture


Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2H2hjTvlI

Wednesday, January 2, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE ALIVYOUKARIBISHA MWAKA MPYA 2013 KIJIJINI KWAKE MSOGA NA WANAKIJIJI


Wanakiji wa Msoga wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani wakiangalia fashifashi wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya kijijini hapo. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakichangayika na wanakijiji wenzao wa kijijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, kuukaribisha mwaka mpya kwa fashifashi na ngoma za utamaduni
 ms3:Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kaka yake Mzee Selemani Kikwete kwa  wanakijiji wenzake  wa kijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakati wa sherehe za  kuukaribisha mwaka mpya kwa fashifashi na ngoma za utamaduni
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakipeana mkono wa heri na wanakijiji wenzao wa kijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, wakati wa kuukaribisha mwaka mpya kwa fashifashi na ngoma za kienyeji.Picha na IKULU

MKE WA WAZIRI MKUU MAMA TUNU PINDA ASHIRIKI MKESHA WA MWAKA MPYA SAMBAMBA NA TAMASHA LA WANAWAKE MKOANI RUKWA (RUKWA WOMEN IN ACTION)



Mama Tunu Pinda mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwasili katika ukumbi wa St. Maurus Chemchem Mjini Sumbawanga jana katika sherehe aliyoalikwa na Mkuu wa Mkoa Rukwa Injinia Stella Manyanya ya kuaga mwaka 2012 na kukaribisha mwaka 2013 iliyoenda sambamba na tamasha kubwa la mwanamke wa Rukwa RUWA (Rukwa Women in Actiion). Tamasha hilo lililobuniwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa lina lengo la kuwanunganisha wanawake wa Mkoa wa Rukwa pamoja katika tamaduni zao tofauti katika kuwainua kiuchumi na kifikra ambapo walishiriki kwa kuonyesha tamaduni zao za ngoma, mavazi na chakula. Lengo la tamasha hilo pamoja na umoja huo ni kwa ajili ya kunadi na kuhamasisha utalii wa ndani, kuwawezesha kinamama wa kipato cha chini, kuhamasisha na kuwezesha vita dhidi ya umaskini, mimba za mashuleni, lishe bora na chanjo za afya kwa watoto wachanga na wanawake wa kipato cha juu kuwawezesha wa kipato cha chini.
Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitoa hotuba yake katika tamasha hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza katika tamasha hilo kumkaribisha mke wa Waziri kuzungumza na washiriki zaidi ya mia sita walihudhuria katika tamasha hilo.
Mama Pinda (kulia), Mama Dora Rajab Rutengwe mke wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi (wa pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Stella Manyanya na wanawake wengine wakijumuika kucheza muziki wa kwaito katika kupasha misuli moto kwenye tamasha hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akionyesha vazi linalotangaza utalii wa ndani na rasilimali muhimu kama misitu, wanyama pori, na samaki.
Ilifika muda washiriki wa maonyesho hayo kupita mbele ya jukwaa kuu tayari kwa kuanza kuonyesha sanaa na mitindo mbalimbali.
Mmoja ya washiriki akionyesha moja ya vazi la kiutamaduni la asili ya makabila ya Rukwa kwa wazee wakati wa msimu wa baridi.
Katibu tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akisakata ngoma ya kinyaturu katika tamasha hilo. Kulia ni mwanae Hussein Chima.
Mama Tatu Chima mke wa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa akimpa zawadi ya shanga za kabila la kinyaturu Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda kabla ya kuanza kucheza ngoma ya kabila hilo. Kulia ni mumewe Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (wa pili kushoto) Injinia Stella Manyanya akishiriki kwenye ngoma ya kabila lake la wangoni waliojumuika kwenye tamasha hilo kuonyesha baadhi ya tamaduni zao. Wa kwanza kushoto akionyesha uwezo mkubwa katika kusakata ngoma hiyo ni mwandishi wa habari wa channel ten Judy Ngonyani.  
Mduara pia umo katika ngoma za kabila la wangoni. 
Washiriki wa kabila la wahaya wakionyesha baadhi ya mavazi ya asili ya kabila lao.
Ngoma za kihaya.
Majaji waliohusika katika katika mashindano ya tamaduni za makabila tofauti ya Mkoani Rukwa, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Kagera, Singida, Kigoma, Shinyanga na Mwanza. Mkoa wa Rukwa ulishinda katika Ngoma.
 Washiriki wa kabila la wafipa wakionyesha baadhi ya mavazi yao ya asili na baadhi ya zana zao za asili. 
 Sound ya ngoma ya kabila la wafipa ikitumbuiza katika tamasha hilo.Kigoda hutumika kusugua chungu ambacho hutoa mlio wa aina yake katika kunogeza ngoma ya kabila hilo.
 Washiriki wa kabila la wafipa wakionyesha tamaduni zao za kusaga unga na ulezi kwa kutumia zana za asili.
 Pombe ya asili ya kabila la wafipa inayotengenezwa kwa ulezi na kunyewa kwa mirija, raha duniani.
 Mambo yetu ya rusha roho nayo yalikuwepo. 
 Palikuwa hapatoshi.
Mvua ya shampen ya kukarisha mwaka mpya 2013 ikifunguliwa na mratibu wa tamasha hilo ambae pia ni Afsa maendeleo ya jamii Mkoa wa Rukwa Ndugu Deonisya Njuyui.
 Cheers kwa mwaka 2013. Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu akigonganisha glass na Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali watu Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashalla na Mke wa aliyekuwa Mbunge jimbo la Sumbawanga Mjini CCM Aeshi Hillal.
 Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Idd Kimanta akinywa togwa iliyoandaliwa na kabila la wahaya.
 Mbunge wa Jimbo la Kalambo Josephat Kandege nae akilamba tongwa.
 Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya wakionja ugali wa muhogo ulioandaliwa na kabila la Waha kutoka Kigoma.
 Ndizi kuku au Kuku ndizi kutoka katika kabila la wanyakyusa la Mkoani Mbeya.
 Maharage yaliyochanganywa na mboga za majani kutoka katika kabila la wanyakyusa la Mkoani Mbeya.
 Mshiriki Leah Mgagama kutoka katika kabila la wangoni akionysha moja ya vazi la kabila hilo na kifaa cha kuhifadhia chakula kisiharibike kijulikanacho kwa jina la "Kijamanda".
 Vazi la kitanzania likiwa na bandera ya taifa.
 Ilikuwepo mitindo mbalimbali ya mavazi.
 Onyesho la mavazi
 Onyesho ya vazi la mjamzito.
 Anthonia Nkyabonaki kutoka kabila la wahaya akionyesha mtindo wa mavazi.Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa

Popular Posts