Pages

Showing posts with label Tabora. Show all posts
Showing posts with label Tabora. Show all posts

Monday, January 7, 2013

Rais Jakaya Kikwete Alivyouteka Mji wa igunga


Mamia ya wananchi wa Igunga Wakilipuka kwa furaha katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika uwanja wa Barafu mjini Igunga baada ya kuzindua ujenzi wa daraja la Ndutu pamoja na mradi mkubwa wa maji utaohudumia asilimia 70 ya wakazi wa Igunga ambapo Rais Jakaya Kikwete aliung'uruma leo hii
Rais Jakaay Mrisho Kikwete akisalimiana kwa kuwapungia mamia ya wananchi wa Igunga katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika uwanja wa Barafu mjini Igunga baada ya kuzindua ujenzi wa daraja la Ndutu pamoja na mradi mkubwa wa maji utaohudumia asilimia 70 ya wakazi wa Igunga.
Rais Jakaay Mrisho Kikwete akihutumia mamia ya wananchi wa Igunga katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika uwanja wa Barafu mjini Igunga baada ya kuzindua ujenzi wa daraja la Ndutu pamoja na mradi mkubwa wa maji utaohudumia asilimia 70 ya wakazi wa Igunga.
Rais Jakaay Mrisho Kikwete akisalimiana na  mamia ya wananchi wa Igunga Mara baada ya kumaliza   mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika uwanja wa Barafu mjini Igunga baada ya kuzindua ujenzi wa daraja la Ndutu pamoja na mradi mkubwa wa maji utaohudumia asilimia 70 ya wakazi wa Igunga.Picha na IKULU

Friday, November 23, 2012

KINANA ALIPOTUA KWA MUDA TABORA NA KUKUTANA NA VIONGOZI WA MKOA


 Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana, akimsalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwasa, wakati alipotua kwenye uwanja wa Ndege wa Mkoani humo leo asubuhi kwa ajili ya kukutana na baadhi ya Viongozi wa CCM wa mkoa huo. Wengine ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na  Seif Khatib, anayeshuka kwenye ngazi ndegeni ni Mwanri.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Tabora alipotua kwa muda mkoani humo wakati akitoka Rukwa kuelekea Geita asubuhi hii.
Mkuu wa mkoa wa Tabora, Fatma Mwasa akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akipotua kwa muda mkoani humo akitokea Rukwa kwenda Geita asubuhi hii.

Sunday, August 26, 2012

Katibu Mkuu wa Chadema Dk Wilbrod Slaa Kwenye Mkutano wa Kuwashukuru Wananchi wa Jimbo la igunga

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, akisalimiana na aliyekuwa mgombea wa ubunge jimbo la Igunga katika uchaguzi mdogo mwaka jana, kupitia Chadema, Mwalimu Joseph Kashindye, walipokutana katika mkutano wa kuwashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa ushiriki wao katika kesi ya uchaguzi wa jimbo hilo, ambayo Chadema kiliibuka mshindi, uliofanytika kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Igunga
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa akikumbatinana na Mbunge wa Maswa Mashariki, Slyvester Kasulumbai, walipokutana katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi wa jimbo la Igunga kwa ushiriki wao katika kesi ya uchaguzi wa jimbo hilo, kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Igunga juzi.
Kutokana na kilichoelezwa kuwekwa kwa lami chini yakiwango katika mlima Sekenke mkoani Singida, imeharibika vibaya kama inavyoonyesha pichani magari yakipita kwa shida baada ya lami hiyo kubomoka kwa kipindi kifupi tangu iwekwe, kama ilivyokutwa jana.Picha na Joseph Senga

MKUTANO WA CHADEMA IGUNGA

Katibu Mkuu wa Chamacha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia wananchi wa mji wa Igunga na vitongoji vyake, katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi kwa ushiriki wao katika kufanikisha kesi ya uchaguzi wa jimbo hilo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga.
Aliyekuwa mgombea wa jimbo la Igunga katika uchaguzi mdogo mwaka jana, kupitia Chadema, mwalimu Joseph Kashindye na aliyekuwa meneja wa kampeni, Slyvester Kasulumbai, wakiwasili kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga, ambako kulifanyika mkutano wa hadhara.Picha zote na Joseph Senga)

Monday, July 2, 2012

ATEKELEZA FAMILIA BAADA YA MKE KUJIFUNGUA WATOTO WANAOFANANA NA NYANI.

Mtoto Alhaj.
Mtoto Alhaj akiwa amesimama.
Mtoto Alhaj akiwa anatembea.
Abdulatifu Sadik (5) akipata kifungua kinywa nje ya nyumbani kwao.
Mwanaharusi Juma akiwa nje ya nyumba yake pamoja na watoto wake Ahaj (10) mwenye shati Nyekundu na Abdulatifu.Picha zote na Nathaniel Limu
---
Mjumbe wa kamati ya shule ya msingi Ndulungu tarafa ya Ndago wilayani Iramba mkoa wa Singida, Sadik Suleman Mnyawi (44), amemtelekeza mke wake mdogo Mwanaharusi Juma (34), kwa zaidi ya miaka miwili na kumsababishia maisha kuwa magumu.Imedaiwa kwamba Mnyawi amemtelekeza mke wake huyo, kwa madai kwamba amezaa watoto wawili wanaofafana na nyani.
Mjumbe huyo wa kamati ya shule, amemtelekeza mke wake mdogo na kumpora nguo zote na kumwachia zile alizokuwa amevaa tu. Pia aliondoka na matandiko yote ya kitandani na kubakisha chaga pekee.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwanaharusi awali alikuwa ameolewa na mwanaume mwingine waliobahatika kupata mtoto mmoja, Fadhili Juma (15).Alisema baada ya kuachana na mwanaume wa kwanza, mwaka 2002, aliolewa na Mnyawi ambaye amemtoroka na kumwacha bila matunzo yoyote ya watoto watatu aliozaa naye.Alisema katika kipindi cha miaka 10 ya ndoa yake na Mnyawi, walifanikiwa kupata watoto watatu kati yao, wawili wakiwa wanafanana na nyani.

“Mtoto wangu yule niliyezaa na mume wa kwanza, Fadhila Juma, yeye yupo darasa la saba mwaka huu. Ramadhani (6) ambaye nimezaa na Mnyawi, yeye anasoma darasa la kwanza hapa Ndulungu”,alisema.

Mwanaharusi alisema kwa watoto wake aliozaa na Mnaywi,Alhaj (10) na Abdulatifu (5) ambao wana sura ya mnyama kutokana na hali zao zilivyo, wameshindwa kuanza shule.
Akifafanua zaidi, alisema watoto hao wanaofanana na nyani, hawasikii wala hawasemi. Mawasiliano yao yanategemea ishara tu.

“Ukiacha matatizo yao ya kutokusikia na kuzungumza, pia wanahema kwa tabu kubwa. Kama huwaoni, ukisikia wanavyohema, unaweza ukafikiria kwamba hao zio binadamu ni nguruwe anahema”,alisema kwa masikitiko.

Mwanaharusi alisema mikono yao ni midogo mno na mifupi na ni dhaifu, matumbo na macho yao ni makubwa. Alhaji pekee ndiye mwenye uwezo wa kusimama na kutembea umbali mfupi na mwenendo wake unafanana na wa nyani.

Hata hivyo, alisema watoto hao wawili aliwazaa wakiwa wana sura za binadamu na afya zao zikiwa njema kabisa. Lakini wakati wanaendelea kukua, ndipo walipoanza kuugua mara kwa mara na kisha kubadilika sura.

“Wakati bado tunaelewana na mume wangu, tuliwahi kumpeleka Alhaji katika hospitali ya mkoa wa Singida. Alichunguzwa na alibainika kuwa na upungufu wa damu. Aliongezewa damu na kisha tuliruhusiwa kurudi nyumbani”,alisema.

Alisema baada ya kurudi nyumbani, haikuchukua muda, Alhaji alianza kuugua tena na baada ya kumshawishi mume wake Mnyawi, wampeleke hospitali ya rufaa, ndipo alipomkimbia na kuhamia kwa mke wake mkubwa.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa,alisema kuanzia wakati huo, anaishi maisha magumu mno ambayo ni ya kuomba omba. Mnyawi pamoja na familia yake, amewabembeleza wamsaidie mizigo wa kuwalea watoto hao, wamegoma kabisa.Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho, Idd Nyauli, alisema wamejitahidi kumshauri Mnyawi amrudie mke wake mdogo ili waweze kuwalea watoto wao pamaja, jitahida hizo zimegonga mwamba baada ya Mnyawi kugoma kumrudia Mwanaharusi.

Naye mratibu elimu wa kata hiyo Mwekwa Mwekwa, alisema watoto hao wawili, shule inayowafaa ni ile ya watoto wenye mtindio wa ubongo na si hizi za kawaida.Jitihada ya kumtafuta Mnyawi ambaye anaishi kijiji hicho cha Ndulungu, hazikuzaa matunda baada ya kuelezwa kwamba baada ya kusikia waandishi wa habari watafika kijijini hapo, alifunga safari na kuelekea jijini Mwanza.

Popular Posts