Pages

Showing posts with label Mwanza. Show all posts
Showing posts with label Mwanza. Show all posts

Thursday, September 6, 2012

CCM YATOA TAMKO MAUAJI YA KUTISHA MWANDISHI WA HABARI MKOANI IRINGA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Itakumbukwa tarehe 02/09/2012 katika operesheni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) mkoani Iringa kulitokea vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mwanahabari mzoefu Ndg. Daudi Mwangosi na kujeruhiwa vibaya kwa askari watatu wa kuzuia fujo.

Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao. CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine.

Tunatoa wito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza swala hili, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini yote - ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha ndugu yetu Daudi Mwangosi.

Pamoja na wito wetu wa kuchunguzwa suala hili kwa umakini na weledi mkubwa, pia tunatoa rai kwamba uchunguzi huu ufanyike kwa kutumia muda mfupi ili ukweli uweze kubainika mapema na hatua zinazostahili ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

Vilevile CCM inasikitishwa sana na mfululizo wa matukio ya watu kupoteza maisha au kujeruhiwa katika mikutano na operesheni mbalimbali zinazoendeshwa na CHADEMA nchini hasa zile zilizofanyika kwa kukaidi amri halali za vyombo vya ulinzi na usalama.

Kutaja matukio baadhi tu ni pamoja na lile la kuuwawa kwa kada wa CCM Mkoani Singida, kuuawa kwa Ndg. Ally Hassan mjini Morogoro, kuuawa kwa Ndg. Daudi Mwangosi Mjini Iringa hivi majuzi,kujeruhiwa kwa askari polisi Iringa na matukio mengine mengi ambayo yametokea wakati wenzetu wa CHADEMA wakiendesha operesheni zao mbalimbali nchini.

Matukio haya si mazuri kutokea kwenye shughuli za Chama cha siasa. Kwakweli ni aibu, inayohitaji uwajibikaji,hata kama ni wa kisiasa. Inapotokea shughuli za chama chako zinasababisha kupotea kwa maisha ya watu kila unapozifanya na bado usitake kuwajibika, inahitaji roho ngumu na ujasiri wa aina yake.

Inakuwa mbaya zaidi pale vifo hivi vinaposababishwa na Chama hicho kutotii amri halali zilizotolewa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi inayovipa pia uhalali vyama vya siasa kuwepo na kuendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria.

Laiti Chama hicho kingesubiri siku chache zilizobakia kabla ya Sensa kuisha kabla ya kuendelea na mikutano yake ni dhahiri mauaji haya yasingetokea. Lakini kauli za kukebehi na uamuzi wa kukaidi amri ya Jeshi la Polisi na kusema "tupo tayari kwa lolote" ni ishara kwamba Chama hiki kiliandaa na kujiandaa na fujo zilizotokea.

Tunatoa wito kwa vyama vya siasa na wanasiasa kwa ujumla kujenga utamaduni wa kuheshimu utawala wa sheria. Amani na utulivu vulivyopo nchini ni kazi nzuri iliyojengwa kwa muda mrefu na waasisi wetu kwa kujenga utamaduni wa kuzingatia utawala wa sheria.

Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Taifa.

Saturday, July 14, 2012

FAINALI YA WHITE DENT QUIZ 2012 JIJINI MWANZA

Chemi cotex Industries Managing Director Lakshmi Narayan Rathi awarding the Whitedent squiz trophy to winning school – Pendo English Medium school – Dar es sallam

Chemi cotex industries Managing director Lakshmi Narayan Rathi (left) awarding the 1 million TSH Gift voucher for buying books for the school to the students of the winning school – Pendo English Medium School
--
Dar es Salaam; 13 July, 2012:Chemi & Cotex industries Ltd, watengenezaji wa watunga ya dawa za meno za Whitedent na bidhaa nyingine za usafi wa kinywa ya leo ina furaha kutangaza fainali ya Whitedent shule squiz 2012.

Washindiwasquizhii mwaka huu ni Pendo English Medium kutoka Mwanza, ambayoilichukuakombe la whitedent Squiz mara baada ya kuwabwagaShule ya Msingi Yombo Vituka Dar es sallam katika fainali hizo.

Timu hiyo ilijishindia kompyuta 9, printer pamoja, vocha za shilingi milioni 1 milioni kwa ajili ya kununua vitabu vya shule, baiskeli kwa ajili ya wanafunzi walioshiriki mbali na vocha zenye thamani ya shilingi 200,000 kwa ajili ya kununua vitabu, Shule ilipatiwa kompyuta 4, printer 1 na vocha za manunuzi za shilingi 400,000 kwa ajili ya kununua vitabu na saa, Vochaya100,000 kwaajiliya kununua vitabu kwa wanafunzi walioshiriki.

Zawadinyinginewalizopewawale walioingia katika hatua ya nusu fainali na robo ni kompyuta, taa za nishati yajua, mipira, dawazameno, miswaki mbali na T-shirt nakujishindiavyetivyotehivivikiwana thamani ya shilingi milioni 30.

Hotuba ya kuhitimisha kutokaChemi&Cotex kwa wanafunzi mjini Mwanza iliwapongeza wanafunzi wotena shule zilizoshinda kwa ushirikiano wao wa hali na mali katika mashindano hayonakwa umma piaikiwa ni pamoja na ziara hasa katika vituo vya mayatima, Dar na
Arusha.
Shindano hili lilihusisha wanafunzi wa darasa la sita wenye umri kati ya miaka 12-13 kwa kuzingatia jinsiaili kuweza kukabialiana na changamoto na wote walipewa zawadi mbalimbali.
Zaidi ya hapo shindano hili lilishirikisha zaidi shughuli za kijamii ambapo washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya robo fainali na nusu fainali walipata fursa ya kutembelea vituo vya yatima kujua maendeleo yao kielimu zaidi na pia kuwapatia zawadi mbalimbali kutoka Chemi&Cotex. Tunayo furaha kubwa kutangaza kuwa chemsha bongo mashulenii mehitimishwa rasmi.
Ends.

Sunday, July 8, 2012

Fainali za shindano la Serengeti Fiesta Mc Shujaa 2012


Pichani kulia ni mmoja wa waratibu wa tamasha la Serengeti Mc Shujaaa-Mwanza,Adam Mchomvu akimtangaza mshindi wa shindano la Serengeti Mc Shujaaa,aitwaye Ramastar pichani shoto ndani ya jijini la Mwanza.Shindano hilo limefanyika jioni ya leo kwenye kiota cha maraha cha Clup Lips,Isamilo jijini humo.Katika mchakato wa shindano hilo kulikuwepo na msisimko mkubwa kwa vijana wengi kujitokeza na kushiriki kikamilifu na kuwa ushindani mkubwa,aidha walijitokeza vijana wapatao 56 na hatimaye kupatikana mshindi mmoja ambaye atakwenda Dar kushindana na wengine kutoka mikoa mbalimbali kwenye kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lililopangwa kufanyika katika viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni.
Fainali ya kumsaka kinara wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa 2012 ndani ya jiji la Mwanza,pichani kulia ni Ramastar akimisikiliza kinara mwenzie Ramside akighani katika hatua ya mwisho kabisa.
Adam Mchomvu akiwa na washiriki wawili wa shindano la Mc Shujaa,kulia ni Ramastar na shoto ni Ramside ambao walionesha umahiri na ushindani mkubwa katika suala zima la kughani mbele ya mashabiki kibao (hawapo pichani) waliojitokeza kushuhudia mpambano huo ndani ya Club Lips,Isamilo jijini Mwanza.
Baadhi ya Mashabiki wakifuatilia mchuano mkali wa kumpata Mc Shujaa ndani ya jiji la Mwanza jioni ya leo.
Pichani kulia ni mmoja wa majaji wa shindano la Serengeti Fiesta Mc Shujaa 2012,Prodyuza Duke akizungumza machache kabla ya shindano halijaanza,shoto kwake ni jaji mwingine na pia ni mmoja wa waratibu wa shindano hilo Reuben Ndege a.k.a Ncha Kali akisikiliza kwa makini.
Jaji Reuben Ndege a.k.a Ncha kali akitoa muongozo kwenye shindano hilo .
Adam Nchomvu akisoma majina ya washiriki waliongia kwenye robo fainali ya Serengeti Fiesta Mc Shujaa 2012
Msanii chipukizi Ramastar akionesha umahiri wake wa kughani.
Baba Johniiii nae akishusha mistari yake mbele ya washiriki walioingia robo fainali.
Mmoja wa washiriki aitwaye Pusha akikamua vilivyo mitindo huru.
Majaji wa shindano la Serengeti Fiesta Mc Shujaa 2012 wakiwa makini katika suala zima la kutafuta kinara wa shindano hilo ambalo kwa asilimia kubwa vijana wengi wamevutiwa nalo,kiasi hata kupelekea vijana wengi kujitokeza na kushiriki safi kabisa.Pichani kulia ni Jaji Ncha Kali,Deey-Classic pamoja na Prodyuza Duke.

Usiku wa Mtu Mzima Dawa Wafana Mwanza


Mmoja wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Ommy Dimpo akijiachia jukwaani na mmoja wa mashabiki waliyejitokeza kucheza nae,kwenye shoo ya Usiku wa Mtu mzima Dawa uliofanyika kwenye kiota cha maraha cha Villa park usiku wa kuamkia leo,jijini Mwanza.Aidha katika makamuzi hayo washabiki wapenzi wa muziki wa kizazi kipya walijaa ile mbaya na palikuwa hapatoshi hata kidogo.

Msanii mahiri wa hip hop hapa nchini,Mwana FA akikamua kitu cha laiti na shabiki wake jukwaani kama picha ionekavyo.
Wacheza shoo wa Ommy Dimpoz wakiwajibika jukwaani.
wasanii wa kundi la Wanaume TMK wakiongozwa na Chege na Temba wakilishambulia jukwaa vilivyo,ama kwa hakika ilikuwa ni shangwe tu kwenye makamuzi ya shoo ya Usiku wa Mtu mzima dawa.
Wasanii Chege na Ydash wote kutoka Wanaume TMK wakiwarusha wakazi wa Mwanza ni kibao chao cha Dar mpaka Moro.
Wanaumeeee...eeeeeh..! Wanauuumeeeee.....halafu mashabiki wanaitikia kwa nguvu kabisa eeeehhhh..!
"Sijui nimtawanyee.....aah huwezi wewe mtu mzima dawa."! Mh Temba akikamua vilivyo na Bibi Cheka jukwaai saafi kabisa huku shangwe zikiwa zinasikika kila kona,kwani Bibi Cheka alionesha uwezo wake mkubwa wa kukamua jukwaa,hata ile mitindo huru nini na niniii yuko swafi mbaya..aaah mbona palinoga Villa Park usiku wa kuamkia leo.
Ommy Dimpoz akikamu mbele ya umati mkubwa ndani ya kiota cha maraha cha Villa Park usiku wa kuamkia leo.
Watu kibao walifurika ndani ya ukumbi wa Villa Park kushuhudia Usiku wa mtu mzima dawa.
Pamoja na kupotea kiaina kwenye gemu ya muziki wa Bongofleva,Ferouz bado nyota yake inaonekana kuwa angavu,alifanya vyema ndani ya ukumbi wa Villa Park,kiasa kwamba shangwe kila wakati zilikuwa za kutosha.
Mkubwaa na wanaweee....na yeyeee yumooo.. ! Mkubwa Fella nae akitafuta kimwana wa kunogesha jukwaa safi kabisa.
Mkali mwingine wa mitindo huru,Mwana FA a.k.a Binadamu akikamua vilivyo ndani ya ukumbi wa Villa Park usiku wa kuamkia leo,kwenye shoo ya usiku wa mkubwa dawa ambao ulifana kwa kiasi kikubwa.Picha zote Zimeletwa hapa na Michuzijr

Monday, July 2, 2012

ATEKELEZA FAMILIA BAADA YA MKE KUJIFUNGUA WATOTO WANAOFANANA NA NYANI.

Mtoto Alhaj.
Mtoto Alhaj akiwa amesimama.
Mtoto Alhaj akiwa anatembea.
Abdulatifu Sadik (5) akipata kifungua kinywa nje ya nyumbani kwao.
Mwanaharusi Juma akiwa nje ya nyumba yake pamoja na watoto wake Ahaj (10) mwenye shati Nyekundu na Abdulatifu.Picha zote na Nathaniel Limu
---
Mjumbe wa kamati ya shule ya msingi Ndulungu tarafa ya Ndago wilayani Iramba mkoa wa Singida, Sadik Suleman Mnyawi (44), amemtelekeza mke wake mdogo Mwanaharusi Juma (34), kwa zaidi ya miaka miwili na kumsababishia maisha kuwa magumu.Imedaiwa kwamba Mnyawi amemtelekeza mke wake huyo, kwa madai kwamba amezaa watoto wawili wanaofafana na nyani.
Mjumbe huyo wa kamati ya shule, amemtelekeza mke wake mdogo na kumpora nguo zote na kumwachia zile alizokuwa amevaa tu. Pia aliondoka na matandiko yote ya kitandani na kubakisha chaga pekee.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwanaharusi awali alikuwa ameolewa na mwanaume mwingine waliobahatika kupata mtoto mmoja, Fadhili Juma (15).Alisema baada ya kuachana na mwanaume wa kwanza, mwaka 2002, aliolewa na Mnyawi ambaye amemtoroka na kumwacha bila matunzo yoyote ya watoto watatu aliozaa naye.Alisema katika kipindi cha miaka 10 ya ndoa yake na Mnyawi, walifanikiwa kupata watoto watatu kati yao, wawili wakiwa wanafanana na nyani.

“Mtoto wangu yule niliyezaa na mume wa kwanza, Fadhila Juma, yeye yupo darasa la saba mwaka huu. Ramadhani (6) ambaye nimezaa na Mnyawi, yeye anasoma darasa la kwanza hapa Ndulungu”,alisema.

Mwanaharusi alisema kwa watoto wake aliozaa na Mnaywi,Alhaj (10) na Abdulatifu (5) ambao wana sura ya mnyama kutokana na hali zao zilivyo, wameshindwa kuanza shule.
Akifafanua zaidi, alisema watoto hao wanaofanana na nyani, hawasikii wala hawasemi. Mawasiliano yao yanategemea ishara tu.

“Ukiacha matatizo yao ya kutokusikia na kuzungumza, pia wanahema kwa tabu kubwa. Kama huwaoni, ukisikia wanavyohema, unaweza ukafikiria kwamba hao zio binadamu ni nguruwe anahema”,alisema kwa masikitiko.

Mwanaharusi alisema mikono yao ni midogo mno na mifupi na ni dhaifu, matumbo na macho yao ni makubwa. Alhaji pekee ndiye mwenye uwezo wa kusimama na kutembea umbali mfupi na mwenendo wake unafanana na wa nyani.

Hata hivyo, alisema watoto hao wawili aliwazaa wakiwa wana sura za binadamu na afya zao zikiwa njema kabisa. Lakini wakati wanaendelea kukua, ndipo walipoanza kuugua mara kwa mara na kisha kubadilika sura.

“Wakati bado tunaelewana na mume wangu, tuliwahi kumpeleka Alhaji katika hospitali ya mkoa wa Singida. Alichunguzwa na alibainika kuwa na upungufu wa damu. Aliongezewa damu na kisha tuliruhusiwa kurudi nyumbani”,alisema.

Alisema baada ya kurudi nyumbani, haikuchukua muda, Alhaji alianza kuugua tena na baada ya kumshawishi mume wake Mnyawi, wampeleke hospitali ya rufaa, ndipo alipomkimbia na kuhamia kwa mke wake mkubwa.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa,alisema kuanzia wakati huo, anaishi maisha magumu mno ambayo ni ya kuomba omba. Mnyawi pamoja na familia yake, amewabembeleza wamsaidie mizigo wa kuwalea watoto hao, wamegoma kabisa.Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho, Idd Nyauli, alisema wamejitahidi kumshauri Mnyawi amrudie mke wake mdogo ili waweze kuwalea watoto wao pamaja, jitahida hizo zimegonga mwamba baada ya Mnyawi kugoma kumrudia Mwanaharusi.

Naye mratibu elimu wa kata hiyo Mwekwa Mwekwa, alisema watoto hao wawili, shule inayowafaa ni ile ya watoto wenye mtindio wa ubongo na si hizi za kawaida.Jitihada ya kumtafuta Mnyawi ambaye anaishi kijiji hicho cha Ndulungu, hazikuzaa matunda baada ya kuelezwa kwamba baada ya kusikia waandishi wa habari watafika kijijini hapo, alifunga safari na kuelekea jijini Mwanza.

Popular Posts